\h LUKA

          INJILI KAMA ILIVYOANDIKWA NA
                 LUKA

\c 1

1 Mheshimiwa Theofilo:
Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati
yetu.
2 Waliandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona kwa macho yao
tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo.
3 Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo
yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango,
4 ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale
uliyofundishwa.

Kuzaliwa kwa Yohane kunatangazwa

5 Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja
jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa
Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni.
6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata
amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.
7 Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa,
nao wote wawili walikuwa wazee sana.

8 Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya
Mungu,
9 Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia
hekaluni ili afukize ubani.
10 Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati
huo wa kufukiza ubani.
11 Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia
wa madhabahu ya kufukizia ubani.
12 Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
13 Lakini malaika akamwambia, “Zakariya, usiogope, kwa maana sala
yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe
utampa jina Yohane.
14 Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya
kuzaliwa kwake.
15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana.

Hatakunywa divai wala kileo,
atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.

16 Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao.

17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya.

Atawapatanisha kina baba na watoto wao;
atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu,
na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”

18 Zakariya akamwambia huyo malaika, “Ni kitu gani
kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke
wangu.”
19 Malaika akamjibu, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu,
na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema.
20 Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno
yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia
yatakapotimia.”

21 Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku
wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni.
22 Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba
alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono,
akabaki bubu.

23 Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani.
24 Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa
muda wa miezi mitano, akisema:
25 “Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea
aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu.”

Kuzaliwa kwa Yesu kunatangazwa

26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende
kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya,
27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake
Yosefu, wa ukoo wa Daudi.
28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema
nyingi! Bwana yu pamoja nawe.”

29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno
haya yanamaanisha nini?
30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia
neema.
31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu.

32 Yeye atakuwa mkuu

na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu.
Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.

33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele,

na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”

34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?”
35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake
Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa
ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.
36 Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba
ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu
walimfahamu kuwa tasa.
37 Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu.”
38 Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama
ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.

Maria anamtembelea Elisabeti

39 Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka
hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yuda.
40 Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti.
41 Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga
tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho
Mtakatifiu,
42 akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye
utakayemzaa amebarikiwa.
43 Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
44 Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni
mwangu aliruka kwa furaha.
45 Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana
aliyokwambia.”

Utenzi wa Maria
\m
46 Naye Maria akasema,

47 “Moyo wangu wamtukuza Bwana,

roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.

48 Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu.

Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.

49 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu,

jina lake ni takatifu.

50 Huruma yake kwa watu wanaomcha

hudumu kizazi hata kizazi.

51 Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:

amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52 amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi,

akawakweza wanyenyekevu.

53 Wenye njaa amewashibisha mema,

matajiri amewaacha waende mikono mitupu.

54 Amemsaidia Israeli mtumishi wake,

akikumbuka huruma yake.

55 Kama alivyowaahidia wazee wetu

Abrahamu na wazawa wake hata milele.”

56 Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu
akarudi nyumbani kwake.

Kuzaliwa kwa Yohane mbatizaji

57 Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto
wa kiume.
58 Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana
amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.

59 Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina
la baba yake, Zakariya.
60 Lakini mama yake akasema, “La, sivyo, bali ataitwa Yohane.”
61 Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina
hilo?”
62 Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake
apewe jina gani.
63 Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo
jina lake.” Wote wakastaajabu.
64 Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa
anaongea akimsifu Mungu.
65 Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali
katika milima ya Yudea.
66 Wote waliosikia mambo hayo waliyatafakari mioyoni mwao wakisema:
“Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika nguvu ya Bwana
ilikuwa pamoja naye.

Utenzi wa Zakariya

67 Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka
ujumbe wa Mungu:

68 “Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli,

kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake.

69 Ametupatia Mwokozi shujaa,

mzawa wa Daudi mtumishi wake.

70 Aliahidi hapo kale

kwa njia ya manabii wake watakatifu,

71 kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu

na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.

72 Alisema atawahurumia wazee wetu,

na kukumbuka agano lake takatifu.

73 Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu,

ni kwamba atatujalia sisi

74 tukombolewe kutoka adui zetu,

tupate kumtumikia bila hofu,

75 kwa unyofu na uadilifu mbele yake,

siku zote za maisha yetu.

76 Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu,

utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;

77 kuwatangazia watu kwamba wataokolewa

kwa kuondolewa dhambi zao.

78 Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.

Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu,

79 na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo,

aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”

80 Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka
alipojionyesha rasmi kwa watu wa Israeli.

\c 2

Yesu anazaliwa
\r
\is (Mat. 1:18-25)
\ie

1 Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka
watu wote chini ya utawala wake wajiandikishe.
2 Kuandikishwa huku kulikuwa mara ya kwanza, wakati Kirenio
alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria.
3 Basi, wote waliohusika walikwenda kujiandikisha, kila mtu katika
mji wake.

4 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya.
Kwa kuwa alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi alikwenda mjini Bethlehemu
mkoani Yuda alikozaliwa Mfalme Daudi.
5 Alikwenda kujiandikisha pamoja na mchumba wake Maria ambaye
alikuwa mja mzito.
6 Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,
7 akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za
kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya
wageni.

Wachungaji na malaika

8 Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani
kulinda mifugo yao.
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana
ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
10 Malaika akawaambia, “Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya
furaha kuu kwa watu wote.
11 Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa
ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.
12 Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkuta mtoto mchanga
amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini.”

13 Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika,
wakamsifu Mungu wakisema:

14 “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni,

na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!”

15 Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji
wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio
hili Bwana alilotujulisha.”

16 Basi, wakaenda mbio, wakamkuta Maria na Yosefu na yule mtoto
mchanga amelazwa horini.
17 Hao wachungaji walipomwona mtoto huyo wakawajulisha wote habari
waliyokuwa wamesikia juu yake.
18 Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na
wachungaji.
19 Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni
mwake.
20 Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu
kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa
wameambiwa.

Mtoto anapewa jina

21 Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa
jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa
mimba.

Yesu anawekwa mbele ya Bwana

22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa
na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye
Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana.
23 Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa
kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.”
24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya
njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana.

25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha
Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa
Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.
26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya
kumwona Masiha wa Bwana.
27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na
wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama
ilivyotakiwa na Sheria,
28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu
na kusema:

29 “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako,

waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani.

30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako,

31 ambao umeutayarisha mbele ya watu wote:

32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa,

na utukufu kwa watu wako Israeli.”

33 Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema
Simeoni juu ya mtoto.
34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu
atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye
atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe,
uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako.”

36 Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti
Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba
tangu alipoolewa.
37 Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka
themanini na minne. Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali
usiku na mchana.
38 Saa hiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na akaeleza
habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa
Yerusalemu.

Kurudi Nazareti

39 Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya
Bwana, walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya.
40 Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya
Mungu ilikuwa pamoja naye.

Mtoto Yesu Hekaluni

41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila
mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka.
42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda
kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi.
43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu
alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari.
44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa
kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta.

46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na
kuwauliza maswali.
47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu
yake ya hekima.
48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake,
akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi
tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.”
49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa
kuwa katika nyumba ya Baba yangu?”
50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia.

51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake
akaweka mambo hayo yote moyoni mwake.
52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi
kupendwa na Mungu na watu.

\c 3

Mahubiri ya Yohane mbatizaji
\r
\is (Mat. 3:1-12; Marko 1:1-8; Yoh. 1:19-28)
\ie

1 Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato
alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa
Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na
Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
2 na Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati
huo ndipo neno la Mungu lilipomjia Yohane, mwana wa Zakariya, kule
jangwani.
3 Basi, Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto
Yordani, akihubiri watu watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
4 Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Sauti ya mtu imesikika jangwani:
<Mtayarishieni Bwana njia yake;
nyosheni mapito yake.

5 Kila bonde litafukiwa,

kila mlima na kilima vitasawazishwa;
palipopindika patanyooshwa,
njia mbaya zitatengenezwa.

6 Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu.”>

7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize:
“Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka
ghadhabu inayokuja?
8 Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema:
<Sisi ni watoto wa Abrahamu.> Nawaambieni hakika, Mungu anaweza
kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
9 Lakini, sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti.
Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.”

10 Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi?”
11 Akawajibu, “Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo;
aliye na chakula afanye vivyo hivyo.”
12 Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza,
“Mwalimu, tufanye nini?”
13 Naye akawaambia, “Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.”
14 Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu,
“Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa
uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”

15 Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza
mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini
anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia
kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria
nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi
ayachome kwa moto usiozimika.”

18 Hivyo, pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu
akiwahubiria Habari Njema.
19 Lakini Yohane alimgombeza Herode, mkuu wa mkoa, kwa sababu
alikuwa amemchukua Herodia, mke wa ndugu yake, na kumfanya mke wake; na
pia kwa ajili ya mabaya yote aliyokuwa amefanya.
20 Kisha Herode akazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohane gerezani.

Yesu anabatizwa
\r
\is (Mat. 3:13-17; Marko 1:9-11)
\ie

21 Watu wote walipokuwa wamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Na
alipokuwa akisali, mbingu zilifunguka,
22 na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti
ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa
nawe.”
\fr 3:22
\f Taz Zab 2:7

Ukoo wa Yesu
\r
\is (Mat. 1:17)
\ie

23 Yesu alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka
thelathini, na watu walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
24 Heli alikuwa mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki,
mwana wa Yanai, mwana wa Yosefu,
25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa
Hesli, mwana wa Nagai,
26 mwana wa Maathi, mwana wa Matathia, mwana wa Shemeni, mwana wa
Yoseki, mwana wa Yuda,
27 mwana wa Yohanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa
Shealtieli, mwana wa Neri,
28 mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu,
mwana wa Eri,
29 mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa
Mathati, mwana wa Lawi,
30 mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu, mwana wa
Yonamu, mwana wa Eliakimu,
31 mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa
Nathani, mwana wa Daudi,
32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni,
mwana wa Nashoni,
33 mwana wa Aminadabu, mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana wa
Hesroni, mwana wa Feresi, mwana wa Yuda,
34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Abrahamu, mwana wa
Tera, mwana wa Nahori,
35 mwana wa Serugi, mwana wa Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi,
mwana wa Sala,
36 mwana wa Kainani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa
Noa, mwana wa Lameki,
37 mwana wa Mathusala, mwana wa Henoki, mwana wa Yaredi, mwana wa
Mahalaleli, mwana wa Kenani,
38 mwana wa Enosi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, aliyekuwa wa
Mungu.

\c 4

Yesu anajaribiwa
\r
\is (Mat. 4:1-11; Marko 1:12-13)
\ie

1 Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu,
akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
2 Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo
wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.
3 Ndipo Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru
jiwe hili liwe mkate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: <Mtu haishi kwa mkate tu.”>

5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara
moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
6 “Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana
nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.”
8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa:

<Utamwabudu Bwana Mungu wako,
na utamtumikia yeye peke yake.”>

9 Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu,
akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu,
10 kwa maana imeandikwa:

<Atawaamuru malaika wake wakulinde,>
\m
11 na tena,

<Watakuchukua mikononi mwao
usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.”>

12 Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa:

<Usimjaribu Bwana Mungu wako.”>

13 Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
\fr 4:10
\f Taz Zab 91:11
\fr 4:11
\f Taz Zab 91:12

Yesu anaanza kazi yake Galilaya
\r
\is (Mat. 4:12-17; Marko 1:14-15)
\ie

14 Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na
habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
15 Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na
wote.

Yesu anakataliwa huko Nazareti
\r
\is (Mat. 13:53-58; Marko 6:1-6)
\ie

16 Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya
Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake.
Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti.
17 Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali
palipoandikwa:

18 “Roho wa Bwana yu juu yangu,

kwani amenipaka mafuta
niwahubirie maskini Habari Njema.
Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru,
vipofu watapata kuona tena;
amenituma niwakomboe wanaoonewa,

19 na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana.”

20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha
akaketi; watu wote wakamkodolea macho.
21 Naye akaanza kuwaambia, “Andiko hili mlilosikia likisomwa,
limetimia leo.”
22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema.
Wakanena, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

23 Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: <Mganga
jiponye mwenyewe>, na pia mtasema: <Yote tuliyosikia umeyafanya kule
Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako.”>
24 Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika
kijiji chake.
25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya
Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa
miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
26 Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke
mjane wa Sarepta, Sidoni.
27 Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye
ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani,
mwenyeji wa Siria.”
28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika
sana.
29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya
kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe
chini.
30 Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.

Mtu mwenye pepo mchafu
\r
\is (Marko 1:21-28)
\ie

31 Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya,
akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.
32 Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.
33 Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na
roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:
34 “We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja
kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa
Mungu!”
35 Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: “Nyamaza! Mtoke mtu
huyu!” Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka
bila kumdhuru hata kidogo.
36 Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, “Hili ni jambo la
ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao
wanatoka!”
37 Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.

Yesu anawaponya watu wengi
\r
\is (Mat. 8:14-17; Marko 1:29-34)
\ie

38 Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni.
Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.
39 Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo
ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.
40 Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali
waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao,
akawaponya wote.
41 Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: “Wewe u
Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema,
maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.

Yesu anahubiri huko Yudea
\r
\is (Marko 1:35-39)
\ie

42 Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu
wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia
ili asiondoke kwao.
43 Lakini yeye akawaambia, “Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za
Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili
hiyo.”
44 Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea.

\c 5

Yesu anawaita wanafunzi wa kwanza
\r
\is (Mat. 4:18-22; Marko 1:16-20)
\ie

1 Siku moja Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu
wengi walikuwa wamemzunguka wakisongana wanalisikiliza neno la Mungu.
2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa; wavuvi wenyewe walikuwa
wametoka, wanaosha nyavu zao.
3 Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni,
alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa.
Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.

4 Alipomaliza kufundisha, akamwambia Simoni, “Peleka mashua mpaka
kilindini, mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki.”
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usiku kucha
bila kupata kitu, lakini kwa kuwa umesema, nitatupa nyavu.”
6 Baada ya kufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hata nyavu zao
zikaanza kukatika.
7 Wakawaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine waje kuwasaidia.
Wakaja, wakazijaza mashua zote mbili samaki, hata karibu zingezama.

8 Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema,
“Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!”
9 Simoni pamoja na wenzake wote walishangaa kwa kupata samaki wengi
vile.
10 Hali kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa
wavuvi wenzake Simoni. Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa
utakuwa ukivua watu.”
11 Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha
yote, wakamfuata.

Yesu anamtakasa mwenye ukoma
\r
\is (Mat. 8:1-4; Marko 1:40-45)
\ie

12 Ikawa, Yesu alipokuwa katika mmojawapo wa miji ya huko, mtu mmoja
mwenye ukoma mwili mzima akamwona. Basi, mtu huyo akaanguka kifudifudi
akamwomba Yesu: “Mheshimiwa, ukitaka, waweza kunitakasa.”

13 Yesu akaunyosha mkono wake, akamgusa na kusema, “Nataka,
takasika!” Mara ule ukoma ukamwacha.
14 Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajionyeshe
kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama
inavyotakiwa na Sheria ya Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona.”

15 Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi
mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
16 Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali
huko.

Yesu anamponya mtu aliyepooza
\r
\is Mat. 9:1-8; Marko 2:1-12
\ie

17 Siku moja Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na walimu wa
Sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu,
walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya
kuponyea wagonjwa.
18 Mara watu wakaja wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala
kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani wamweke mbele ya Yesu.
19 Lakini kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani.
Basi, wakapanda juu ya dari, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo
aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
20 Yesu alipoona jinsi walivyokuwa na imani kubwa, akamwambia huyo
mtu, “Rafiki, umesamehewa dhambi zako.”

21 Walimu wa Sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu
anayemkufuru Mungu kwa maneno yake? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi
ila Mungu peke yake!”
22 Yesu alitambua mawazo yao, akawauliza, “Mnawaza nini mioyoni
mwenu?
23 Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, <Umesamehewa dhambi,> au
kusema, <Simama utembee>?
24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kusamehe
dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua
kitanda chako uende zako nyumbani.”
25 Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua
kitanda chake akaenda zake nyumbani huku akimtukuza Mungu.
26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema:
“Tumeona maajabu leo.”

Lawi anaitwa kuwa mfuasi
\r
\is (Mat. 9:9-13; Marko 2:13-17)
\ie

27 Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtoza ushuru mmoja
aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, “Nifuate!”
28 Lawi akaacha yote, akamfuata.

29 Kisha Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake; na
kundi kubwa la watoza ushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja
nao.
30 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakawanung’unikia wafuasi wake
wakisema: “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye
dhambi?”
31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini
wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.
32 Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, ili wapate kutubu.”

Suala juu ya kufunga
\r
\is (Mat. 9:14-17; Marko 2:18-22)
\ie

33 Watu wengine wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohane mbatizaji
hufunga mara nyingi na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo
hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
34 Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwataka wale walioalikwa arusini
wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao?
35 Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao, na
wakati huo ndipo watakapofunga.”

36 Yesu akawaambia mfano huu: “Hakuna mtu akataye kiraka cha nguo
mpya na kukitia katika vazi kuukuu; kama akifanya hivyo, atakuwa
amelikata hilo vazi jipya, na hicho kiraka hakitachukuana na hilo vazi
kuukuu.
37 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; kwani
hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, divai itamwagika, na viriba
vitaharibika.
38 Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!
39 Wala hakuna mtu ambaye hutamani kunywa divai mpya baada ya kunywa
ya zamani, kwani husema: <Ile ya zamani ni nzuri zaidi.”>

\c 6

Suala juu ya siku ya Sabato
\r
\is (Mat. 12:1-8; Marko 2:23-28)
\ie

1 Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano,
na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje
zake kwa mikono, wakala.
2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya jambo ambalo si
halali siku ya Sabato?”
3 Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na
wenzake wakati walipokuwa na njaa?
4 Yeye aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate
iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, ni
makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kula mikate hiyo.”
5 Hivyo akawaambia, “Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato.”

Mtu mwenye mkono uliopooza
\r
\is (Mat. 12:9-14; Marko 3:1-16)
\ie

6 Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia katika sunagogi,
akafundisha. Mle ndani mlikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa
umepooza.
7 Walimu wa Sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisingizio cha
kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku
ya Sabato.
8 Lakini Yesu alijua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono
uliopooza, “Inuka, simama katikati.” Yule mtu akaenda akasimama
katikati.
9 Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato
kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au
kuyaangamiza?”
10 Baada ya kuwatazama wote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu,
“Nyosha mkono wako.” Naye akafanya hivyo, na mkono wake ukawa mzima
tena.
11 Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea
Yesu maovu.

Yesu anawateua mitume kumi na wawili
\r
\is (Mat. 10:1-4; Marko 3:13-19)
\ie

12 Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku
kucha akimwomba Mungu.
13 Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akachagua
kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
14 Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake,
Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo,
15 Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zelote),
16 Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.

Yesu anafundisha na kuponya watu
\r
\is (Mat. 4:23-25)
\ie

17 Baada ya kushuka mlimani pamoja na mitume, Yesu alisimama mahali
palipokuwa tambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na
umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya
Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
18 Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu.
19 Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani
yake na kuwaponya wote.

Heri na ole
\r
\is (Mat. 5:1-12)
\ie

20 Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema:

“Heri ninyi mlio maskini,
maana Ufalme wa Mungu ni wenu.

21 Heri ninyi mnaosikia njaa sasa,

maana baadaye mtashiba.
Heri ninyi mnaolia sasa,
maana baadaye mtacheka kwa furaha.

22 “Heri yenu ninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga,
watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu!
23 Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo
lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo
hivyo.

24 Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri,

maana mmekwisha pata faraja yenu.

25 Ole wenu ninyi mnaoshiba sasa,

maana baadaye mtasikia njaa.
Ole wenu ninyi mnaocheka kwa furaha sasa,
maana baadaye mtaomboleza na kulia.

26 Ole wenu ninyi iwapo watu wote wanawasifu,

maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.

Kuwapenda maadui
\r
\is (Mat. 5:38-48; 7:12a)
\ie

27 “Lakini nawaambieni ninyi mnaonisikiliza: wapendeni adui zenu,
watendeeni mema wale wanaowachukieni.
28 Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale
wanaowatendea vibaya.
29 Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang’anya
koti lako mwachie pia shati lako.
30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang’anya mali yako usimtake
akurudishie.
31 Watendeeni wengine kama mnavyotaka wawatendee ninyi.

32 “Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je, mtapata
tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale
wanaowapenda wao.
33 Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata
tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo!
34 Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je,
mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili
warudishiwe kima kilekile!
35 Ila nyinyi wapendeni adui zenu, na kuwatendea mema; kopesheni
bila kutazamia malipo, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto
wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani
na walio wabaya.
36 Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.

Kuwahukumu wengine
\r
\is (Mat. 7:1-5)
\ie

37 “Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine,
nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
38 Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea
mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata
kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho
ambacho Mungu atatumia kwenu.”

39 Akawaambia mfano huu: “Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu
mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni.
40 Mwanafunzi hamshindi mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha
hitimu huwa kama mwalimu wake.
41 Unawezaje kukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwenzio, usione
boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe?
42 Au, unawezaje kumwambia mwenzako, <Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi
katika jicho lako,> na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako
mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na
hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika
jicho la ndugu yako.

Mti hujulikana kwa matunda yake
\r
\is (Mat. 7:17-20; 12:34b-35)
\ie

43 “Mti mwema hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda
mazuri.
44 Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu
hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
45 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyo
moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya katika hazina mbaya iliyo
moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni
mwake.

Wajenzi wa namna mbili
\r
\is (Mat. 7:24-27)
\ie

46 “Mbona mwaniita <Bwana, Bwana,> na huku hamtimizi yale
ninayosema?
47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonyesha alivyo yeyote yule anayekuja
kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:
48 Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na
kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa
maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa
imejengwa imara.
49 Lakini yeyote anayesikia maneno yangu lakini asifanye chochote,
huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi.
Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka
na kuharibika kabisa!”

\c 7

Yesu anamponya mtumishi wa Jemadari
\r
\is (Mat. 8:5-13; Yoh. 4:43-54)
\ie

1 Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda
Kafarnaumu.
2 Huko kulikuwa na jemadari mmoja Mroma ambaye alikuwa na mtumishi
wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu kufa.
3 Yule jemadari aliposikia habari za Yesu, aliwatuma wazee fulani
Wayahudi waende kumwomba aje amponye mtumishi wake.
4 Walipofika kwa Yesu, walimsihi sana, wakasema: “Huyu anastahili
afanyiwe jambo hilo,
5 maana analipenda taifa letu, na ndiye aliyetujengea lile
sunagogi.”
6 Basi, Yesu akaenda pamoja nao. Alipokuwa karibu kufika nyumbani
kwa yule jemadari Mroma, yule jemadari aliwatuma marafiki zake wamwambie
Yesu: “Bwana, usijisumbue zaidi, maana mimi sistahili uingie nyumbani
mwangu.
7 Ndio maana sikujiona nastahili hata kuja kwako; amuru tu, na
mtumishi wangu atapona.
8 Mimi pia ni mtu niliye chini ya mamlaka, na ninao askari chini
yangu. Namwambia mmoja, <Nenda!>, naye huenda; namwambia mwingine,
<Njoo!> naye huja; na nikimwambia mtumishi wangu, <Fanya hiki!>,
hufanya.”

9 Yesu aliposikia hayo, alishangaa; halafu akauelekea ule umati wa
watu uliokuwa unamfuata, akasema, “Sijaona imani kubwa namna hii hata
katika Israeli.”
10 Wale watu walipowasili nyumbani walimkuta yule mtumishi hajambo
kabisa.

Yesu anamfufua mtoto wa mama mjane

11 Baadaye kidogo Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na
wafuasi wake pamoja na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
12 Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba
maiti ya kijana mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji
ule walikuwa pamoja na huyo mama.
13 Bwana alipomwona mama huyo, alimwonea huruma, akamwambia,
“Usilie.”
14 Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa
wanalichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
15 Yule aliyekufa akaketi, akaanza kuongea. Na Yesu akamkabidhi kwa
mama yake.
16 Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema:
“Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”
17 Habari hizo zikaenea kote katika Uyahudi na katika nchi za
jirani.

Wajumbe kutoka kwa Yohane mbatizaji
\r
\is (Mat. 11:2-19)
\ie

18 Wanafunzi wa Yohane walimpa habari Yohane juu ya mambo hayo yote.
Naye Yohane, baada ya kuwaita wawili kati ya wanafunzi wake,
19 aliwatuma kwa Bwana wamwulize: “Wewe ndiye yule ajaye, au
tumtazamie mwingine?”
20 Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji
ametutuma kwako tukuulize: <Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie
mwingine?”>

21 Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponya watu wengi waliokuwa
wanateseka kwa magonjwa na waliopagawa na pepo wabaya, akawawezesha
vipofu wengi kuona tena.
22 Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale
mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma
wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini
wanahubiriwa Habari njema.
23 Heri mtu yule ambaye hana mashaka nami!”

24 Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza
kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kule jangwani, hivi
mlitaka kuona kitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa na upepo?
25 Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia
mavazi maridadi? La hasha! Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya
anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
26 Basi, niambieni, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii?
Naam, hakika ni zaidi ya nabii.
27 Huyu Yohane ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu:

<Hapa ni mtumishi wangu, asema Bwana;
ninamtuma akutangulie,
akutayarishie njia.”>
\m
28 Yesu akamalizia kwa kusema, “Nawaambieni, kati ya binadamu wote
hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, yule
aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkubwa zaidi kuliko yeye.”

29 Waliposikia hayo watu wote na watoza ushuru waliusifu wema wa
Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
30 Lakini Mafarisayo na walimu wa Sheria walikataa mpango wa Mungu
uliowahusu wakakataa kubatizwa na Yohane.

31 Yesu akaendelea kusema, “Basi, nitawafananisha watu wa kizazi
hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani?
32 Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi
kimoja na kingine: <Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza!
Tumeomboleza, lakini hamkulia!>
33 Kwa maana Yohane alikuja, yeye alifunga na hakunywa divai, nanyi
mkasema: <Amepagawa na pepo!>
34 Akaja Mwana wa Mtu; anakula na kunywa, mkasema: <Mwangalieni
mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!>
35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote
wale wanaoikubali.”

Yesu nyumbani kwa Simoni Mfarisayo

36 Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake.
Akaingia nyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
37 Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja aliyekuwa anaishi
maisha mabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo
Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
38 Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi
yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu
kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
39 Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni
mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa
namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
40 Yesu akamwambia huyo Mfarisayo, “Simoni, ninacho kitu cha
kukwambia.” Naye Simoni akamwambia, “Ndio Mwalimu, sema.” Yesu
akasema,
41 “Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa
dinari mia tano, na mwingine hamsini.
42 Waliposhindwa kulipa madeni yao, huyo mtu aliwasamehe wote
wawili. Sasa ni yupi kati ya hao wawili atampenda zaidi huyo bwana?”
43 Simoni akamjibu, “Ni dhahiri kwamba yule aliyesamehewa deni
kubwa zaidi atampenda zaidi yule bwana.” Yesu akamwambia, “Sawa.”

44 Halafu akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, “Unamwona
huyu mwanamke, sivyo? Basi, mimi nilipoingia hapa nyumbani kwako
hukunipa maji ya kunawa miguu yangu; lakini mwanamke huyu ameniosha
miguu yangu kwa machozi yake na kunipangusa kwa nywele zake.
45 Wewe hukunisalimu kwa kunibusu, lakini huyu mwanamke tangu
nilipoingia hapa amekuwa akiibusu miguu yangu.
46 Wewe hukunionyesha ukarimu wako kwa kunipaka mafuta kichwani,
lakini huyu mwanamke amefanya hivyo kwa kunipaka mafuta miguu yangu.
47 Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa
ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo.”
48 Basi, Yesu akamwambia yule mwanamke, “Umesamehewa dhambi zako.”

49 Na hapo wale waliokuwa pamoja naye mezani wakaulizana, “Ni mtu
wa namna gani huyu awezaye kusamehe dhambi?”
50 Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda
kwa amani.”

\c 8

Wanawake walioandamana na Yesu

1 Baada ya hayo, Yesu alipitia katika miji na vijiji akitangaza
Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
2 Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na
kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye
Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba;
3 Yoana, mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine
kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.

Mfano wa mpanzi
\r
\is (Mat. 13:1-9; Marko 4:1-9)
\ie

4 Kundi kubwa la watu lilikuwa linakusanyika, na watu walikuwa
wanamjia Yesu kutoka kila mji. Naye akawaambia mfano huu:
5 “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda zile
mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga, na
ndege wakazila.
6 Nyingine zilianguka penye mawe, na baada ya kuota zikanyauka kwa
kukosa maji.
7 Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba
ilipoota ikazisonga.
8 Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa asilimia
mia.” Baada ya kusema hayo, akapaaza sauti, akasema, “Mwenye masikio
na asikie!”

Kusudi la kufundisha kwa mifano
\r
\is (Mat. 13:10-17; Marko 4:10-12)
\ie

9 Wanafunzi wake wakamwuliza Yesu maana ya mfano huo.
10 Naye akajibu, “Ninyi mmejaliwa kujua siri za Ufalme wa Mungu,
lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama
wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.

Yesu anafafanua mfano wa mpanzi
\r
\is (Mat. 13:18-23; Marko 4:13-20)
\ie

11 “Basi, maana ya mfano huu ni hii: mbegu ni neno la Mungu.
12 Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu wale wanaosikia lile
neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini na
hivyo wakaokoka.
13 Zile zilizoanguka penye mawe zinaonyesha watu wale ambao
wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Hata hivyo, kama zile
mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na
wanapojaribiwa hukata tamaa.
14 Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu wale wanaosikia
lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi,
mali na anasa za maisha, na hawazai matunda yakakomaa.
15 Na zile zilizoanguka kwenye udongo mzuri ndio watu wale
wanaolisikia lile neno, wakalizingatia kwa moyo mwema na wa utii. Hao
huvumilia mpaka wakazaa matunda.

Taa iliyofunikwa kwa debe
\r
\is (Marko 4:21-25)
\ie

16 “Watu hawawashi taa na kuifunika kwa chombo au kuiweka mvunguni.
Lakini huiweka juu ya kinara ili watu wanapoingia ndani wapate kuona
mwanga.

17 “Chochote kilichofichwa kitafichuliwa na siri yoyote
itagunduliwa na kujulikana hadharani.

18 “Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu
ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani kuwa
anacho, kitachukuliwa.”

Mama na ndugu zake Yesu
\r
\is (Mat. 12:46-50; Marko 3:31-35)
\ie

19 Hapo mama na ndugu zake Yesu wakamjia, lakini hawakuweza
kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu.
20 Yesu akapewa habari kwamba mama na ndugu zake walikuwa nje,
wanataka kumwona.
21 Lakini Yesu akawaambia watu wote, “Mama yangu na ndugu zangu ni
wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika.”

Yesu anaamuru dhoruba itulie
\r
\is (Mat. 8:23-27; Marko 4:35-41)
\ie

22 Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake,
akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ng’ambo.” Basi, wakaanza safari.
23 Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi,
akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya
mashua, wakawa katika hatari.
24 Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, “Bwana,
Bwana! Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaikemea dhoruba na mawimbi, navyo
vikatulia, kukawa shwari.
25 Kisha akawaambia, “Iko wapi imani yenu?” Lakini wao walishangaa
na kuogopa huku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba
na mawimbi, navyo vinamtii?”

Yesu anamponya mtu aliyepagawa na pepo
\r
\is (Mat. 8:28-34; Marko 5:1-20)
\ie

26 Wakaendelea na safari, wakafika pwani ya nchi ya Wagerase
inayokabiliana na Galilaya, ng’ambo ya ziwa.
27 Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo
alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo, hakuwa anavaa nguo, wala
hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.
28 Alipomwona Yesu, alipiga kelele na kujitupa chini mbele yake, na
kusema kwa sauti kubwa “We, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu una shauri
gani nami? Ninakusihi usinitese!”
29 Alisema hivyo kwa kuwa Yesu alikwishamwambia huyo pepo mchafu
amtoke mtu huyo. Pepo huyo mchafu alikuwa anamvamia mtu huyo mara
nyingi, na ingawa watu walimweka ndani na kumfunga kwa minyororo na
pingu, lakini kila mara alivivunja vifungo hivyo, akakimbizwa na pepo
huyo mchafu hadi jangwani.
30 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina
langu ni <Jeshi”>–kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
31 Hao pepo wakamsihi asiwaamuru wamtoke na kwenda kwenye shimo
lisilo na mwisho.
\il 5
ic
\is Pwani ya Gerase (Luka 8:26)
\ie

32 Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao
pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
33 Kwa hiyo pepo hao wakamtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe,
nao wakaporomoka kwenye ule mteremko mkali, wakatumbukia ziwani,
wakazama majini.

34 Wale wachungaji walipoona yote yaliyotokea walikimbia, wakaenda
kuwapa watu habari, mjini na mashambani.
35 Watu wakaja kuona yaliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule
mtu aliyetokwa na pepo ameketi karibu na Yesu, amevaa nguo, ana akili
zake, wakaogopa.
36 Wale watu walioshuhudia tukio hilo waliwaeleza hao jinsi yule mtu
alivyoponywa.
37 Wakazi wa nchi ya Gerase walishikwa na hofu kubwa. Kwa hiyo
wakamwomba Yesu aondoke, aende zake. Hivyo Yesu alipanda tena mashua,
akaondoka.
38 Yule mtu aliyetokwa na wale pepo akamsihi aende pamoja naye.
Lakini Yesu hakumruhusu, bali akamwambia,
39 “Rudi nyumbani ukaeleze yote Mungu aliyokutendea.” Basi, yule
mtu akaenda akitangaza kila mahali katika mji ule mambo yote Yesu
aliyomtendea.

Binti Yairo na mwanamke mmoja wanaponywa
\r
\is (Mat. 9:18-26; Marko 5:21-43)
\ie

40 Yesu aliporudi upande mwingine wa ziwa, kundi la watu
lilimkaribisha, kwa maana wote walikuwa wanamngojea.
41 Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa
miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,
42 kwa kuwa binti yake wa pekee, mwana wa pekee mwenye umri wa miaka
kumi na miwili, alikuwa mahututi.
Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
43 Kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye
alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili,
ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna
aliyefaulu kumponya.
44 Huyo mwanamke alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
Papo hapo akaponywa ugonjwa wake wa kutokwa damu.
45 Yesu akasema, “Ni nani aliyenigusa?” Wote wakasema kwamba
hapakuwa na mtu aliyemgusa. Naye Petro akasema, “Mwalimu, umati wa watu
umekuzunguka na kukusonga!”
46 Lakini Yesu akasema, “Kuna mtu aliyenigusa, maana nimehisi nguvu
imenitoka.”
47 Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza
akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya
wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponyeshwa mara moja.
48 Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa
amani.”

49 Alipokuwa bado akiongea, Yairo akaletewa habari kutoka nyumbani:
“Binti yako ameshakufa, ya nini kumsumbua Mwalimu zaidi?”
50 Yesu aliposikia hayo akamwambia Yairo, “Usiogope; amini tu, naye
atapona.”

51 Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye,
isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
52 Watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili yake. Lakini
Yesu akawaambia, “Msilie, kwa maana mtoto hajafa, amelala tu!”
53 Nao wakamcheka kwa sababu walijua kwamba alikuwa amekufa.
54 Lakini Yesu akamshika mkono akasema, “Mtoto amka!”
55 Roho yake ikamrudia, akaamka mara. Yesu akaamuru wampe chakula.
56 Wazazi wake walishangaa, lakini Yesu akawaamuru wasimwambie mtu
yeyote hayo yaliyotendeka.

\c 9

Yesu anawatuma wale kumi na wawili
\r
\is (Mat. 10:5-15; Marko 6:7-13)
\ie

1 Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo juu ya pepo wote,
na uwezo wa kuponya wagonjwa.
2 Halafu akawatuma waende kuhubiri Ufalme wa Mungu na kuponya
wagonjwa.
3 Akawaambia, “Mnaposafiri msichukue chochote: msichukue fimbo,
wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.
4 Nyumba yoyote mtakayoingia na kukaribishwa, kaeni humo mpaka
mtakapoondoka katika kijiji hicho.
5 Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi
mnapotoka kung’uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
6 Basi, wakaanza safari, wakapitia vijijini wakihubiri Habari Njema
na kuponya wagonjwa kila mahali.

Wasiwasi wa Herode
\r
\is (Mat. 14:1-12; Marko 6:14-29)
\ie

7 Sasa, mtawala Herode, alipata habari za mambo yote yaliyokuwa
yanatendeka, akawa na wasiwasi kwa vile walikuwa wakisema: “Yohane
amefufuka kutoka wafu!”
8 Wengine walisema kwamba Eliya ametokea, na wengine walisema kwamba
mmojawapo wa manabii wa kale amerudi duniani.
9 Lakini Herode akasema, “Huyo Yohane nilimkata kichwa; sasa ni
nani huyu ninayesikia habari zake?” Akawa na hamu ya kumwona.

Yesu anawalisha chakula watu elfu tano
\r
\is (Mat. 14:13-21; Marko 6:30-44; Yoh. 6:1-14)
\ie

10 Wale mitume waliporudi, walimweleza yote waliyoyafanya. Yesu
akawachukua, wakaenda peke yao mjini Bethsaida.
11 Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu
akawakaribisha akawazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu, akawaponya wale
waliohitaji kuponywa.

12 Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea
wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu,
wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni
nyikani.”
13 Lakini Yesu akawaambia, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamjibu,
“Hatuna chochote ila mikate mitano na samaki wawili. Labda twende
wenyewe tukawanunulie chakula watu wote hawa!”
14 (Walikuwepo pale wanaume wapatao elfu tano.) Basi, Yesu
akawaambia wanafunzi wake, “Waambieni watu waketi katika makundi ya
watu hamsinihamsini.”
15 Wanafunzi wakafanya walivyoambiwa, wakawaketisha wote.
16 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili,
akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi
wake wawagawie watu.
17 Wakala wote, wakashiba; wakakusanya makombo ya chakula, wakajaza
vikapu kumi na viwili.

Petro anamkiri Yesu kuwa Kristo
\r
\is (Mat. 16:13-19; Marko 8:27-29)
\ie

18 Siku moja, Yesu alikuwa anasali peke yake, na wanafunzi wake
walikuwa karibu. Basi, akawauliza, “Eti watu wanasema mimi ni nani?”
19 Nao wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa wewe ni Yohane mbatizaji,
wengine wanasema wewe ni Eliya, hali wengine wanasema kuwa wewe ni mmoja
wa manabii wa kale ambaye amefufuka.”
20 Hapo akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?” Petro
akajibu, “Wewe ndiwe Kristo wa Mungu.”

Yesu anazungumzia kifo chake
\r
\is (Mat. 16:20-28; Marko 8:30-9:1)
\ie

21 Halafu Yesu akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hiyo.
22 Akaendelea kusema: “Ni lazima Mwana wa Mtu apate mateso mengi na
kukataliwa na wazee na makuhani wakuu na walimu wa Sheria; atauawa,
lakini siku ya tatu atafufuliwa.”
23 Kisha akawaambia watu wote, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi
wangu, ni lazima ajikane nafsi yake, auchukue msalaba wake kila siku,
anifuate.
24 Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza;
lakini atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayaokoa.
25 Je, kuna faida gani mtu kuupata utajiri wote wa dunia kwa
kujipoteza au kujiangamiza yeye mwenyewe?
26 Mtu akinionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu
atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na wa
Baba na wa malaika watakatifu.
27 Nawaambieni kweli, kuna wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla
ya kuuona Ufalme wa Mungu.”

Yesu anageuka sura
\r
\is (Mat. 17:1-8; Marko 9:2-8)
\ie

28 Yapata siku nane baada ya kusema hayo, Yesu aliwachukua Petro,
Yohane na Yakobo, akaenda nao mlimani kusali.
29 Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa
meupe na kung’aa sana.
30 Na watu wawili wakaonekana wakizungumza naye, nao ni Mose na
Eliya,
31 ambao walitokea wakiwa wenye utukufu, wakazungumza naye juu ya
kifo chake ambacho angekikamilisha huko Yerusalemu.
32 Petro na wenzake walikuwa wamelemewa na usingizi mzito, hata
hivyo waliamka, wakauona utukufu wake, wakawaona na wale watu wawili
waliokuwa wamesimama pamoja naye.
33 Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia
Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba tupo hapa: basi, tujenge vibanda vitatu:
kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.”–Kwa kweli hakujua
anasema nini.

34 Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika;
na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.
35 Sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ndiye Mwanangu
niliyemchagua, msikilizeni.”
36 Baada ya hiyo sauti kusikika, Yesu alionekana akiwa peke yake.
Wanafunzi walikaa kimya juu ya tukio hilo, na wakati ule hawakumwambia
mtu yeyote mambo hayo waliyoyaona.

Yesu anamponya mtoto mwenye pepo mbaya
\r
\is (Mat. 17:14-18; Marko 9:14-27)
\ie

37 Kesho yake walipokuwa wakishuka kutoka kule mlimani, kundi kubwa
la watu lilikutana na Yesu.
38 Hapo, mtu mmoja katika lile kundi akapaaza sauti, akasema,
“Mwalimu! Ninakusihi umwangalie mwanangu–mwanangu wa pekee!
39 Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia
kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache
upesi.
40 Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.”
41 Yesu akasema, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka!
Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini?” Kisha akamwambia huyo mtu,
“Mlete mtoto wako hapa.”
42 Wakati mtoto huyo alipokuwa anamjia Yesu, yule pepo alimwangusha
chini na kumtia kifafa. Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu akamponya
mtoto na kumkabidhi kwa baba yake.
43 Watu wote wakashangazwa na uwezo mkuu wa Mungu.

Yesu anaongea tena juu ya kifo chake
\r
\is (Mat. 17:22-23; Marko 9:30-32)
\ie
Wale watu walipokuwa bado wanashangaa juu ya mambo yote aliyofanya,
Yesu aliwaambia wanafunzi wake,
44 “Tegeni masikio, myasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda
kutiwa mikononi mwa watu.”
45 Lakini wao hawakuelewa maana ya usemi huo. Jambo hilo lilikuwa
limefichwa kwao ili wasitambue; nao wakaogopa kumwuliza juu ya msemo
huo.

Ni nani aliye mkuu?
\r
\is (Mat. 18:1-5; Marko 9:33-37)
\ie

46 Kukatokea majadiliano kati ya wale wanafunzi kuhusu nani kati yao
aliyekuwa mkuu zaidi.
47 Yesu aliyajua mawazo yaliyokuwa mioyoni mwao; basi akamchukua
mtoto mdogo akamweka karibu naye,
48 akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina
langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule
aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye
mkubwa kuliko wote.”

Asiyepingana nanyi yuko upande wenu
\r
\is (Marko 9:38-40)
\ie

49 Yohane alidakia na kusema, “Bwana, tumemwona mtu mmoja akitoa
pepo kwa kulitumia jina lako nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si
mmoja wetu.”
50 Lakini Yesu akamwambia, “Msimkataze; kwani asiyepingana nanyi
yuko upande wenu.”

Wasamaria wanakataa kumkaribisha Yesu

51 Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye
alikata shauri kwenda Yerusalemu.
52 Basi, akawatuma wajumbe wamtangulie, nao wakaenda wakaingia
kijiji kimoja cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.
53 Lakini wenyeji wa hapo hawakutaka kumpokea kwa sababu alikuwa
anaelekea Yerusalemu.
54 Basi, wanafunzi wake, kina Yohane na Yakobo, walipoona hayo,
wakasema, “Bwana, wataka tuamuru moto ushuke kutoka mbinguni
uwateketeze?”
55 Lakini yeye akawageukia, akawakemea.fa
56 Wakatoka, wakaenda kijiji kingine.
\fm a
\fr 9.55
\f
\is Baadhi ya makala huongeza,\ie akasema, “Hamjui ni roho ya namna
gani mliyo nayo; kwa maana Mwana wa Mtu hakuja kuyaangamiza maisha ya
watu, bali kuyaokoa.”

Wanaostahili kuwa wafuasi
\r
\is (Mat. 8:19-22)
\ie

57 Walipokuwa wakisafiri njiani, mtu mmoja akamwambia Yesu,
“Nitakufuata kokote utakakokwenda.”
58 Yesu akasema, “Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini
Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.”

59 Kisha akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Lakini huyo akasema,
“Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.”
60 Yesu akamwambia, “Waache wafu wazike wafu wao; bali wewe nenda
ukatangaze Ufalme wa Mungu.”

61 Na mtu mwingine akamwambia, “Nitakufuata, lakini niruhusu kwanza
nikawaage wale walio nyumbani kwangu.”
62 Yesu akamwambia, “Yeyote anayeshika jembe tayari kulima na huku
anaangalia nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”

\c 10

Yesu anawatuma wafuasi sabini na wawili

1 Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili,
akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo
yeye mwenyewe alitaka kwenda.
2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa
hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.
3 Sasa nendeni; fahamuni kwamba ninawatuma ninyi kama kondoo
wanaokwenda kati ya mbwa mwitu.
4 Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote
njiani.
5 Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: <Amani iwe
katika nyumba hii!>
6 Kama akiwako mwenye kupenda amani, amani yenu itakaa naye, la
sivyo, itawarudieni.
7 Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana
mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba
ile.
8 Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni
wanavyowapeni.
9 Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieni watu: <Ufalme wa Mungu
umekaribia kwenu.>
10 Lakini mkiingia katika mji wowote, wasipowakaribisheni, tokeni;
nanyi mpitapo katika barabara zao semeni:
11 <Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu
tunawakung’utieni. Lakini, jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.>
12 Hakika nawaambieni, siku ile mji huo utapata adhabu kubwa zaidi
kuliko ile ya watu wa Sodoma.

Ole kwa miji isiyotubu
\r
\is (Mat. 11:20-24)
\ie

13 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza
iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake
wangalikwishavaa mavazi ya gunia kitambo, na kukaa katika majivu
kuonyesha kwamba wametubu.
14 Hata hivyo, Siku ya Hukumu ninyi mtapata adhabu kubwa zaidi
kuliko ile ya watu wa Tiro na Sidoni.
15 Na wewe Kafarnaumu, unataka kujikweza mpaka mbinguni? La;
utaporomoshwa mpaka Kuzimu.”

16 Halafu akasema, “Anayewasikiliza ninyi, ananisikiliza mimi; na
anayekataa kuwapokea ninyi, anakataa kunipokea mimi. Yeyote anayekataa
kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”

Wale sabini na wawili wanarudi

17 Baadaye, wale sabini na wawili walirudi wamejaa furaha, wakisema,
“Bwana, hata pepo wametutii tulipolitaja jina lako.”
18 Yeye akawaambia, “Nilimwona Shetani jinsi alivyokuwa anaporomoka
kama umeme kutoka mbinguni.
19 Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng’e, na uwezo juu
ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.
20 Hata hivyo, msifurahi kwa sababu pepo wamewatii, bali furahini
kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”
\il 5
ic
\is Ng’e (Luka 10:19)
\ie

Furaha ya Yesu
\r
\is (Mat. 11:25-27; 13:16-17)
\ie

21 Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema,
“Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa umewaficha
wenye hekima na elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba,
ndivyo ilivyokupendeza.”

22 Kisha akasema, “Baba yangu ameweka yote mikononi mwangu. Hakuna
amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala amjuaye Baba ni nani ila Mwana, na
yeyote yule ambaye Mwana anataka kumfunulia hayo.”

23 Halafu akawaelekea wafuasi wake akawaambia, “Heri wanaoona yale
mnayoyaona ninyi!
24 Hakika, manabii na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona ninyi
wasiyaone, na kusikia yale mnayoyasikia wasiyasikie.”

Mfano wa Msamaria mwema

25 Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka
kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?”
26 Yesu akamwuliza, “Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?”
27 Akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho
yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani
yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
28 Yesu akawaambia, “Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi.”

29 Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu,
“Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu
kwenda Yeriko. Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyang’anya
mali yake na kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu.
31 Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona,
akapita kando.
32 Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali akamwona, akapita
kando.
33 Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu
alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma.
34 Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai; na
kuyafunga halafu akampandisha juu ya punda wake akampeleka katika nyumba
moja ya wageni akamuuguza.
35 Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba,
akamwambia, <Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi,
nitakulipa nitakaporudi.”>
36 Kisha Yesu akauliza, “Kati ya hao watatu, ni yupi aliyeonyesha
kuwa jirani yake yule aliyevamiwa na majambazi?”
37 Yule mwalimu wa Sheria akamjibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.”
Yesu akamwambia, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”

Yesu nyumbani kwa Martha na Maria

38 Walipokuwa safarini, waliingia katika kijiji kimoja na mwanamke
mmoja, aitwaye Martha, alimkaribisha nyumbani kwake.
39 Martha alikuwa na dada yake aitwaye Maria; huyu aliketi karibu na
Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40 Lakini Martha alikuwa anashughulika na mambo mengi. Basi,
akamwendea Yesu, akamwambia, “Bwana, hivi hujali kwamba dada yangu
ameniacha nishughulike peke yangu? Mwambie basi, anisaidie.”
41 Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha, unahangaika na kusumbuka
kwa mambo mengi.
42 Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho
hakuna mtu atakayemnyag’anya.”

\c 11

Yesu anafundisha juu ya kusali
\r
\is (Mat. 6:9-13; 7:7-11)
\ie

1 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akisali. Alipomaliza kusali,
mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tunakuomba utufundishe
kusali kama Yohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake.”
2 Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni:

<Baba!
Jina lako litukuzwe;
Ufalme wako ufike.

3 Utupe daima chakula chetu cha kila siku.

4 Utusamehe dhambi zetu,

maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea;
wala usitutie katika majaribu.”>

5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake
usiku wa manane, akamwambia: <Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu,
6 kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha
kumpa.>
7 Naye, akiwa ndani angemjibu: <Usinisumbue! Nimekwisha funga
mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!>
8 Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake,
lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote
anachohitaji.
9 Kwa hiyo, ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni, nanyi mtapata, bisheni
nanyi mtafunguliwa.
10 Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye
hufunguliwa.
11 Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya
samaki?
12 Na kama akimwomba yai, je, atampa ng’e?
13 Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri.
Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale
wanaomwomba.”

Yesu na Beelzebuli
\r
\is (Mat. 12:22-3; Marko 3;20-27)
\ie

14 Siku moja Yesu alikuwa anamfukuza pepo aliyemfanya mtu mmoja kuwa
bubu. Basi, huyo pepo alipomtoka, yule mtu akaweza kuongea hata umati wa
watu ukashangaa.
15 Lakini baadhi ya watu hao wakasema, “Anamfukuza pepo kwa uwezo
wa Beelzebuli, mkuu wa pepo.”
16 Wengine, wakimjaribu, wakamtaka afanye ishara kuonyesha kama
alikuwa na idhini kutoka mbinguni.
17 Lakini yeye, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme
wowote uliofarakana wenyewe, hauwezi kudumu; kadhalika, jamaa yeyote
inayofarakana huangamia.
18 Kama Shetani anajipinga mwenyewe, utawala wake utasimamaje?
Mnasemaje, basi, kwamba ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli?
19 Kama ninafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, watoto wenu
huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo, wao ndio watakaowahukumu
ninyi.
20 Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa uwezo wa Mungu, basi jueni
kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.

21 “Mtu mwenye nguvu anapolinda jumba lake kwa silaha, mali yake
yote iko salama.
22 Lakini akija mwenye nguvu zaidi akamshambulia na kumshinda, huyo
huziteka silaha zake alizotegemea na kugawanya nyara.
23 Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya
pamoja nami, hutawanya.

Kurudi kwa pepo mbaya
\r
\is (Mat. 12:43-45)
\ie

24 “Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu fulani, huzururazurura jangwani
akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata, hujisemea: <Nitarudi kwenye
makao yangu nilikotoka.>
25 Anaporudi, huikuta ile nyumba imefagiwa na kupambwa.
26 Basi, huenda na kuwachukua pepo wengine saba waovu zaidi kuliko
yeye; wote huenda na kumwingia mtu yule. Hivyo, basi hali ya mtu huyo
sasa huwa mbaya zaidi kuliko pale mwanzo.”

Furaha ya kweli

27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu,
akasema kwa sauti kubwa: “Heri tumbo lililokuzaa, na maziwa
yaliyokunyonyesha!”
28 Lakini Yesu akasema, “Lakini heri zaidi wale wanaolisikia neno
la Mungu na kulishika.”

Wanataka mwujiza

(Mat 12:38-42)

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi
hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote
isipokuwa ile ya Yona.
30 Jinsi Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninewi, ndivyo pia Mwana
wa Mtu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki.
31 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa,
naye atashuhudia kwamba kina hatia. Yeye alisafiri kutoka mbali, akaja
kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni; kumbe hapa pana mkuu zaidi
kuliko Solomoni.
32 Watu wa Ninewi watatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, na
watashuhudia kwamba kizazi hiki kina hatia. Hao watu wa Ninewi walitubu
kwa sababu ya mahubiri ya Yona; na hapa pana mkuu zaidi kuliko Yona!

Mwanga wa mwili
\r
\is (Mat. 5:15; 6:22-23)
\ie

33 “Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa pishi, bali huiweka
juu ya kinara ili watu wanaoingia ndani wapate kuona mwanga.
34 Jicho lako ni kama taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako
wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia
utakuwa katika giza.
35 Uwe mwangalifu basi mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.
36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote
yenye giza, mwili huo utang’aa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia
kwa mwanga wake.”

Yesu anawalaumu Mafarisayo na walimu wa Sheria
\r
\is (Mat. 23:1-36; Marko 12-38-40)
\ie

37 Yesu alipokuwa akiongea, Mfarisayo mmoja alimkaribisha chakula
nyumbani kwake, naye akaenda, akaketi kula chakula.
38 Huyo Mfarisayo alistaajabu kuona kwamba alikula chakula bila
kunawa.
39 Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo huosha kikombe na sahani kwa
nje, lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu.
40 Wapumbavu ninyi! Je, aliyetengeneza nje si ndiye aliyetengeneza
ndani pia?
41 Toeni kwa maskini vile vitu vilivyomo ndani, na vingine vyote
vitakuwa halali kwenu.

42 “Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoza watu zaka hata
juu ya majani ya kukolezea chakula, mchicha na majani mengine, na huku
hamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu. Mambo haya iliwapasa muwe
mmeyazingatia bila kuyasahau yale mengine.

43 “Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kuketi mbele
mahali pa heshima katika masunagogi, na kusalimiwa kwa heshima
hadharani.
44 Ole wenu, kwa sababu mko kama makaburi yaliyofichika; watu
hutembea juu yake bila kufahamu.”

45 Mmoja wa walimu wa Sheria akamwambia, “Mwalimu, maneno yako
yanatukashifu na sisi pia.”
46 Yesu akamjibu, “Na ninyi walimu wa Sheria, ole wenu; maana
mnawatwika watu mizigo isiyochukulika, huku ninyi wenyewe hamnyoshi hata
kidole kuwasaidia.
47 Ole wenu, kwa kuwa mnajenga makaburi ya manabii wale ambao wazee
wenu waliwaua.
48 Kwa hiyo mnashuhudia na kukubaliana na matendo ya wazee wenu;
maana wao waliwaua hao manabii, nanyi mnajenga makaburi yao.
49 Kwa hiyo, Hekima ya Mungu ilisema hivi: <Nitawapelekea manabii na
mitume, lakini watawaua baadhi yao, na kuwatesa wengine.>
50 Matokeo yake ni kwamba kizazi hiki kitaadhibiwa kwa sababu ya
damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa ulimwengu;
51 tangu kumwagwa damu ya Abeli mpaka kifo cha Zakariya ambaye
walimuua kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, hakika kizazi
hiki kitaadhibiwa kwa matendo haya.

52 “Ole wenu ninyi walimu wa Sheria, kwa sababu mmeuficha ule
ufunguo wa mlango wa elimu; ninyi wenyewe hamkuingia na mmewazuia
waliokuwa wanaingia wasiingie.”

53 Alipokuwa akitoka pale, wale Mafarisayo na walimu wa Sheria
wakaanza kumshambulia vikali na kumsonga kwa maswali mengi
54 ili wapate kumnasa kwa maneno yake.

\c 12

Onyo kuhusu unafiki
\r
\is (Mat. 10:26-27)
\ie

1 Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa
wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na
chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.
2 Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichika
kitafichuliwa.
3 Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga,
na kila mliyonong’ona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya
nyumba.

Anayestahili kuogopwa
\r
\is (Mat. 10:28-31)
\ie

4 “Nawaambieni ninyi rafiki zangu: msiwaogope wale wanaoua mwili,
wasiweze kufanya kitu kingine zaidi.
5 Nitawaonyesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: mwogopeni yule
ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu.
Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.
6 Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti kumi, au sivyo?
Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
7 Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope,
basi, ninyi mna thamani zaidi kuliko shomoro wengi!

Kumkiri na kumkana Kristo
\r
\is (Mat. 10:32-33; 12:32; 10:19-20)
\ie

8 “Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni
wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu
huyo ni wake.
9 Lakini, mtu yeyote anayenikana mbele ya watu, naye atakanwa mbele
ya malaika wa Mungu.

10 “Yeyote anayesema neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa;
lakini anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

11 “Watakapowapeleka ninyi mbele ya masunagogi na mbele ya wakuu na
watawala msiwe na wasiwasi juu ya jinsi mtakavyojitetea au jinsi
mtakavyosema.
12 Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisheni kile
mnachopaswa kusema.”

Mfano wa tajiri mpumbavu

13 Mtu mmoja katika ule umati wa watu akamwambia, “Mwalimu, mwambie
ndugu yangu tugawane urithi aliotuachia baba.”
14 Yesu akamjibu, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi mwamuzi au
msuluhishi kati yenu?”

15 Basi, akawaambia wote, “Jihadharini na kila aina ya tamaa; maana
uzima wa mtu hautegemei wingi wa vitu alivyo navyo.”
16 Kisha akawaambia mfano: “Kulikuwa na tajiri mmoja ambaye shamba
lake lilizaa mavuno mengi.
17 Tajiri huyo akafikiri moyoni mwake: <Nitafanyaje nami sina mahali
pa kuhifadhia mavuno yangu?
18 Nitafanya hivi: nitabomoa ghala zangu na kujenga kubwa zaidi, na
humo nitahifadhi mavuno yangu yote na mali yangu.
19 Hapo nitaweza kuiambia roho yangu: sasa unayo akiba ya matumizi
kwa miaka na miaka. Ponda mali, ule, unywe na kufurahi.>
20 Lakini Mungu akamwambia: <Mpumbavu wewe; leo usiku roho yako
itachukuliwa. Na vitu vile vyote ulivyojilundikia vitakuwa vya nani?”>
21 Yesu akamaliza kwa kusema “Ndivyo ilivyo kwa mtu anayejilundikia
mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”

Mtumaini Mungu
\r
\is (Mat. 6:25-34)
\ie

22 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa sababu hiyo
nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula mnachohitaji ili kuishi,
wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu.
23 Kwa sababu uzima ni bora kuliko chakula, na mwili ni bora kuliko
mavazi.
24 Chukueni kwa mfano, kunguru: hawapandi, hawavuni wala hawana
ghala yoyote. Hata hivyo, Mungu huwalisha. Ninyi mna thamani zaidi
kuliko ndege!
25 Ni nani kati yenu kwa kuwa na wasiwasi anaweza kuongeza urefu wa
maisha yake?
26 Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini kuwa na
wasiwasi juu ya yale mengine?
27 Angalieni maua jinsi yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayafumi.
Hata hivyo, nawahakikishieni kwamba hata Solomoni mwenyewe na fahari
zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
28 Lakini, kama Mungu hulivika vizuri jani la shambani ambalo leo
liko na kesho latupwa motoni, je, hatawafanyia ninyi zaidi? Enyi watu
wenye imani haba!

29 “Basi, msivurugike akili, mkihangaika daima juu ya mtakachokula
au mtakachokunywa.
30 Kwa maana hayo yote ndiyo yanayohangaikiwa na watu wasiomjua
Mungu. Baba yenu anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo.
31 Shughulikieni kwanza Ufalme wa Mungu, na hayo yote mtapewa kwa
ziada.

Utajiri mbinguni
\r
\is (Mat. 6:19-21)
\ie

32 “Msiogope, enyi kundi dogo! Maana Baba yenu amependa kuwapeni
Ufalme.
33 Uzeni mali yenu mkawape maskini misaada. Jifanyieni mifuko
isiyochakaa, na jiwekeeni hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi
hawakaribii, wala nondo hawaharibu.
34 Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.

Watumishi waangalifu

35 “Muwe tayari! Jifungeni mkanda kiunoni, na taa zenu ziwe
zinawaka;
36 muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka arusini,
ili wamfungulie mara atakapobisha hodi.
37 Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta
wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni,
atawaketisha mezani na kuwahudumia.
38 Heri yao watumishi hao ikiwa bwana wao atawakuta wanakesha hata
ikiwa atarudi usiku wa manane au alfajiri.
39 Jueni kwamba, kama mwenye nyumba angejua saa ambayo mwizi
atakuja, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
40 Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa
msiyoitazamia.”

Mtumishi mwaminifu na asiye mwaminifu
\r
\is (Mat. 24:45-51)
\ie

41 Petro akamwambia, “Bwana, mfano huo ni kwa ajili yetu tu, au ni
kwa ajili ya watu wote?”
42 Bwana akajibu, “Ni nani basi, mtumishi aliye mwaminifu na mwenye
busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape
chakula wakati ufaao?
43 Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta
akifanya hivyo.
44 Hakika atampa madaraka juu ya mali yake yote.
45 Lakini, kama mtumishi huyo atafikiri moyoni mwake: na kusema:
<Bwana wangu amekawia sana kurudi> halafu aanze kuwapiga watumishi
wenzake, wa kiume au wa kike, na kula, kunywa na kulewa,
46 bwana wake atarudi siku asiyoitazamia na saa asiyoijua;
atamkatilia mbali na kumweka fungu moja na wasioamini.fb
47 Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki
tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana.
48 Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa
kidogo. Aliyepewa vingi atatakiwa vingi; aliyekabidhiwa vingi zaidi
atatakiwa kutoa vingi zaidi.
\fm b
\fr 12:46
\fk atamkata vipandevipande;
\f
\is au
\ie atamtupa nje.

Yesu ni sababu ya utengano wa watu
\r
\is (Mat. 10:34-36)
\ie

49 “Nimekuja kuwasha moto duniani, laiti ungekuwa umewaka tayari!
50 Ninao ubatizo ambao inanipasa niupokee; jinsi gani
ninavyohangaika mpaka ukamilike!
51 Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Hata kidogo; si amani
bali utengano.
52 Na tangu sasa, jamaa ya watu watano itagawanyika; watatu dhidi ya
wawili, na wawili dhidi ya watatu.
53 Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama
dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mama mkwe dhidi ya mke wa
mwanawe na huyo dhidi ya mama mkwe wake.”

Kufahamu majira
\r
\is (Mat. 16:2-3)
\ie

54 Yesu akayaambia tena makundi ya watu, “Mnapoona mawingu
yakitokea upande wa magharibi, mara mwasema: <Mvua itanyesha>, na kweli
hunyesha.
55 Mnapoona upepo wa kusi unavuma, mwasema <Kutakuwa na hali ya
joto> na ndivyo inavyokuwa.
56 Enyi wanafiki! Mnajua kutabiri hali ya hewa kwa kuangalia dunia
na anga; kwa nini basi, hamwezi kujua maana ya nyakati hizi?

Patana na adui yako
\r
\is (Mat. 5:25-26)
\ie

57 “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya?
58 Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali
kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya
hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
59 Hakika hutatoka huko nakwambia, mpaka utakapomaliza kulipa senti
ya mwisho.”

\c 13

Acheni dhambi zenu au mtakufa

1 Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa
Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja
wanyama wao wa tambiko.
2 Naye Yesu akawaambia, “Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu
zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo?
3 Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu,
mtaangamia kama wao.
4 Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa;
mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi
Yerusalemu?
5 Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.”

Mfano wa mtini usiozaa

6 Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini
katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake,
lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
7 Basi, akamwambia mfanyakazi wake: <Angalia! Kwa miaka mitatu
nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu.
Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?>
8 Lakini naye akamjibu: <Bwana, tuuache tena mwaka huu;
nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea.
9 Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza
kuukata.”>

Yesu anamponya mama mmoja siku ya Sabato

10 Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato.
11 Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka
kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo,
mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
12 Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa
wako.”
13 Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa
anamtukuza Mungu.
14 Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa
amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale,
“Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe
magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”

15 Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua
ng’ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku
hiyo ni ya Sabato?
16 Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema
kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo
vyake siku ya Sabato?”
17 Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu
wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.

Mfano wa mbegu ndogo ya haradali
\r
\is (Mat. 13:31-32; Marko 4:30-32)
\ie

18 Yesu akauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana na nini?
Nitaulinganisha na nini?
19 NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda
shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota
vyao katika matawi yake.”

Mfano wa chachu
\r
\is (Mat. 13:33)
\ie

20 Tena akauliza: “Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini?
21 Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na
unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote.”

Mlango mwembamba
\r
\is (Mat. 7:13-14, 21-23)
\ie

22 Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia
mijini na vijijini, akihubiri.
23 Mtu mmoja akamwuliza, “Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni
wachache?”
24 Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango
mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini
hawataweza.

25 “Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango.
Ninyi mtasimama nje na kuanza kupiga hodi mkisema: <Bwana, tufungulie
mlango.> Lakini yeye atawajibu: <Sijui mmetoka wapi.>
26 Nanyi mtaanza kumwambia: <Sisi ndio wale tuliokula na kunywa
pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu.>
27 Lakini yeye atasema: <Sijui ninyi mmetoka wapi; ondokeni mbele
yangu, enyi nyote watenda maovu.>
28 Ndipo mtakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona
Abrahamu, Isaka na Yakobo, na manabii wote wapo katika Ufalme wa Mungu,
lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje!
29 Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na
kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Ufalme wa Mungu.
30 Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa
kwanza watakuwa wa mwisho.”

Upendo wa Yesu kwa Yerusalemu
\r
\is (Mat. 23:37-39)
\ie

31 Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu
wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode
anataka kukuua.”
32 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: <Leo na
kesho ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha
kazi yangu.>
33 Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na
safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.

34 “Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe
wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako
pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake,
Lakini wewe umekataa.
35 Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Naam, hakika nawaambieni,
hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: <Abarikiwe huyo ajaye kwa
jina la Bwana.”>

\c 14

Yesu anamponya mtu mmoja

1 Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja
wa viongozi wa Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
2 Mbele yake Yesu palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa
kuvimba mwili.
3 Yesu akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, “Je, ni halali au
la kumponya mtu siku ya sabato?”
4 Lakini wao wakakaa kimya. Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya,
akamwacha aende zake.
5 Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au
ng’ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya
Sabato?”
6 Nao hawakuweza kumjibu swali hilo.

Ukarimu na unyenyekevu

7 Yesu aliona jinsi wale walioalikwa walivyokuwa wanajichagulia
nafasi za heshima, akawaambia mfano:
8 “Kama mtu akikualika arusini, usiketi mahali pa heshima isije
ikawa amealikwa mwingine mheshimiwa kuliko wewe;
9 na mwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na kukwambia: <Mwachie huyu
nafasi.> Hapo utaaibika mbele ya wote na kulazimika kwenda kuchukua
nafasi ya mwisho.
10 Bali ukialikwa kwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ili mwenyeji
wako atakapokuja akwambie: <Rafiki, njoo hapa mbele, mahali pazuri
zaidi.> Hapo utakuwa umeheshimika mbele ya wote wanaoketi pamoja nawe.
11 Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha,
atakwezwa.”

12 Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, “Kama ukiwaandalia watu
karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani
zako walio matajiri, wasije nao wakakualika nawe ukawa umelipwa kile
ulichowatendea.
13 Badala yake, unapofanya karamu, waalike maskini, vilema viwete na
vipofu,
14 nawe utakuwa umepata baraka, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa.
Maana Mungu atakupa tuzo lako wakati watu wema watakapofufuka.”

Mfano wa karamu kubwa
\r
\is (Mat. 22:1-10)
\ie

15 Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana
heri mtu yule atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu.”

16 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu
wengi.
17 Wakati wa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wake awaambie
walioalikwa, <Njoni, kila kitu ni tayari.>
18 Lakini wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza
akamwambia mtumishi: <Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda
kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.>
19 Mwingine akasema: <Nimenunua ng’ombe jozi tano wa kulima; sasa
nimo njiani kwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.>
20 Na mwingine akasema: <Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.>
21 Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule
mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: <Nenda upesi kwenye
barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete,
vipofu na waliolemaa.>
22 Baadaye, mtumishi huyo akasema: <Bwana mambo yamefanyika kama
ulivyoamuru, lakini bado iko nafasi.>
23 Yule bwana akamwambia mtumishi: <Nenda katika barabara na
vichochoro vya mji uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.
24 Kwa maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa
atakayeonja karamu yangu.”>

Gharama ya kuwa mfuasi
\r
\is (Mat. 10:37-38)
\ie

25 Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi,
akawageukia akawaambia,
26 “Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke
wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe,
hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi
wangu.
28 Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara
hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha
kutosha cha kumalizia?
29 La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu
watamcheka
30 wakisema: <Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.>

31 “Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme
mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari
wake elfu ishirini?
32 Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani
wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
33 Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi
wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho.

Chumvi isiyo na ladha
\r
\is (Mat. 5:13; Marko 9:50)
\ie

34 “Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na
nini?
35 Haifai kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia
mbali. Sikieni basi, kama mna masikio!”

\c 15

Mfano wa kondoo aliyepotea
\r
\is (Mat. 18:12-14)
\ie

1 Siku moja, watoza ushuru na wahalifu wengi walikwenda kumsikiliza
Yesu.
2 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakaanza kunung’unika: “Mtazameni
mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.”
3 Yesu akawajibu kwa mfano:
4 “Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao
amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na
kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
5 Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha.
6 Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake akiwaambia, <Furahini
pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.>
7 Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa
ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini
na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu.
\il 5
ic
\is Kondoo aliyepotea (Luka 15:4)
\ie

Sarafu iliyopotea

8 “Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha,
akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta
kwa uangalifu mpaka aipate.
9 Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake akisema, <Furahini pamoja
nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.>
10 Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu
kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.”

Mfano wa mwana mpotevu

11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana
wawili.
12 Yule mdogo, alimwambia baba yake: <Baba, nipe urithi wangu.> Naye
akawagawia mali yake.
13 Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na
fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.
14 Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi
ile, naye akaanza kuhangaika.
15 Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka
shambani mwake kulisha nguruwe.
16 Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu
aliyempa kitu.
17 Alipoanza kupata akili akafikiri: <Mbona kuna wafanyakazi wengi
wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
18 Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na
nimekukosea wewe pia.
19 Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi
wako.>
20 Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu
mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia,
akamkumbatia na kumbusu.

21 “Mwanawe akamwambia: <Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea
wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.>
22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: <Haraka! Leteni nguo
nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!
23 Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!
24 Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa
amepotea, lakini sasa amepatikana.> Wakaanza kufanya sherehe.

25 “Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi
na kukaribia nyumbani akasikia vifijo na ngoma.
26 Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: <Kuna nini?>
27 Huyo mtumishi akamwambia: <Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba
yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.>
28 Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani.
Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.
29 Lakini yeye akamjibu: <Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia,
sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana
mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
30 Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba,
mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.>
31 Baba yake akamjibu: <Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na
kila nilicho nacho ni chako.
32 Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako
alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa
amepatikana.”>

\c 16

Karani mjanja

1 Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Tajiri mmoja alikuwa na karani
wake. Huyu karani alichongewa kwamba alitumia ovyo mali ya tajiri wake.
2 Yule tajiri akamwita akamwambia: <Ni mambo gani haya ninayosikia
juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana
huwezi kuwa karani tena.>
3 Yule karani akafikiri: <Bwana wangu amenifukuza kazi ya ukarani;
nitafanya nini? Kwenda kulima siwezi; kwenda kuombaomba kama maskini ni
aibu.
4 Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze
kunikaribisha nyumbani kwao.>
5 Basi, akawaita wadeni wa bwana wake, mmoja mmoja, akamwambia yule
wa kwanza: <Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?>
6 Yeye akamjibu: <Mapipa mia ya mafuta ya zeituni.> Yule karani
akamwambia: <Chukua hati yako ya deni, keti haraka, andika hamsini.>
7 Kisha akamwuliza mdeni mwingine: <Wewe unadaiwa kiasi gani?> Yeye
akamjibu: <Magunia mia ya ngano.> Yule karani akamwambia: <Chukua hati
yako ya deni, andika themanini.>

8 “Basi, yule bwana akamsifu huyo karani asiye mwaminifu, kwa kuwa
alitumia busara. Kwa maana watu wa dunia hii wana busara zaidi na mambo
yao kuliko watu wa mwanga.”

9 Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni
marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, mweze
kupokewa nao katika makao ya milele.
10 Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu
katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo,
hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
11 Kama basi, ninyi si hamjawa waaminifu mali mbaya za dunia, ni
nani atakayewakabidhi zile mali za kweli?
12 Na kama hamjakuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani
atakayewakabidhi mali yenu wenyewe?

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana
atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na
kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Misemo kadha ya Yesu
\r
\is (Mat. 11:12-13;5:31-32; Marko 10:11-12)
\ie

14 Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, kwa vile wao walikuwa
wanapenda sana fedha, wakamdharau Yesu.
15 Hapo akawaambia, “Ninyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakini
Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu
mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka.

16 “Sheria na maandishi ya manabii vilikuweko mpaka wakati wa
Yohane mbatizaji. Tangu hapo, Ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja
anauingia kwa nguvu.
17 Lakini ni rahisi zaidi mbingu na dunia kupita, kuliko hata herufi
moja ya Sheria kufutwa.

18 “Yeyote anayemwacha mke wake na kuoa mwingine, anazini; na
yeyote anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Tajiri na Lazaro

19 “Palikuwa na mtu mmoja tajiri, ambaye alikuwa anavaa mavazi ya
bei kubwa sana ya rangi ya zambarau, na ya kitani safi, na kufanya
sherehe kila siku.
20 Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa
vidonda na alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri.
21 Lazaro alitamani kula makombo yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri;
na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba vidonda vyake!

22 “Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua,
wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.
23 Huyo tajiri, alikuwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho
yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
24 Basi, akaita kwa sauti: <Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume
Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe
ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.>
25 Lakini Abrahamu akamjibu: <Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema
yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye
anatulizwa, nawe unateswa.
26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili
wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu
kuja kwetu wasiweze.>
27 Huyo aliyekuwa tajiri akasema: <Basi baba, nakuomba umtume aende
nyumbani kwa baba yangu,
28 maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye
mateso.>
29 Lakini Abrahamu akamwambia: <Ndugu zako wanao Mose na manabii;
waache wawasikilize hao.>
30 Lakini yeye akasema: <Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka
kutoka wafu na kuwaendea, watatubu.>
31 Naye Abrahamu akasema: <Kama hawawasikilizi Mose na manabii,
hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu.”>

\c 17

Vikwazo
\r
\is (Mat. 18:6-7,21-22; Marko 9:42)
\ie

1 Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa
kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule
atakayevisababisha.
2 Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia
na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
3 Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.
4 Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako
akisema <Nimetubu>, lazima umsamehe.”

Imani

5 Mitume wakamwambia Bwana, “Utuongezee imani.”
6 Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama
chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: <Ng’oka
ukajipandikize baharini>, nao ungewatii.

Jukumu la mtumishi

7 “Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au
anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: <Haraka,
njoo ule chakula?>
8 La! Atamwambia: <Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia
mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.>
9 Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?
10 Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni:
<Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa
kufanya.”>

Yesu anawatakasa wakoma kumi

11 Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa
Samaria na Galilaya.
12 Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma
walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
13 Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!”
14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.”
Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
15 Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa
sauti kubwa.
16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo
alikuwa Msamaria.
17 Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako
wapi?
18 Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu
mgeni?”
19 Halafu akamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako; imani yako
imekuponya.”

Kuja kwa Ufalme wa Mungu
\r
\is (Mat. 24:23-28, 37-41)
\ie

20 Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu
utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa namna
itakayoweza kuonekana.
21 Wala hakuna atakayeweza kusema, <Uko hapa>, au <Uko pale>. Kwa
kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu.”

22 Halafu akawaambia wanafunzi wake, “Siku zinakuja ambapo
mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
23 Na watu watawaambieni: <Tazameni yuko hapa>; ninyi msitoke wala
msiwafuate.
24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga
upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
25 Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na
kizazi hiki.
26 Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku
za Mwana wa Mtu.
27 Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule
Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
28 Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na
kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
29 Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti
vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
30 Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.

31 “Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani
kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
32 Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
33 Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote
anayeipoteza, ataiokoa.
34 Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja,
mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja
atachukuliwa na mwingine ataachwa.”fc

\fm c
\fr 17:35
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 36: Watu wawili watakuwa shambani; mmoja
atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie

36 missing
37 Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Ulipo
mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”

\c 18

Mfano wa mjane na hakimu

1 Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali
daima bila kukata tamaa.
2 Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa
anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
3 Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye
alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake
kutoka kwa adui yake.
4 Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini,
mwishowe akajisemea: <Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu,
5 lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo
ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!”>

6 Basi, Bwana akaendelea kusema, “Sikieni jinsi alivyosema huyo
hakimu mbaya.
7 Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao
wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza?
8 Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani
duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?”

Mfano wa Mfarisayo na mtoza ushuru

9 Halafu Yesu aliwaambia pia mfano wa wale ambao walijiona kuwa wema
na kuwadharau wengine.
10 “Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo,
na mwingine mtoza ushuru.
11 Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: <Ee Mungu,
nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au
wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
12 Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato
langu.>
13 Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata
kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema:
<Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.>
14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa
amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza
atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa.”

Yesu anawabariki watoto wadogo
\r
\is (Mat. 19:13-15; Marko 10:13-16)
\ie

15 Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake.
Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali.
16 Lakini Yesu akawaita kwake akisema: “Waacheni hao watoto waje
kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu
kama hawa.
17 Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama
mtoto mdogo, hataingia katika Ufalme huo.”

Tajiri mmoja
\r
\is (Mat. 19:16-30; Marko 10:17-31)
\ie

18 Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, “Mwalimu mwema,
nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele?”
19 Yesu akamwambia, “Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila
Mungu peke yake.
20 Unazijua amri: <Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo;
waheshimu baba yako na mama yako.”>
21 Yeye akasema, “Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.”
22 Yesu aliposikia hayo akamwambia, “Unatakiwa bado kufanya kitu
kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na
hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate.”
23 Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu
alikuwa tajiri sana.

24 Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo
vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
25 Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano,
kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
26 Wale watu waliposikia hayo, wakasema, “Nani basi,
atakayeokolewa?”
27 Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa
Mungu.”

28 Naye Petro akamwuliza, “Na sisi je? Tumeacha vitu vyote
tukakufuata!”
29 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba
au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30 atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa
milele wakati ujao.”

Yesu anasema mara ya tatu juu ya kifo na ufufuo wake
\r
\is (Mat. 20:17-19; Marko 10:32-34)
\ie

31 Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia,
“Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na
manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
32 Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya
na kumtemea mate.
33 Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka.”
34 Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa
wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.

Yesu anamponya kipofu
\r
\is (Mat. 20:29-34; Marko 10:46-52)
\ie

35 Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu
ameketi njiani akiomba.
36 Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?”
37 Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”
38 Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
39 Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini
yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie;”
40 Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu
alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
41 “Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba
nipate kuona tena.”
42 Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”
43 Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu
akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.

\c 19

Yesu na Zakayo

1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.
2 Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu
wa watoza ushuru tena mtu tajiri.
3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa
watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.
4 Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona
Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.
5 Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia,
“Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.”
6 Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.
7 Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung’unika wakisema,
“Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.”
8 Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi
nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang’anya mtu yeyote
kitu, nitamrudishia mara nne.”
9 Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile
huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.
10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
\il 5
ic
\is Mkuyu (Luka 19:4)
\ie

Mfano wa fedha
\r
\is (Mat. 25:14-30)
\ie

11 Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia
mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani
kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)
12 Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme
aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme,
halafu arudi.
13 Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa
kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: <Fanyeni nazo biashara mpaka
nitakaporudi.>
14 Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe
waende wakaseme: <Hatumtaki huyu atutawale.>

15 “Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme,
na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze
kujua kila mmoja amepata faida gani.
16 Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: <Mheshimiwa, faida
iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.>
17 Naye akamwambia: <Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa
mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!>
18 Mtumishi wa pili akaja, akasema: <Mheshimiwa, faida iliyopatikana
ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.>
19 Naye akamwambia pia: <Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji
mitano.>

20 “Mtumishi mwingine akaja, akasema: <Chukua fedha yako;
niliificha salama katika kitambaa,
21 kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu
ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.>
22 Naye akamwambia: <Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi
mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na
kuchuma nisichopanda.
23 Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua
pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?>
24 Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: <Mnyang’anyeni hizo fedha,
mkampe yule aliyepata faida mara kumi.>
25 Nao wakamwambia: <Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi
hicho mara kumi!>
26 Naye akawajibu: <Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa.
Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
27 Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao,
waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.”>

Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe
\r
\is (Mat. 21:1-11; Marko 11:1-11; Yoh. 12:12-19)
\ie

28 Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea
Yerusalemu.
29 Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa
Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
30 akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu.
Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye
hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.
31 Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, <Bwana ana
haja naye.”>

32 Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.
33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza,
“Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?”
34 Nao wakawajibu, “Bwana anamhitaji.”
35 Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika
mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.
36 Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao
barabarani.

37 Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa
Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na
kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;
38 wakawa wanasema: “Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana.
Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!”

39 Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu,
wakamwambia Yesu, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!”
40 Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo
mawe yatapaza sauti.”

Yesu anauombolezea Yerusalemu

41 Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia
42 akisema: “Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini
sasa yamefichika machoni pako.
43 Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma,
watakuzingira na kukusonga pande zote.
44 Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako;
hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati
Mungu alipokujia kukuokoa.”

Yesu anaingia Hekaluni
\r
\is (Mat. 21:12-17; Marko 11:15-19; Yoh. 2:13-22)
\ie

45 Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje
wafanyabiashara
46 akisema, “Imeandikwa: <Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala>;
lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.”

47 Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu
wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,
48 lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa
wakimsikiliza kwa makini kabisa.

\c 20

Suala juu ya mamlaka ya Yesu
\r
\is (Mat. 21:23-27; Marko 11:27-33)
\ie

1 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na
kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria
pamoja na wazee walifika,
2 wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?”
3 Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali:
4 mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”
5 Lakini wao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitoka mbinguni, yeye
atatuuliza: <Mbona hamkumsadiki?>
6 Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe,
maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii.”
7 Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.”
8 Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa
mamlaka gani.”

Shamba la mizabibu
\r
\is (Mat. 21:33-46; Marko 12:1-12)
\ie

9 Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima
shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi
ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
10 Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale
wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale
wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.
11 Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga
huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.
12 Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza,
wakamfukuza.
13 Yule mwenye shamba akafikiri: <Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu
mpenzi; labda watamjali yeye.>
14 Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: <Huyu ndiye mrithi.
Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.>
15 Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua.” Yesu
akauliza, “Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?
16 Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na atawapa wakulima wengine
hilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikia maneno hayo, walisema:
“Hasha! Yasitukie hata kidogo!”

17 Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Maandiko haya Matakatifu
yana maana gani basi?

<Jiwe walilokataa waashi,
sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!>
\m
18 Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo, atavunjika vipandevipande;
na likimwangukia mtu yeyote, litamsaga kabisa.”

Suala juu ya kulipa kodi
\r
\is (Mat. 22:15-22; Marko 12:13-17)
\ie

19 Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo
ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu
waliogopa watu.
20 Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani
wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo
waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali.
21 Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na
kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe
wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
22 Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”

23 Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24 “Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?”
25 Nao wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Yesu akawaambia, “Basi, mpeni
Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Mungu vilivyo vyake Mungu.”
26 Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo
wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.

Suala juu ya ufufuo
\r
\is (Mat. 22:23-33; Marko 12:18-27)
\ie

27 Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia
Yesu, wakasema:
28 “Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani
akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue
huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.
29 Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa
na baadaye akafa bila kuacha mtoto.
30 Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;
31 na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote
saba–wote walikufa bila kuacha watoto.
32 Mwishowe akafa pia yule mwanamke.
33 Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa
nani? Alikuwa ameolewa na wote saba.”

34 Yesu akawaambia, “Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;
35 lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa
ufufuo, hawataoa wala kuolewa.
36 Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika,
na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.
37 Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha
jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko
Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana
kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
38 Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai;
maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye.”

39 Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema
kabisa.”
40 Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali
mengine.

Suala juu ya Kristo
\r
\is (Mat. 22:41-46; Marko 12:35-37)
\ie

41 Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi:

<Bwana alimwambia Bwana wangu:
Keti upande wangu wa kulia

43 mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.>
\m
44 Ikiwa Daudi anamwita yeye, <Bwana,> basi atakuwaje mwanawe?”

Yesu anawaonya walimu wa Sheria
\r
\is (Mat.23:1-36; Marko 12:38-40)
\ie

45 Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,
46 “Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita
wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi
mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika
karamu.
47 Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala
ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!”

\c 21

Sadaka ya mama mjane
\r
\is (Marko 12:41-44)
\ie

1 Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia
sadaka zao katika hazina ya Hekalu,
2 akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili
ndogo.
3 Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mama huyu mjane ametia zaidi
katika hazina kuliko wote.
4 Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya
mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu
alichohitaji kwa kuishi.”

Yesu anatabiri kuteketezwa kwa Hekalu
\r
\is (Mat. 24:1-1-2; Marko 13:1-2)
\ie

5 Baadhi ya wanafunzi walikuwa wanazungumza juu ya Hekalu, jinsi
lilivyopambwa kwa mawe ya thamani, pamoja na sadaka zilizotolewa kwa
Mungu. Yesu akasema,
6 “Haya yote mnayoyaona–zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja
litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”

Taabu na mateso
\r
\is (Mat. 24:3-14; Marko 13:3-13)
\ie

7 Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni
ishara gani zitakazoonyesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”

8 Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi
watatokea na kulitumia jina langu wakisema: <Mimi ndiye>, na, <Wakati
ule umekaribia>. Lakini ninyi msiwafuate!
9 Basi, mtakaposikia habari za vita na misukosuko, msitishike; maana
ni lazima hayo yatokee kwanza, lakini mwisho wa yote, bado.”

10 Halafu akaendelea kusema: “Taifa moja litapigana na taifa
lingine, na ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine.
11 Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, kutakuwa na
njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
12 Lakini kabla ya kutokea hayo yote, watawatieni nguvuni,
watawatesa na kuwapelekeni katika masunagogi na kuwatia gerezani;
mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu.
13 Hii itawapeni fursa ya kushuhudia Habari Njema.
14 Muwe na msimamo huu mioyoni mwenu: hakuna kufikiria kabla ya
wakati juu ya jinsi mtakavyojitetea,
15 kwa sababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasaha wa maneno na hekima,
hivyo kwamba zenu hawataweza kustahimili wala kupinga.
16 Wazazi wenu, ndugu, jamaa na rafiki zenu watawasaliti ninyi; na
baadhi yenu mtauawa.
17 Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu.
18 Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea.
19 Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.

Yesu anatabiri kuharibiwa kwa mji wa Yerusalemu
\r
\is (Mat. 24:15-21; Marko 13:14-19)
\ie

20 “Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo
mtambue ya kwamba wakati umefika ambapo mji huo utaharibiwa.
21 Hapo walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke;
na wale walio mashambani wasirudi mjini.
22 Kwa maana siku hizo ni siku za adhabu, ili yote yaliyoandikwa
yatimie.
23 Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa
na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
24 Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika
nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine,
hadi nyakati zao zitakapotimia.

Kuja kwa Mwana wa Mtu
\r
\is (Mat. 24:29-31; Marko 13:24-27)
\ie

25 “Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota. Mataifa
duniani yatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasi kutokana na mshindo wa
mawimbi ya bahari.
26 Watu watazirai kwa sababu ya uoga, wakitazamia mambo
yatakayoupata ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
27 Halafu, watamwona Mwana wa Mtu akija katika wingu, mwenye nguvu
na utukufu mwingi.
28 Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa
vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia.”

Mfano wa mtini
\r
\is (Mat. 24:32-35; Marko 13:28-31)
\ie

29 Kisha akawaambia mfano: “Angalieni mtini na miti mingine yote.
30 Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba wakati
wa kiangazi umekaribia.
31 Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba
Ufalme wa Mungu umekaribia.
32 Nawaambieni hakika, kizazi hiki cha sasa hakitapita kabla ya hayo
yote kutendeka.
33 Mbingu na dunia vitapita, lakini maneno yangu hayatapita.

Lazima kuwa macho

34 “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na
shughuli za maisha haya. La sivyo, Siku ile itawajieni ghafla.
35 Kwa maana itawajia kama mtego, wote wanaoishi duniani pote.
36 Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya
kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya
Mwana wa Mtu.”

37 Wakati wa mchana, siku hizo, Yesu alikuwa akifundisha watu
Hekaluni; lakini usiku alikuwa akienda katika mlima wa Mizeituni na
kukaa huko.
38 Watu wote walikuwa wanakwenda Hekaluni asubuhi na mapema, wapate
kumsikiliza.

\c 22

Njama za kumwua Yesu
\r
\is (Mat. 26:1-5; Marko 14:-2; Yoh. 11:45-53)
\ie

1 Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa
inakaribia.
2 Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya
kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.

Yuda anakubali kumsaliti Yesu
\r
\is (Mat. 26:14-16; Marko 14:10-11)
\ie

3 Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale
mitume kumi na wawili.
4 Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa Hekalu
kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao.
5 Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha.
6 Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao
bila umati wa watu kujua.

Maandalio ya karamu ya Pasaka
\r
\is (Mat. 26:17-25; Marko 14:12-21; Yoh. 13:21-30)
\ie

7 Basi, siku ya Mikate Isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku
ambayo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa.
8 Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, “Nendeni
mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka.”
9 Nao wakamwuliza, “Unataka tuiandae wapi?”
10 Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana
na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba
atakayoingia.
11 Mwambieni mwenye nyumba: <Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile
chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?>
12 Naye atawaonyesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa.
Andalieni humo.”
13 Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa
amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.

Karamu ya Bwana
\r
\is (Mat. 26:26-30; Marko 14:22-26;1 Kor. 11:23-25)
\ie

14 Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.
15 Akawaambia, “Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla
ya kuteswa kwangu.
16 Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika
Ufalme wa Mungu.”

17 Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema, “Pokeeni, mgawanye
ninyi kwa ninyi.
18 Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka
Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

19 Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema,
“Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa
kunikumbuka.”
20 Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema,
“Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu
inayomwagika kwa ajili yenu.fd
\fm d
\fr 22:19b-20
\fk Huu ni mwili…kwa ajili yenu.”
\f
\is Makala nyingine hazina maneno haya ya Yesu.
\ie

21 “Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani.
22 Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole
wake mtu anayemsaliti.”

23 Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya
jambo hilo.

Ubishi juu ya ukuu

24 Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao
anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko wengine.
25 Yesu akawaambia, “Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa
mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu.
26 Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni
lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi.
27 Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula
chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula
chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.

28 “Ninyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu;
29 na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyo hivyo nami
nitawakabidhi ninyi Ufalme.
30 Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na mtaketi
katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Yesu anabashiri kwamba Petro atamkana

(Mat.26:31-35; Marko 14:27-31; Yoh. 13:36-38)

31 “Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta ninyi kama
mtu anavyopepeta ngano.
32 Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe
utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.”
33 Naye Petro akamjibu, “Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe
gerezani, na hata kufa.”
34 Yesu akamjibu, “Nakwambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo
utakuwa umenikana mara tatu.”

Wakati wa hatari

35 Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, “Wakati nilipowatuma bila
mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?” Wakajibu,
“La.”
36 Naye akawaambia, “Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha
auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga,
auze koti lake anunue mmoja.
37 Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: <Aliwekwa
kundi moja na wahalifu,> ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu
yanafikia ukamilifu wake.”
38 Nao wakasema, “Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili.” Naye
akasema, “Basi!”

Yesu anasali
\r
\is (Mat. 26:36-46; Marko 14;32-42)
\ie

39 Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika
mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata.
40 Alipofika huko akawaambia, “Salini, msije mkaingia katika
kishawishi.”
41 Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe,
akapiga magoti, akasali:
42 “Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo,
mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.”
43 Hapo, malaika kutoka mbinguni, akamtokea ili kumtia moyo.
44 Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho
likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.fe
\fm e
\fr 22:43-44
\f Baadhi ya Makala hazina aya hizi.
\il 5
ic
\is Mlima wa Mizeituni (Luka 22:39)
\ie

45 Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala,
kwani walikuwa na huzuni.
46 Akawaambia, “Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika
kishawishi.”

Yesu anatiwa nguvuni
\r
\is (Mat. 26:47-56; Marko 14:43-50; Yoh. 18:3-11)
\ie

47 Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule
aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda
kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
48 Lakini Yesu akamwambia, “Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa
kumbusu?”
49 Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, “Bwana, tutumie
panga zetu?”
50 Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata
sikio lake la kulia.
51 Hapo, Yesu akasema, “Acha! Hii inatosha.” Akaligusa sikio la
mtu huyo akaliponya.

52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa
Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu
kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?
53 Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku Hekaluni hamkunitia nguvuni.
Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza.”

Petro anamkana Yesu
\r
\is (Mat. 26:57-58; Marko 14:53-54,66-72; Yoh. 18:12-18,25-27)
\ie

54 Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa Kuhani
Mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali.
55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja
Petro akiwa miongoni mwao.
56 Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto,
akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu.”
57 Lakini Petro akakana akisema, “Wee! simjui mimi.”
58 Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe ni
mmoja wao.” Lakini Petro akajibu “Bwana we; si mimi!”

59 Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, “Hakika huyu
alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati.”
60 Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na
papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.

61 Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale
aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara
tatu.”
62 Hapo akatoka nje, akalia sana.

Yesu anadhihakiwa na kupigwa
\r
\is (Mat. 26:67-68; Marko 14:65)
\ie

63 Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki.
64 Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, “Ni nani
aliyekupiga? Hebu bashiri tuone!”
65 Wakamtolea maneno mengi ya matusi.

Yesu mbele ya Baraza
\r
\is (Mat. 26:59-66; Marko 14:55-64; Yoh. 18:19-24)
\ie

66 Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho
kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele
ya Baraza hilo.
67 Nao wakamwambia, “Twambie! Je, wewe ndiwe Kristo?” Lakini Yesu
akawaambia, “Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki;
68 na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu.
69 Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia
wa Mungu Mwenyezi.”

70 Hapo wote wakasema, “Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?” Naye
akasema, “Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye.”
71 Nao wakasema, “Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe
tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe.”sw4323

\c 23

Yesu mbele ya Pilato
\r
\is (Mat. 27:1-2,11-14; Marko 15:1-5; Yoh. 18:28-38)
\ie

1 Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya
Pilato.
2 Wakaanza kumshtaki wakisema: “Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha
watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni
Kristo, Mfalme.”
3 Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Yesu
akamjibu, “Wewe umesema.”
4 Pilato akawaambia makuhani wakuu na umati wa watu, “Sioni kosa
lolote katika mtu huyu.”
5 Lakini wao wakasisitiza wakisema: “Anawachochea watu kwa
mafundisho yake katika nchi yote ya Yudea; alianza Galilaya, na sasa
yuko hapa.”

Yesu anapelekwa kwa Herode

6 Pilato aliposikia hayo, akauliza, “Je, mtu huyu ni mwenyeji wa
Galilaya?”
7 Alipojua kwamba Yesu alikuwa chini ya utawala wa Herode,
akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa Yerusalemu.

8 Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia
habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa
macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu
akitenda mwujiza.
9 Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu
hakumjibu neno.
10 Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakajitokeza mbele, wakatoa
mashtaka yao kwa nguvu sana.
11 Basi, herode pamoja na maaskari wake, wakamwaibisha Yesu na
kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa
Pilato.
12 Herode na Pilato, ambao hapo awali walikuwa maadui, tangu siku
hiyo wakawa marafiki.

Yesu ahukumiwa kifo
\r
\is (Mat. 27:17-26; Marko 15:6-15; Yoh. 18:39-19:16)
\ie

13 Basi, Pilato akaitisha mkutano wa makuhani wakuu, viongozi na
watu,
14 akawaambia, “Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa
anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele
yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.
15 Wala si mimi tu, bali hata Herode hakuona kosa lolote, kwa maana
amemrudisha kwangu. Ni dhahiri kwamba mtu huyu hakufanya chochote
kinachostahili adhabu ya kifo.
16 Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia.”ff
\fm f
\fr 23:16
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 17:
\ie Kila sikukuu ya Pasaka, ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa
mmoja.

17 missing
18 Lakini wote wakapiga kelele pamoja: “Mwondoe huyo, utufungulie
Baraba!” (((
19 Baraba alikuwa ametiwa ndani kwa kusababisha uasi katika mji na
pia kwa sababu ya kuua.)

20 Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena;
21 lakini wao wakapiga kelele: “Msulubishe, msulubishe!”
22 Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanya kosa gani? Sioni kosa
lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu
nimwachilie.”

23 Lakini wao wakazidi kupiga kelele kwa nguvu sana, kwamba Yesu ni
lazima asulubiwe. Mwishowe, sauti zao zikashinda.
24 Basi, Pilato akaamua kwamba matakwa yao yatimizwe.
25 Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa
ametiwa gerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoa Yesu kwao,
wamfanyie walivyotaka.

Yesu anasulubiwa msalabani
\r
\is (Mat. 27:32-44; Marko 15:21-32; Yoh. 19:17-27)
\ie

26 Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni
wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule
msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
27 Watu, umati kwa umati, walimfuata; miongoni mwao wakiwemo
wanawake waliokuwa wanaomboleza na kumlilia.
28 Yesu akawageukia, akasema, “Enyi kina mama wa Yerusalemu!
Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya watoto
wenu.
29 Maana, hakika siku zitakuja ambapo watasema: <Heri yao wale walio
tasa, ambao hawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto!>
30 Wakati huo, ndipo watu wataanza kuiambia milima: <Tuangukieni!>
na vilima, <Tufunikeni!>
31 Kwa maana, kama watu wanautendea mti mbichi namna hiyo, itakuwaje
kwa mti mkavu?”

32 Waliwachukua pia watu wengine wawili, wahalifu, wauawe pamoja
naye.
33 Walipofika mahali paitwapo, “Fuvu la Kichwa,” ndipo
wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa
kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.”
Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
35 Watu wakawa wamesimama pale wakitazama. Nao viongozi wakamdhihaki
wakisema: “Amewaokoa wengine; sasa na ajiokoe mwenyewe, kama yeye ndiye
Kristo, mteule wa Mungu!”
36 Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki
37 wakisema: “Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe
mwenyewe.”

38 Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake:
“Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.”

39 Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana
akisema: “Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe,
utuokoe na sisi pia.”
40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: “Wewe
humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.
41 Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale
tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”
42 Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika
ufalme wako.”
43 Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami
peponi.”

Yesu anakufa msalabani
\r
\is (Mat. 27:45-56; Marko 15:33-41; Yoh. 19:28-30)
\ie

44 Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza
likafunika nchi yote mpaka saa tisa,
45 na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka vipande
viwili.
46 Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, naiweka roho yangu mikononi
mwako.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
\il 5
ic
\is Msalaba na mawingu (Luka 23:44)
\ie

47 Hapo, yule jemadari alipoona yaliyotukia akamsifu Mungu akisema:
“Hakika huyu alikuwa mtu mwema.”
48 Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio
hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa
huzuni.
49 Marafiki zake wote pamoja na wale wanawake walioandamana naye
kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali kutazama tukio hilo.

Mazishi ya Yesu
\r
\is (Mat. 27:57-61; Marko 15:42-47; Yoh. 19:38-42)
\ie

50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yosefu, mwenyeji wa kijiji kimoja
cha Wayahudi kiitwacho Armathaya. Alikuwa mtu mwema anayeheshimika;
51 Alikuwa akitazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja
wa Baraza kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.
52 Basi, yeye alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.
53 Kisha, akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda
ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba,
ambalo halikuwa limetumika.
54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa
yanaanza.

55 Wale wanawake walioandamana na Yesu kutoka Galilaya walimfuata
Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa
56 Halafu, walirudi nyumbani, wakatayarisha manukato na marashi
kuyapaka mwili wa Yesu.
Siku ya Sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria.

\c 24

Kufufuka kwa Yesu
\r
\is (Mat. 28:1-10; Marko 16:1-18; Yoh. 20:1-10)
\ie

1 Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini
wakichukua yale manukato waliyotayarisha.
2 Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi.
3 Walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu.
4 Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili
waliovaa mavazi yenye kung’aa sana, wakasimama karibu nao.
5 Hao wanawake wakaingiwa na hofu, wakainama chini. Ndipo wale watu
wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu?
6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni aliyowaambieni alipokuwa kule
Galilaya:
7 <Ni lazima Mwana wa Mtu atolewe kwa watu waovu, nao
watamsulubisha, na siku ya tatu atafufuka.”>

8 Hapo wanawake wakayakumbuka maneno yake,
9 wakarudi kutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumi na mmoja na
wengine habari za mambo hayo yote.
10 Hao waliotoa habari hizo kwa mitume ni: Maria Magdalene, Yoana na
Maria mama wa Yakobo, pamoja na wanawake wengine walioandamana nao.
11 Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo
hawakuamini.
12 Lakini Petro alitoka, akaenda mbio hadi kaburini. Alipoinama
kuchungulia ndani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbani huku akiwa
anashangaa juu ya hayo yaliyotokea.

Safari kwenda Emau
\r
\is (Marko 16:12-13)
\ie

13 Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda
katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja
kutoka Yerusalemu.
14 Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia.
15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea,
akatembea pamoja nao.
16 Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua.

17 Akawauliza, “Mnazungumza nini huku mnatembea?” Nao wakasimama
kimya, nyuso zao wamezikunja kwa huzuni.
18 Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgeni peke yako
Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?”
19 Naye akawajibu, “Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mambo
yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda
na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
20 Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa,
wakamsulubisha.
21 Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiye angeikomboa Israeli.
Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka.
22 Tena, wanawake wengine wa kwetu wametushtua. Walikwenda kaburini
mapema asubuhi,
23 wasiukute mwili wake. Wakarudi wakasema kwamba walitokewa na
malaika waliowaambia kwamba alikuwa hai.
24 Wengine wetu walikwenda kaburini wakashuhudia yale waliyosema hao
wanawake; ila yeye hawakumwona.”

25 Kisha Yesu akawaambia, “Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo
yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii?
26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu
wake?”
27 Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko
Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.

28 Walipokikaribia kile kijiji walikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya
kana kwamba anaendelea na safari;
29 lakini wao wakamsihi wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana
kunakuchwa, na usiku unakaribia.” Basi, akaingia kijijini, akakaa
pamoja nao.
30 Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki,
akaumega, akawapa.
31 Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka
kati yao.
32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu
wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”
33 Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu: wakawakuta wale
mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika
34 wakisema, “Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni.”
35 Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani,
na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.

Yesu anawatokea wanafunzi wake
\r
\is (Mat. 28:16-20; Marko 16:14-18; Yoh. 20:19-23; Mate. 1:6-8)
\ie

36 Wanafunzi wote wawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe
akasimama kati yao, akawaambia “Amani kwenu.”
37 Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.
38 Lakini yeye akawaambia, “Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na
mashaka mioyoni mwenu?
39 Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe.
Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.”

40 Baada ya kusema hayo, akawaonyesha mikono na miguu.
41 Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao,
na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, “Mnacho chakula chochote hapa?”
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.
43 Akakichukua, akala, wote wakimwona.
44 Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia
nilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote
yaliyoandikwa juu yangu katika Sheria ya Mose na katika vitabu vya
manabii na katika kitabu cha Zaburi.”

45 Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko
Matakatifu.
46 Akawaambia, “Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na
siku ya tatu atafufuka kutoka wafu,
47 na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia na
Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu na kusamehewa dhambi.
48 Ninyi ni mashahidi wa mambo hayo.
49 Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma,
lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”

Yesu anapaa mbinguni
\r
\is (Marko 16:19-20; Mate. 1:9-11)
\ie

50 Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake
juu, akawabariki.
51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.
52 Wao wakamwabudu, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:
53 wakakaa muda wote Hekaluni wakimsifu Mungu.