BARUA KWA
                 WAEBRANIA

\h WAEBRANIA

Mungu anasema kwa njia ya Mwanae
\c 1

1 Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna
nyingi kwa njia ya manabii,
2 lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye
ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu na akamteua avimiliki
vitu vyote.
3 Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya
Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada
ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni,
upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
\fr 1:5
\f taz Zab 2:7
\fr 1:7
\f taz Zab 104:4

Ukuu wa Mwana wa Mungu

4 Mwana ni mkuu zaidi kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na
Mungu ni kuu zaidi kuliko jina lao.
5 Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:

“Wewe ni Mwanangu;
Mimi leo nimekuwa Baba yako.”
Wala hakusema juu ya malaika yeyote:
“Mimi nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa Mwanangu.”
\m
6 Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wa kwanza
ulimwenguni, alisema:

“Malaika wote wa Mungu
wanapaswa kumwabudu.”
\m
7 Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema:

“Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo,
na watumishi wake kuwa ndimi za moto.”
\m
8 Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema:

“Utawala wako ee Mungu,
wadumu milele na milele!
Wewe wawatawala watu wako kwa haki.

9 Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu.

Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuweka wakfu
na kukumiminia furaha kubwa zaidi kuliko wenzako.”
\m
10 Pia alisema:

“Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo,
mbingu ni kazi ya mikono yako.

11 Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima,

zote zitachakaa kama vazi.

12 Utazikunjakunja kama koti,

nazo zitabadilishwa kama vazi.
Lakini wewe ni yuleyule daima,
na maisha yako hayatakoma.”
\m
13 Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:

“Keti upande wangu wa kulia,
mpaka niwaweke adui zako
chini ya miguu yako.”
\fr 1:8-9
\f taz Zab 45:6-7
\fr 1:10-12
\f taz Zab 102:25-27
\fr 1:13
\f taz Zab 110:1

14 Malaika ni roho tu wanaomtumikia Mungu, na Mungu huwatuma
wawasaidie wale watakaopokea wokovu.

Wokovu mkuu
\c 2

1 Kwa sababu hiyo tunapaswa kuzingatia kwa makini zaidi yote
tuliyosikia, ili tusije tukapotoshwa.
2 Ujumbe ule waliopewa wazee wetu na malaika ulionyeshwa kuwa kweli,
hata mtu yeyote ambaye hakuufuata au hakuutii aliadhibiwa kama
alivyostahili.
3 Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza
Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia
walituthibitishia kwamba ni kweli.
4 Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya
miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu
kadiri ya mapenzi yake.

Mkurugenzi wa wokovu

5 Mungu hakuwaweka malaika wautawale ulimwengu ujao, yaani ulimwengu
ule tunaoongea habari zake.
6 Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko:

“Mtu ni nini ee Mungu, hata umfikirie;
mwanaadamu ni nini hata umjali?

7 Ulimfanya kwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kuliko malaika;

ukamvika taji ya utukufu na heshima,

8 ukaweka kila kitu chini ya miguu yake, avitawale.”
\fr 2:6-8
\f taz Zab 8:4-6
\m Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote yaani
bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu
vyote sasa.
9 Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa
chini zaidi kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu
wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya
kifo alichoteseka.
10 Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu
vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili
awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye
anayewaongoza kwenye wokovu.

11 Yeye anawatakasa watu dhambi zao, naye pamoja na wale
waliotakaswa, wote wanaye Baba mmoja. Ndiyo maana Yesu haoni aibu
kuwaita hao ndugu zake;
12 kama asemavyo:

“Ee Mungu,
nitawatangazia ndugu zangu matendo yako.
Nitakusifu katika kusanyiko lao.”
\m
13 Tena asema:

“Nitamwekea Mungu tumaini langu.”
\m Na tena:

“Mimi niko hapa pamoja na watoto alionipa Mungu.”
\fr 2:12
\f taz Zab 22:22

14 Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na
damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya
hivyo ili kwa njia ya kifo chake amwangamize Ibilisi, ambaye ana mamlaka
juu ya kifo,
15 na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwa maisha yao yote kwa
sababu ya hofu yao ya kifo.
16 Maana ni wazi kwamba yeye hakuja kwa ajili ya kuwasaidia malaika,
bali kama yasemavyo Maandiko; “Anawasaidia wazawa wa Abrahamu.”
17 Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe
Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia
Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe.
18 Na, anaweza sasa kuwasaidia wale wanaojaribiwa na kuteswa.

Yesu ni mkuu kuliko Mose
\c 3

1 Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya
Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
2 Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama
vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
3 Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe.
Hali kadhalika naye Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
4 Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani–na Mungu ndiye mjenzi wa
vitu vyote.
5 Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi,
na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
6 Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba
ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti
wetu katika kile tunachotumainia.
\fr 3:7-11
\f taz Zab 95:7-11

Pumziko kwa watu wa Mungu

7 Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu:

“Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,

8 msiifanye mioyo yenu kuwa migumu

kama wazee wenu walivyokuwa
wakati walipomwasi Mungu;
kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,

9 Huko wazee wenu walinijaribu

na kunichunguza, asema Bwana,
ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu kwa miaka arobaini.

10 Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema,

<Fikira za watu hawa zimepotoka,
hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.>

11 Basi, nilikasirika, nikaapa:

<Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko.”>

12 Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye
na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu
sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu
asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
14 Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa
uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
\fr 3:15
\f taz Zab 95:7-8

15 Maandiko yasema hivi:

“Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
msiifanye mioyo yenu kuwa migumu
kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu.”

16 Ni akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale
wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
17 Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini?
Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule
jangwani.
18 Mungu alipoapa: “Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko,”
alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
19 Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
\fr 4:3
\f taz Zab 95:11

\c 4

1 Mungu alituahidia kwamba tutaweza kupata pumziko hilo alilosema.
Basi, na tuogope ili yeyote kati yenu asije akashindwa kupata pumziko
hilo.
2 Maana Habari Njema imehubiriwa kwetu kama vile ilivyohubiriwa kwa
hao watu wa kale. Lakini ujumbe huo haukuwafaa chochote, maana
waliusikia lakini hawakuupokea kwa imani.
3 Basi, sisi tunaoamini tunapata pumziko hilo aliloahidi Mungu. Kama
alivyosema:

“Nilikasirika, nikaapa:
<Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko.”>
\fr 4:5
\f taz Zab 95:11
\fr 4:7
\f taz Zab 95:7-8
\m Mungu alisema hayo ingawa kazi yake ilikuwa imekwisha malizika tangu
alipoumba ulimwengu.
4 Maana Maandiko yasema mahali fulani kuhusu siku ya saba: “Mungu
alipumzika siku ya saba, akaacha kazi zake zote.”
5 Tena jambo hili lasemwa pia: “Hawataingia huko ambako ningewapa
pumziko.”
6 Wale waliotangulia kuhubiriwa Habari Njema hawakupata pumziko hilo
kwa sababu hawakuamini. Wapo, basi, wengine ambao wangejaliwa kulipata.
7 Jambo hili ni wazi, kwani Mungu aliweka siku nyingine ambayo
inaitwa “Leo”. Miaka mingi baadaye Mungu alisema juu ya hiyo siku kwa
maneno ya Daudi katika Maandiko yaliyokwisha tajwa:

“Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
msiifanye mioyo yenu kuwa migumu.”

8 Kama Yoshua angaliwapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema
baadaye juu ya siku nyingine.
9 Kwa hiyo, basi, bado lipo pumziko kwa watu wa Mungu kama kule
kupumzika kwake Mungu siku ya saba.
10 Maana, kila anayepata pumziko aliloahidi Mungu atapumzika baada
ya kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika baada ya yake.
11 Basi, tujitahidi kupata pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni
mwenu atakayeshindwa, kama walivyofanya wao kwa sababu ya ukosefu wao wa
imani.

12 Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali zaidi kuliko upanga
wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho
hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na mafuta. Neno hilo
huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.
13 Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu
kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake. Kwake, sisi sote tutapaswa kutoa
hoja ya matendo yetu.

Yesu Kuhani Mkuu

14 Basi, tunapaswa kuzingatia kwa uthabiti imani tunayoiungama.
Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka kwa Mungu mwenyewe–Yesu,
Mwana wa Mungu.
15 Huyu Kuhani Mkuu wetu si mmoja ambaye hawezi kutuunga mkono
katika unyonge wetu, ila ni Kuhani Mkuu ambaye alijaribiwa kama sisi kwa
kila namna lakini hakutenda dhambi.
16 Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu, palipo na
neema, ili tukajipatie huruma na neema ya kutusaidia wakati wa lazima.

\c 5

1 Kila kuhani mkuu huchaguliwa kutoka miongoni mwa watu kwa ajili ya
kumtumikia Mungu kwa niaba yao, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya
dhambi zao.
2 Maadamu yeye mwenyewe yu dhaifu anaweza kuwaonea huruma wale
wasiojua kitu na wanaofanya makosa.
3 Na kwa vile yeye mwenyewe ni dhaifu, anapaswa kutolea dhabihu si
tu kwa ajili ya watu, bali pia kwa ajili ya dhambi zake.
4 Hakuna mtu awezaye kujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani
mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa
Aroni.
\fr 5:5
\f taz Zab 2:7
\fr 5:6
\f taz Zab 110:4

5 Hali kadhalika naye Kristo hakujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa
kuhani mkuu, bali Mungu alimwambia:

“Wewe ni Mwanangu;
mimi leo nimekuwa baba yako.”
\m
6 Alisema pia mahali pengine:

“Wewe ni kuhani milele,
kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”

7 Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi,
alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kutoka
kifo; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu.
8 Lakini, ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwa njia
ya mateso.
9 Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa
wale wote wanaomtii,
10 naye Mungu akamteua kuwa kuhani mkuu kufuatana na utaratibu wa
ukuhani wa Melkisedeki.

Onyo kuhusu uasi

11 Tunayo Mengi ya kusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumu
kuwaelezeni, kwa sababu ninyi si wepesi wa kuelewa.
12 Sasa mngalipaswa kuwa tayari walimu, lakini mnahitaji bado mtu wa
kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo ya ujumbe wa Mungu. Badala ya kula
chakula kigumu, mnapaswa bado kunywa maziwa.
13 Kila anayepaswa kunywa maziwa huyo ni mtoto bado, hajui uadilifu
ni nini.
14 Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, ambao
wanaweza kubainisha mema na mabaya.

\c 6

1 Basi, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa na kuyaacha nyuma yale
mafundisho ya mwanzo ya Kikristo. Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa
kurudia yale mafundisho ya mwanzo kama vile kuachana na matendo ya kifo,
kumwamini Mungu;
2 mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na
hukumu ya milele.
3 tusonge mbele! Hayo tutayafanya, Mungu akitujalia.

4 Maana watu wanaoiasi imani yao inawezekanaje kuwarudisha watubu
tena? Watu hao walikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu, walikwisha onja
zawadi ya mbinguni na kushirikishwa Roho Mtakatifu;
5 walikwisha onja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao,
6 kisha wakaiasi imani yao! Haiwezekani kuwarudisha watubu tena, kwa
sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu na kumwaibisha hadharani.

7 Mungu huibariki ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa
mara, na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima.
8 Lakini kama ardhi hiyo ikiota miti ya miiba na magugu, haina
faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto.

9 Lakini, ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tunalo tumaini
kubwa juu ya hali yenu. Tunajua kwamba mmepokea baraka zile bora za
wokovu wenu.
10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo
mlioonyesha kwa ajili ya jina lake katika huduma mliyowapa na mnayowapa
sasa watu wake.
11 Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyohiyo mpaka
mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia.
12 Msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye uvumilivu
na hivyo wanapokea yake aliyoahidi Mungu.

Ahadi ya Mungu ni ya kweli

13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe,
maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
14 Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.”
15 Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo alipokea kile
alichoahidiwa na Mungu.
16 Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko wao, na
kiapo hicho husuluhisha ubishi wote.
17 Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo
akawaonyesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake.
18 Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi
kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi
tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini
lililowekwa mbele yetu.
19 Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo ni
imara na thabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu la mbinguni mpaka
patakatifu ndani.
20 Yesu ametangulia kuingia humo kwa niaba yetu, na amekuwa kuhani
mkuu milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
\fr 6:20
\f taz Zab 110:4

Kuhani Melkisedeki
\c 7

1 Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu.
Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme,
Melkisedeki alikutana naye akambariki,
2 naye Abrahamu akampa sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa
navyo. (Maana ya kwanza ya jina hili Melkisedeki ni “Mfalme wa
Uadilifu”; na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia
lina maana ya “Mfalme wa Amani.”)
3 Baba yake na mama yake hawatajwi, wala ukoo wake hautajwi;
haisemwi alizaliwa lini au alikufa lini. Anafanana na Mwana wa Mungu, na
anaendelea kuwa kuhani daima.

4 Basi, mwaona jinsi mtu huyu alivyokuwa maarufu. Baba Abrahamu
alimpa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyoteka vitani.
5 Tunajua vilevile kwamba kufuatana na Sheria, wana wa Lawi ambao ni
makuhani, wanayo haki ya kuchukua sehemu ya kumi kutoka kwa watu, yaani
ndugu zao, ingawaje nao ni watoto wa Abrahamu.
6 Lakini huyo Melkisedeki hakuwa wa ukoo wa Lawi, hata hivyo
alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu; tena akambariki yeye ambaye
alikuwa amepewa ahadi ya Mungu.
7 Hakuna mashaka hata kidogo kwamba anayebariki ni mkuu zaidi kuliko
yule anayebarikiwa.
8 Tena, hao makuhani wanaopokea sehemu ya kumi, ni watu ambao hufa;
lakini hapa anayepokea sehemu ya kumi, yaani Melkisedeki, anasemekana
kwamba hafi.
9 Twaweza, basi, kusema kwamba Abrahamu alipotoa sehemu moja ya
kumi, Lawi (ambaye watoto wake hupokea sehemu moja ya kumi) alitoa
sehemu moja ya kumi pia.
10 Maana Lawi hakuwa amezaliwa bado, bali ni kama alikuwa katika
mwili wa baba yake, Abrahamu, wakati Melkisedeki alipokutana naye.

11 Kutokana na ukuhani wa Walawi, watu wa Israeli walipewa Sheria.
Sasa, kama huduma ya Walawi ingalikuwa kamilifu hapangekuwa tena na haja
ya kutokea ukuhani mwingine tofauti, ukuhani ambao umefuata utaratibu wa
ukuhani wa Melkisedeki, na si ule wa Aroni.
12 Maana ukuhani ukibadilika ni lazima Sheria nayo ibadilike.
13 Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake,
alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake
aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
14 Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda
ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.

Kuhani mwingine

15 Tena jambo hili ni dhahiri zaidi: kuhani mwingine anayefanana na
Melkisedeki amekwisha tokea.
16 Yeye hakufanywa kuwa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu,
bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
17 Maana Maandiko yasema: “Wewe ni kuhani milele, kufuatana na
utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”
18 Basi, ile amri ya zamani ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na
isiyofaa kitu.
19 Maana Sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini
sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo
tunaweza kumkaribia Mungu.
\fr 7:17
\fr taz Zab 110:4
\fr 7:21
\f taz Zab 110:4

20 Zaidi ya hayo hapa pana kiapo cha Mungu. Wakati wale wengine
walipofanywa makuhani hapakuwako kiapo.
21 Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia:

“Bwana ameapa,
wala hataigeuza nia yake:
<Wewe ni kuhani milele.”>

22 Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano
lililo bora zaidi.

23 Kuna tofauti nyingine pia: hao makuhani wengine walikuwa wengi
kwa sababu walikufa na hawakuweza kuendelea na kazi yao.
24 Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake
hauondoki kwake.
25 Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu
kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.

26 Basi, Yesu ndiye Kuhani Mkuu ambaye anatufaa sana katika mahitaji
yetu. Yeye ni mtakatifu, hana hatia wala dhambi ndani yake; hayumo
katika kundi la wenye dhambi na ameinuliwa mpaka juu mbinguni.
27 Yeye si kama wale makuhani wakuu wengine; hana haja ya kutoa
dhabihu kila siku, kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa
ajili ya dhambi za watu. Yeye alifanya hivyo mara moja tu wakati
alipojitoa yeye mwenyewe, na hiyo yatosha kwa nyakati zote.
28 Sheria ya Mose huwateua watu waliokuwa dhaifu kuwa makuhani
wakuu; lakini ahadi ya Mungu aliyoifanya kwa kiapo na ambayo imefika
baada ya sheria imemteua Mwana ambaye amefanywa mkamilifu milele.
\fr 8:1
\f taz Zab 110:1

Yesu Kuhani wetu Mkuu
\c 8

1 Basi, jambo muhimu katika hayo tunayosema ni hili: sisi tunaye
Kuhani Mkuu wa namna hiyo, ambaye anaketi upande wa kulia wa kiti cha
enzi cha Mwenyezi Mungu mbinguni.
2 Yeye hutoa huduma ya Kuhani Mkuu katika Mahali Patakatifu sana,
yaani ndani ya ile hema ya kweli iliyojengwa na Bwana, siyo na binadamu.
\il 5
ic
\is Kuhani Mkuu (Ebr. 8:1,2)
\ie

3 Kila Kuhani Mkuu ameteuliwa kumtolea Mungu vipawa na dhabihu, na
hivyo Kuhani Mkuu wetu lazima pia awe na kitu cha kutolea.
4 Kama yeye angekuwa wa hapa duninani, asingekuwa kamwe kuhani,
kwani wako makuhani wengine wanaotoa sadaka kufuatana na Sheria.
5 Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko
mbinguni. Ndivyo pia ilivyokuwa kwa Mose. Wakati alipokuwa karibu
kuitengeneza ile hema, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana
na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.”
6 Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora zaidi
kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni
bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora
zaidi.

7 Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari,
hakungalikuwa na haja ya agano la pili.
8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema:

“Siku zinakuja, asema Bwana,
ambapo nitafanya agano jipya
na watu wa Israeli
na kabila la Yuda.

9 Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zao

siku ile nilipowaongoza kwa mkono kutoka nchi ya Misri.
Hawakuwa waaminifu kwa agano langu;
na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.

10 Na hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo,
asema Bwana:

Nitaweka sheria zangu akilini mwao,
na kuziandika mioyoni mwao.
Mimi nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.

11 Hakuna mtu atakayemfundisha mwananchi mwenzake,

wala atakayemwambia ndugu yake:
<Mjue Bwana.>
Maana watu wote, wadogo na wakubwa,
watanijua mimi.

12 Nitawasamehe makosa yao,

wala sitakumbuka tena dhambi zao.”

13 Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza;
na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.

Ibada ya duniani na ya mbinguni
\c 9

1 Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na pia mahali
patakatifu pa ibada palipojengwa na watu.
2 Palitengenezwa hema ambayo sehemu yake ya nje iliitwa Mahali
Patakatifu. Humo mlikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyotolewa
kwa Mungu.
3 Nyuma ya pazia la pili, kulikuwa na hema iliyoitwa Mahali
Patakatifu Kupita Pote.
4 Humo mlikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia ubani,
na Sanduku la Agano, ambalo lilikuwa limepakwa dhahabu pande zote, na
ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabu kilichokuwa na mana; fimbo ya
Aroni iliyokuwa imechanua majani, na vile vibao viwili vilivyoandikwa
agano.
5 Juu ya hilo Sanduku kulikuwa na viumbe vilivyodhihirisha kuweko
kwa Mungu, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi
huondolewa. Lakini sasa, hatuwezi kusema kinaganaga juu ya mambo hayo.

6 Mipango hiyo ilitekelezwa kisha ikawa desturi kwa makuhani kuingia
kila siku katika hema ya nje kutoa huduma zao.
7 Lakini kuhani Mkuu peke yake ndiye anayeingia katika lile hema la
pili; naye hufanya hivyo mara moja tu kwa mwaka. Anapoingia ndani huwa
amechukua damu ambayo anamtolea Mungu kwa ajili yake mwenyewe na kwa
ajili ya dhambi ambazo watu wamezitenda bila wao wenyewe kujua.
8 Kutokana na taratibu hizo Roho Mtakatifu anafundisha wazi kwamba
wakati ile hema ya nje ingali ipo imesimama, njia ya kuingia Mahali
Patakatifu haijafunguliwa.
9 Jambo hili ni mfano wa nyakati za sasa. Linaonyesha kwamba zawadi
na dhabihu zinazotolewa kwa Mungu haziwezi kuifanya mioyo ya wale
wanaoabudu kuwa mikamilifu,
10 kwani haya yote yanahusika na vyakula, vinywaji na taratibu
mbalimbali za kutawadha. Yote hayo ni maagizo ya njenje tu; na nguvu
yake hukoma wakati Mungu atakaporekebisha vitu vyote.

11 Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa Kuhani Mkuu wa mambo yaliyo
mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema
iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani
isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.
12 Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa
amechukua damu ya mbuzi wala ng’ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye
mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele.
13 Watu waliokuwa najisi kidini waliweza kutakasika na kuwa safi
waliponyunyiziwa damu ya mbuzi na ya ng’ombe pamoja na majivu ya ndama.
14 Lakini, kwa damu ya Kristo, mambo makuu zaidi hufanyika! Kwa
nguvu za Roho wa milele, Kristo alijitolea mwenyewe dhabihu kamilifu kwa
Mungu. Damu yake itatutakasa dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo
kifo, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai.

15 Kwa hiyo, Kristo ndiye aliyeratibisha agano jipya ili wale
walioitwa na Mungu wazipokee baraka za milele walizoahidiwa. Watazipata,
kwani kifo kimetokea ambacho huwakomboa watu kutoka yale makosa
waliyofanya wakati wa lile agano la kale.

16 Kwa kawaida wosia hutambuliwa tu kama kifo cha yule aliyeufanya
huo wosia kimethibitishwa.
17 Wosia hauwezi kutekelezwa mpaka kumetokea kifo, kwani wosia hauna
maana ikiwa mwenye kuufanya bado anaishi.
18 Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu
kumwagwa.
19 Kwanza Mose aliwatangazia watu wote amri zote kama ilivyokuwa
katika Sheria; kisha akachukua damu ya ndama pamoja na maji, na kwa
kutumia majani ya mti uitwao husopo na pamba nyekundu, akakinyunyizia
kile kitabu cha Sheria na hao watu wote.
20 Mose alisema: “Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na
Mungu mlitii.”
21 Vilevile Mose aliinyunyizia damu ile hema na vyombo vya ibada.
22 Naam, kadiri ya Sheria karibu kila kitu chaweza kutakaswa kwa
damu, na dhambi nazo zaondolewa tu ikiwa damu imemwagwa.

Sadaka ya Kristo huondoa dhambi za watu

23 Vitu hivi ambavyo ni mfano tu wa mambo halisi ya mbinguni,
vililazimika kutakaswa kwa namna hiyo. Lakini vitu vya mbinguni huhitaji
dhabihu iliyo bora zaidi.
24 Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono
ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. yeye aliingia
mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.
25 Kuhani Mkuu wa Wayahudi huingia Mahali Patakatifu kila mwaka
akiwa amechukua damu ya mnyama; lakini Kristo hakuingia humo ili ajitoe
mwenyewe mara nyingi,
26 maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi
tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa nyakati hizi zinapokaribia mwisho
wake, yeye ametokea mara moja tu, kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye
mwenyewe dhabihu.
27 Basi, kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele
ya hukumu ya Mungu,
28 vivyo hivyo Kristo naye alijitoa dhabihu mara moja tu kwa ajili
ya kuziondoa dhambi za wengi. Atakapotokea mara ya pili si kwa ajili ya
kupambana na dhambi, bali ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomngojea.

\c 10

1 Sheria ya Wayahudi si picha kamili ya mambo yale halisi: ni kivuli
tu cha mema yanayokuja. Dhabihu zilezile hutolewa daima, mwaka baada ya
mwaka. Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihu hizo, kuwafanya wale
wanaoabudu wawe wakamilifu?
2 Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao
kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na dhabihu hizo zote
zingekoma.
3 Lakini dhabihu hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi
zao.
4 Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
\fr 10:5-7
\f taz Zab 40:6-8

5 Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia
Mungu:

“Hukutaka dhabihu wala sadaka,
lakini umenitayarishia mwili.

6 Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.

7 Hapo nikasema:

<Niko hapa ee Mungu,
tayari kufanya mapenzi yako
kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha Sheria.”>
\m
8 Kwanza alisema: “Hutaki, wala hupendezwi na dhabihu na sadaka,
sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa
sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na Sheria.
9 Kisha akasema: “Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya mapenzi
yako.” Hivyo Mungu alibatilisha dhabihu za zamani na mahali pake
akaweka dhabihu nyingine moja.
10 Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza mapenzi ya Mungu, sisi tunatakaswa
dhambi zetu kwa ile dhabihu ya mwili wake aliyotoa mara moja tu,
ikatosha.

11 Kila kuhani Myahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoa dhabibu
zilezile mara nyingi, dhabibu ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
12 Lakini Kristo alitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi, dhabihu
ifaayo milele, kisha akaketi upande wa kulia wa Mungu.
13 Huko anangoja mpaka adui zake watakapowekwa kama kibao chini ya
miguu yake.
14 Basi, kwa dhabihu yake moja tu, amewafanya kuwa wakamilifu milele
wale wanaotakaswa dhambi zao.
\fr 10:12-13
\f taz Zab 110:1

15 Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:

16 “Hili ndilo agano nitakalofanya nao,

katika siku zijazo, asema Bwana:
Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao,
na kuziandika akilini mwao.”
\m
17 Kisha akaongeza kusema:

“Sitakumbuka tena dhambi zao,
wala vitendo vyao vya uhalifu.”
\m
18 Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa
dhabihu za kuondoa dhambi.

19 Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia
Mahali Patakatifu.
20 Yeye ametufungulia njia mpya na yenye uzima kupitia lile pazia,
yaani kwa njia ya mwili wake mwenyewe.
21 Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya
Mungu.
22 Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa
mioyo iliyotakaswa dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji
safi.
23 Tushikilie imara tumaini lile tunalokiri, maana Mungu aliyefanya
ahadi zake ni mwaminifu.
24 Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya
kupendana na kutenda mema.
25 Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine
wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, Siku ile
ya Bwana inakaribia.

26 Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu
ukweli, hakuna dhabihu iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa
dhambi.
27 Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali
utakaowaangamiza wote wanaompinga.
28 Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawa bila ya huruma kukiwa
na ushahidi wa watu wawili au watatu.
29 Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya
agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili
kupata adhabu kali ya namna gani?
30 Maana tunamfahamu yule aliyesema, “Mimi nitalipiza kisasi, mimi
nitalipiza,” na ambaye alisema pia, “Bwana atawahukumu watu wake.”
31 Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!

32 Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa
Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, ninyi mlistahimili.
33 Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara
nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo.
34 Mlishiriki mateso ya wafungwa, na mliponyang’anywa mali yenu
mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya
kudumu milele.
35 Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa.
36 Mnahitaji kuwa na uvumilivu, ili mweze kufanya anayotaka Mungu na
kupokea kile alichoahidi.
37 Maana kama yasemavyo Maandiko:

“Bado kidogo tu,
na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.

38 Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi;

walakini akirudi nyuma,
mimi sitapendezwa naye.”
\m
39 Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea,
ila sisi tunaamini na tunaokolewa.

Imani
\c 11

1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki
kabisa mambo tusiyoyaona.
2 Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya imani
yao.
\fr 11:3
\f taz Zab 33:6,9

3 Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la
Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.

4 Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu iliyokuwa bora zaidi
kuliko ile ya Kaini. Kwa imani yake alikubaliwa na Mungu kuwa mwadilifu;
Mungu mwenyewe alizikubali sadaka zake. Kwa imani yake ingawa amekufa,
bado ananena.

5 Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana
tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla
ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
6 Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila
mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba
huwatuza wale wanaomtafuta.

7 Kwa imani Noa alionywa na Mungu juu ya mambo ya baadaye ambayo
hakuweza kuyaona bado. Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamo
aliokolewa yeye pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo ulimwengu
ulihukumiwa, naye Noa akapokea uadilifu unaotokana na imani.

8 Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi
ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda,
Abrahamu alihama.
9 Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu.
Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia
walishiriki ahadi ileile.
10 Maana Abrahamu alikuwa akingojea mji wenye misingi imara, mji
ambao Mungu mwenyewe ndiye fundi aliyeubuni na kuujenga.
11 Kwa imani hata Sara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake,
kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimba ingawaje alikuwa amepita umri.
12 Kwa hiyo, kutoka katika mtu huyo mmoja, Abrahamu, ambaye alikuwa
kama amekufa, walitokea watu wengi wasiohesabika kama vile nyota za
mbinguni na mchanga wa pwani.
\fr 11:13
\f taz Zab 39:12

13 Watu hawa wote walikufa wakiwa na imani. Walikufa kabla ya
kupokea mambo ambayo Mungu alikuwa ameahidi, lakini kwa mbali waliyaona,
wakashangilia, na kukiri wazi kwamba wao walikuwa wageni na wakimbizi
duniani.
14 Watu wanaosema mambo kama hayo, huonyesha wazi kwamba wanaitafuta
nchi yao wenyewe.
15 Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata
nafasi ya kurudi huko.
16 Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya
mbinguni. Ndiyo maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa
sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.

17 Kwa imani, Abrahamu alimtoa mwanae Isaka sadaka wakati Mungu
alipomjaribu. Huyo Abrahamu ndiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu,
lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa dhabihu mwanae wa pekee,
18 ingawa Mungu alikuwa amemwambia: “Wazawa wako watatokana na
Isaka.”
19 Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu: na kwa
namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanae kutoka wafu.

20 Kwa imani Isaka aliwabariki Yakobo na Esau, wapate baraka
zitakazokuja baadaye.

21 Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa
wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ile fimbo yake.

22 Kwa imani Yosefu alipokuwa karibu kufa, alinena juu ya kutoka kwa
Waisraeli katika nchi ya Misri, na pia akawaachia maagizo kuhusu mifupa
yake.

23 Kwa imani wazazi wa Mose walimficha huyo mtoto kwa muda wa miezi
mitatu baada ya kuzaliwa kwake. Walimwona kuwa ni mtoto mzuri, wala
hawakuiogopa amri ya mfalme.

24 Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa
binti Farao.
25 Aliona ni afadhali kuteseka pamoja na watu wa Mungu kuliko
kufurahia raha ya dhambi kwa kitambo kidogo.
26 Alitambua kwamba kuteseka kwa ajili ya Masiha kuna faida kubwa
zaidi kuliko utajiri wote wa nchi ya Misri, maana alikuwa anatazamia
tuzo la baadaye.

27 Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira
ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona
yule Mungu asiyeonekana.
28 Kwa imani aliadhimisha siku ya Pasaka, akaamuru damu inyunyizwe
juu ya milango, ili yule Malaika Mwangamizi asiwaue wazaliwa wa kwanza
wa Israeli.

29 Kwa imani watu wa Israeli walivuka bahari ya Shamu, kana kwamba
ilikuwa nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo walikufa
maji.

30 Kwa imani kuta za mji wa Yeriko zilianguka watu wa Israeli
walipokwisha zunguka kwa muda wa siku saba.
31 Kwa imani Rahabu aliyekuwa malaya hakuangamia pamoja na wale
waliomwasi Mungu, kwa sababu aliwakaribisha wale wapelelezi.

32 Basi, niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kueleza juu ya
Gedeoni, Baraki, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii.
33 Kwa imani hawa wote walipigana vita na wafalme, wakashinda.
Walitenda mambo adili, wakapokea yale aliyoahidi Mungu. Walifunga vinywa
vya simba,
34 Walizima mioto mikali, waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa
dhaifu lakini walipata nguvu. Walikuwa hodari katika vita wakashinda
majeshi ya kigeni.
35 Na, wanawake walioamini walirudishiwa wafu wao wakiwa
wamefufuliwa.
Baadhi yao walikataa kufunguliwa, wakateswa mpaka kufa ili wapate
kufufuliwa na kuingia katika maisha bora zaidi.
36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa
minyororo na kutupwa gerezani.
37 Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga.
Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi,
walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
38 Ulimwengu haukustahili kuwa na watu hao. Walitangatanga jangwani
na mlimani, wakaishi katika mashimo na mapango ya ardhi.

39 Watu hawa wote walionekana kuwa mashujaa kwa sababu ya imani yao.
Hata hivyo, hawakupokea yale ambayo Mungu aliwaahidia,
40 maana Mungu alikuwa ameazimia mpango ulio bora zaidi kwa ajili
yetu; yaani wao wangeufikia ukamilifu wakiwa pamoja nasi.

Bwana atufunza kuwa na nidhamu
\c 12

1 Sisi tunalo kundi hili kubwa la mashahidi mbele yetu. Kwa hiyo
tuondoe kila kizuizi kinachotuzuia, na dhambi ile inayotung’ang’ania.
Tupige mbio kwa uvumilivu katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu.
2 Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye
ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia
kifo msalabani, bila kujali juu ya aibu yake, na sasa anaketi upande wa
kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili
upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate
tamaa.
4 Maana katika kupambana na dhambi, ninyi hamjapigana mpaka kiasi
cha kumwaga damu yenu.
5 Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja
ninyi kuwa wanawe?

“Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana,
wala usife moyo anapokukanya.

6 Maana Bwana humwadhibu kila anayempenda,

humpinga kila anayekubali kuwa mwanae.”
\m
7 Vumilieni adhabu kwani ni mafundisho; Mungu huwatendea ninyi kama
wanawe. Maana ni mwana gani asiyeadhibiwa na baba yake?
8 Lakini msipoadhibiwa kama wana wengine, basi, ninyi si wanawe,
bali ni wana haramu.
9 Zaidi ya hayo sisi tunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hata
wanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidi Baba yetu wa kiroho ili
tupate kuishi.
10 Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe
walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu
wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
11 Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini
wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka
katika maisha adili!

Mafundisho na maonyo

12 Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu
yaliyo dhaifu.
13 Endeleeni kutembea katika njia iliyonyoka, ili kile kilicholemaa
kisiumizwe, bali kiponywe.

14 Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya
utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama
hayo.
15 Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe
waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu
yake.
16 Jihadharini ili miongoni mwenu pasiwe na mtu mwasherati au mtu
asiyemcha Mungu kama Esau, aliyeuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa
mlo mmoja.
17 Ninyi mnafahamu kwamba hata alipotaka kuipata tena ile baraka
iliyokuwa yake, alikataliwa, maana hakupata tena nafasi ya kutubu,
ingawa aliitafuta kwa machozi.

18 Ninyi hamkuwasili mlimani Sinai, ambao unaweza kushikika kama
walivyofanya watu wa Israeli, hamkufika kwenye moto uwakao, penye giza,
tufani,
19 mvumo wa tarumbeta na sauti ya maneno. Wale waliosikia sauti hiyo
waliomba wasisikie tena neno jingine,
20 kwani hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Atakayegusa
mlima huu, hata kama ni mnyama, atapigwa mawe.”
21 Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema,
“Naogopa na kutetemeka.”

22 Lakini ninyi mmefika katika mlima wa Sioni, kwenye mji wa Mungu
aliye hai. Mmefika Yerusalemu, mji wa mbinguni, ambapo wamekusanyika
malaika elfu nyingi wasiohesabika.
23 Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu,
ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye
hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa kuwa
wakamilifu.
24 Mmefika kwa Yesu ambaye ameratibisha agano jipya, na ambaye damu
yake iliyomwagika inasema mambo mema zaidi kuliko ile ya Abeli.

25 Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza yeye ambaye anasema
nanyi. Kama wale walikataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani
hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule
anayetuonya kutoka mbinguni?
26 Wakati ule sauti ilitetemesha nchi, lakini sasa ameahidi:
“Nitatetemesha nchi tena, lakini si nchi tu bali pia mbingu.”
27 Neno hili: “tena” linatuonyesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa
vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa.

28 Sisi basi, na tushukuru kwani tunapokea utawala usiotikisika.
Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada
na hofu;
29 maana Mungu wetu kweli ni moto mkali unaoteketeza.

Jinsi ya kumpendeza Mungu
\c 13

1 Endeleeni kupendana kidugu.
2 Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu
wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
3 Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao.
Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao.

4 Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe
kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
\fr 13:6
\f taz Zab 118:6

5 Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo.
Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”
6 Ndiyo maana tunathubutu kusema:

“Bwana ndiye msaada wangu,
sitaogopa.
Binadamu atanifanya nini?”

7 wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu.
Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
8 Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele.
9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema
ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya
chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.

10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema
la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.
11 Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali
Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao
wanyama huteketezwa nje ya kambi.
12 Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake
mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji.
13 Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake.
14 Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule
unaokuja.
15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima,
yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake.
16 Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu
zinazompendeza Mungu.

17 Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu
usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama
mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa
huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

18 Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana
twataka kufanya lililo sawa daima.
19 Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi
iwezekanavyo.

Sala

20 Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu
wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la
milele.
21 Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze
mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale
yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.

Maneno ya mwisho

22 Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni
moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni.
23 Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha
funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja
kwenu.

24 Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa
Italia wanawasalimuni.
25 Tunawatakieni nyote neema ya Mungu.
\z

\id JAS SW60.ALL 19-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT
\h YAKOBO

          BARUA YA
                 YAKOBO

          Salamu

\c 1

1 Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia
ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam!

Imani na hekima

2 Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali,
3 kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni
uvumilivu.
4 Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho,
mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
5 Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa
kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na
kwa ukarimu.
6 Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na
mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na
upepo.
7-8 Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika
mwenendo wake wote, asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa
Bwana.

Umaskini na utajiri

9 Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza,
10 naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri
atatoweka kama ua la porini.
11 Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua
yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri
ataangamizwa katika shughuli zake.

Majaribio

12 Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha
stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale
wanaompenda.
13 Kama mtu akijaribiwa, asiseme: “Ninajaribiwa na Mungu.” Maana
Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.
14 Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
15 Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.

16 Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike!
17 Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka
kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya
ugeugeu.
18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili
tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake.

Kusikia na kutenda

19 Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe
mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa
kukasirika.
20 Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki.
21 Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu;
jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu,
ambao waweza kuziokoa nafsi zenu.

22 Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali
litekelezeni kwa vitendo.
23 Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama
mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo.
24 Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi
alivyo.
25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa
watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau
baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu
anachofanya.

26 Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi
kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe.
27 Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii:
Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe
usichafuliwe na ulimwengu huu.

Onyo kuhusu ubaguzi
\c 2

1 Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu,
msiwabague watu kamwe.
2 Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu
anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa
mavazi machafu.
3 Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na
kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini:
“Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
4 je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana
na fikira mbaya?

5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni
maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na
kupokea Utawala aliowaahidia wale wanaompenda.
6 Lakini ninyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio
wanaowakandamizeni na kuwapeleka mahakamani?
7 Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa?

8 Kama mnaitimiza ile sheria ya Utawala kama ilivyoandikwa katika
Maandiko Matakatifu: “Mpende binadamu mwenzako kama unavyojipenda wewe
mwenyewe”, mtakuwa mnafanya vema kabisa.
9 Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheria
inawahukumu ninyi kuwa mna hatia.
10 Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja
Sheria yote.
11 Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue”. Kwa
hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.
12 Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria
iletayo uhuru.
13 Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na
huruma. Lakini huruma hushinda hukumu.

Imani na matendo

14 Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini
haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa?
15 Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula.
16 Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto
na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
17 Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

18 Lakini mtu anaweza kusema: “Wewe unayo imani, mimi ninayo
matendo!” Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila
matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
19 Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo
huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.
20 Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo
imekufa?
21 Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa
matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu.
22 Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani
yake ilikamilishwa kwa matendo yake.
23 Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu
alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na
hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu.”
24 Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo
yake na si kwa imani peke yake.

25 Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa
kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia
waende zao kwa kupitia njia nyingine.

26 Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila
matendo imekufa.

Ulimi
\c 3

1 Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu. Kama mjuavyo, sisi walimu
tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.
2 Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu,
na anaweza kutawala nafsi yake yote.
3 Sisi huwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii; na kwa njia
hiyo twaweza kuwaongoza kokote tunakotaka.
4 Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali,
huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha
anakotaka.
5 Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia
makuu sana.
\il 5
ic
\is Farasi waliofungwa lijamu (Yak. 3:3)
\ie
Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima,
unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu
zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.
7 Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe
vyote–wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini.
8 Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu,
hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.
9 Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo
twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
10 Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu
zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.
11 Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu
pamoja?
12 Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu
waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji
matamu.

Hekima itokayo juu mbinguni

13 Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe
jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema
yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi,
msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.
15 Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya
ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.
16 Maana popote palipo na wivu na ubinafsi hapo pana fujo na kila
aina ya uovu.
17 Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda
amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo
mema; haina ubaguzi wala unafiki.
18 Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika
amani.

Urafiki na ulimwengu
\c 4

1 Mapigano na magombano yote kati yenu yanatoka wapi? Hutoka katika
tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.
2 Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani
sana kupata vitu, lakini hamvipati, hivyo mnagombana na kupigana.
Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu.
3 Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba
ili mpate kutosheleza tamaa zenu.
4 Ninyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba
kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa
rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.
5 Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure,
yanaposema: “Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa.”
6 Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo
Maandiko: “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema
wanyenyekevu.”

7 Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye
atawakimbieni.
8 Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu
enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!
9 Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na
furaha yenu iwe huzuni kubwa.
10 Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.

Onyo kuhusu kumhukumu ndugu

11 Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake na
kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu Sheria. Kama ukiihukumu Sheria,
basi, wewe huitii Sheria, bali waihukumu.
12 Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka Sheria na kuhukumu. Ni yeye
peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata
umhukumu binadamu mwenzako?

Onyo kuhusu majivuno

13 Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: “Leo au kesho tutakwenda
katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata
faida.”
14 Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama
ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena.
15 Mngalipaswa kusema: “Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki
au kile.”
16 Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni
mabaya.

17 Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa
kulifanya, anatenda dhambi.

Onyo kwa matajiri
\c 5

1 Na sasa sikilizeni enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya
taabu zitakazowajieni.
2 Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo.
3 Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi
dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia
mali katika siku hizi za mwisho!
4 Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba
yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu
kimefika masikioni mwa Bwana, Mwenye Nguvu.
5 Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa.
Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa.
6 Mmemhukumu na kumwua mtu asiye na hatia, naye hakuwapigeni.

Subira na sala

7 Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja.
Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno mazuri.
Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.
8 Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana
siku ya kuja kwake Bwana inakaribia.

9 Ndugu zangu, msinung’unikiane ninyi kwa ninyi msije mkahukumiwa na
Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.
10 Ndugu, mkitaka kuona mfano wa subira na uvumilivu katika mateso,
fikirini juu ya manabii ambao walinena kwa jina la Bwana.
11 Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari
za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni.
Maana Bwana amejaa huruma na rehema.
\fr 5:11
\f taz Zab 103:8

12 Zaidi ya hayo yote, ndugu zangu, msiape kwa mbingu, wala kwa
dunia, wala kwa kitu kingine chochote. Semeni “Ndiyo” kama maana yenu
ni ndiyo, na “La” kama maana yenu ni la, na hapo hamtahukumiwa na
Mungu.

13 Je, pana mtu yeyote miongoni mwenu aliye na shida? Anapaswa
kusali. Je, yuko mwenye furaha? Anapaswa kuimba nyimbo za sifa.
14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao
watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu,
na dhambi alizotenda zitaondolewa.
16 Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate
kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.
17 Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo mvua
isinyeshe, nayo haikunyesha nchini kwa muda wa miaka mitatu na miezi
sita.
18 Kisha akaomba tena, mvua ikanyesha kutoka angani na nchi ikatoa
mazao yake.

19 Ndugu zangu, mmoja wenu akipotoka kuhusu ukweli, na mwingine
akamrudisha,
20 fahamuni kwamba, huyo anayemrudisha mwenye dhambi kutoka njia
yake ya upotovu, ataiokoa roho yake kutoka kifo, na dhambi nyingi
zitaondolewa.
\z

\id 1PE SW61.ALL 19/03/90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA KWANZA YA
                 PETRO

\h 1 PETRO
\c 1

1 Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo nawaandikia ninyi wateule wa Mungu
Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia,
Kapadokia, Asia na Bithunia.
2 Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa
watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu
yake.
Nawatakieni neema na amani tele.

Tumaini imara

3 Asifiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake
kuu alitufanya tuzaliwe upya kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujalia
tumaini lenye uzima,
4 na hivyo tunatazamia kupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekea
watu wake. Mungu amewawekeeni baraka hizo mbinguni ambako haziwezi kuoza
au kuharibika au kufifia.
5 Hizo zitakuwa zenu ninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa
nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni
mwa nyakati.

6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo,
itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.
7 Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe
ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu
ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate
kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu
Kristo atakapofunuliwa.
8 Ninyi mnampenda ingawaje hamjamwona, na mnamwamini ingawa
hamumwoni sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka,
9 kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani
yenu.

10 Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya
wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.
11 Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati
alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya
mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
12 Mungu aliwafunulia kwamba wakati walipokuwa wanasema juu ya hayo
mambo ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe
waliowatangazieni Habari Njema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwa
kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa
ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.

Mwito wa kuishi maisha matakatifu

13 Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha. Wekeni
tumaini lenu lote katika baraka ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo
atakapoonekana!
14 Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena
tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.
15 Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama
vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.
16 Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

17 Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye
humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni
wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
18 Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu
usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye
kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
19 bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama
mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
20 Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa,
akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.
21 Kwa njia yake, ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na
kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.

22 Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na
kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
23 Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si
kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
24 Kama Maandiko yasemavyo:

“Kila binadamu ni kama nyasi,
na utukufu wake wote ni kama maua ya porini.
Nyasi hunyauka na maua huanguka.

25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.”
\m Neno hilo ni hiyo Habari Njema iliyohubiriwa kwenu.

Jiwe hai na taifa takatifu
\c 2

1 Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa
visiweko tena.
2 Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa
kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua
na kukombolewa.
3 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni
mwema.”

4 Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu;
lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamani kubwa.
5 Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho,
ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea dhabihu za kiroho
zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
6 Maana Maandiko Matakatifu yasema:

“Tazama!
Naweka huko sioni jiwe kuu la msingi,
jiwe la thamani kubwa nililoliteua.
Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa.”
\m
7 Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa
wale wasioamini,

“Jiwe walilokataa waashi,
sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
\m
8 Tena Maandiko yasema:

“Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa,
mwamba wa kuwaangusha watu.”
\m Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo
walivyopangiwa tangu mwanzo.

9 Lakini ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu;
watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu
aliyewaiteni kutoka gizani akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.
10 Wakati mmoja ninyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa ninyi ni
watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa
mmeipokea.

Watumishi wa Mungu

11 Wapenzi wangu, nawasihi ninyi kama wageni na wakimbizi hapa
duniani! Achaneni na tamaa za mwili ambazo hupingana na roho.
12 Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema
kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze
kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu Siku ya kuja kwake.

13 Basi, jiwekeni chini ya mamlaka yote ya kibinadamu, kwa ajili ya
Bwana: utii kwa mfalme aliye mtawala mkuu,
14 utii kwa wakuu wa mikoa ambao wameteuliwa naye kuwaadhibu
wahalifu na kuwasifu watendao mema.
15 Maana Mungu anataka mweze kuyakomesha maneno ya kijinga ya watu
wasio na akili kwa matendo mema mnayofanya.
16 Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha
ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu.
17 Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni
Mungu, mheshimuni mfalme.

Mfano wa mateso ya Kristo

18 Enyi watumishi wa nyumbani, watiini wakuu wenu kwa heshima yote,
wawe wema na wapole au wenye kuchukiza.
19 Maana kama mnavumilia maumivu ya mateso msiyostahili kwa sababu
mwajua kwamba Mungu anataka hivyo, basi Mungu atawafadhili.
20 Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa
sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa
mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
21 Hayo ndiyo mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili
yenu, akawaachieni mfano, ili muufuate mwenendo wake.
22 Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika
mdomoni mwake.
23 Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa
vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki.
24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya
msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa
majeraha yake, ninyi mmeponywa.
25 Ninyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa
mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.

Mume na mke
\c 3

1 Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako
waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona
mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
2 kwani wataona jinsi mwenendo wenu ulivyo safi na wa kumcha Mungu.
3 Katika kujipamba kwenu msitegemee mambo ya njenje, kama vile
mitindo ya kusuka nywele, kujivalia vitu vya dhahabu na nguo maridadi.
4 Bali, uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa
kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa
thamani kubwa mbele ya Mungu.
5 Ndivyo walivyojipamba hapo kale wanawake waadilifu waliomtumainia
Mungu; walijiweka chini ya mamlaka ya waume zao.
6 Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Ninyi
mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.

7 Kadhalika nanyi waume, katika kuishi na wake zenu mnapaswa
kutambua kwamba wao ni dhaifu na hivyo muwatendee kwa heshima; maana nao
pia watapokea pamoja nanyi zawadi ya uzima anayowapeni Mungu. Hapo ndipo
sala zenu hazitakataliwa.

Kuteseka kwa sababu ya kutenda mema

8 Mwisho nasema hivi: mnapaswa kuwa na moyo mmoja, na fikira moja;
mnapaswa kupendana kidugu, kuwa wapole na wanyenyekevu ninyi kwa ninyi.
9 Msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni
baraka, maana ninyi mliitwa na Mungu mpate kupokea baraka.
10 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Anayetaka kufurahia maisha,
na kuona siku za fanaka,
anapaswa kuacha kusema mabaya
na kuacha kusema uongo.

11 Na ajiepushe na uovu, atende mema,

atafute amani na kuizingatia.

12 Maana Bwana huwatazama kwa wema waadilifu

na kuzisikiliza sala zao.
Lakini huwapa kisogo watu watendao maovu.”

13 Ni nani atakayeweza kuwadhuru ninyi kama mkizingatia kutenda
mema?
14 Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema,
basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika
wasiwasi.
15 Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari
kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,
16 lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema,
kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema
kama Wakristo, waone aibu.
17 Maana ni afadhali kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, kama Mungu
akipenda, kuliko kuteseka kwa sababu ya kutenda uovu.
18 Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu;
alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili
awapeleke ninyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
19 na kwa maisha yake ya kiroho alikwenda kuwahubiria wale roho
waliokuwa kifungoni.
20 Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi
wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni
watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa majini,
21 ambayo yalikuwa mfano wa ubatizo unaowaokoa ninyi sasa. Ubatizo
si shauri la kuondoa uchafu mwilini, bali ni ahadi kwa Mungu
inayofanyika katika dhamiri njema. Huwaokoeni kwa njia ya ufufuo wa Yesu
Kristo,
22 ambaye alikwenda mbinguni na sasa amekaa upande wa kulia wa
Mungu, anatawala juu ya malaika, wakuu na wenye enzi.

Maisha mapya
\c 4

1 Maadamu Kristo aliteseka kimwili, nanyi pia mnapaswa kujiimarisha
kwa nia hiyo yake; maana mtu akisha teseka kimwili hahusiki tena na
dhambi.
2 Tangu sasa, basi, maisha yaliowabakia kuishi hapa duniani
yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, si na tamaa za kibinadamu.
3 Wakati uliopita mlikuwa na muda mrefu wa kufanya mambo wanayofanya
watu wasiomjua Mungu. Mliishi maisha ya anasa, ubinafsi, ulevi, ugomvi,
kunywa mno na ya ibada haramu za sanamu.
4 Sasa, watu hao wasiomjua Mungu wanashangaa wanapoona kwamba
hamwandamani nao tena katika hali ya kuishi vibaya, na hivyo
wanawatukaneni.
5 Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu
aliye tayari kuwahukumu wazima na wafu!
6 Kwa sababu hiyo, hao waliokufa ambao walikuwa wamehukumiwa katika
maisha yao ya kimwili kama anavyohukumiwa kila mmoja, walihubiriwa
Habari Njema kusudi katika maisha yao ya kiroho waishi kama aishivyo
Mungu.

Uwakili mwema wa zawadi za Mungu

7 Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na
utaratibu na nidhamu, ili mweze kusali.
8 Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika
dhambi nyingi.
9 Muwe na ukarimu ninyi kwa ninyi bila kunung’unika.
10 Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa
faida ya wengine, kama vile uwakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu.
11 Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu;
anayetumika anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili
katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye
utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.

Kuteseka Kikristo

12 Wapenzi wangu, msishangae kuhusu majaribio makali mnayopata kana
kwamba mnapatwa na kitu kisicho cha kawaida.
13 Ila furahini kwamba mnashiriki mateso ya Kristo ili mweze kuwa na
furaha tele wakati utukufu wake utakapofunuliwa.
14 Heri yenu ikiwa mnatukanwa kwa sababu ya jina la Kristo; jambo
hilo lamaanisha kwamba Roho mtukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu
yetu.
15 Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa
sababu ni muuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
16 Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi asione
aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la
Kristo.

17 Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake
Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi mwisho wake
utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
18 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Ni vigumu kwa watu waadilifu kuokolewa;
itakuwaje basi kwa wasiomcha Mungu na wenye dhambi?”
\m
19 Kwa hiyo, wale wanaoteseka kufuatana na matakwa ya Mungu,
wanapaswa, kwa matendo yao mema, kujiweka chini ya Muumba wao ambaye ni
wa kuaminika kabisa.

Kundi la Mungu
\c 5

1 wazee! Mimi niliye mzee ninalo ombi moja kwenu wazee wenzangu. Mimi
mwenyewe nilishuhudia kwa macho yangu mateso ya Kristo na natumaini
kuushiriki ule utukufu utakaofunuliwa. Mimi nawaombeni
2 mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mlitunze si kwa
kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa
tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
3 Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali
muwe mfano kwa hilo kundi.
4 Na wakati Mchungaji Mkuu atakapotokea, ninyi mtapokea taji ya
utukufu isiyofifia.

5 Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya
wazee. Ninyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana
Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini
huwajalia neema wanyenyekevu.”
6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue
wakati ufaao.
7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka
kama simba angurumaye akitafuta mawindo.
9 Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote
duniani wanapatwa na mateso hayohayo.
10 Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote
na ambaye anawaiteni muushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana
na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na
msingi imara.
11 Kwake uwe uwezo milele! Amina.

Salamu za mwisho

12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu
ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba
jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.

13 Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni
wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
14 Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo.
Nawatakieni amani ninyi mlio wake Kristo.
\z

\id 2PE SW62.ALL 19-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PILI YA
                 PETRO

\h 2 PETRO
\c 1

1 Mimi Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia
ninyi ambao, kwa wema wake Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo, mmejaliwa
imani ileile ya thamani kuu tuliyojaliwa sisi.

2 Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu Bwana
wetu.

Mmeitwa na kuteuliwa na Mungu

3 Kwa uwezo wake wa kimungu, Mungu ametujalia mambo yote
tunayohitaji, ili tuishi maisha ya kumcha Mungu kwa kumjua yeye
aliyetuita tuushiriki utukufu na wema wake yeye mwenyewe.
4 Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo
alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya
zilizomo duniani, na mpate kuishiriki hali yake ya kimungu.
5 Kwa sababu hiyo, fanyeni bidii ya kuongeza fadhila katika imani
yenu: ongezeni elimu katika fadhila yenu,
6 kuwa na kiasi katika elimu yenu, uvumilivu katika kuwa na kiasi,
uchaji wa Mungu katika uvumilivu wenu,
7 udugu katika uchaji wenu, na mapendo katika udugu wenu.
8 Mkiwa na sifa hizo zote kwa wingi, zitawawezesheni kuwa watendaji
na kupata faida katika kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau
kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.

10 Kwa hiyo basi, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuufanya huo wito
wenu mlioitiwa na Mungu uwe jambo la kudumu katika maisha yenu; kama
mkiishi namna hiyo hamtaanguka kamwe.
11 Kwa namna hiyo mtafaulu kupewa haki kamili ya kuingia katika
Utawala wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

12 Kwa hiyo nitaendelea kuwakumbusheni daima mambo haya, ingawa
mmekwisha yafahamu, na mko imara katika ukweli mlioupokea.
13 Nadhani ni jambo jema kwangu, muda wote niishio hapa duniani,
kuwapeni moyo na kuwakumbusheni juu ya mambo haya.
14 Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama
Bwana alivyoniambia waziwazi.
15 Basi, nitajitahidi kuwapatieni njia ya kuyakumbuka mambo haya
kila wakati, baada ya kufariki kwangu.

Tuliuona utukufu wa Kristo

16 Wakati tulipowafundisheni juu ya ukuu wa kuja kwake Bwana wetu
Yesu Kristo, hatukutegemea hadithi tupu zisizo na msingi. Sisi tuliuona
utukufu wake kwa macho yetu wenyewe.
17 Sisi tulikuwapo wakati alipopewa heshima na kutukuzwa na Mungu
Baba, wakati sauti ilipomjia kutoka kwake yeye aliye Utukufu Mkuu,
ikisema: “Huyu ni Mwanangu mpenzi, nimependezwa naye.”
18 Tena, sisi wenyewe tulisikia sauti hiyo kutoka mbinguni wakati
tulipokuwa pamoja naye juu ya ule mlima mtakatifu.

19 Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi
mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali
penye giza mpaka Siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi
utakapong’ara mioyoni mwenu.
20 Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye
kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
21 Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu,
bali watu walinena ujumbe wa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Walimu wa uongo
\c 2

1 Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo walimu wa
uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na
kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla
maangamizi yao wenyewe.
2 Tena watu wengi watazifuata hizo njia zao mbaya, kwa sababu yao,
wengine wataipuuza Njia ya ukweli.
3 Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za
uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yu tayari, na Mwangamizi
wao yu macho!

4 Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa
katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea Siku ile ya Hukumu.
5 Mungu hakuihurumia dunia ya hapo kale, bali alileta gharika kuu
juu ya nchi ile ya watu wasiomcha Mungu; lakini Noa ambaye alihubiri
uadilifu, Mungu alimwokoa pamoja na watu wengine saba.
6 Mungu aliadhibu miji ya Sodoma na Gomora, akaiteketeza kwa moto,
akaifanya iwe mfano wa mambo yatakayowapata watu wasiomcha Mungu.
7 Alimwokoa Loti, mtu mwema, ambaye alisikitishwa sana na mwenendo
mbaya wa watu hao waasi.
8 Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake
ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
9 Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu
watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi Siku
ile ya hukumu,
10 hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka.
Watu hao ni washupavu na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu
viumbe vitukufu vya juu.
11 Lakini malaika, ambao wana uwezo na nguvu zaidi kuliko hao walimu
wa uongo, hawawashtaki na kuwatukana hao mbele ya Bwana.
12 Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na
wanyama wasio na akili, ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na
kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,
13 na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao
ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za
mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga
nanyi katika karamu zenu, bali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
14 Macho yao yamejaa uzinzi na uwezo wao wa kutenda dhambi hauna
kikomo. Huwaongoza watu walio dhaifu mpaka mitegoni. Mioyo yao imezoea
kuwa na tamaa ya mali. Wapo chini ya laana ya Mungu!
15 Wameiacha njia iliyonyoka, wakapotoka na kuifuata njia aliyofuata
Balaamu, mwana wa Beori, ambaye alipendelea kupata faida kwa kufanya
udanganyifu,
16 akakaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena
kwa sauti ya binadamu, akaukomesha wazimu wa huyo nabii.

17 Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu
yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza
kuu.
18 Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa
zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na
watu waishio katika udanganyifu.
19 Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni
watumwa wa upotovu–maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.
20 Watu waliokwisha ponyoka katika upotovu wa ulimwengu kwa kupata
kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kisha wakakubali kunaswa na
kutawaliwa tena na upotovu huo, hali yao itakuwa mbaya zaidi kuliko
awali.
21 Ingalikuwa afadhali kwao kama wasingalijua kamwe njia hiyo ya
uadilifu kuliko kujua na kisha kuiacha na kupoteza amri takatifu
waliyopokea.
22 Ipo mithali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,”
na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika
matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.

Siku ya Bwana
\c 3

1 Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua
hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa
kuwakumbusheni mambo haya.
2 Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa na manabii watakatifu, na ile
amri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa na mitume wenu.
3 Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao
mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki ninyi
4 na kusema: “Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi? Mambo ni
yaleyale tangu babu zetu walipokufa; hali ya vitu ni ileile kama
ilivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!”
5 Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo
mbingu na nchi zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji;
6 na kwa maji hayo, yaani yale maji ya gharika kuu, dunia ya wakati
ule iliangamizwa.
7 Lakini mbingu na nchi za sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa
ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya Siku ile ambapo
watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.
\fr 3:8
\f taz Zab 90:4

8 Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana,
hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja.
9 Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine
wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana
hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.

10 Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka
kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo
dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
11 Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je, ninyi mnapaswa
kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu,
12 mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi–Siku ambayo
mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili
vitayeyushwa kwa joto.
13 Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na
dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.

14 Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnangojea Siku ile, fanyeni bidii
kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
15 Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni
mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia
hekima aliyopewa na Mungu.
16 Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala
hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo
ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha
sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi
yao wenyewe.

17 Lakini ninyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe
na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka
katika msimamo wenu imara.
18 Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu
na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina.
\z

\id 1JN SW63.ALL 19/03/90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA KWANZA YA
                 YOHANE

\h 1 YOHANE
\c 1

Neno la uzima

1 Habari hii ya yahusu Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo. Sisi
tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na
kulishika kwa mikono yetu wenyewe.
2 Uzima huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na
kuwaambieni juu ya uzima huo wa milele uliokuwa kwa Baba na
uliodhihirishwa kwetu.
3 Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi pia ili
nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae
Yesu Kristo.
4 Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.

Mungu ni mwanga

5 Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo
hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.
6 Tukisema kwamba tuna umoja naye,na papo hapo twaishi gizani,
tutakuwa tumesema uongo kwa maneno na matendo.
7 Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga,
basi tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae,
inatutakasa dhambi zote.

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe na ukweli
haumo ndani yetu.
9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na
mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
10 Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu
mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.

\c 2

Kristo msaada wetu

1 Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi.
Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea
kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa.
2 Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu; wala si dhambi zetu sisi
tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.

3 Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba
tunamjua.
4 Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu
huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake.
5 Lakini mtu yeyote anayeshika neno la Mungu, huyo ndiye aliye na
upendo kamili wa Mungu ndani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na
hakika kwamba tunaungana naye:
6 mtu yeyote anayesema kwamba ameungana na Mungu, anapaswa kuishi
kama alivyoishi Yesu Kristo.

Amri mpya

7 Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri
ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule
ujumbe mliousikia.
8 Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli
wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza
linatoweka, na mwanga wa ukweli umekwisha anza kuangaza.

9 Yeyote asemaye kwamba yumo katika mwanga, lakini anamchukia ndugu
yake, mtu huyo bado yumo gizani.
10 Yeyote ampendaye ndugu yake, yuko katika mwanga, na hamna
chochote ndani yake kiwezacho kumkwaza mtu mwingine.
11 Lakini anayemchukia ndugu yake, yumo gizani; anatembea gizani, na
hajui anakokwenda, maana giza limempofusha.

12 Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa kuwa dhambi zenu zimeondolewa
kwa jina la Kristo.
13 Nawaandikieni ninyi kina baba kwani mnamjua yeye ambaye amekuwako
tangu mwanzo, Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mmemshinda yule
Mwovu.

14 Nawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mnamjua Baba.
Nawaandikieni ninyi kina baba, kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako
tangu mwanzo. Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la
Mungu limo ndani yenu na mmemshinda yule Mwovu.

15 Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu
anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.
16 Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona
watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki
kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.
17 Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita;
lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Adui wa Kristo

18 Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba adui wa Kristo
anakuja, na sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua
kwamba mwisho u karibu.
19 Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na
ndiyo maana walituacha; Kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi.
Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa
kamwe wa kwetu.

20 Ninyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na
hivyo mnaujua ukweli.
21 Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamuujui ukweli, bali kwa sababu
mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.

22 Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha. Mtu wa
namna hiyo ni adui wa Kristo–anamkana Baba na Mwana.
23 Maana yeyote anayemkana Mwana, anamkana pia Baba; na yeyote
anayemkubali Mwana, anampata Baba pia.

24 Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae mioyoni mwenu.
Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishi
daima katika umoja na Mwana na Baba.
25 Na ahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: uzima wa milele.

26 Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha
ninyi.
27 Lakini, kwa upande wenu ninyi, Kristo aliwamiminieni Roho wake.
Na kama akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu
yeyote. Maana Roho wake anawafundisheni kila kitu na mafundisho yake ni
ya kweli, si ya uongo. Basi shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki
katika muungano na Kristo.

28 Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe
hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu Siku ya kuja kwake.
29 Mnajua kwamba Kristo ni mwadilifu kabisa; basi, mnapaswa kujua
pia kwamba kila mtu atendaye mambo adili ni mtoto wa Mungu.

\c 3

Watoto wa Mungu

1 Oneni basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa
Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi,
kwani haumjui Mungu.
2 Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa, lakini bado
haijaonekana wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba wakati
Kristo atakapotokea, tutafanana naye kwani tutamwona vile alivyo.
3 Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi
kama vile Kristo alivyo safi kabisa.

4 Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni
uvunjaji wa sheria.
5 Mnajua kwamba Kristo alikuja kuziondoa dhambi zetu, na kwamba
kwake hamna dhambi yoyote.
6 Basi, kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi dhambi;
lakini kila mtu atendaye dhambi hakupata kamwe kumwona, wala kumjua
Kristo.
7 Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu
atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo
mwadilifu kabisa.
8 Lakini atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maana Ibilisi ametenda
dhambi tangu mwanzo. Lakini Mwana wa Mungu alikuja duniani kuiharibu
kazi ya Ibilisi.

9 Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya
kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa
Mungu.
10 Lakini yeyote asiyetenda mambo maadilifu, au asiyempenda ndugu
yake, huyo si mtoto wa Mungu. Hiyo ndiyo tofauti iliyoko kati ya watoto
wa Mungu na watoto wa Ibilisi.

Pendaneni

11 Na, ujumbe mliousikia tangu mwanzo ndio huu: Tunapaswa kupendana!
12 Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua
ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa
maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!

13 Basi, ndugu zangu, msishangae kama ulimwengu unawachukia ninyi.
14 Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia
katika uzima kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo
hubaki katika kifo.
15 Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba
muuaji yeyote yule hana uzima wa milele ndani yake.
16 Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha
yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa
ajili ya ndugu zetu.
17 Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu
yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma,
anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu?
18 Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa
kweli na wa vitendo.

Uthabiti wetu mbele ya Mungu

19 Hivyo ndivyo tuwezavyo kuwa na hakika kwamba sisi ni watu wa
ukweli; na hatutakuwa na wasiwasi mbele ya Mungu.
20 Kwa maana, hata kama dhamiri yetu yatuhukumu, twajua kwamba Mungu
ni mkuu zaidi kuliko dhamiri, na kwamba yeye ajua kila kitu.
21 Wapenzi wangu, kama dhamiri yetu haina lawama juu yetu, basi,
twaweza kuwa na uthabiti mbele ya Mungu,
22 na twaweza kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii
amri zake na kufanya yale yanayompendeza.
23 Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Kristo, na kupendana
kama alivyotuamuru.
24 Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na
Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu
ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.

\c 4

Roho wa kweli na wa uongo

1 Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa
Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa
Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni.
2 Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu: Kila
anayekiri kwamba Kristo alikuja, akawa binadamu, mtu huyo anaye Roho wa
Mungu.
3 Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye
kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyi
mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili
ulimwenguni!

4 Lakini ninyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao
manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu zaidi kuliko
roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu.
5 Wao husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani
wao ni wa ulimwengu.
6 Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu
asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua
tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo.

Mungu ni upendo

7 Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu
aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.
8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo.
9 Na Mungu alionyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee
ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake.
10 Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda
Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae awe
sadaka ya kutuondolea dhambi zetu.

11 Wapenzi wangu, ikiwa Mungu alitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswa
kupendana.
12 Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana
Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani
yetu.

13 Tunajua kwamba tunaishi katika umoja na Mungu, naye Mungu anaishi
katika umoja nasi, kwani yeye ametupa Roho wake.
14 Sisi tumeona na kuwaambia wengine kwamba Baba alimtuma Mwanae awe
Mwokozi wa ulimwengu.
15 Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi
katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu.
16 Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi.
Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika
muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye.
17 Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri Siku
ile ya Hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo.
18 Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza uoga
wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga
huhusikana na adhabu.

19 Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
20 Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake,
huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi
kumpenda Mungu ambaye hamwoni.
21 Basi, hii ndiyo amri aliyotupa Kristo: Anayempenda Mungu anapaswa
pia kumpenda ndugu yake.

\c 5

Tumeushinda ulimwengu

1 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu;
na, anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.
2 Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: Kwa
kumpenda Mungu na kuzitii amri zake;
3 maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu,
4 maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi
ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: kwa imani yetu.
5 Nani, basi, awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yule anayeamini kwamba
Yesu ni Mwana wa Mungu.

Ushahidi juu ya Kristo

6 Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu
ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho
anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli.
7 Basi, wako mashahidi watatu:
8 Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana.
9 Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito
zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae.
10 Anayemwamini mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini
asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi
alioutoa Mungu juu ya Mwanae.
11 Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uzima wa milele,
na uzima huo uko kwa Bwana.
12 Yeyote, aliye na Mwana wa Mungu anao uzima huo; asiye na Mwana wa
Mungu, hana uzima.

Uzima wa milele

13 Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uzima wa milele ninyi
mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu.
14 Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba
tukimwomba chochote kadiri ya mapenzi yake, yeye hutusikiliza.
15 Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba
yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba atupatia yote
tunayomwomba.

16 Mtu akimwona ndugu yake ametenda dhambi isiyompeleka kwenye kifo
anapaswa kumwombea kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Nasema jambo
hili kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi
yenye kumpeleka mtu kwenye kifo nami sisemi kwamba mnapaswa kumwomba
Mungu kwa ajili ya hiyo.

17 Kila tendo lisilo adilifu ni dhambi, lakini kuna dhambi
isiyompeleka mtu kwenye kifo.

18 Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa
sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru.

19 Tunajua kwamba sisi ni wake Mungu ingawa ulimwengu wote
unatawaliwa na yule Mwovu.

20 Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili
tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli–katika
muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio
uzima wa milele.

21 Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu.
\z

\id 2JN SW64.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PILI YA
                 YOHANE

\h 2 YOHANE
\c 1

1 Mimi Mzee nakuandikia wewe Bimkubwa mteule, pamoja na watoto wako
ninaowapenda kweli. Wala si mimi tu ninayewapenda, bali pia wote
wanaoujua ule ukweli wanawapenda ninyi,
2 kwa sababu ukweli unakaa nasi milele.

3 Neema na huruma na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu
Kristo, Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika ukweli na upendo.

Ukweli na upendo

4 Nilifurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanaishi katika
ukweli kama Baba alivyotuamuru.
5 Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hili si
amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.
6 Upendo maana yake ni kuishi kwa kuzitii amri zake Mungu. Amri
niliyoisikia tangu mwanzo ndiyo hii: mnapaswa nyote kuishi katika
upendo.

7 Wadanganyifu wengi wamezuka duniani, watu ambao hawakiri kwamba
Yesu Kristo amekuja kwetu akawa binadamu. Mtu asemaye hivyo ni
mdanganyifu na ni Adui wa Kristo.
8 Basi, jihadharini ninyi wenyewe ili msije mkapoteza kile
mlichokishugulikia, bali mpate tuzo lenu kamili.

9 Asiyezingatia na kudumu katika mafundisho ya Kristo, bali
anayakiuka, hana Mungu. Lakini anayedumu katika mafundisho hayo anaye
Baba na Mwana.
10 Basi, kama mtu akija kwenu bila kuwaleteeni mafundisho hayo,
msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu.
11 Maana anayemsalimu mtu huyo, anashirikiana naye katika matendo
yake maovu.

Hatima

12 Ninayo mengi ya kuwaambieni lakini sipendi kufanya hivyo kwa
karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza
nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
13 Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu.
\z

\id 3JN SW65.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT
\h 3 YOHANE

          BARUA YA TATU YA
                 YOHANE

\c 1

1 Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, rafiki yangu, ninayekupenda kweli.

2 Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia
afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni.
3 Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakaiambia juu ya
uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
4 Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto
wangu wanaishi katika ukweli.

Uaminifu wa Gayo

5 Mpenzi wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu,
hata kama ni wageni.
6 Ndugu hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali
uwasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu,
7 Maana wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea
msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini.
8 Basi, sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate
kushiriki katika kazi yao kwa ajili ya ukweli.

Diotrefe na Demetrio

9 Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye
hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
10 Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno
mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa
kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine
wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuzia nje ya kanisa.

11 Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila
atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona
Mungu.

12 Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi
pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni
kweli.

Salamu za mwisho

13 Ninayo bado mengi ya kukwambia, lakini sipendi kuyaandika kwa
kalamu na wino.
14 Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.

15 Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu
wote kila mmoja binafsi.
\z

\id JUD SW66.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT
\h YUDA

          BARUA YA
                 YUDA

\c 1

1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia
ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na
katika ulinzi wa Yesu Kristo.

2 Nawatakieni huruma, amani na upendo kwa wingi.

Walimu wa uongo

3 Ndugu wapenzi, wakati nimo katika jitihada ya kuwaandikieni juu ya
ule wokovu tunaoshiriki sote, nimeona lazima ya kuwaandikieni na
kuwahimizeni mwendelee kupigana kwa ajili ya imani ambayo Mungu
amewajalia watu wake mara moja tu kwa wakati wote.
4 Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni
mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe
wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake kiongozi
na Bwana wetu. Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu awali hukumu
inayowangojea watu hao.

5 Nataka kuwakumbusheni mambo fulani ambayo mmekwisha yajua:
kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika
nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
6 Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao
ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe
Siku ile kuu.
7 Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake;
wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo
yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo
kwa watu wote.

8 Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. ndoto zao huwaongoza katika
kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana
viumbe vitukufu vya huko juu.
9 Hata Mikaeli, malaika mkuu, hakufanya hivyo. Katika ule ubishi
kati yake na Ibilisi waliobishana juu ya mwili wa Mose, Mikaeli
hakuthubutu kumhukumu Ibilisi kwa matusi; ila alisema: “Bwana mwenyewe
na akukaripie.”
10 Lakini watu hawa hutukana chochote wasichokielewa; mambo yaleyale
wanayoyajua kwa silika kama vile wanyama wanayoyajua ndiyo
yanayowaangamiza.
11 Ole wao! Watu hao wamefuata mwenendo uleule wa Kaini. Kwa ajili
ya fedha, wamejiingiza katika mkosi uleule wa Baalamu. Wameasi kama Kora
alivyoasi na wameangamizwa kama yeye alivyoangamizwa.
12 Kwa makelele yao yasiyo na adabu, watu hao ni kama madoa machafu
katika mikutano yenu ya karamu ya Bwana. Hujipendelea wao wenyewe tu, na
wako kama mawingu yanayopeperushwa huko na huko na upepo bila ya kuleta
mvua. Wao ni kama miti isiyozaa matunda hata wakati wa majira yake,
wamekufa kabisa.
13 Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu
yanaonekana dhahiri kama vile mapovu ya mawimbi. Wao ni kama nyota
zinazotangatanga, ambao Mungu amewawekea mahali pao milele katika giza
kuu.

14 Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu
ya watu hawa: “Sikilizeni! Bwana atakuja pamoja na maelfu ya malaika
wake watakatifu
15 kutoa hukumu juu ya binadamu wote, kuwahukumu wote kwa ajili ya
matendo yao yote maovu waliyotenda na kwa ajili ya maneno yote mabaya
ambayo watu waovu walimkashifu nayo.”

16 Watu hawa wananung’unika daima na kuwalaumu watu wengine. Hufuata
tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kusudi wafaulu
katika mipango yao.

Maonyo na maagizo

17 Lakini ninyi wapenzi wangu, kumbukeni yale mliyoambiwa hapo awali
ni mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo.
18 Waliwaambieni: “Siku za mwisho zitakapofika, watatokea watu
watakaowadhihaki ninyi, watu wafuatao tamaa zao mbaya.”
19 Hao ndio watu wanaosababisha mafarakano, watu wanaotawaliwa na
tamaa zao za kidunia, watu wasio na Roho wa Mungu.
20 Lakini ninyi, wapenzi wangu, endeleeni kujijenga kikamilifu
katika imani yenu takatifu. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
21 na kubaki katika upendo wa Mungu, mkiwa mnamngojea Bwana wetu
Yesu Kristo awapeni uzima wa milele kwa huruma yake.

22 Muwe na huruma kwa watu walio na mashaka;
23 waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni; na kwa wengine muwe na
huruma pamoja na hofu, lakini chukieni hata mavazi yao ambayo
yamechafuliwa na tamaa zao mbaya.

Sala ya sifa

24 Kwake yeye awezaye kuwalinda msije mkaanguka, na kuwaleta ninyi
bila hatia mpaka mbele ya utukufu wake,
25 kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu,
ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote,
sasa na hata milele! Amina.