We Love God!

God: "I looked for someone to take a stand for me, and stand in the gap" (Ezekiel 22:30)

You're not God's judge. One day you'll discover it's the other way around

Bible – swahili_partial_NT – act

\h MATENDO

MATENDO YA MITUME
\c 1

1 Ndugu Theofilo,
\m Katika kitabu cha kwanza niliandika juu ya mambo yote Yesu aliyotenda
na kufundisha tangu mwanzo wa kazi yake
2 mpaka siku ile alipochukuliwa mbinguni. Kabla ya kuchukuliwa
mbinguni aliwapa maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu wale mitume
aliowachagua.
3 Kwa muda wa siku arobaini baada ya kifo chake aliwatokea mara
nyingi kwa namna ambazo zilithibitisha kabisa kwamba alikuwa hai.
Walimwona, naye aliongea nao juu ya ufalme wa Mungu.
4 Wakati walipokutana pamoja aliwaamuru hivi: “Msiondoke
Yerusalemu, bali ngojeeni ile zawadi aliyoahidi Baba, zawadi ambayo
mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
5 Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache,
ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Yesu anapaa mbinguni

6 Basi, mitume walipokutana pamoja na Yesu, walimwuliza, “Je Bwana,
wakati huu ndipo utakaporudisha ule ufalme kwa Israeli?”
7 Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira ya mambo hayo viko
chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.
8 Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa
nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya
Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”
9 Baada ya kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwa
mbinguni; wingu likamficha wasimwone tena.

10 Walipokuwa bado wanatazama juu angani, akiwa anakwenda zake, mara
watu wawili waliokuwa wamevaa nguo nyeupe walisimama karibu nao,
11 wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama
angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni
atakuja tena namna hiyohiyo mliivyomwona akienda mbinguni.”

Mathia anachaguliwa ashike nafasi ya Yuda

12 Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka mlima wa Mizeituni ulioko
karibu kilomita moja kutoka mjini.
13 Walipofika mjini waliingia katika chumba ghorofani ambamo
walikuwa wanakaa; nao walikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipo na
Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na
Yuda mwana wa Yakobo.
14 Hawa wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha
wa kadha, na Maria mama yake Yesu, na ndugu zake.

15 Siku chache baadaye, kulikuwa na mkutano wa waumini, karibu watu
mia moja na ishirini. Petro alisimama mbele yao,
16 akasema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko
Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi,
alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu
nguvuni.
17 Yuda alikuwa mmoja wa kikundi chetu maana alichaguliwa ashiriki
huduma yetu.
(((
18 “Mnajua kwamba yeye alinunua shamba kwa zile fedha alizopata
kutokana na kitendo chake kiovu. Akaanguka chini, akapasuka na matumbo
yake yakamwagika nje.
19 Kila mtu katika Yerusalemu alisikia habari za tukio hilo na
hivyo, kwa lugha yao, wakaliita lile shamba <Hekeli Dama>, maana yake,
<Shamba la Damu.>)
20 Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi:

<Nyumba yake ibaki mahame;
mtu yeyote asiishi ndani yake.>
\m Tena imeandikwa:

<Mtu mwingine achukue nafasi yake katika huduma hiyo.>
\m
21-22 Kwa hiyo, ni lazima mtu mwingine ajiunge nasi kama shahidi wa
ufufuo wake Bwana Yesu. Anapaswa kuwa mmoja wa wale waliokuwa katika
kundi letu wakati wote Bwana alipokuwa anasafiri pamoja nasi, tangu
wakati Yohane alipokuwa anabatiza mpaka siku ile Yesu alipochukuliwa
kutoka kwetu kwenda mbinguni.”

23 Basi, wakataja majina ya watu wawili; wa kwanza Yosefu aliyeitwa
Barsaba (au pia Yusto), na wa pili Mathia.
24 Kisha wakasali: “Bwana, wewe unajua mioyo ya watu wote. Hivyo,
utuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua
25 ili achukue nafasi hii ya huduma ya kitume aliyoacha Yuda akaenda
mahali pake mwenyewe.”
26 Hapo, wakapiga kura; kura ikampata Mathia, naye akaongezwa katika
idadi ya wale mitume wengine kumi na mmoja.

\c 2

Roho Mtakatifu anawashukia waumini

1 Siku ya Pentekoste ilipofika, waumini wote walikuwa wamekusanyika
pamoja.
2 Ghafla, sauti ikasikika kutoka angani; sauti iliyokuwa kama ya
upepo mkali, ikajaza ile nyumba yote walimokuwa wamekaa.
3 Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kama ndimi za moto,
vikagawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali
kadiri Roho alivyowawezesha.

5 Na huko Yerusalemu walikuwako Wayahudi, watu wamchao Mungu,
waliotoka katika kila nchi duniani.
6 Waliposikia sauti hiyo, kundi kubwa la watu lilikusanyika. Wote
walishtuka sana kwani kila mmoja wao aliwasikia hao waumini wakisema kwa
lugha yake mwenyewe.
7 Walistaajabu na kushangaa, wakisema, “Je, hawa wote tunaowasikia
wakisema hivi, si wenyeji wa Galilaya?
8 Imekuwaje, basi, kwamba kila mmoja wetu anawasikia wakisema kwa
lugha yake mwenyewe?
9 Baadhi yetu ni Waparthi, Wamedi na Waelami; wengine ni wenyeji wa
Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto na Asia,
10 Frugia na Pamfulia, Misri na sehemu za Libya karibu na Kurene;
wengine wetu ni wageni kutoka Roma,
11 Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka
Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe
mambo makuu ya Mungu.”
12 Wote walishangaa na kufadhaika huku wakiulizana, “Hii ina maana
gani?”
13 Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai
mpya!”

Hotuba ya Petro

14 Lakini Petro alisimama pamoja na wale kumi na mmoja akaanza
kuwahutubia watu kwa sauti kubwa: “Ndugu Wayahudi nanyi nyote mnaokaa
hapa Yerusalemu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
15 Watu hawa hawakulewa kama mnavyodhani; mbona ni saa tatu tu
asubuhi?
16 Ukweli ni kwamba jambo hili ni lile alilosema nabii Yoeli:

17 <Katika siku zile za mwisho, asema Bwana,

nitawamiminia binadamu wote Roho wangu.
Watoto wenu, wanaume kwa wanawake,
watautangaza ujumbe wangu;
vijana wenu wataona maono,
na wazee wenu wataota ndoto.

18 Naam, hata watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

nitawamiminia Roho wangu, siku zile,
nao watautangaza ujumbe wangu.

19 Nitatenda miujiza juu angani,

na ishara chini duniani;
kutakuwa na damu, moto na moshi mzito;

20 jua litatiwa giza,

na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,
kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana.

21 Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.>

22 “Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti
alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa
miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake,
kama mnavyojua.
23 Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba
Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya
wamsulubishe.
24 Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu akamwokoa katika maumivu ya
kifo kwa maana haingewezekana kabisa kifo kimfunge.
25 Maana Daudi alisema juu yake hivi:

<Nilimwona Bwana mbele yangu daima;
yuko nami upande wangu wa kulia,
na hivyo sitatikisika.

26 Kwa hiyo, moyo wangu ulifurahi;

tena nilipiga vigelegele vya furaha.
Mwili wangu utakaa katika tumaini;

27 kwa kuwa hutaiacha roho yangu katika kuzimu,

wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

28 Umenionyesha njia za kuufikia uzima,

kuwako kwako kwanijaza furaha!>

29 “Ndugu zangu, napenda kuwaambieni waziwazi juu ya mambo
yaliyompata Daudi, babu yetu. Yeye alikufa, akazikwa, tena kaburi lake
liko papa hapa petu mpaka leo.
30 Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia
kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.
31 Daudi aliona kabla mambo yatakayofanywa na Mungu na hivyo akasema
juu ya ufufuo wa Kristo wakati aliposema: <Hakuachwa kuzimu, mwili wake
haukuoza.>
32 Basi, Mungu alimfufua huyo Yesu na sisi sote ni mashahidi wa
tukio hilo.
33 Yesu aliinuliwa juu mpaka upande wa kulia wa Mungu, akapokea
kutoka kwa Baba ile zawadi aliyoahidi yaani Roho Mtakatifu; na mnachoona
sasa na kusikia ni mmiminiko wa huyo Roho.
34 Maana Daudi mwenyewe, hakupanda mpaka mbinguni; ila yeye alisema:

<Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia,

35 hadi nitakapowafanya adui zako kibao cha kukanyagia miguu yako.>

36 “Watu wote wa Israeli wanapaswa kufahamu kwa hakika kwamba huyo
Yesu mliyemsulubisha ninyi, ndiye huyo ambaye Mungu amemfanya kuwa Bwana
na Kristo.”

37 Basi, watu waliposikia hayo, walichomwa moyo, wakawauliza Petro
na wale mitume wenzake: “Ndugu zetu, tufanye nini?”
38 Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la
Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile zawadi ya
Roho Mtakatifu.
39 Maana, ahadi ile ilikuwa kwa ajili yenu, kwa ajili ya watoto
wenu, kwa ajili ya wote wanaokaa mbali; na kwa ajili ya kila mtu ambaye
Bwana Mungu wetu atamwita kwake.”

40 Kwa maneno mengine mengi, Petro alisisitiza na kuwahimiza watu
akisema, “Jiokoeni katika kizazi hiki kiovu.”
41 Wengi waliyakubali maneno yake, wakabatizwa. Watu wapatao elfu
tatu wakaongezeka katika kile kikundi siku hiyo.
42 Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja
kidugu, kumega mkate na kusali.

Maisha ya kila siku ya wale waumini

43 Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila
mtu akajawa na hofu.
44 Waumini wote waliendelea kuwa kitu kimoja na mali zao waligawana
pamoja.
45 Walikuwa wakiuza mali na vitu vyao kisha wakagawana fedha kadiri
ya mahitaji ya kila mmoja.
46 Waliendelea kukutana pamoja kila siku Hekaluni. Lakini wakati wa
kumega mkate, walikutana katika nyumba zao na wakakishiriki chakula
hicho kwa furaha na moyo mkunjufu.
47 Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana
aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.

\c 3

Petro na Yohane wanamponya kiwete mmoja

1 Siku moja, saa tisa alasiri, Petro na Yohane walikuwa wanakwenda
Hekaluni, wakati wa sala.
2 Na pale karibu na mlango wa Hekalu uitwao “Mlango Mzuri”,
palikuwa na mtu mmoja, kiwete tangu kuzaliwa. Watu walimbeba huyo mtu
kila siku na kumweka hapo ili aombe chochote kwa wale waliokuwa
wakiingia Hekaluni.
3 Alipowaona Petro na Yohane wakiingia Hekaluni, aliwaomba wampe
chochote.
4 Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia,
“Tutazame!”
5 Naye akawageukia, akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
6 Kisha Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu lakini kile
nilicho nacho nitakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, tembea!”
7 Halafu, akamshika mkono wa kulia, akamwinua. Papo hapo miguu na
magoti yake yakapata nguvu.
8 Akaruka, akasimama na kuanza kutembea. Halafu akaingia pamoja nao
Hekaluni, akitembea na kurukaruka huku akimtukuza Mungu.
9 Watu wote waliokuwa hapo walimwona akitembea na kumsifu Mungu.
10 Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule
“Mlango Mzuri” wa Hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa
yaliyompata.

Hotuba ya Petro

11 Watu wote, wakiwa na mshangao mkubwa wakaanza kukimbilia mahali
palipoitwa “Ukumbi wa Solomoni,” ambapo yule mtu alikuwa bado
anaandamana na Petro na Yohane.
12 Basi, Petro alipowaona watu hao akawaambia, “Wananchi wa
Israeli, kwa nini mnashangazwa na jambo hili? Mbona mnatukodolea macho
kana kwamba ni kwa nguvu zetu au utakatifu wetu sisi wenyewe tumemfanya
mtu huyu aweze kutembea?
13 Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza
Yesu mtumishi wake. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na
kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.
14 Alikuwa mtakatifu na mwema; lakini ninyi mlimkataa, mkataka mtu
mwingine aliyekuwa muuaji afunguliwe.
15 Basi, mlimuua yule ambaye ni chanzo cha uzima. Lakini Mungu
alimfufua, na sisi ni mashahidi wa tukio hilo.
16 Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu
mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya
kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.

17 “Sasa ndugu zangu, nafahamu kwamba ninyi na wakuu wenu mlitenda
hayo kwa sababu ya kutojua kwenu.
18 Lakini ndivyo Mungu alivyotimiza yale aliyotangaza zamani kwa
njia ya manabii wote, kwamba ilikuwa lazima Kristo wake ateseke.
19 Basi, tubuni mkamrudie Mungu ili afute dhambi zenu.
20 Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na
kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu.
21 Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa
kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake
watakatifu wa tangu zamani.
22 Kwa maana Mose alisema, <Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii
kama mimi kutoka kati yenu ninyi wenyewe.
23 Yeyote yule ambaye hatamsikiliza nabii huyo atatengwa mbali na
watu wa Mungu na kuangamizwa.>
24 Manabii wote, kuanzia Samweli na wale waliomfuata, walitangaza
habari za mambo haya ambayo yamekuwa yakitendeka siku hizi.
25 Ahadi zile Mungu alizotoa kwa njia ya manabii ni kwa ajili yenu;
na mnashiriki lile agano Mungu alilofanya na babu zenu, kama
alivyomwambia Abrahamu: <Kwa njia ya wazawa wako, jamaa zote za dunia
zitabarikiwa.>
26 Basi, ilikuwa kwa ajili yenu kwanza kwamba Mungu alimfufua
mtumishi wake, alimtuma awabariki kwa kumfanya kila mmoja wenu aachane
kabisa na maovu yake.”

Petro na Yohane wanapelekwa mahakamani
\c 4

1 Petro na Yohane walipokuwa bado wanawahutubia watu, makuhani na
mkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na Masadukayo *walifika.
2 Walikasirika sana, maana hao mitume walikuwa wanawahubiria watu
kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba wafu
watafufuka.
3 Basi, waliwatia nguvuni na kwa kuwa usiku ulikuwa umekaribia,
wakawaweka chini ya ulinzi mpaka kesho yake.
4 Lakini wengi kati ya wale waliosikia ujumbe wao waliamini, na
idadi ya waumini ikawa imefika karibu elfu tano.

5 Kesho yake, viongozi wa Wayahudi, wazee na walimu wa Sheria,
walikusanyika pamoja huko Yerusalemu.
6 Walikutana pamoja na Anasi, Kayafa, Yohane, Aleksanda na wengine
waliokuwa wa ukoo wa Kuhani Mkuu.
7 Waliwasimamisha mitume mbele yao, wakawauliza, “Ninyi mmefanya
jambo hili kwa nguvu gani na kwa jina la nani?”

8 Hapo, Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akawaambia,
“Viongozi na wazee wa watu!
9 Ikiwa mnatuuliza leo juu ya kile kitendo chema alichofanyiwa yule
mtu aliyekuwa kiwete na jinsi alivyopata kuwa mzima,
10 basi, ninyi na watu wote wa Israeli mnapaswa kujua kwamba mtu
huyu anasimama mbele yenu leo, mzima kabisa, kwa nguvu ya jina lake Yesu
wa Nazareti ambaye ninyi mlimsulubisha, lakini Mungu akamfufua kutoka
wafu.
11 Huyu ndiye ambaye Maandiko Matakatifu yanasema:

<Jiwe mlilokataa ninyi waashi,
sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.>
\m
12 Wokovu haupatikani kwa mtu mwingine yeyote, kwa maana duniani
pote, binadamu hawakupewa jina la mtu mwingine ambaye sisi tunaweza
kuokolewa naye.”

13 Hao wazee wa baraza, wakiwa wanajua kwamba Petro na Yohane
walikuwa watu wasio na kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juu ya
jinsi walivyosema kwa uhodari. Wakatambua kwamba walikuwa wamejiunga na
Yesu.
14 Lakini walipomwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao,
hawakuweza kusema kitu.
15 Hivyo, waliwaamuru watoke nje ya baraza, nao wakabaki ndani
wakizungumza kwa faragha.
16 Wakaulizana, “Tufanye nini na watu hawa? Kila mtu anayeishi
Yerusalemu anajua kwamba mwujiza huu wa ajabu umefanyika, nasi hatuwezi
kukana jambo hilo.
17 Lakini ili tupate kuzuia jambo hili lisienee zaidi kati ya watu,
tuwaonye wasiongee na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”

18 Kwa hiyo wakawaita tena ndani, wakawaonya wasiongee tena
hadharani, wala kufundisha kwa jina la Yesu.
19 Lakini Petro na Yohane wakawajibu, “Amueni ninyi wenyewe kama ni
haki mbele ya Mungu kuwatii ninyi kuliko kumtii yeye.
20 Kwa maana hatuwezi kuacha kusema juu ya mambo yale tuliyoyaona na
kuyasikia.”
21 Basi, hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukali zaidi, halafu
wakawaacha huru. Hawakuweza kuwapa adhabu kwa sababu watu wote walikuwa
wakimtukuza Mungu kwa sababu ya tukio hilo.
22 Huyo mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya arobaini.

Waumini wanamwomba Mungu awaimarishe

23 Mara tu walipoachwa huru, Petro na Yohane walirudi kwa wenzao,
wakawaeleza yale waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee.
24 Waliposikia habari hiyo waliungana pamoja katika kumwomba Mungu
wakisema, “Bwana, wewe ni Muumba wa mbingu na nchi, bahari na vyote
vilivyomo!
25 Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, babu yetu Daudi, aseme kwa nguvu
ya Roho Mtakatifu:

<Kwa nini mataifa yameghadhibika?
Mbona watu wamefanya mipango ya bure?

26 Wafalme wa dunia walijiweka tayari,

na watawala walikutana pamoja,
ili kumwasi Bwana na Kristo wake.>

27 “Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa
Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga
Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye umemtia mafuta.
28 Naam, walikutana ili wafanye yale ambayo ulikusudia na kupanga
tangu mwanzo kwa uwezo wako na mapenzi yako.
29 Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitisho vyao. Utuwezeshe sisi
watumishi wako kuhubiri neno lako kwa uhodari.
30 Nyosha mkono wako uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina
la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu.”

31 Walipomaliza kusali, pale mahali walipokuwa wamekutanika
pakatikiswa, nao wote wakajazwa Roho Mtakatifu. Wote wakaanza kuhubiri
neno la Mungu bila uoga.

Waliishi kama jamaa moja

32 Jumuiya yote ya waumini ilikuwa moyo mmoja na roho moja. Hakuna
hata mmoja aliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwa mali yake binafsi,
ila waligawana vyote walivyokuwa navyo.
33 Mitume walishuhudia kwa nguvu nyingi kufufuka kwa Bwana Yesu,
naye Mungu akawapa baraka nyingi.
34 Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maana waliokuwa na
mashamba au nyumba walikuwa wanaviuza
35 na kuwakabidhi mitume fedha hizo, zikagawiwa kila mmoja kadiri ya
mahitaji yake.

36 Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwa wa Kupro, jina lake Yosefu,
ambaye mitume walimwita jina Barnaba (maana yake, “Mtu mwenye kutia
moyo”).
37 Yeye pia alikuwa na shamba lake, akaliuza; akazichukua zile
fedha, akawakabidhi mitume.

\c 5

Udanganyifu wa Anania na Safira

1 Mtu mmoja aitwaye Anania na mkewe Safira waliuza shamba lao
vilevile.
2 Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha
alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
3 Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo
wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya
fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
4 Kabla ya kuliuza lilikuwa mali yako, na baada ya kuliuza, bado
hizo fedha zilikuwa zako uzitumie utakavyo. Kwa nini basi, uliamua
moyoni mwako kufanya jambo la namna hii? Hukumdanganya mtu; umemdanganya
Mungu!”
5 Anania aliposikia hayo, akaanguka chini, akafa. Watu wote
waliosikia habari ya tukio hilo waliogopa sana.
6 Vijana wakafika wakaufunika mwili wake, wakamtoa nje, wakamzika.

7 Baada ya muda wa saa tatu hivi, mke wake, bila kufahamu mambo
yaliyotukia, akaingia mle ndani.
8 Petro akamwambia, “Niambie! Je, kiasi hiki cha fedha ndicho
mlichopata kwa kuuza lile shamba?” Yeye akamjibu, “Naam, ni kiasi
hicho.”
9 Naye Petro akamwambia, “Mbona mmekula njama kumjaribu Roho wa
Bwana? Sikiliza! Wale watu waliokwenda kumzika mume wako, sasa wako
mlangoni na watakuchukua wewe pia.”
10 Mara Safira akaanguka mbele ya miguu ya Petro, akafa. Wale vijana
walipoingia, walimkuta amekwisha kufa; hivyo wakamtoa nje, wakamzika
karibu na mume wake.
11 Kanisa lote pamoja na wote waliosikia habari ya tukio hilo,
waliogopa sana.

Mitume wanafanya miujiza na maajabu mengi

12 Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini
walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
13 Mtu yeyote mwingine ambaye hakuwa mwamini hakuthubutu kujiunga
nao. Hata hivyo, watu wengine wasiokuwa wa imani hiyo waliwasifu.
14 Idadi ya watu waliomwamini Bwana, wanaume kwa wanawake,
iliongezeka zaidi na zaidi.
15 Kwa sababu hiyo, watu walikuwa wakipeleka wagonjwa barabarani na
kuwalaza juu ya vitanda na mikeka ili Petro akipita, walau kivuli chake
kiwaguse baadhi yao.
16 Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kando kando ya
Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu,
nao wote wakaponywa.

Mitume wanateswa

17 Kisha, Kuhani Mkuu na wenzake waliokuwa wa kikundi cha Masadukayo
wa mahali hapo, wakawaonea mitume wivu.
18 Basi, wakawatia nguvuni, wakawafunga ndani ya gereza kuu.
19 Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza,
akawatoa nje, akawaambia,
20 “Nendeni mkasimame Hekaluni na kuwaambia watu kila kitu kuhusu
maisha haya mapya.”
21 Mitume walitii, wakaingia Hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza
kufundisha.
Kuhani Mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu,
yaani halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi halafu wakawatuma watu
gerezani wawalete wale mitume.
22 Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani.
Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni,
23 wakisema, “Tulikuta gereza limefungwa kila upande na walinzi
wakilinda milango. Lakini tulipofungua hatukumkuta mtu yeyote ndani.”
24 Mkuu wa walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari
hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
25 Akafika mtu mmoja, akawaambia, “Wale watu mliowafunga gerezani,
hivi sasa wamo Hekaluni, wanawafundisha watu.”
26 Hapo mkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na watu wake walikwenda
Hekaluni, akawaleta. Lakini hawakuwakamata kwa kutumia nguvu, maana
waliogopa kwamba watu wangewapiga mawe.

27 Basi, wakawapeleka, wakawasimamisha mbele ya Baraza. Kuhani Mkuu
akawaambia,
28 “Tuliwakatazeni waziwazi kufundisha kwa jina la mtu huyu; sasa
mmeyaeneza mafundisho yenu pote katika Yerusalemu na mnakusudia
kutuwekea lawama ya kifo cha mtu huyo.”

29 Hapo Petro, akiwa pamoja na wale mitume wengine, akajibu,
“Lazima tumtii Mungu, na siyo binadamu.
30 Mungu wa babu zetu alimfufua Yesu baada ya ninyi kumwua kwa
kumtundika msalabani.
31 Huyu ndiye yule aliyekwezwa na Mungu mpaka upande wake wa kulia,
akawa kiongozi na Mwokozi, ili awawezeshe watu wa Israeli watubu, wapate
kusamehewa dhambi zao.
32 Sisi ni mashahidi wa tukio hilo, naye Roho Mtakatifu ambaye Mungu
amewapa wale wanaomtii, anashuhudia pia tukio hilo.”

33 Wajumbe wote wa lile Baraza waliposikia hayo, wakawaka hasira,
hata wakaamua kuwaua.
34 Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu
wa Sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya
lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.
35 Kisha akawaambia wale wajumbe wa Baraza, “Wananchi wa Israeli,
tahadhari kabla ya kutekeleza hicho mnachotaka kuwatenda watu hawa!
36 Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema
kuwa mtu wa maana na watu karibu mia nne wakajiunga naye. Lakini
aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
37 Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa
Galilaya. Huyu naye, aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa,
na wafuasi wake wakatawanyika.
38 Na sasa pia mimi nawaambieni, msiwachukulie watu hawa hatua
yoyote; waacheni! Kwa maana, ikiwa mpango huu au shughuli hii yao
imeanzishwa na binadamu, itatoweka yenyewe.
39 Lakini kama imeanzishwa na Mungu, siyo tu kwamba hamtaweza
kuwashinda, bali mtajikuta mnapigana na Mungu.”
Basi, wakakubaliana naye.
40 Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na
kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende
zao.
41 Basi, mitume wakatoka nje ya ule mkutano wa halmashauri wakiwa
wamejaa furaha, kwani walistahili kuaibishwa kwa ajili ya jina la Yesu.
42 Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya
Kristo, Hekaluni na nyumbani mwa watu.

Wasaidizi saba wa mitume
\c 6
1 Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea
manung’uniko kati ya wanafunzi waliosema Kigiriki na wale waliosema
Kiebrania. Wale waliosema Kigiriki walinung’unika kwamba wajane wao
walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
2 Kwa hiyo, mitume kumi na wawili waliita jumuiya yote ya wanafunzi,
wakasema, “Si vizuri sisi tuache kulihubiri neno la Mungu ili
tushughulikie ugawaji wa mahitaji.
3 Hivyo, ndugu zetu, chagueni miongoni mwenu watu saba wenye sifa
njema, waliojawa na Roho na wenye hekima; nasi tutawakabidhi jukumu
hilo.
4 Sisi, lakini, tutashughulika na sala na kazi ya kuhubiri neno la
Mungu.”

5 Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua
Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujawa na Roho Mtakatifu,
Filipo, Prokoro, Nikanora, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye
hapo awali alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.
6 Wakawaweka mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono.

7 Neno la Mungu likazidi kuenea na idadi ya waumini huko Yerusalemu
ikaongezeka zaidi, na kundi kubwa la makuhani wakaipokea imani.

Stefano anatiwa nguvuni

8 Mungu alimjalia Stefano neema tele, akampa nguvu nyingi hata akawa
anatenda miujiza na maajabu kati ya watu.
9 Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya
watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”,
nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
10 Lakini hawakuweza kumshinda kwa sababu ya hekima yake na kwa
sababu ya yule Roho aliyeongoza maneno yake.
11 Kwa hiyo waliwahonga watu kadhaa waseme: “Tumemsikia Stefano
akisema maneno ya kumkashifu Mose na kumkashifu Mungu.”
12 Kwa namna hiyo, waliwachochea watu, wazee na walimu wa Sheria.
Basi, wakamjia Stefano, wakamkamata na kumleta mbele ya Baraza kuu.
13 Walileta Barazani mashahidi wa uongo ambao walisema, “Mtu huyu
haachi kamwe kusema maneno ya kupakashifu mahali hapa patakatifu na
Sheria ya Mose.
14 Kwa maana tulikwisha msikia akisema eti huyo Yesu wa Nazareti
atapaharibu kabisa mahali hapa na kufutilia mbali desturi zile
tulizopokea kutoka kwa Mose.”
15 Wote waliokuwa katika kile kikao cha Baraza walimkodolea macho
Stefano, wakauona uso wake umekuwa kama wa malaika.

Hotuba ya Stefano
\c 7
1 Basi, Kuhani Mkuu akamwuliza, “Je, mambo haya ni kweli?”
2 Naye Stefano akasema, “Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni!
Mungu alimtokea baba yetu Abrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kabla
hajaenda kukaa kule Harani.
3 Mungu alimwambia: <Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo
wako; nenda katika nchi nitakayokuonyesha!>
4 Kwa hivyo, Abrahamu alihama nchi ya Kaldayo, akaenda kukaa Harani.
Baada ya kifo cha baba yake, Mungu alimtoa tena Harani akaja kukaa
katika nchi hii mnayokaa sasa.
5 Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata
hivyo, alimwahidia kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje
wakati huu hakuwa na mtoto.
6 Mungu alimwambia hivi: <Wazao wako watapelekwa katika nchi
inayotawaliwa na watu wengine, na huko watafanywa watumwa na kutendewa
vibaya kwa muda wa miaka mia nne.
7 Lakini mimi nitalihukumu taifa hilo litakalowafanya watumwa. Kisha
nitawatoa katika nchi hiyo ili waje kuniabudu mahali hapa.>
8 Halafu Mungu aliifanya tohara iwe ishara ya agano. Hivyo, Abrahamu
alimtahiri mtoto wake Isaka, siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka,
vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi
na wawili vivyo hivyo.

9 “Wale mababu walimwonea wivu Yosefu, wakamuuza utumwani Misri.
Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,
10 akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na
hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa
ile nchi na nyumba ya kifalme.
11 Kisha, kulizuka njaa kubwa katika nchi yote ya Misri na Kanaani,
ikasababisha dhiki kubwa. Babu zetu hawakuweza kupata chakula chochote.
12 Basi, Yakobo alipopata habari kwamba huko Misri kulikuwa na
nafaka, aliwatuma watoto wake, yaani babu zetu, waende huko Misri mara
ya kwanza.
13 Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake,
na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
14 Yosefu alituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote, jumla watu
sabini na tano, waje Misri.
15 Hivyo, Yakobo alikwenda Misri ambako yeye na babu zetu wengine
walikufa.
16 Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi Abrahamu
alilonunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.

17 “Wakati ulipotimia Mungu aitimize ahadi aliyompa Abrahamu, idadi
ya wale watu kule Misri ilikwisha ongezeka na kuwa kubwa zaidi.
18 Mwishowe, mfalme mmoja ambaye hakumtambua Yosefu alianza kutawala
huko Misri.
19 Alilifanyia taifa letu ukatili, akawatendea vibaya babu zetu kwa
kuwalazimisha waweke nje watoto wao wachanga ili wafe.
20 Mose alizaliwa wakati huo. Alikuwa mtoto mzuri sana. Alilelewa
nyumbani kwa muda wa miezi mitatu,
21 na alipotolewa nje, binti wa Farao alimchukua, akamlea kama mtoto
wake.
22 Mose alifundishwa mambo yote ya hekima ya Wamisri akawa mashuhuri
kwa maneno na matendo.

23 “Alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kwenda kuwaona
ndugu zake Waisraeli.
24 Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na
kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri. (((
25 Alidhani kwamba Waisraeli wenzake wangeelewa kwamba Mungu
angemtumia yeye kuwakomboa, lakini hawakuelewa hivyo.)
26 Kesho yake, aliwaona Waisraeli wawili wakipigana, akajaribu
kuwapatanisha, akisema: <Ninyi ni ndugu; kwa nini basi, kutendeana
vibaya ninyi kwa ninyi?>
27 Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema:
<Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wa watu?
28 Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?>
29 Baada ya kusikia hayo Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi
ya Midiani na huko akapata watoto wawili.

30 “Miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana alimtokea Mose
katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto kule jangwani karibu na mlima
Sinai.
31 Mose alistaajabu sana kuona jambo hilo hata akasogea karibu ili
achungulie; lakini alisikia sauti ya Bwana:
32 <Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo!>
Mose akatetemeka kwa hofu na wala hakuthubutu kutazama zaidi.
33 Bwana akamwambia: <Vua viatu vyako maana hapa unaposimama ni
mahali patakatifu.
34 Nimeyaona mabaya wanayotendewa watu wangu kule Misri. Nimesikia
kilio chao, nami nimekuja kuwaokoa. Basi sasa, nitakutuma Misri.>

35 “Huyu Mose ndiye yule watu wa Israeli waliyemkataa waliposema:
<Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?> Kwa njia ya
yule malaika aliyemtokea katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto, Mungu
alimtuma Mose huyo awe kiongozi na mkombozi.
36 Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na
maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa
muda wa miaka arobaini.
37 Mose ndiye aliyewaambia watu wa Israeli: <Mungu atawateulieni
nabii kama mimi kutoka katika ndugu zenu ninyi wenyewe.>
38 Wakati watu wa Israeli walipokutana pamoja kule jangwani, Mose
ndiye aliyekuwako huko pamoja nao. Alikuwa huko pamoja na babu zetu na
yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai; ndiye aliyekabidhiwa yale
maneno yaletayo uzima atupe sisi.

39 “Lakini yeye ndiye babu zetu waliyemkataa kumsikiliza;
walimsukuma kando, wakatamani kurudi Misri.
40 Walimwambia Aroni: <Tutengenezee miungu itakayotuongoza njiani,
maana hatujui yaliyompata Mose huyu aliyetuongoza kutoka Misri!>
41 Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na
kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
42 Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga,
kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii:

<Enyi watu wa Israeli!
Si mimi mliyenitolea dhabihu na sadaka
kwa muda wa miaka arobaini kule jangwani!

43 Ninyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki,

na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani.
Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu.
Kwa sababu hiyo nitakupeleka mateka mbali kupita Babuloni!>
\m
44 Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema lililoshuhudia
kuweko kwa Mungu. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye;
nakala kamili ya kile alichoonyeshwa.
45 Kisha babu zetu walilipokezana wao kwa wao mpaka wakati wa
Yoshua, walipoinyakua ile nchi kutoka kwa mataifa ambayo Mungu
aliyafukuza mbele yao. Hapo lilikaa mpaka nyakati za Daudi.
46 Daudi alipata upendeleo kwa Mungu, akamwomba Mungu ruhusa ya
kumjengea makao yeye aliye Mungu wa Yakobo.
47 Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba.

48 “Hata hivyo, Mungu Mkuu haishi katika nyumba zilizojengwa na
binadamu; kama nabii asemavyo:

49 <Bwana asema:

Mbingu ni kiti changu cha enzi
na dunia ni kiti changu cha kuwekea miguu.

50 Ni nyumba ya namna gani basi mnayoweza kunijengea,

na ni mahali gani nitakapopumzika?
Vitu hivi vyote ni mimi nimevifanya, au sivyo?>

51 “Enyi wakaidi wakuu! Mioyo na masikio yenu ni kama ya watu wa
mataifa. Ninyi ni kama baba zenu. Siku zote mnampinga Roho Mtakatifu.
52 Je, yuko nabii yeyote ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua hao
Mungu aliowatuma watangaze kuja kwake yule Mwenye Haki. Na sasa, ninyi
mmemsaliti, mkamuua.
53 Ninyi mliipokea ile Sheria iliyoletwa kwenu na Malaika, lakini
hamkuitii.”

Stefano anauawa

54 Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana,
wakamsagia meno kwa hasira.
55 Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu
mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa
Mungu.
56 Akasema, “Tazameni! Ninaona mbingu zimefunuliwa na Mwana wa Mtu
amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57 Hapo, watu wote katika kile kikao cha Baraza, wakapiga kelele na
kuziba masikio yao kwa mikono yao. Kisha wakamrukia wote kwa pamoja,
58 wakamtoa nje ya mji, wakampiga mawe. Wale mashahidi wakayaweka
makoti yao chini ya ulinzi wa kijana mmoja jina lake Saulo.
59 Waliendelea kumpiga mawe Stefano, huku akiwa anasali: “Bwana
Yesu, ipokee roho yangu!”
60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa
sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.

\c 8
1 Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa sawa.

Kanisa linaanza kuteswa
Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote,
isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za
mashambani za Yudea na Samaria.
2 Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia maombolezo
makubwa.

3 Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda
katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia
gerezani.

Injili inahubiriwa katika Samaria

4 Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule
ujumbe.
5 Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa
wenyeji wa hapo.
6 Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na
kuona ile miujiza aliyoifanya.
7 Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka
wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na
waliolemaa waliponywa.
8 Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.

9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa
amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu
wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
10 Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema,
“Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa <Nguvu Kubwa.”>
11 Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi
wake kwa muda mrefu.
12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya
Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na
wanaume.
13 Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa akiandamana na
Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.

14 Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari kwamba
wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro
na Yohane.
15 Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu;
16 maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote kati yao;
walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
17 Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao
wakampokea Roho Mtakatifu.
18 Hapo Simoni aling’amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume
waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha
akisema,
19 “Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono,
apokee Roho Mtakatifu.”

20 Lakini Petro akamjibu, “Potelea mbali na fedha zako kwa vile
unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
21 Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako
hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
22 Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza
kukusamehe fikira kama hizo.
23 Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa
dhambi!”
24 Simoni akajibu, “Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije
likanipata lolote kati ya hayo mliyosema.”

25 Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe
wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari
Njema katika vijiji vingi vya Samaria.

Filipo anambatiza ofisa mmoja wa Ethiopia

26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini
kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita
jangwani.)
27 Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo
kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea
nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa
Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo
alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
28 Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya.
29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari
hilo ukafuatane nalo.”
30 Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma
katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, “Je, unaelewa
hayo unayosoma?”
31 Huyo mtu akamjibu, “Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?”
Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
32 Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa
hii:

“Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa;
kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya,
yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.

33 Alifedheheshwa na kunyimwa haki.

Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake,
kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”

34 Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema
juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu
mwingine?”
35 Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu,
akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
36 Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji
na huyo ofisa akasema, “Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha
kunizuia nisibatizwe?”fa
37 missing
38 Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili,
Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
39 Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo
Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa
furaha.
40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri
Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea.
\fm a
\fr 8:36
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 37:
\ie Filipo akasema, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza
kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana
wa Mungu.”

\c 9

Kuongoka kwa Saulo
\r
\is (Mate. 22:6-16, 26:12-18)
\ie

1 Wakati huo Saulo alikuwa akizidisha vitisho vikali vya kuwaua
wafuasi wa Bwana. Alikwenda kwa Kuhani Mkuu,
2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi
kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia ya
Bwana, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.

3 Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga
kutoka angani ulimwangazia pande zote.
4 Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: “Saulo, Saulo! Kwa
nini unanitesa?”
5 Naye Saulo akauliza, “Ni nani wewe Bwana?” Na ile sauti ikajibu,
“Mimi ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
6 Lakini simama sasa, uingie mjini na huko utaambiwa unachopaswa
kufanya.”
7 Wale watu waliokuwa wanasafiri pamoja na Saulo walisimama pale,
wakiwa hawana la kusema; walisikia ile sauti lakini hawakumwona mtu.
8 Saulo aliinuka, na alipofumbua macho yake hakuweza kuona chochote;
hivyo wale watu wakamwongoza kwa kumshika mkono mpaka mjini Damasko.
9 Saulo alikaa siku tatu bila kuona, na wakati huo hakula au kunywa
chochote.

10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana
akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa,
Bwana.”
11 Naye Bwana akamwambia, “Jitayarishe uende kwenye barabara
inayoitwa Barabara ya Moja kwa Moja, na katika nyumba ya Yuda umtake mtu
mmoja kutoka Tarso aitwaye Saulo. Sasa anasali;
12 na katika maono ameona mtu aitwaye Anania akiingia ndani na
kumwekea mikono ili apate kuona tena.”
13 Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia habari za mtu huyu
kutoka kwa watu wengi; nimesikia juu ya mabaya aliyowatendea watu wako
huko Yerusalemu.
14 Na amekuja hapa akiwa na mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu
kuwatia nguvuni wote wanaoomba kwa jina lako.”
15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe
chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa
watu wa Israeli.
16 Mimi mwenyewe nitamwonyesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa
ajili ya jina langu.”

17 Basi, Anania akaenda, akaingia katika hiyo nyumba. Kisha akaweka
mikono yake juu ya Saulo, akasema, “Ndugu Saulo, Bwana ambaye ndiye
Yesu mwenyewe aliyekutokea ulipokuwa njiani kuja hapa, amenituma ili
upate kuona tena na kujazwa Roho Mtakatifu.”
18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka macho ya Saulo, akaweza
kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
19 Na baada ya kula chakula, nguvu zake zikamrudia.

Saulo anahubiri huko Damasko
Saulo alikaa siku chache pamoja na wafuasi huko Damasko.
20 Mara alianza kuhubiri katika masunagogi kwamba Yesu ni Mwana wa
Mungu.
21 Watu wote waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, mtu huyu si
yuleyule aliyewaua wale waliokuwa wanaomba kwa jina hili kule
Yerusalemu? Tena alikuja hapa akiwa na madhumuni ya kuwatia nguvuni watu
hao na kuwapeleka kwa makuhani!”

22 Saulo alizidi kupata nguvu, na kwa jinsi alivyothibitisha wazi
kwamba Yesu ndiye Kristo, Wayahudi wa huko Damasko walivurugika kabisa.
23 Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi walikusanyika na kufanya
mpango wa kumwua Saulo.
24 Lakini Saulo alipata habari ya mpango huo. Usiku na mchana
walilinda milango ya kuingia mjini ili wapate kumwua.
25 Lakini wakati wa usiku wanafunzi wake walimchukua, wakamteremsha
chini ndani ya kapu kubwa kwa kupitia nafasi iliyokuwako ukutani.
\il 5
ic
\is Wakamteremsha nje ndani ya kapu (Mat 9:25)
\ie

Saulo anarudi Yerusalemu

26 Saulo alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na wale wanafunzi.
Lakini wote walimwogopa, na hawakuweza kuamini kwamba yeye amekuwa
mfuasi.
27 Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na
kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana
alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila
uoga kule Damasko.
28 Basi, Saulo alikaa pamoja nao, akatembelea Yerusalemu yote
akihubiri neno la Bwana bila hofu.
29 Pia aliongea na kubishana na Wayahudi wasemao Kigiriki, lakini
wao walijaribu kumwua.
30 Wale ndugu walipogundua jambo hilo walimchukua Saulo, wakampeleka
Kaisarea, wakamwacha aende zake Tarso.

31 Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya,
na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka
likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.

Enea anaponywa

32 Petro alipokuwa anasafirisafiri kila mahali alifika pia kwa watu
wa Mungu waliokuwa wanaishi Luda.
33 Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Enea ambaye kwa muda wa miaka
minane alikuwa amelala kitandani kwa sababu alikuwa amepooza.
34 Basi, Petro akamwambia, “Enea, Yesu Kristo anakuponya. Amka
utandike kitanda chako.” Enea akaamka mara.
35 Wakazi wote wa Luda na Saroni walimwona Enea, na wote wakamgeukia
Bwana.

Dorka anaponywa

36 Kulikuwa na mfuasi mmoja mwanamke mjini Yopa aitwaye Tabitha (kwa
Kigiriki ni Dorka, maana yake, Paa). Huyo mwanamke alikuwa akitenda mema
na kuwasaidia maskini daima.
37 Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili
wake, wakauzika katika chumba ghorofani.
38 Yopa si mbali sana na Luda; kwa hiyo wafuasi waliposikia kwamba
Petro alikuwa Luda, wakawatuma watu wawili kwake na ujumbe: “Njoo kwetu
haraka iwezekanavyo.”
39 Basi, Petro akaenda pamoja nao. Alipofika alipelekwa ghorofani
katika kile chumba. Huko wajane wengi walimzunguka Petro wakilia na
kumwonyesha makoti na nguo ambazo Dorka alikuwa akitengeneza wakati
alipokuwa hai.
40 Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha
akamgeukia yule maiti, akasema, “Tabitha, amka” Naye akafumbua macho
yake na alipomwona Petro, akaketi.
41 Petro akamsaidia kusimama, halafu akawaita wale watu wa Mungu na
wale wajane, akamkabidhi kwao akiwa mzima.
42 Habari ya tukio hili ilienea kila mahali huko Yopa, na watu wengi
wakamwamini Bwana.
43 Petro alikaa siku kadhaa huko Yopa, akiishi kwa mtu mmoja
mtengenezaji wa ngozi aitwaye Simoni.

\c 10

Petro na Kornelio

1 Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, Jemadari wa
kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu;
alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali
daima.
3 Yapata saa tisa mchana, aliona dhahiri katika maono malaika wa
Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!”
4 Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia,
“Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea
sala na sadaka zako kwa maskini.
5 Sasa, watume watu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa
jina lingine Petro.
6 Yeye yumo nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi ambaye nyumba
yake iko karibu na bahari.”
7 Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio
aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye
alikuwa mcha Mungu,
8 akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.

9 Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu
kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana
ili kusali.
10 Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa
kinatayarishwa, alipatwa na usingizi mzito akaona maono.
11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa
chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.
12 Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: wanyama
wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani.
13 Akasikia sauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!”
14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho
ni najisi au kichafu.”

15 Ile sauti ikasikika tena ikimwambia: “Usiviite najisi vitu
ambavyo Mungu amevitakasa!”
16 Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu
mbinguni.

17 Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hilo maono
alilokuwa ameliona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua
nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
18 Wakaita kwa sauti: “Je, kuna mgeni humu aitwaye Simoni Petro?”

19 Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa lile maono, na hapo Roho
akamwambia, “Sikiliza! kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.
20 Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi
niliyewatuma.”
21 Basi, Petro akateremka chini, akawaambia hao watu, “Mimi ndiye
mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”
22 Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha
Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote ametutuma. Aliambiwa
na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote
ulicho nacho cha kusema.”
23 Petro akawaalika ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule.
Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa
huko Yopa walifuatana naye.
24 Siku ya pili yake, walifika Kaisarea na huko Kornelio alikuwa
anawangojea pamoja na jamaa na marafiki aliokuwa amewaalika.
25 Petro alipokuwa anaingia, Kornelio alitoka nje kumlaki, akapiga
magoti mbele yake na kuinama chini kabisa.
26 Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni
binadamu tu.”
27 Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani
ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika.
28 Petro akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote
amekatazwa na Sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa
mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi
au mchafu.
29 Kwa sababu hiyo, mliponiita nimekuja bila kusita. Basi,
nawaulizeni: kwa nini mmeniita?”
30 Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa
alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa
mavazi yenye kun’gaa alisimama mbele yangu,
31 akasema: <Kornelio! Sala yako na sadaka zako kwa maskini
vimekubaliwa na Mungu.
32 Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina
lingine Petroi; yuko nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi karibu na
bahari.>
33 Kwa hiyo nilikutumia ujumbe bila kuchelewa, nawe umefanya vyema
kuja. Sasa, sisi tuko mbele ya Mungu, kusikiliza chochote ambacho bwana
amekuamuru kusema.”

Hotuba ya Petro

34 Hapo Petro akaanza kusema: “Sasa nimetambua kwamba hakika Mungu
hana ubaguzi.
35 Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda haki anapokelewa
naye.
36 Huu ndio ule ujumbe Mungu alioupeleka kwa watu wa Israeli,
akitangaza Habari Njema iletayo amani kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni
Bwana wa wote.
37 Ninyi mnajua jambo lililotukia katika nchi yote ya Wayahudi
kuanzia Galilaya baada ya ule ubatizo aliohubiri Yohane.
38 Mnajua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia
Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko
na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi.
39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya
Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
40 lakini Mungu alimfufua siku ya tatu, akamfanya aonekane
41 si kwa watu wote ila kwa wale Mungu aliokwisha wachagua wawe
mashahidi wake, yaani sisi tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya
kufufuka kwake kutoka wafu.
42 Alituamuru kuihubiri Habari Njema kwa watu wote na kushuhudia
kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa na Mungu awe Mwamuzi wa wazima na wafu.
43 Manabii wote waliongea juu yake kwamba kila mtu atakayemwamini
atasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake.”

Kornelio na jamaa yake wanampokea Roho Mtakatifu

44 Wakati Petro alipokuwa bado anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu
aliwashukia wote waliokuwa wanasikiliza ujumbe huo.
45 Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa
walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia zawadi ya Roho Mtakatifu watu
wa mataifa mengine pia;
46 maana waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali wakimtukuza
Mungu. Hapo Petro akasema,
47 “Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi wenyewe
tulivyompokea. Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuia wasibatizwe kwa
maji?”
48 Basi, akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Kisha
wakamwomba akae nao kwa siku chache.

\c 11

Taarifa ya Petro kwa kanisa la Yerusalemu

1 Mitume na ndugu kule Yudea walisikia kwamba watu wa mataifa mengine
pia walikuwa wamelipokea neno la Mungu.
2 Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini
waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:
3 “Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula
pamoja nao!
4 Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu
mwanzo:

5 “Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu
kama shuka kubwa likishushwa chini kutoka mbinguni likiwa limeshikwa
pembe zake nne, likawekwa kando yangu.
6 Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne,
wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
7 Kisha nikasikia sauti ikiniambia: <Petro amka, chinja, ule.>
8 Lakini mimi nikasema: <La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au
kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.>
9 Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: <Usiviite najisi vitu
ambavyo Mungu amevitakasa.>
10 Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa
juu mbinguni.
11 Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea
waliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.
12 Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita
waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa
Kornelio.
13 Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama
nyumbani mwake na kumwambia: <Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye
Simoni, kwa jina lingine Petro.
14 Yeye atakuambia maneno ambayo kwayo wewe na jamaa yako yote
mtaokolewa.>
15 Na nilipoanza tu kuongea, Roho Mtakatifu aliwashukia kama
alivyotushukia sisi pale awali.
16 Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: <Yohane alibatiza
kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.>
17 Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine zawadi
ileile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani
hata nijaribu kumpinga Mungu?”
18 Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema,
“Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na
uzima!”

Kanisa la Antiokia

19 Kutokana na mateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa, waumini
walitawanyika. Wengine walikwenda mpaka Foinike, Kupro na Antiokia
wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu.
20 Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda
Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine
wakiwahubiria ile Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
21 Bwana aliwasaidia na idadi kubwa ya watu iliamini na kumgeukia
Bwana.
22 Habari ya jambo hilo ikasikika kwa lile kanisa la Yerusalemu.
Hivyo wakamtuma Barnaba aende Antiokia.
23 Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu,
alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
24 Barnaba alikuwa mtu mwema na mwenye kujaa Roho Mtakatifu na
imani. Kundi kubwa la watu lilivutwa kwa Bwana.
25 Kisha, Barnaba alikwenda Tarso kumtafuta Saulo
26 Alipompata, alimleta Antiokia. Nao wote wawili walikaa na lile
kanisa kwa mwaka wote mzima wakifundisha kundi kubwa la watu. Huko
Antiokia, ndiko, kwa mara ya kwanza, wafuasi waliitwa Wakristo.
\il 5
ic
\is Antiokia (Mat 11:19)
\ie

27 Wakati huohuo, manabii kadhaa walikuja Antiokia kutoka
Yerusalemu.
28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho
akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo
ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).
29 Wale wanafunzi waliamua kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake
apeleke chochote ili kuwasaidia wale ndugu waliokuwa wanaishi Yudea.
30 Basi, wakafanya hivyo na kupeleka mchango wao kwa wazee wa kanisa
kwa mikono ya Barnaba na Saulo.

\c 12

Kanisa linadhulumiwa zaidi

1 Karibu wakati huohuo, mfalme Herode alianza kuwatesa baadhi ya
Wakristo.
2 Alimwua kwa upanga Yakobo ndugu yake Yohane.
3 Alipoona kuwa kitendo hiki kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea,
akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya Mikate Isiyotiwa
chachu.)
4 Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini
ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia
kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
5 Basi, Petro alipokuwa gerezani, kanisa lilikuwa linamwombea kwa
Mungu kwa moyo.

Malaika anamtoa Petro gerezani

6 Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani,
Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo
miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
7 Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza
kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa akisema, “Amka upesi!” Mara
ile minyororo ikaanguka kutoka katika mikono yake.
8 Malaika akamwambia, “Jifunge mshipi wako, vaa viatu vyako.”
Akafanya hivyo. Kisha huyo malaika akamwambia, “Vaa koti lako,
unifuate.”
9 Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo
malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
10 Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika
kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia
wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na
mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.

11 Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua
kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa kutoka katika
mkono wa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli
waliyotazamia.”

12 Alipotambua hivyo alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa
Maria mama yake Yohane aitwaye Marko. Humo watu wengi walikuwa
wamekusanyika wakisali.
13 Petro alibisha mlango wa nje na mtumishi mmoja msichana aitwaye
Roda, akaenda mlangoni kuitikia.
14 Huyo msichana aliitambua sauti ya Petro akafurahi mno, hata
badala ya kuufungua ule mlango, akakimbilia ndani na kuwaambia kwamba
Petro alikuwa amesimama nje mlangoni.
15 Wakamwambia yule msichana, “Una wazimu!” Lakini yeye
akasisitiza kwamba ilikuwa kweli. Nao wakamwambia, “Huyo ni malaika
wake.”
16 Wakati huo Petro alikuwa anaendelea kupiga hodi. Mwishowe
walifungua mlango, wakamwona, wakashangaa.
17 Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana
alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa
Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.

18 Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu
yaliyokuwa yamempata Petro.
19 Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo
aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko
Yudea akaenda Kaisarea ambako alikaa.

Kifo cha Herode

20 Herode alikasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Lakini wao
walimpelekea wajumbe. Nao wakafaulu kwanza kumpata Blasto awe upande
wao. Blasto alikuwa msimamizi mkuu wa ikulu ya mfalme. Kisha,
wakamwendea Herode wakamwomba kuwe na amani, kwa maana nchi yao
ilitegemea nchi ya mfalme kwa chakula.

21 Siku moja iliyochaguliwa, Herode akiwa amevaa mavazi rasmi na
kuketi katika kiti cha kifalme aliwahutubia watu.
22 Wale watu walimpigia kelele za shangwe wakisema, “Hii ni sauti
ya mungu, si ya mtu.”
23 Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu
hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
24 Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua.

25 Baada ya Barnaba na Saulo kutekeleza shughuli zao, walitoka tena
Yerusalemu wakamchukua Yohane aitwaye pia Marko.

\c 13

Barnaba na Saulo wanateuliwa na kutumwa

1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa
manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia
Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na
mfalme Herode, na Saulo.
2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho
Mtakatifu alisema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi
niliyowaitia.”
3 Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono,
wakawaacha waende zao.

Mitume wanahubiri kule Kupro

4 Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu,
walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha
Kupro.
5 Walipofika Salami walihubiri neno la Mungu katika masunagogi ya
Kiyahudi. Yohane (Marko) alikuwa msaidizi wao.

6 Walitembea toka upande mmoja wa kisiwa mpaka Pafo upande wa pili,
na huko walimkuta mchawi mmoja Myahudi aitwaye Baryesu ambaye
alijisingizia kuwa nabii.
7 Huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mkuu wa kile kisiwa, ambaye
alikuwa mtu mwelewa sana. Sergio Paulo aliwaita Barnaba na Saulo ili
asikie neno la Mungu.
8 Lakini huyo mchawi Elima (kama alivyokuwa anaitwa kwa Kigiriki),
alijaribu kuwapinga ili kumzuia huyo mkuu wa kisiwa asije akaigeukia
imani ya Kikristo.
9 Basi, Saulo ambaye aliitwa pia Paulo, akiwa amejaa Roho Mtakatifu,
alimkodolea macho huyo mchawi,
10 akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni
mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli;
hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.
11 Sasa, mkono wa Bwana utakuadhibu: utakuwa kipofu na hutaweza
kuuona mwanga wa jua kwa kitambo.” Mara kila kitu kikawa kama ukungu na
giza kwake, akaanza kwenda huku na huku akitafuta mtu wa kumshika mkono
amwongoze.
12 Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa muumini;
akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.

Barnaba na Paulo mjini Antiokia Pisidia

13 Kutoka Pafo, Paulo na wenzake walipanda meli wakaenda hadi Perga
katika Pamfulia; lakini Yohane (Marko) aliwaacha, akarudi Yerusalemu.
14 Lakini wao waliendelea na safari toka Pisga hadi mjini Antiokia
Pisidia. Siku ya Sabato waliingia ndani ya Sunagogi, wakakaa.

15 Baada ya masomo katika kitabu cha Sheria ya Mose na katika
maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu:
“Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”
16 Basi, Paulo alisimama, akatoa ishara kwa mkono, akaanza kuongea:
“Wananchi wa Israeli na wengine wote mnaomcha Mungu, sikilizeni!
17 Mungu wa taifa hili la Israeli aliwateua babu zetu na kuwafanya
wawe taifa kubwa walipokuwa ugenini kule Misri. Mungu aliwatoa huko kwa
uwezo wake mkuu.
18 Aliwavumilia kwa muda wa miaka arobaini kule jangwani.
19 Aliyaangamiza mataifa ya nchi ya Kanaani akawapa hao watu wake
ile nchi kuwa mali yao.
20 Miaka mia nne na hamsini ilipita, halafu akawapatia waamuzi
wawaongoze mpaka wakati wa nabii Samweli.
21 Hapo wakapendelea kuwa na mfalme, na Mungu akawapa Saulo, mtoto
wa Kishi wa kabila la Benyamini, awe mfalme wao kwa muda wa miaka
arobaini.
22 Baada ya kumwondoa Saulo, Mungu alimteua Daudi kuwa mfalme wao.
Mungu alionyesha kibali chake kwake akisema: <Nimemwona Daudi mtoto wa
Yese; ni mtu anayepatana na moyo wangu; mtu ambaye atatimiza yale yote
ninayotaka kuyatenda.>
23 Kutokana na ukoo wake mtu huyu, Mungu, kama alivyoahidi,
amewapelekea watu wa Israeli Mwokozi, ndiye Yesu.
24 Kabla ya kuja kwake Yesu, Yohane alimtangulia akiwahubiria watu
wote wa Israeli kwamba ni lazima watubu na kubatizwa.
25 Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: <Mnadhani
mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na
mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.>
\fr 13:22
\f taz Zab 89:20

26 “Ndugu, ninyi mlio watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wengine wote
mnaomcha Mungu! Ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu.
27 Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye
kuwa Mwokozi. Wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila
Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu
Yesu adhabu ya kifo.
28 Ingawa hawakumpata na hatia inayostahili auawe, walimwomba Pilato
amhukumu auawe.
29 Na baada ya kutekeleza yote yaliyokuwa yameandikwa kumhusu yeye,
walimshusha kutoka msalabani, wakamweka kaburini.
30 Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu.
31 Naye, kwa siku nyingi aliwatokea wale waliofuatana naye kutoka
Galilaya mpaka Yerusalemu. Hao ndio walio sasa mashahidi wake kwa watu
wa Israeli.
32-33 Sisi tumekuja hapa kuwaleteeni Habari Njema: jambo lile Mungu
alilowaahidia babu zetu amelitimiza sasa kwa ajili yetu sisi tulio
wajukuu wao kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Kama ilivyoandikwa katika
zaburi ya pili:

<Wewe ni Mwanangu,
mimi leo nimekuwa baba yako.>
\fr 13:33
\f taz Zab 2:7
\fr 13:35
\f taz Zab 16:10
\m
34 Na juu ya kumfufua kutoka wafu, asipate tena kurudi huko na
kuoza, Mungu alisema hivi:

<Nitakupa baraka takatifu na za kweli nilizomwahidia Daudi.>
\m
35 Naam, na katika sehemu nyingine za zaburi asema:

<Hutamwacha Mtakatifu wako aoze.>
\m
36 Sasa, Daudi mwenyewe alitimiza mapenzi ya Mungu wakati wake;
kisha akafa na kuzikwa karibu na wazee wake, na mwili wake ukaoza.
37 Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka wafu hakupata kuoza.
38-39 Jueni wazi, ndugu zangu, kwamba ujumbe kuhusu kusamehewa
dhambi unahubiriwa kwenu kwa njia ya Yesu Kristo; na ya kwamba kila
mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo
halingewezekana kwa njia ya Sheria ya Mose.
40 Jihadharini basi, msije mkapatwa na yale yaliyosemwa na manabii:

41 <Sikilizeni enyi wenye madharau,

shangaeni mpotee!
Kwa maana kitu ninachofanya sasa, nyakati zenu,
ni kitu ambacho hamtakiamini hata kama mtu akiwaelezeni.”>

42 Paulo na Barnaba walipokuwa wanatoka katika ile sunagogi, wale
watu waliwaalika waje tena siku ya Sabato iliyofuata, waongee zaidi juu
ya mambo hayo.
43 Mkutano huo ulipomalizika, Wayahudi wengi na watu wa mataifa
mengine waliokuwa wameongokea dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na
Barnaba. Hao mitume waliongea nao, wakawatia moyo waendelee kuishi
wakitegemea neema ya Mungu.

44 Siku ya Sabato iliyofuata, karibu kila mtu katika ule mji alikuja
kusikiliza neno la Bwana.
45 Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu,
wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.
46 Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi,
wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni ninyi kwanza;
lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uzima wa milele, basi,
tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.
47 Maana Bwana alituagiza hivi:

<Nimekuteua wewe uwe mwanga kwa mataifa,
uwe njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.”>

48 Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi,
wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uzima
wa milele, wakawa waumini.

49 Neno la Bwana likaenea kila mahali katika sehemu ile.
50 Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake wa tabaka ya juu wa
mataifa mengine ambao walikuwa wacha Mungu, na wanaume maarufu wa mji
huo. Wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba, wakawafukuza kutoka katika eneo
lao.
51 Basi, mitume wakayakung’uta mavumbi yaliyokuwa katika miguu yao
kama onyo, kisha wakaenda Ikonio.
52 Lakini hao wafuasi walikuwa wamejaa furaha na Roho Mtakatifu.

\c 14

Paulo na Barnaba huko Ikonio

1 Kule Ikonio, mambo yalikuwa kama yalivyokuwa kule Antiokia; Paulo
na Barnaba walikwenda katika sunagogi la Wayahudi wakaongea kwa uhodari
hata Wayahudi wengi na Wagiriki wakawa waumini.
2 Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwa waumini walichochea na
kutia chuki katika mioyo ya watu wa mataifa mengine ili wawapinge hao
ndugu.
3 Paulo na Barnaba waliendelea kukaa huko kwa muda mrefu. Waliongea
kwa uhodari juu ya Bwana, naye Bwana akathibitisha ukweli wa ujumbe
walioutoa juu ya neema yake, kwa kuwawezesha kutenda miujiza na maajabu.
4 Watu wa mji huo waligawanyika: wengine waliwaunga mkono Wayahudi,
na wengine walikuwa upande wa mitume.

5 Mwishowe, baadhi ya watu wa mataifa mengine na Wayahudi,
wakishirikiana na wakuu wao, waliazimu kuwatendea vibaya hao mitume na
kuwapiga mawe.
6 Mitume walipogundua jambo hilo, walikimbilia Lustra na Derbe, miji
ya Lukaonia, na katika sehemu za jirani,
7 wakawa wanahubiri Habari Njema huko.

Paulo na Barnaba huko Lustra na Derbe

8 Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa amelemaa miguu
tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe.
9 Mtu huyo alikuwa anamsikiliza Paulo alipokuwa anahubiri. Paulo
alimtazama kwa makini, na alipoona kuwa alikuwa na imani ya kuweza
kuponywa,
10 akasema kwa sauti kubwa, “Simama wima kwa miguu yako!” Huyo mtu
aliyelemaa akainuka ghafla, akaanza kutembea.
11 Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele
kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”
12 Barnaba akaitwa Zeu, na Paulo, kwa vile yeye ndiye aliyekuwa
anaongea, akaitwa Herme.
13 Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali
na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa
watu akataka kuwatambikia mitume.
\fr 14:15
\f taz Zab 146:6

14 Barnaba na Paulo walipopata habari hiyo waliyararua mavazi yao na
kukimbilia katika lile kundi la watu wakisema kwa sauti kubwa:
15 “Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama
ninyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi
sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi,
bahari na vyote vilivyomo.
16 Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda.
17 Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema
anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati
wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
18 Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu
wasiwatambikie.

19 Lakini Wayahudi kadhaa walikuja kutoka Antiokia na Ikonio,
wakawafanya watu wajiunge nao, wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi
nje ya mji wakidhani amekwisha kufa.
20 Lakini waumini walipokusanyika na kumzunguka, aliamka akarudi
mjini. Kesho yake, yeye pamoja na Barnaba walikwenda Derbe.

Paulo na Barnaba wanarudi mjini Antiokia Siria

21 Baada ya Paulo na Barnabas kuhubiri Habari Njema huko Derbe na
kupata wafuasi wengi, walifunga safari kwenda Antiokia kwa kupitia
Lustra na Ikonio.
22 Waliwaimarisha waumini wa miji hiyo na kuwatia moyo wabaki imara
katika imani. Wakawaambia, “Ni lazima sisi sote tupitie katika taabu
nyingi ili tuingie katika ufalme wa Mungu.”
23 Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada
ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye
walikuwa wanamwamini.

24 Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia, walifika Pamfulia.
25 Baada ya kuhubiri ule ujumbe huko Perga, walikwenda Atalia.
26 Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo
awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya
kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.

27 Walipofika huko Antiokia walifanya mkutano wa kanisa la mahali
hapo, wakawapa taarifa juu ya mambo Mungu aliyofanya pamoja nao, na
jinsi alivyowafungulia mlango watu wa mataifa mengine mlango wa kuingia
katika imani.
28 Wakakaa pamoja na wale waumini kwa muda mrefu.

\c 15

Mkutano maalumu wa kanisa Yerusalemu

1 Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza
kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na
mapokeo ya Sheria ya Mose, hamtaweza kuokolewa.”
2 Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na
Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini
kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume
na wazee kuhusu jambo hilo.

3 Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na
Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu.
Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
4 Walipofika Yerusalemu walikaribishwa na kanisa, mitume na wazee;
nao wakawapa taarifa juu ya yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
5 Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo
walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na
kufundishwa kuifuata Sheria ya Mose.”

6 Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalum wa kuchunguza jambo
hilo.
7 Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama, akasema, “Ndugu
zangu, ninyi mnafahamu kwamba hapo awali Mungu alipenda kunichagua mimi
miongoni mwenu niihubiri Habari Njema, ili watu wa mataifa wapate
kusikia na kuamini.
8 Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba
amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
9 Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao
kwa imani.
10 Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini
mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
11 Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao,
tunaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu.”

12 Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo
wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati
ya watu wa mataifa mengine.
13 Walipomaliza kuongea, Yakobo alianza kusema: “Ndugu zangu,
nisikilizeni!
14 Simoni ameeleza jinsi Mungu hapo awali alivyojishughulisha na
watu wa mataifa mengine, akachagua baadhi yao wawe watu wake.
15 Jambo hili ni sawa kabisa na maneno ya manabii, kama Maandiko
Matakatifu yasemavyo:

16 <Baada ya mambo haya nitarudi.

Nitaijenga tena ile nyumba ya Daudi iliyoanguka;
nitayatengeneza magofu yake na kuijenga tena.

17 Hapo watu wengine wote,

watu wa mataifa yote niliowaita wawe wangu,
watamtafuta Bwana.

18 Ndivyo asemavyo Bwana,

aliyefanya jambo hili lijulikane tangu kale.>

19 “Kwa hiyo, uamuzi wangu ni huu: tusiwataabishe watu wa mataifa
wanomgeukia Mungu.
20 Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa
najisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu; wajiepushe na uasherati; wasile
mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu.
21 Kwa maana kwa muda mrefu maneno ya Mose yamekuwa yakihubiriwa
katika kila mji na kusomwa katika masunagogi yote kila siku ya Sabato.”
\il 5
ic
\is Sanamu za miungu (Mat. 15:20)
\ie

Barua kwa waumini wasio Wayahudi

22 Mitume, wazee na kanisa lote waliamua kuwachagua watu fulani
miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Basi,
wakamchagua Yuda aitwaye pia Barsaba, na Sila ambao wote walikuwa
wanajulikana zaidi kati ya ndugu.
23 Wakawapa barua hii:
\in “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni ninyi ndugu wa
mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
24 Tumesikia kwamba watu wengine kutoka huku kwetu waliwavurugeni
kwa maneno yao, wakaitia mioyo yenu katika wasiwasi. Lakini wamefanya
hivyo bila ya idhini yoyote kutoka kwetu.
25 Hivyo, tumeamua kwa pamoja kuwachagua watu kadhaa na kuwatuma
kwenu pamoja na wapenzi wetu Barnaba na Paulo,
26 ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu
Yesu Kristo.
27 Kwa hiyo, tunawatuma Yuda na Sila kwenu; hawa watawaambieni wao
wenyewe haya tuliyoandika.
28 Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi
ya mambo haya muhimu:
29 Msile vyakula vilivyotambikiwa sanamu; msinywe damu; msile nyama
ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema
kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”

30 Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita
mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
31 Walipoisoma hiyo barua, maneno yake yaliwatia moyo, wakafurahi
sana.
32 Yuda na Sila, ambao nao walikuwa manabii, walizungumza na hao
ndugu kwa muda mrefu wakiwatia moyo na kuwaimarisha.
33 Baada ya kukaa huko kwa muda fulani, ndugu wa Antiokia waliwaaga
wakiwatakia amani, kisha wakarudi kwa wale waliokuwa wamewatuma.fb
\fm b
\fr 15:33
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 34:
\ie Lakini Sila aliamua kubaki.

34 missing
35 Paulo na Barnaba walibaki huko Antiokia kwa muda; wakafundisha na
kuhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.

Paulo na Barnaba wanaachana

36 Baada ya siku kadhaa, Paulo alimwambia Barnaba, “Turudi
tukawatembelee wale ndugu katika kila mji tulikolihubiri neno la Bwana
tukajionee jinsi wanavyoendelea.”
37 Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko.
38 Lakini Paulo hakupendelea kumchukua Marko, ambaye awali aliwaacha
kule Pamfulia na kukataa kushiriki katika kazi yao.
39 Basi kukatokea ubishi mkali kati yao, na wakaachana. Barnaba
akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro.
40 Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo
kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.
41 Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia akiyaimarisha
makanisa.

\c 16

Timotheo anajiunga na Paulo na Sila

1 Paulo alifika Derbe na Lustra, ambako aliishi mfuasi mmoja aitwaye
Timotheo. Mama yake ambaye pia alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini
baba yake alikuwa Mgiriki.
2 Timotheo alikuwa na sifa kubwa kati ya wale ndugu wa Lustra na
Ikonio.
3 Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo
alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu
hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.
4 Walipokuwa wanapita katika ile miji waliwapa watu yale maagizo
yaliyotolewa na mitume na wazee kule Yerusalemu, wakawaambia
wayazingatie.
5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya
waumini ikaongezeka kila siku.

Paulo anaona maono kule Troa

6 Walipitia sehemu za Frugia na Galatia kwani Roho Mtakatifu
hakuwaruhusu kuhubiri huo ujumbe mkoani Asia.
7 Walipofika kwenye mipaka ya Musia, walijaribu kuingia mkoani
Bithunia, lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu.
8 Basi, walipitia Musia, wakaenda moja kwa moja mpaka Troa.
9 Usiku huo, Paulo aliona ono ambalo alimwona mtu mmoja wa Makedonia
amesimama pale na kumwomba: “Vuka, uje Makedonia ukatusaidie.”
10 Mara baada ya Paulo kuona ono hilo, tulijitayarisha kwenda
Makedonia bila kukawia, tukiwa na hakika kwamba Mungu ametuita
tuwapelekee Habari Njema.

Kuongoka kwa Ludia

11 Kutoka Troa, tulisafiri kwa meli moja kwa moja mpaka Samothrake,
na kesho yake tukatia nanga Neapoli.
12 Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya
Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku
kadhaa.
13 Siku ya Sabato tulitoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto ambapo
tulidhani ya kuwa ni mahali pa kusali. Tuliketi, tukaongea na wanawake
waliokusanyika mahali hapo.
14 Miongoni mwa wale waliotusikiliza alikuwa mwanamke mmoja mcha
Mungu aitwaye Ludia mwenyeji wa Thuatira, ambaye alikuwa mfanyabiashara
ya nguo za kitani za rangi ya zambarau. Bwana aliufungua moyo wake hata
akayapokea yale maneno Paulo aliyokuwa anasema.
15 Baada ya huyo mama pamoja na jamaa yake kubatizwa, alitualika
akisema, “Kama kweli mmeona kwamba mimi namwamini Bwana, karibuni
nyumbani kwangu mkakae.” Akatuhimiza twende.

Paulo na Sila wanatiwa nguvuni

16 Siku moja, tulipokuwa tunakwenda mahali pa kusali, msichana mmoja
aliyekuwa na pepo mwenye uwezo wa kuagua alikutana nasi. Msichana huyo
alikuwa anawapatia matajiri wake fedha nyingi kwa uaguzi wake.
17 Basi, huyo msichana alimfuata Paulo na sisi, akipiga kelele na
kusema, “Hawa watu ni watumishi wa Mungu Mkuu. Wanawatangazieni njia ya
wokovu.”
18 Akawa anafanya hivyo kwa siku nyingi hata siku moja Paulo
alikasirika, akamgeukia na kumwambia huyo pepo, “Nakuamuru kwa jina la
Yesu Kristo, mtoke huyu!” Mara huyo pepo akamtoka.

19 Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata
mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka
hadharani, mbele ya wakuu.
20 Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na
wanafanya fujo katika mji wetu.
21 Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Roma haturuhusiwi
kuzikubali wala kuzifuata.”
22 Kundi la watu likajiunga nao, likawashambulia. Wale mahakimu
wakawatatulia Paulo na Sila mavazi yao, wakaamuru wapigwe viboko.
23 Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza
akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.
24 Kutokana na maagizo hayo, huyo askari aliwaweka katika chumba cha
ndani kabisa cha gereza na kuifunga miguu yao kwenye nguzo.

25 Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na
kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa
wanasikiliza.
26 Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa
misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo
iliyowafunga hao wafungwa ikaachana.
27 Askari wa gereza alipoamka na kuiona milango ya gereza
imefunguliwa, alidhani kwamba wafungwa wote walikuwa wametoroka na hivyo
akauchomoa upanga wake, akataka kujiua.
28 Lakini Paulo akaita kwa sauti kubwa: “Usijidhuru mwenyewe kwa
maana sisi sote tuko hapa.”

29 Baada ya kumwita mtu alete taa, huyo askari wa gereza alikimbilia
ndani, akajitupa mbele ya miguu ya Paulo na Sila huku akitetemeka kwa
hofu.
30 Halafu aliwaongoza nje, akawauliza, “Waheshimiwa, nifanye nini
nipate kuokoka?”
31 Wao wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa pamoja na
jamaa yako yote.”
32 Basi, wakamhubiria neno la Bwana yeye pamoja na jamaa yake.
33 Yule askari aliwachukua saa ileile ya usiku akawasafisha majeraha
yao, kisha yeye na jamaa yake wakabatizwa papo hapo.
34 Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula.
Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa
wanamwamini Mungu.

35 Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema,
“Wafungueni wale watu.”
36 Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: “Mahakimu wametuma
ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani.”
37 Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa,
walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia
ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao
wenyewe waje hapa watufungulie.”
38 Hao maofisa waliwapasha habari mahakimu juu ya jambo hilo, nao
waliposikia kwamba Paulo na Sila walikuwa raia wa Roma, waliogopa.
39 Hivyo, walikwenda kuwataka radhi na baada ya kuwatoa ndani
waliwaomba watoke katika mji ule.
40 Paulo na Sila walitoka gerezani, wakaenda nyumbani kwa Ludia.
Huko walionana na ndugu waumini na baada ya kuwatia moyo wakaondoka.

Fujo Thesalonika kutokana na mahubiri
\c 17

1 Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonika
ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi.
2 Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake akajadiliana nao
Sabato tatu mfululizo, akatumia Maandiko Matakatifu.
3 Aliyaeleza na kuonyesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka
kutoka wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye
Kristo.”
4 Baadhi yao walikubali wakajiunga na Paulo na Sila. Kadhalika,
idadi kubwa ya Wagiriki waliomcha Mungu pamoja na wanawake wengi wa
tabaka la juu, walijiunga nao.

5 Lakini Wayahudi wakaona wivu; wakawakodi wafidhuli sokoni,
wakafanya kikundi na kuzusha fujo mjini kote. Wakaivamia nyumba ya
Yasoni wakitumaini kuwapata humo Paulo na Sila ili wawalete hadharani.
6 Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu
wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: “Watu hawa wamekuwa
wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini.
7 Yasoni amewakaribisha nyumbani kwake. Wote wanafanya kinyume cha
amri ya Kaisari wakisema eti <Kuna mfalme mwingine aitwaye Yesu.”>
8 Kwa maneno hayo waliwatia wasiwasi wakuu wa mji na kundi la watu.
9 Wakawafanya Yasoni na wenzake watoe dhamana, kisha wakawaacha
waende zao.

Katika Berea

10 Usiku, wale ndugu waliwahimiza Paulo na Sila waende Berea. Mara
tu walipofika huko, walikwenda katika sunagogi la Wayahudi.
11 Watu wa huko walikuwa wasikivu zaidi kuliko wale wa Thesalonika.
Waliupokea ule ujumbe kwa hamu kubwa, wakawa wanayachunguza Maandiko
Matakatifu kila siku, ili kuona kama yale waliyosema Paulo na Sila
yalikuwa kweli.
12 Wengi wao waliamini na pia wanawake wa Kigiriki wa tabaka la juu
na wanaume pia.

13 Lakini, Wayahudi wa Thesalonika walipogundua kwamba Paulo alikuwa
anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya
fujo na kuchochea makundi ya watu.
14 Wale ndugu wakamsindikiza haraka aende pwani lakini Sila na
Timotheo walibaki Berea.
15 Wale ndugu waliomsindikiza Paulo walikwenda pamoja naye mpaka
Athene. Kisha, wakarudi pamoja na maagizo kutoka kwa Paulo kwamba Sila
na Timotheo wamfuate upesi iwezekanavyo.

Paulo anaongea na watu wa Athene

16 Paulo alipokuwa anawasubiri Sila na Timotheo huko Athene, moyo
wake ulighadhibika sana alipoona jinsi mji huo ulivyokuwa umejaa sanamu
za miungu.
17 Alijadiliana na Wayahudi na watu wengine waliomcha Mungu katika
sunagogi; na kila siku alikuwa na majadiliano sokoni pamoja na wowote
wale waliojitokeza.
18 Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye.
Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa
Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema,
“Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”
19 Hivyo walimchukua Paulo, wakampeleka Areopago, wakasema,
“Tunataka kujua jambo hili jipya ulilokuwa unazungumzia.
20 Vitu vingine tulivyosikia kwa masikio yetu vinaonekana kuwa
viroja kwetu. Tungependa kujua mambo haya yana maana gani.”
21 Wananchi wa Athene na wakazi wengine wa huko walikuwa wanatumia
wakati wao wote kuhadithiana na kusikiliza habari mpyampya.
\il 5
ic
\is Kilima cha Areopago mjini Athene (Mat. 17:15-22)
\ie

22 Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema,
“Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba ninyi, kwa vyovyote, ni watu wa
dini sana.
23 Sababu yenyewe ni kwamba katika pitapita yangu niliangalia sanamu
zenu za ibada nikakuta madhabahu moja ambayo imeandikwa: <Kwa ajili ya
Mungu yule Asiyejulikana.> Basi, huyo mnayemwabudu bila kujua, ndiye
ninayemhubiri kwenu.
24 Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu
na nchi; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.
25 Wala hatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote
kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha
kupumua na anawapa kila kitu.
26 Kutokana na mtu mmoja aliumba mataifa yote na kuyawezesha kuishi
duniani kote. Aliamua na kupanga kabla kabisa lini na wapi mataifa hayo
yangeishi.
27 Alifanya hivyo, ili mataifa hayo yapate kumfuata, na kama vile
kwa kupapasapapasa, yapate kumfikia. Hata hivyo lakini, Mungu hayuko
mbali na kila mmoja wetu.
28 Kama alivyosema mtu mmoja:

<Ndani yake yeye sisi tunaishi,
tunajimudu, na tuko!>
\m Ni kama washairi wenu wengine walivyosema:

<Sisi ni watoto wake.>
\m
29 Ikiwa basi, sisi ni watoto wa Mungu, haifai kumfikiria Mungu kuwa
kama dhahabu, fedha au hata jiwe lililochongwa na kutiwa nakshi na
binadamu.
30 Mungu alifanya kama kwamba haoni nyakati zile watu walipokuwa
wajinga. Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahali watubu.
31 Kwa maana amekwisha weka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa
haki kwa njia ya mtu mmoja aliyemteua. Mungu amewathibitishia wote jambo
hili kwa kumfufua mtu huyo kutoka wafu!”

32 Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu,
wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, “Tunataka
kukusikia tena juu ya jambo hili!”
33 Hivyo, Paulo aliwaacha, akatoka barazani.
34 Lakini watu kadhaa waliandamana naye, wakawa waumini. Miongoni
mwao walikuwa Dionisio wa Areopago, mwanamke mmoja aitwaye Damari na
wengineo.

Paulo kule Korintho
\c 18

1 Baada ya hayo, Paulo aliondoka Athene, akaenda Korintho.
2 Huko Korintho, alimkuta Myahudi mmoja aitwaye Akula, mzaliwa wa
Ponto. Akula pamoja na mkewe aitwaye Priskila, walikuwa wamerudi kutoka
Italia siku hizohizo kwa sababu Kaisari Klaudio alikuwa ameamuru
Wayahudi wote waondoke Roma. Paulo alikwenda kuwaona,
3 na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama alivyokuwa
yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
4 Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu
kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

5 Baada ya Sila na Timotheo kuwasili kutoka Makedonia, Paulo alianza
kutumia wakati wake wote kwa ajili ya kuhubiri, akawathibitishia
Wayahudi kwamba Yesu ndiye Kristo.
6 Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung’uta mavazi yake mbele
yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote
juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.”
7 Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu
aitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi.
8 Lakini Krispo, mkuu wa sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na
jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na
kubatizwa.

9 Siku moja usiku, Bwana alimwambia Paulo katika maono: “Usiogope,
endelea kuhubiri tu bila kufa moyo,
10 maana mimi niko pamoja nawe. Hakuna mtu atakayejaribu kukudhuru
maana hapa mjini pana watu wengi walio upande wangu.”
11 Basi, Paulo alikaa huko akifundisha neno la Mungu kati yao kwa
muda wa mwaka mmoja na nusu.

12 Lakini wakati Galio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Akaya, Wayahudi
walimvamia Paulo kwa pamoja na kumpeleka mahakamani.
13 Wakasema, “Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu
wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na Sheria.”
14 Kabla tu Paulo hajaanza kusema, Galio aliwaambia Wayahudi,
“Sikilizeni enyi Wayahudi! Kama kweli jambo hili lingekuwa juu ya
uhalifu au uovu ningekuwa tayari kuwasikilizeni.
15 Lakini kama ni shauri la ubishi kuhusu maneno na majina ya Sheria
yenu, amueni ninyi wenyewe. Mimi sitaki kuwa hakimu wa mambo haya!”
16 Basi, akawafukuza kutoka mahakamani.
17 Nao wote wakamkamata Sosthene ambaye alikuwa kiongozi wa
sunagogi, wakampiga palepale mbele ya mahakama. Lakini Galio hakujali
kitendo hicho hata kidogo.

Paulo anarudi tena Antiokia

18 Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi.
Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula.
Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa
ameweka.
19 Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda
katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.
20 Walimwomba akae nao muda mrefu zaidi, lakini hakupenda.
21 Bali alipokuwa anaondoka, alisema, “Mungu akipenda nitakuja
kwenu tena.” Akaondoka Efeso kwa meli.

22 Meli ilitia nanga Kaisarea, naye Paulo akaenda Yerusalemu
kulisalimia lile kanisa, kisha akaenda Antiokia.
23 Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia
sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.

Apolo anahubiri Efeso na Korintho

24 Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika
Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa
Maandiko Matakatifu.
25 Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa
motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu. Akafundisha kwa usahihi ingawa
alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
26 Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya
sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo Njia ya Mungu kwa usahihi
zaidi.
27 Apolo alipoamua kwenda Akaya, wale ndugu walimtia moyo kwa
kuwaandikia wafuasi kule Akaya wampokee. Alipofika huko, aliweza kwa
msaada wa neema ya Mungu, kuwasaidia sana wale ndugu waliopata kuwa
waumini;
28 kwa maana aliendelea kwa uhodari kuwashinda Wayahudi hadharani
akithibitisha kwa Maandiko Matakatifu kuwa Yesu ni Kristo.

Paulo anahubiri kule Efeso
\c 19

1 Wakati Apolo alipokuwa Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara,
akafika Efeso ambako aliwakuta wanafunzi kadhaa.
2 Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?”
Nao wakamjibu, “La! Hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu
hatujasikia.”
3 Naye akasema, “Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?” Wakamjibu,
“Ubatizo wa Yohane.”
4 Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha
kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye
alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
5 Baada ya kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6 Basi, Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia,
wakaanza kusema lugha mbalimbali na kutangaza ujumbe wa Mungu.
7 Wote jumla, walikuwa watu wapatao kumi na wawili.

8 Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi,
akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya Ufalme wa Mungu.
9 Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza
kuongea vibaya hadharani juu ya Njia ya Bwana. Hapo Paulo alivunja
uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza
nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.
10 Aliendelea kufanya hivyo kwa muda wa miaka miwili hata wakazi
wote wa Asia, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, wakaweza kusikia neno
la Bwana.

Watoto wa Skewa wanajaribu kupunga pepo wabaya

11 Mungu alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo.
12 Watu walikuwa wakichukua leso na nguo nyingine za kazi ambazo
Paulo alikuwa amezitumia, wakazipeleka kwa wagonjwa, nao wakaponywa
magonjwa yao; na wale waliokuwa na pepo wabaya wakatokwa na pepo hao.
13 Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya, walisafiri huko na
huko, wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa
wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: “Ninawaamuru kwa jina la
Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
14 Watoto saba wa Skewa, Kuhani Mkuu wa Kiyahudi, walikuwa miongoni
mwa hao waliokuwa wanafanya hivyo.
15 Lakini pepo mbaya aliwajibu, “Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia
Paulo, lakini ninyi ni nani?”
16 Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo,
akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba
wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
17 Kila mtu huko Efeso, Myahudi na asiye Myahudi, alisikia juu ya
tukio hilo. Wote waliingiwa na hofu, wakalitukuza jina la Bwana Yesu.
18 Waumini wengi walijitokeza wakakiri hadharani mambo waliyokuwa
wametenda.
19 Wengine waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali,
walikusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya
vitabu hivyo, wakaona yafikia vipande vya fedha elfu hamsini.
20 Kwa namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu
zaidi.

Ghasia Efeso

21 Baada ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia
Makedonia na Akaya. Alisema, “Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona
Roma pia.”
22 Hivyo, aliwatuma wawili wa wasaidizi wake, Timotheo na Erasto,
wamtangulie kwenda Makedonia, naye akabaki kwa muda huko Asia.

23 Wakati huo ndipo kulipotokea ghasia kubwa huko Efeso kwa sababu
ya hiyo Njia ya Bwana.
24 Kulikuwa na mfua fedha mmoja aitwaye Demetrio, ambaye alikuwa na
kazi ya kutengeneza sanamu za nyumba ya mungu wa kike aitwaye Artemi.
Shughuli hiyo iliwapatia mafundi faida kubwa.
25 Demetrio aliwakusanya hao wafanyakazi pamoja na wengine waliokuwa
na kazi kama hiyo, akawaambia, “Wananchi, mnafahamu kwamba kipato chetu
kinatokana na biashara hii.
26 Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya,
si tu hapa Efeso, ila pia kote katika Asia. Yeye amewashawishi na
kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu ile iliyotengenezwa na watu si
miungu hata kidogo.
27 Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si
hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi
kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia
yote inamwabudu, zitakwisha.”
\il 5
ic
\is Sanamu ya mungu Artemi (Mate. 19:24,35)
\ie

28 Waliposikia hayo, waliwaka hasira, wakaanza kupiga kelele: “Mkuu
ni Artemi, wa Efeso!”
29 Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa
Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka
kwenye ukumbi wa michezo.
30 Paulo mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale
waumini walimzuia.
31 Maofisa wengine wa huo mkoa wa Asia, waliokuwa rafiki zake,
walimtumia Paulo ujumbe wakimsihi asijihatarishe kwa kwenda kwenye
ukumbi wa michezo.
32 Wakati huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine
lile, mpaka hata ule mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya
kukutana kwao.
33 Kwa vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya
watu katika ule umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria
watu kwa mkono akitaka kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja
walipiga kelele: “Mkuu ni Artemi wa Efeso!” Wakaendelea kupayukapayuka
hivyo kwa muda wa saa mbili.
35 Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia,
“Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi
wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka
mbinguni.
36 Hakuna anayeweza kukana mambo haya. Hivyo basi, tulieni; msifanye
chochote bila hadhari.
37 Mmewaita watu hawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumba ya mungu
wala kumtukana mungu wetu wa kike.
38 Kama, basi Demetrio na wafanyakazi wake wana mashtaka yao kuhusu
watu hawa, yapo mahakama na wakuu wa mikoa; wanaweza kushtakiana huko.
39 Kama mna matatizo mengine, yapelekeni katika kikao halali.
40 Kwa maana tungaliweza kushtakiwa kwa kusababisha ghasia kutokana
na vituko vya leo. Ghasia hii haina msingi halali na hatungeweza kutoa
sababu za kuridhisha za ghasia hiyo.”
41 Baada ya kusema hayo aliuvunja mkutano.

Paulo anakwenda tena Makedonia na Ugiriki
\c 20

1 Ile ghasia ya Efeso ilipokwisha tulia Paulo aliwaita pamoja wale
waumini, akawatia moyo. Kisha akawaaga, akasafiri kwenda Makedonia.
2 Alipitia sehemu za nchi zile akiwatia watu moyo kwa maneno mengi.
Halafu akafika Ugiriki.
3 ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda
Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya;
hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.
4 Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea, aliandamana naye; pia
Aristarko na Sekundo kutoka Thesalonika, Gayo kutoka Derbe, Timotheo,
Tukiko na Trofimo wa mkoa wa Asia.
5 Hao walitutangulia na kutungojea kule Troa.
6 Sisi, baada ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, tulipanda meli
kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa
kwa muda wa juma moja.

Kukutana na waumini wa Troa kwa mara ya mwisho

7 Jumamosi jioni, tulikutana ili kumega mkate. Kwa vile Paulo
alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliwahutubia watu na kuendelea
kuongea nao hadi usiku wa manane.
8 Katika chumba tulimokuwa, ghorofani, kulikuwa na taa nyingi
zinawaka.
9 Kijana mmoja aitwaye Eutuko alikuwa ameketi dirishani wakati Paulo
alipokuwa anaendelea kuhutubu. Eutuko alianza kusinzia kidogokidogo na
hatimaye usingizi ukambana, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu.
Wakamwokota amekwisha kufa.
10 Lakini Paulo alishuka chini, akainama, akamkumbatia na kusema,
“Msiwe na wasiwasi maana kuna uhai bado ndani yake.”
11 Kisha akapanda tena ghorofani, akamega mkate, akala. Aliendelea
kuhubiri kwa muda mrefu hadi alfajiri, halafu akaondoka.
12 Wale watu walimchukua yule kijana nyumbani akiwa mzima kabisa,
wakapata kitulizo kikubwa.

Safari kutoka Troa kwenda Mileto

13 Sisi tulipanda meli tukatangulia kwenda Aso ambako tungemchukua
Paulo. Ndivyo alivyopanga; maana alitaka kufika huko kwa kupitia nchi
kavu.
14 Basi, alitukuta kule Aso, tukampandisha melini, tukaenda
Mitulene.
15 Kutoka huko tulisafiri tukafika Kio kesho yake. Siku ya pili,
tulitia nanga Samo na kesho yake tukafika Mileto.
16 Paulo alikuwa amekusudia kuendelea na safari kwa meli bila
kupitia Efeso ili asikawie zaidi huko Asia. Alikuwa na haraka ya kufika
Yerusalemu kwa sikukuu ya Pentekoste kama ingewezekana.

Paulo anawaaga wazee wa Efeso

17 Kutoka Mileto Paulo alituma ujumbe kwa wazee wa Efeso wakutane
naye.
18 Walipofika kwake aliwaambia, “Mnajua jinsi nilivyotumia wakati
wote pamoja nanyi tangu siku ile ya kwanza nilipofika Asia.
19 Mnajua jinsi nilivyomtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, kwa
machozi na matatizo yaliyonipata kutokana na mipango ya hila ya
Wayahudi.
20 Mnajua kwamba sikusita hata kidogo kuwahubiria hadharani na
nyumbani mwenu na kuwafundisha chochote ambacho kingewasaidieni.
21 Niliwaonya wote–Wayahudi kadhalika na watu wa mataifa, wamgeukie
Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu.
22 Sasa, sikilizeni! Mimi, nikiwa ninamtii Roho, nakwenda Yerusalemu
bila kufahamu yatakayonipata huko.
23 Ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu ananithibitishia katika
kila mji kwamba vifungo na mateso ndivyo vinavyoningojea.
24 Lakini, siuthamini uhai wangu kuwa ni kitu sana kwangu. Nataka tu
nikamilishe ule utume wangu na kumaliza ile kazi aliyonipa Bwana Yesu
niifanye, yaani nitangaze Habari Njema ya neema ya Mungu.

25 “Nimekuwa nikienda huko na huko kati yenu nikiuhubiri Ufalme wa
Mungu. Sasa lakini, najua hakuna hata mmoja wenu atakayeniona tena.
26 Hivyo, leo hii ninawathibitishieni rasmi kwamba ikijatokea
akapotea mmoja wenu, mimi sina lawama yoyote.
27 Kwa maana sikusita hata kidogo kuwatangazieni azimio lote la
Mungu.
28 Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu
amewaweka ninyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo
amejipatia kwa damu ya Mwanae.
29 Nafahamu vizuri sana kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu
wakali watawavamieni, na hawatakuwa na huruma kwa kundi hilo.
30 Hata kutoka miongoni mwenu watatokea watu ambao watasema mambo ya
uongo ili kuwapotosha watu na kuwafanya wawafuate wao tu.
31 Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu,
usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi.

32 “Na sasa basi, ninawaweka ninyi chini ya ulinzi wa Mungu na
ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga ninyi na kuwawezesha
mzipate zile baraka alizowawekea watu wake.
33 Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za
mtu yeyote.
34 Mnajua ninyi wenyewe kwamba nimefanya kazi kwa mikono yangu
mwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na ya wenzangu.
35 Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili
hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu
mwenyewe: <Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.”>

36 Baada ya kusema hayo, Paulo alipiga magoti pamoja nao wote,
akasali.
37 Wote walikuwa wanalia; wakamwaga kwa kumkumbatia na kumbusu.
38 Jambo lililowahuzunisha zaidi lilikuwa neno alilosema kwamba
hawangemwona tena. Basi, wakamsindikiza hadi melini.

\c 21

Safari ya Paulo kwenda Yerusalemu

1 Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka
Kosi. Kesho yake tulifika Rodo, na kutoka huko tulikwenda Patara.
2 Huko, tulikuta meli iliyokuwa inakwenda Foinike, hivyo tulipanda,
tukasafiri.
3 Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia
upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro
ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
4 Tulikuta waumini huko, tukakaa pamoja nao kwa muda wa juma moja.
Waumini hao wakawa waongea kwa nguvu ya Roho, wakamwambia Paulo asiende
Yerusalemu.
5 Lakini muda wetu ulipokwisha tuliondoka. Wote pamoja na wanawake
na watoto wao walitusindikiza mpaka nje ya mji. Tulipofika pwani, sote
tulipiga magoti tukasali.
6 Kisha tuliagana; sisi tukapanda meli nao wakarudi makwao.

7 Sisi tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai
ambapo tuliwasalimu ndugu zetu, tukakaa nao siku moja.
8 Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisarea tulikwenda
nyumbani kwa mhubiri Filipo. Yeye alikuwa mmoja wa wale saba
waliochaguliwa kule Yerusalemu.
9 Alikuwa na binti watatu ambao walikuwa na kipaji cha unabii.
10 Baada ya kukaa huko siku kadhaa, nabii mmoja aitwaye Agabo
alifika kutoka Yudea.
11 Alitujia, akachukua mkanda wa Paulo, akajifunga mikono na miguu,
akasema “Roho Mtakatifu asema hivi: <Wayahudi kule Yerusalemu
watamfunga namna hii mtu mwenye ukanda na kumtia mikononi mwa watu wa
mataifa.”>

12 Tuliposikia hayo, sisi na wale watu wengine waliokuwa hapo
tulimsihi Paulo asiende Yerusalemu.
13 Lakini yeye alijibu, “Mnataka kufanya nini? Mnataka kuvunja moyo
wangu kwa machozi? Niko tayari siyo tu kutiwa ndani kule Yerusalemu, ila
hata kufa kwa ajili ya Bwana Yesu.”
14 Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: “Mapenzi ya
Bwana yafanyike”

15 Baada ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea
na safari kwenda Yerusalemu.
16 Wengine kati ya wale wafuasi wa Kaisarea walienda pamoja nasi,
wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye
kwa muda. Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa muumini
kwa siku nyingi.

Paulo anakwenda kumwamkia Yakobo

17 Tulipofika Yerusalemu, ndugu waumini walitupokea vizuri sana.
18 Kesho yake Paulo alikwenda pamoja nasi kumwamkia Yakobo, na wazee
wote wa kanisa walikuwako pia.
19 Baada ya kuwasalimu, Paulo aliwapa taarifa kamili kuhusu yote
Mungu aliyokuwa ametenda kati ya mataifa kwa njia ya utumishi wake.
20 Waliposikia hayo, walimtukuza Mungu. Kisha wakamwambia Paulo,
“Ndugu, unaweza kuona kwamba kuna maelfu ya Wayahudi ambao sasa
wamekuwa waumini na wote hao wanashika kwa makini Sheria ya Mose.
21 Wamepata habari zako kwamba umekuwa ukiwafundisha Wayahudi
wanaoishi kati ya mataifa mengine kuwa wasiijali Sheria ya Mose,
wasiwatahiri watoto wao na kwamba wasizifuate mila za Wayahudi.
22 Sasa, mambo yatakuwaje? Ni dhahiri kuwa watapata habari kwamba
umekwisha wasili hapa.
23 Basi, fanya kama tunavyokushauri. Tunao hapa watu wanne ambao
wameweka nadhiri.
24 Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na gharama
zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua
kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba
wewe binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya Sheria za Mose.
25 Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa waumini,
tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: wasile chochote
kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama
aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”
26 Basi, kesho yake Paulo aliwachukua wale watu akafanya ibada ya
kujitakasa pamoja nao. Kisha akaingia Hekaluni kutoa taarifa kuhusu
mwisho wa siku za kujitakasa na kuhusu dhabihu itakayotolewa kwa ajili
ya kila mmoja wao.

Paulo anatiwa nguvuni ndani ya Hekalu

27 Wakati siku hizo saba zilipokaribia kuisha, Wayahudi waliokuwa
wametoka katika mkoa wa Asia walimwona Paulo Hekaluni. Wakachochea
hasira kati ya kundi lote la watu, wakamtia nguvuni
28 wakipiga kelele: “Wananchi wa Israeli, msaada, msaada! Huyu
ndiye yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo yanayopinga watu
wa Israeli, yanayopinga Sheria ya Mose na mahali hapa patakatifu. Hata
sasa amewaingiza watu wa mataifa mengine Hekaluni na kupatia najisi
mahali hapa patakatifu.”
29 Sababu ya kusema hivyo ni kwamba walikuwa wamemwona Trofimo
mwenyeji, wa Efeso, akiwa pamoja na Paulo mjini, wakadhani kwamba Paulo
alikuwa amemwingiza Hekaluni.

30 Mji wote ulienea ghasia; watu wakaja kutoka pande zote,
wakamkamata Paulo, wakamburuta, wakamtoa nje ya Hekalu na papo hapo
milango ya Hekalu ikafungwa.
31 Walikuwa tayari kumuua, lakini habari zilimfikia mkuu wa jeshi la
Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.
32 Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari, akalikabili
lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha
kumpiga Paulo.
33 Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na kuamuru
afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, “Ni mtu gani huyu, na
amefanya nini?”
34 Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki
na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi
hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo
ndani ya ngome.
35 Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika kumbeba kwa
sababu ya fujo za watu.
36 Kwa maana kundi kubwa la watu walimfuata wakipiga kelele,
“Muulie mbali!”
\il 5
ic
\is Ngome (Mate. 21:34,37)
\ie

Paulo anajitetea

37 Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba mkuu wa
jeshi akisema, “Naweza kukwambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akamjibu,
“Je unajua Kigiriki?
38 Kwani wewe si yule Mmisri ambaye hivi majuzi alianzisha uasi na
kuwaongoza majahili elfu nne hadi jangwani?”
39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika
Kilikia; mimi ni raia wa mji maarufu. Tafadhali, niruhusu niongee na
watu.
40 Yule mkuu wa jeshi akamruhusu. Hivyo Paulo alisimama juu ya
ngazi, akawapungia mkono wale watu na walipokaa kimya, akaanza kuongea
nao kwa Kiebrania.

\c 22

1 “Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni sasa nikijitetea mbele
yenu!”
2 Waliposikia akiongea nao kwa Kiebrania wakazidi kukaa kimya zaidi
kuliko hapo awali. Naye Paulo akaendelea kusema,
3 “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini
nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli.
Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti Sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa
moyo wote kwa Mungu kama ninyi wenyewe mlivyo hivi leo.
4 Niliwatesa hata kuwaua wale watu waliofuata Njia hii. Niliwatia
nguvuni wanaume kwa wanawake na kuwafunga gerezani.
5 Kuhani Mkuu na baraza lote la wazee wanaweza kushuhudia jambo
hilo. Kutoka kwao nilipokea barua walioandikiwa wale ndugu Wayahudi
waliokuwa huko Damasko. Nilikwenda Damasko ili niwatie nguvuni watu hao
na kuwaleta wamefungwa mpaka Yerusalemu ili waadhibiwe.

Paulo anaongea juu ya kuongoka kwake
\r
\is (Mate. 9:1-19; 26:12-18)
\ie

6 “Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita
mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande
zote.
7 Hapo nilianguka chini, nikasikia sauti ikiniambia: <Saulo, Saulo!
Kwa nini unanitesa?>
8 Nami nikauliza: <Nani wewe, Bwana?> Naye akaniambia: <Mimi ni Yesu
wa Nazareti ambaye wewe unamtesa.>
9 Wale wenzangu waliuona ule mwanga lakini hawakusikia sauti ya yule
aliyeongea nami.
10 Basi, mimi nikauliza: <Nifanye nini Bwana?> Naye Bwana
akaniambia: <Simama, nenda Damasko na huko utaambiwa yote ambayo
umepangiwa kufanya.>
11 Kutokana na ule mwanga mkali sikuweza kuona na hivyo iliwabidi
wale wenzangu kuniongoza kwa kunishika mkono mpaka nikafika Damasko.

12 “Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu,
mwenye kuitii Sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi
waliokuwa wanaishi Damasko.
13 Yeye alikuja kuniona, akasimama karibu nami, akasema: <Ndugu
Saulo! Ona tena.> Papo hapo nikaona tena, nikamwangalia.
14 Halafu Anania akasema: <Mungu wa babu zetu amekuchagua upate
kujua matakwa yake na kumwona yule mtumishi wake mwadilifu na kumsikia
yeye mwenyewe akiongea.
15 Kwa maana utamshuhudia kwa watu wote ukiwaambia yale uliyoyaona
na kuyasikia.
16 Sasa basi, ya nini kukawia zaidi? Simama ubatizwe na uondolewe
dhambi zako kwa kuliungama jina lake.>

Wito wa Paulo kuwahubiria watu wa mataifa

17 “Basi, nilirudi Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali Hekaluni,
niliona maono.
18 Nilimwona Bwana akiniambia: <Haraka! Ondoka Yerusalemu upesi kwa
maana watu wa hapa binadamu hawataukubali ushuhuda wako juu yangu.>
19 Nami nikamjibu: <Bwana, wao wanajua wazi kwamba mimi ni yule
aliyekuwa anapitapita katika masunagogi na kuwatia nguvuni na kuwapiga
wale waliokuwa wanakuamini.
20 Na kwamba wakati shahidi wako Stefano alipouawa, mimi binafsi
nilikuwako pale nikakubaliana na kitendo hicho na kuyalinda makoti ya
wale waliokuwa wanamuua.>
21 Naye Bwana akaniambia: <Nenda; ninakutuma mbali kwa mataifa
mengine.”>

22 Mpaka hapa, wale watu walikuwa wanamsikiza, lakini aliposema
maneno haya, walianza kusema kwa sauti kubwa, “Mwondoe duniani! Mtu wa
namna hiyo hastahili kuishi.”
23 Waliendelea kupayukapayuka huku wakitikisa makoti yao na kurusha
vumbi angani.
24 Mkuu wa jeshi aliwaamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya
ngome, akawaambia wamchape viboko ili wapate kujua kisa cha Wayahudi
kumpigia kelele.
25 Lakini walipokwisha mfunga ili wamchape viboko, Paulo alimwuliza
jemadari mmoja aliyesimama hapo, “Je, ni halali kwenu kumpiga viboko
raia wa Roma kabla hajahukumiwa?”
26 Yule jemadari aliposikia hayo, alimpasha habari mkuu wa jeshi
akisema, “Unataka kufanya nini? Mtu huyu ni raia wa Roma!”
27 Basi, mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamwambia, “Niambie; je,
wewe ni raia wa Roma?” Paulo akamjibu, “Naam.”
28 Mkuu wa jeshi akasema, “Mimi nami nimekuwa raia wa Roma kwa
kulipa gharama kubwa.” Paulo akasema, “Lakini mimi ni raia wa Roma kwa
kuzaliwa.”
29 Wale watu ambao walikuwa tayari kumchunguza Paulo walitoweka
mara. Hata yule mkuu wa jeshi aliogopa alipojua kwamba Paulo ni raia wa
Roma na kwamba alikuwa amekwisha mfunga minyororo.

Paulo mahakamani

30 Kesho yake, mkuu wa jeshi alitaka kujua mashtaka kamili ambayo
Wayahudi walikuwa wamemwekea Paulo. Hivyo, alimfungua Paulo minyororo,
akaamuru makuhani wakuu na Baraza lote wafanye kikao. Kisha alimleta
Paulo, akamsimamisha mbele ya Baraza.

\c 23

1 Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema,
“Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele
ya Mungu.”
2 Hapo Kuhani Mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa wamesimama karibu
na Paulo wampige kofi mdomoni.
3 Basi, Paulo akamwambia, “Mungu mwenyewe atakupiga kofi wewe uliye
kama ukuta uliopakwa chokaa! Unawezaje kukaa hapo ili unihukumu kisheria
na huku wewe mwenyewe unaivunja Sheria kwa kuamuru nipigwe?”
4 Watu waliokuwa wamesimama pale wakamwambia Paulo, “Unamtukana
Kuhani Mkuu wa Mungu!”
5 Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kama yeye ni Kuhani Mkuu.
Maana Maandiko yasema hivi: <Usiseme vibaya juu ya mtawala wa watu
wako.”>

6 Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza
wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaaza sauti
yake mbele ya Baraza: “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa
Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu
watafufuka.”
7 Baada ya kusema hivyo, mzozo mkali ulitokea kati ya Mafarisayo na
Masadukayo na mkutano ukagawanyika sehemu mbili.
8 Kisa chenyewe kilikuwa hiki: Masadukayo hushikilia kwamba wafu
hawafufuki, hakuna malaika, na roho nazo hazipo. Lakini Mafarisayo
husadiki hayo yote matatu.
9 Kelele ziliongezeka na baadhi ya walimu wa Sheria wa kikundi cha
Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni
chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au
malaika ameongea naye.”

10 Mzozo ulizidi kuwa mwingi hata mkuu wa jeshi akaogopa kwamba
Paulo angeraruliwa vipandevipande. Kwa hiyo, aliwaamuru askari wake
kuingia kati ya lile kundi, wamtoe Paulo na kumrudisha ndani ya ngome.

11 Usiku uliofuata, Bwana alisimama karibu na Paulo, akamwambia,
“Jipe moyo! Umenishuhudia katika Yerusalemu, utafanya vivyo hivyo mjini
Roma.”

Wayahudi wanafanya mpango kumuua Paulo

12 Kulipokucha, Wayahudi walifanya kikao cha faragha. Wakala kiapo:
“Hatutakula wala kunywa mpaka tutakapokuwa tumekwisha muua Paulo.”
13 Watu zaidi ya arobaini ndio waliokula njama kufanya hivyo.
14 Basi, walikwenda kwa makuhani wakuu na wazee, wakasema, “Sisi
tumeapa kwamba hatutaonja chochote kwa vinywa vyetu mpaka hapo
tutakapokuwa tumemuua Paulo.
15 Sasa basi, ninyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi
ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili
zaidi juu yake. Tuko tayari kumuua hata kabla hajafika karibu.”

16 Lakini mtoto wa kiume wa dada yake Paulo alisikia juu ya mpango
huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
17 Hapo Paulo akamwita mmoja wa askari, akamwambia, “Mchukue kijana
huyu kwa mkuu wa jeshi; ana kitu cha kumwambia.”
18 Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa
jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana
huyu kwako kwa maana ana jambo la kukwambia.”
19 Mkuu wa jeshi alimshika huyo kijana mkono, akampeleka mahali pa
faragha, akamwuliza, “Una nini cha kuniambia?”
20 Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo
Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili
zaidi juu yake.
21 Lakini wewe usikubali kwa maana kuna watu zaidi ya arobaini walio
tayari kumvamia. Wameapa kutokula wala kunywa mpaka watakapokuwa
wamemuua. Sasa wako tayari, wanangojea tu uamuzi wako.”
22 Mkuu wa jeshi alimwacha aende zake akimwonya asimwambie mtu
yeyote kwamba amemletea habari hizo.

Paulo anapelekwa kwa mkuu wa mkoa

23 Basi, mkuu wa jeshi aliwaita askari wawili akawaambia, “Wekeni
tayari askari mia mbili, wapanda farasi sabini na askari mia mbili wa
mikuki, waende Kaisarea; muwe tayari kuondoka kabla ya saa tatu leo
usiku.
24 Wekeni farasi kadhaa kwa ajili ya Paulo; mfikisheni salama kwa
Felisi, mkuu wa mkoa.”
25 Halafu mkuu huyo wa jeshi akaandika barua hivi:

26 “Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu
wa mkoa. Salamu!

27 “Wayahudi walimkamata mtu huyu na karibu wangemuua kama
nisingalifahamishwa kwamba yeye ni raia wa Roma na hivyo nikaenda pamoja
na askari nikamwokoa.
28 Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha
mashtaka yao.
29 Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu
kadha wa kadha za Sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote
kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
30 Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za
kumuua, niliamua kumleta kwako. Nikamwambia washtaki wake walete
mashtaka yao mbele yako.”

31 Basi, hao askari walimchukua Paulo kama walivyoamriwa;
wakampeleka usiku uleule mpaka Antipatri.
32 Kesho yake askari wa miguu walirudi ngomeni, wakawaacha wale
askari wapanda farasi waendelee na safari pamoja na Paulo.
33 Walipofika Kaisarea walimpa mkuu wa mkoa ile barua na kumweka
Paulo chini ya mamlaka yake.
34 Felisi alipoisoma hiyo barua aliwauliza Paulo ametoka mkoa gani.
Alipofahamishwa kwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia,
35 akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako
kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa
Herode.

\c 24

Wayahudi wanamshtaki Paulo

1 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania aliwasili Kaisarea pamoja na
wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea yule
mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
2 Paulo aliitwa na Tertulo akafungua mashtaka hivi:
“Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na
marekebisho ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
3 Tunalipokea jambo hili kwa furaha daima na kutoa shukrani nyingi
kwako kila mahali.
4 Lakini, bila kupoteza wakati wako zaidi, tunakusihi kwa wema wako,
usikilize taarifa yetu fupi.
5 Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye huanzisha ghasia
kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa kile chama
cha Wanazareti.
6 Tena alijaribu kulikufuru Hekalu nasi tukamtia nguvuni. Kama
ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki
kwayo.”fc
7 missing
8 missing
9 Nao Wayahudi waliunga mkono mashtaka hayo wakisema kwamba hayo
yote yalikuwa kweli.
\fm c
\fr 24:6b-8a
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 5b-8a:
\ie Tulitaka kumhukumu kufuatana na Sheria yetu. 7 Lakini Lusia, mkuu wa
jeshi, aliingilia kati, akamchukua kwa nguvu kutoka mikononi mwetu. 8
Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.

Paulo anajitetea mbele ya Felisi

10 Basi, mkuu wa mkoa alimwashiria Paulo aseme. Naye Paulo akasema,
“Nafurahi kujitetea mbele yako nikijua kwamba umekuwa hakimu wa taifa
hili kwa miaka mingi.
11 Unaweza kujihakikishia kwamba si zaidi ya siku kumi na mbili tu
zimepita tangu nilipokwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Wayahudi hawakunikuta nikijadiliana na mtu yeyote. Hawakunikuta
nikichochea watu Hekaluni wala katika masunagogi yao, wala mahali
pengine popote katika mji huo.
13 Wala hawawezi kuthibitisha mashtaka waliyotoa juu yangu.
14 Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu na wazee
wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha
uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na
manabii.
15 Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo, kwamba watu,
wema na wabaya, watafufuka.
16 Kwa hiyo ninajitahidi daima kuwa na dhamiri njema mbele ya Mungu
na mbele ya watu.

17 “Baada ya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudi Yerusalemu ili
kuwapelekea wananchi wenzangu msaada na kutoa dhabihu.
18 Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta Hekaluni,
nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi la
watu wala ghasia.
19 Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia; hao ndio
wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana chochote
cha kusema dhidi yangu.
20 Au, waache hawa walio hapa waseme kosa waliloliona kwangu wakati
niliposimama mbele ya Baraza lao kuu,
21 isipokuwa tu maneno haya niliyosema niliposimama mbele yao:
<Mnanihukumu leo hii kwa sababu ya kushikilia kwamba wafu
watafufuliwa!”>

22 Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo Njia
vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi
hiyo wakati Luisa, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”
23 Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini, lakini awe
na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.

Paulo mbele ya Felisi na Drusila

24 Baada ya siku chache, Felisi alifika pamoja na mkewe Drusila
ambaye alikuwa Myahudi. Aliamuru Paulo aletwe, akamsikiliza akiongea juu
ya kumwamini Yesu Kristo.
25 Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu ya
kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa,
akasema, “Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata
nafasi.”
26 Wakati huohuo alikuwa anatumaini kwamba Paulo angempa fedha. Kwa
sababu hii alimwita Paulo mara kwa mara na kuzungumza naye.

27 Baada ya miaka miwili, Porkio Festo alichukua nafasi ya Felisi,
akawa mkuu wa Mkoa. Kwa kuwa alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, Felisi
alimwacha Paulo kizuizini.

\c 25

Paulo anakata rufani kwa Kaisari

1 Siku tatu baada ya kufika mkoani, Festo alitoka Kaisarea, akaenda
Yerusalemu.
2 Makuhani wakuu pamoja na viongozi wa Wayahudi walimpa habari
kuhusu mashtaka yaliyokuwa yanamkabili Paulo. Walimsihi Festo
3 awafanyie fadhili kwa kumleta Paulo Yerusalemu; walikuwa wamekula
njama wamuue akiwa njiani.
4 Lakini Festo alijibu, “Paulo atabaki kizuizini kule Kaisarea na
mimi nitakwenda huko karibuni.
5 Waacheni viongozi wenu waende huko pamoja nami wakatoe mashtaka
yao juu yake kama amefanya chochote kiovu.”

6 Festo alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi hivi, kisha akarudi
Kaisarea. Kesho yake alikwenda barazani, akaamuru Paulo aletwe ndani.
7 Wakati Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu
walimzunguka wakaanza kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo
hawakuweza kuthibitisha.
8 Kwa kujitetea, Paulo alisema, “Mimi sikufanya kosa lolote kuhusu
Sheria ya Wayahudi, wala kuhusu Hekalu, wala kumhusu Kaisari.”
9 Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi na hivyo akamwuliza
Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu na huko ukahukumiwe mbele yangu
kuhusu mashtaka haya?”
10 Paulo akajibu, “Nasimama mbele ya mahakama ya Kaisari na papa
hapa ndipo ninapopaswa kupewa hukumu. Kama unavyojua vizuri,
sikuwatendea Wayahudi ubaya wowote.
11 Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo,
siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka
waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa
Kaisari!”

12 Basi, baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia
Paulo, “Umekata rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari.”

Festo anamweleza Agripa habari za Paulo

13 Siku chache baadaye, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisarea
ili kutoa heshima zao kwa Festo.
14 Walikuwa huko siku kadhaa naye Festo akamweleza mfalme kesi ya
Paulo: “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Felisi alimwacha kizuizini.
15 Nilipokwenda Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi
walimshtaki na kuniomba nimhukumu.
16 Lakini mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu
aadhibiwe kabla mshtakiwa hajakutana na washtaki wake ana kwa ana na
kupewa fursa ya kujitetea kuhusu hayo mashtaka.
17 Basi, walipofika hapa sikukawia, ila nilifanya kikao mahakamani
kesho yake, nikaamuru mtu huyo aletwe.
18 Washtaki wake walisimama lakini hawakutoa mashtaka maovu kama
nilivyokuwa ninatazamia.
19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao
na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo
anashikilia kwamba yu hai.
20 Sikujua la kufanya kuhusu shauri hilo. Basi, nilimwuliza Paulo
kama angependa kwenda mahakamani kule Yerusalemu kwa ajili ya mashtaka
hayo.
21 Lakini Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka
uamuzi wa shauri hilo ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae
kizuizini mpaka nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.”
22 Basi Agripa akamwambia Festo, “Ningependa kumsikia mtu huyu mimi
mwenyewe.” Festo akamwambia, “Utamsikia kesho.”

Paulo mbele ya Agripa na Bernike

23 Hivyo, kesho yake, Agripa na Bernike walifika kwa shangwe katika
ukumbi wa mkutano wakiwa wameandamana na wakuu wa majeshi na viongozi wa
mji. Festo aliamuru Paulo aletwe ndani,
24 Kisha akasema, “Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi!
Hapa mbele yenu yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule
Yerusalemu walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
25 Lakini mimi sikuona kuwa alikuwa ametenda chochote kibaya hata
astahili kupewa adhabu ya kifo. Lakini, kwa vile Paulo mwenyewe alikata
rufani kwa Kaisari, niliamua kumpeleka.
26 Kwa upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia
Kaisari juu yake. Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako
mfalme Agripa, ili baada ya kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
27 Kwa maana nadhani itakuwa kichekesho kumpeleka mfungwa bila
kutaja wazi mashtaka yanayomkabili.”

\c 26

Paulo anajitetea mbele ya Agripa

1 Basi, Agripa akamwambia Paulo, “Unaruhusiwa kujitetea.” Hapo
Paulo alinyosha mkono wake akajitetea hivi:
2 “Mfalme Agripa, ninajiona mwenye bahati leo kujitetea mbele yako
kuhusu yale mashtaka yote ambayo Wayahudi walikuwa wamesema juu yangu.
3 Hasa kwa vile wewe mwenyewe ni mtaalamu wa desturi za Wayahudi na
migogoro yao, ninakuomba basi unisikilize kwa uvumilivu.

4 “Wayahudi wanajua habari za maisha yangu tangu utoto, jinsi
nilivyoishi tangu mwanzo kati ya taifa langu huko Yerusalemu.
5 Wananifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia, kama
wakipenda, kwamba tangu mwanzo niliishi kama mmoja wa kikundi chenye
siasa kali zaidi katika dini yetu, yaani kikundi cha Mafarisayo.
6 Na sasa niko hapa nihukumiwe kwa sababu ninaitumainia ile ahadi
ambayo Mungu aliwaahidia babu zetu.
7 Ahadi hiyo ndiyo ileile inayotumainiwa na makabila kumi na mawili
ya taifa letu, wakimtumikia Mungu kwa dhati mchana na usiku. Mheshimiwa
mfalme, Wayahudi wananishtaki kwa sababu ya tumaini hilo!
8 Kwa nini ninyi mnaona shida sana kuamini kwamba Mungu huwafufua
wafu?
9 Kwa kweli mimi mwenyewe niliamini kwamba ni wajibu wangu kufanya
mambo mengi kulipinga jina la Yesu wa Nazareti.
10 Mambo hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Mimi binafsi,
nikiwa nimepewa mamlaka kutoka kwa makuhani wakuu, nilipata kuwatia
gerezani wengi wa watu wa Mungu. Nao walipohukumiwa kuuawa, nilipiga
kura ya kukubali.
11 Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote
nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata
nikawasaka mpaka miji ya mbali.

Paulo anaeleza alivyoongoka
\r
\is (Mate. 9:1-19; 22:6-16)
\ie

12 “Kwa mujibu huohuo, nilikwenda Damasko wakati mmoja, nikiwa na
mamlaka na maagizo kutoka kwa makuhani wakuu.
13 Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona
mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi
na wale wasafiri wenzangu.
14 Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa
Kiebrania: <Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda
anayepiga teke fimbo ya bwana wake.>
15 Mimi nikauliza: <Ni nani wewe Bwana?> Naye Bwana akajibu: <Mimi
ni Yesu ambaye wewe unamtesa.
16 Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi
kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo
na yale ambayo bado nitakuonyesha.
17 Nitakuokoa na watu wa Israeli na watu wa mataifa mengine ambao
mimi ninakutuma kwao.
18 Utayafumbua macho yao na kuwawezesha watoke gizani na kuingia
katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukie Mungu; ili
kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya
wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu.>

Paulo anaongea juu ya utumishi wake

19 “Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuwa mkaidi kwa maono hilo la
mbinguni.
20 Ila nilianza kuhubiri kwanza kwa watu wa Damasko, halafu kwa wale
wa Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine.
Niliwahimiza wamgeukie Mungu na kuonyesha kwa vitendo kwamba
wamebadilisha mioyo yao.
21 Kwa sababu hiyo, Wayahudi walinikamata nikiwa Hekaluni,
wakajaribu kuniua.
22 Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama
imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale
ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;
23 yaani ilimpasa Kristo ateseke na kuwa wa kwanza kufufuka kutoka
wafu, ili atangaze kwamba mwanga wa ukombozi unawaangazia sasa watu
wote, Wayahudi na pia watu wa mataifa mengine.”

24 Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa
sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia
wazimu!”
25 Lakini Paulo akasema, “Sina wazimu mheshimiwa Festo: Ninachosema
ni ukweli mtupu.
26 Wewe Mfalme unayafahamu mambo haya, kwa hiyo ninaweza kuongea
bila uoga mbele yako. Sina mashaka kwamba matukio hayo yanajulikana
kwako maana jambo hili halikutendeka mafichoni.
27 Mfalme Agripa, je, una imani na manabii? Najua kwamba unaamini.”
28 Agripa akamjibu Paulo, “Kidogo tu utanifanya Mkristo!”
29 Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu,
si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi,
lakini bila hii minyororo.”

30 Hapo mfalme Agripa, mkuu wa mkoa, Bernike na wale wote waliokuwa
pamoja nao, walisimama.
31 Walipokwisha ondoka, waliambiana, “Mtu huyu hakufanya chochote
kinachostahili adhabu ya kifo au kifungo.”
32 Naye Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kufunguliwa
kama asingalikuwa amekata rufani kwa Kaisari.”

\c 27

Paulo anasafiri kwenda Roma

1 Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na
wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi
katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”
2 Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari
kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa
Makedonia kutoka Thesalonika, alikuwa pamoja nasi.
3 Kesho yake tulitia nanga katika bandari ya Sidoni. Yulio
alimtendea Paulo vizuri kwa kumruhusu awaone rafiki zake na kupata
mahitaji yake.
4 Kutoka huko tuliendelea na safari, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa
unavuma kwa kasi kutujia kwa mbele, tulipitia upande wa kisiwa cha Kupro
ambapo upepo haukuwa mwingi.
5 Halafu tulivuka bahari ya Kilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura,
mji wa Lukia.
6 Hapo yule ofisa alikuta meli moja ya Aleksandria iliyokuwa
inakwenda Italia, na hivyo akatupandisha ndani.

7 Kwa muda wa siku nyingi tulisafiri polepole, na kwa shida tulifika
karibu na Nido. Kwa sababu upepo ulikuwa bado unatupinga, tuliendelea
mbele moja kwa moja tukapitia upande wa Krete karibu na rasi Salmone
ambapo upepo haukuwa mwingi.
8 Tulipita kando yake polepole tukafika mahali paitwapo “Bandari
Nzuri”, karibu na mji wa Lasea.

9 Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa
imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo
aliwapa onyo:
10 “Waheshimiwa, nahisi kwamba safari hii itakuwa ya shida na
hasara nyingi si kwa shehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu.”
11 Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni ya nahodha na ya
mwenye meli kuliko yale aliyosema Paulo.
12 Kwa kuwa bandari hiyo haikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wa
baridi, wengi walipendelea kuendelea na safari, ikiwezekana mpaka
Foinike. Foinike ni bandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibi na
kaskazini-magharibi; na huko wangeweza kukaa wakati wa baridi.

Dhoruba kali baharini

13 Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani
wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang’oa nanga, wakaiendesha meli karibu
sana na pwani ya Krete.
14 Lakini haukupita muda, upepo mkali uitwao “Upepo wa Kaskazi”
ulianza kuvuma kutoka kisiwani.
15 Upepo uliipiga ile meli, na kwa kuwa hatukuweza kuukabili,
tukaiacha ikokotwe na huo upepo.
16 Kisiwa kimoja kiitwacho Kanda kilitukinga kidogo na ule upepo; na
tulipopita kusini mwake tulifaulu, ingawa kwa shida, kuusalimisha ule
mtumbwi wa meli.
17 Wale wanamaji waliuvuta mtumbwi ndani, kisha wakaizungushia meli
kamba na kuifunga kwa nguvu. Waliogopa kwamba wangeweza kukwama kwenye
ufuko wa bahari, pwani ya Libya. Kwa hiyo walishusha matanga na kuiacha
meli ikokotwe na upepo.
18 Dhoruba iliendelea kuvuma na kesho yake wakaanza kutupa nje
shehena ya meli.
19 Siku ya tatu, wakaanza pia kutupa majini vifaa vya meli kwa
mikono yao wenyewe.
20 Kwa muda wa siku nyingi hatukuweza kuona jua wala nyota; dhoruba
iliendelea kuvuma sana, hata matumaini yote ya kuokoka yakatuishia.

21 Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati
yao, akasema, “Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza
na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka
shida hii na hasara hizi zote.
22 Lakini sasa ninawaombeni muwe na moyo; hakuna hata mmoja wenu
atakayepoteza maisha yake; meli tu ndiyo itakayopotea.
23 Kwa maana jana usiku malaika wa yule Mungu ambaye mimi ni wake na
ambaye mimi ninamwabudu alinitokea,
24 akaniambia: <Paulo usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya
Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote
wanaosafiri nawe wasiangamie.>
25 Hivyo, waheshimiwa, jipeni moyo! Maana ninamwamini Mungu kwamba
itakuwa sawa kama nilivyoambiwa.
26 Lakini ni lazima tutatupwa ufukoni mwa kisiwa fulani.”

27 Usiku wa siku ya kumi na nne, tulikuwa tunakokotwa huku na huku
katika bahari ya Adria. Karibu na usiku wa manane wanamaji walijihisi
kuwa karibu na nchi kavu.
28 Hivyo walitafuta kina cha bahari kwa kuteremsha kamba iliyokuwa
imefungiwa kitu kizito, wakapata kina cha mita arobaini. Baadaye
wakapima tena wakapata mita thelathini.
29 Kwa sababu ya kuogopa kukwama kwenye miamba, waliteremsha nanga
nne nyuma ya meli; wakaomba kuche upesi.
30 Wanamaji walitaka kutoroka, na walikwisha kuteremsha ule mtumbwi
majini, wakijisingizia kwamba wanakwenda kuteremsha nanga upande wa
mbele wa meli.
31 Lakini Paulo alimwambia yule ofisa wa jeshi na askari wake,
“Kama wanamaji hawa hawabaki ndani ya meli, hamtaokoka.”
32 Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule
mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji.
33 Karibu na alfajiri, Paulo aliwahimiza wote wale chakula: “Kwa
siku kumi na nne sasa mmekuwa katika mashaka na bila kula; hamjala kitu
chochote.
34 Basi, ninawasihi mle chakula kwa maana mnakihitaji ili mweze
kuendelea kuishi. Maana hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea.”
35 Baada ya kusema hivyo, Paulo alichukua mkate, akamshukuru Mungu
mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.
36 Hapo wote wakapata moyo, nao pia wakala chakula.
37 Jumla tulikuwa watu mia mbili na sabini na sita katika meli.
38 Baada ya kila mmoja kula chakula cha kutosha, walipunguza uzito
wa meli kwa kutupa nafaka baharini.

Meli inavunjika

39 Kulipokucha, wanamaji hawakuweza kuitambua nchi ile, ila waliona
ghuba moja yenye ufuko; wakaamua kutia nanga huko kama ikiwezekana.
40 Hivyo walikata nanga na kuziacha baharini, na wakati huohuo
wakazifungua kamba zilizokuwa zimeufunga usukani, kisha wakatweka tanga
moja mbele kushika upepo, wakaelekea ufukoni.
41 Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana,
na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila
kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa
mapigo ya nguvu ya mawimbi.

42 Askari walitaka kuwaua wafungwa wote kwa kuogopa kwamba
wangeogelea hadi pwani na kutoroka.
43 Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia
wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na
kuogelea hadi pwani,
44 na wengine wafuate wakijishikilia kwenye mbao au kwenye vipande
vya meli iliyovunjika. Ndivyo sisi sote tulivyofika salama pwani.

\c 28

Yaliyompata Paulo huko Malta

1 Tulipokwisha fika salama kwenye nchi kavu, tuligundua kwamba kile
kisiwa kinaitwa Malta.
2 Wenyeji wa hapo walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwa inaanza
kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyo waliwasha moto, wakatukaribisha.
3 Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo,
kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa
Paulo mkononi na kujishikilia hapo.
4 Wenyeji wa pale walipokiona kile kiumbe kinaning’inia kwenye mkono
wake waliambiana, “Bila shaka mtu huyu amekwisha ua mtu, na ingawa
ameokoka kuangamia baharini, <Haki> haitamwacha aendelee kuishi!”
5 Lakini Paulo alikikung’utia kile kiumbe motoni na hakuumizwa hata
kidogo.
6 Wale watu walikuwa wakitazamia kwamba angevimba au hapohapo
angeanguka chini na kufa. Baada ya kungojea kwa muda mrefu bila kuona
kwamba Paulo amepatwa na jambo lolote lisilo la kawaida, walibadilisha
fikira zao juu yake, wakasema kuwa ni mungu.

7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile
kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku
tatu.
8 Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani,
mgonjwa, ana homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali,
akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.
9 Kutokana na tukio hilo, wagonjwa wote katika kile kisiwa walikuja
wakaponywa.
10 Watu walitupatia zawadi mbalimbali na wakati tulipoanza tena
safari, walitia ndani ya meli masurufu tuliyohitaji.

Safari kutoka Malta kwenda Roma

11 Baada ya miezi mitatu tulianza tena safari yetu kwa meli moja ya
Aleksandria iitwayo “Miungu Pacha”. Meli hiyo ilikuwa imetia nanga
kisiwani wakati wote wa baridi.
12 Tulifika katika mji wa Sirakusa, tukakaa hapo kwa siku tatu.
13 Toka huko tuling’oa nanga, tukazunguka na kufika Regio. Baada ya
siku moja, upepo ulianza kuvuma kutoka kusini, na baada ya siku mbili
tulifika bandari ya Potioli.
14 Huko tuliwakuta ndugu kadhaa ambao walituomba tukae nao kwa juma
moja. Hivi ndivyo tulivyopata kufika Roma.
15 Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye
soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu,
akapata moyo.

Paulo mjini Roma

16 Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na
askari mmoja wa kumlinda.
\il 5
ic
\is Barabara mjini Roma (Mate. 28:15)
\ie

17 Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiyahudi wa
mahali hapo. Walipokusanyika, Paulo aliwaambia, “Wananchi wenzangu,
mimi, ingawa sikufanya chochote kibaya wala kupinga desturi za wazee
wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemu na kutiwa mikononi mwa Waroma.
18 Waliponihoji na kuona kwamba sikuwa na hatia yeyote, walitaka
kuniacha.
19 Lakini Wayahudi wengine walipinga jambo hilo, nami nikalazimika
kukata rufani kwa Kaisari, ingawa sikuwa na chochote cha kuwashtaki
wananchi wenzangu.
20 Ni kwa sababu hiyo nimeomba kuonana na kuongea nanyi, maana
nimefungwa minyororo hii kwa sababu ya tumaini lile la Israeli.”

21 Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea,
wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema
chochote kibaya juu yako.
22 Lakini tunafikiri inafaa tusikie kutoka kwako mwenyewe mambo
yaliyo kichwani mwako. Kwa maana tujualo sisi kuhusu hicho kikundi ni
kwamba kinapingwa kila mahali.”

23 Basi, walipanga naye siku kamili ya kukutana, na wengi wakafika
huko alikokuwa anakaa. Tangu asubuhi mpaka jioni Paulo aliwaeleza na
kuwafafanulia juu ya Ufalme wa Mungu akijaribu kuwafanya wakubali habari
juu ya Yesu kwa kutumia Sheria ya Mose na maandiko ya manabii.
24 Baadhi yao walikubali maneno yake, lakini wengine hawakuamini.
25 Basi, kukawa na mtengano wa fikira kati yao. Walipokuwa
wanakwenda zao, Paulo alisema jambo hili, “Kweli ni sawa yale
aliyoyanena Roho Mtakatifu kwa wazee wenu kwa njia ya nabii Isaya
26 akisema:

<Nenda kwa watu hawa ukawaambie:
kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa;
kutazama mtatazama, lakini hamtaona.

27 Maana akili za watu hawa zimepumbaa,

wameziba masikio yao,
wamefumba macho yao.
La sivyo, wangeona kwa macho yao,
wangesikia kwa masikio yao.
Wangeelewa kwa akili zao,
na kunigeukia, asema Bwana,
nami ningewaponya.”>

28 Halafu Paulo akamaliza na kusema, “Jueni basi, kwamba ujumbe wa
Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watu wa mataifa. Wao
watasikiliza!”fd
\fm d
\fr 28:28
\f Baadhi ya makala zina aya 29: Paulo alipokwisha sema hayo, Wayahudi
walijiondokea huku wakiwa wanabishana vikali wao kwa wao.

29 missing
30 Kwa muda wa miaka miwili mizima Paulo aliishi katika nyumba
aliyoipanga yeye mwenyewe; akawa anawakaribisha wote waliofika
kumsalimu.
31 Alikuwa akihubiri Ufalme wa Mungu na kufundisha juu ya Bwana Yesu
Kristo kwa uhodari, bila kizuizi.