\h MATHAYO

          INJILI KAMA ILIVYOANDIKWA NA
                 MATHAYO

\c 1

Ukoo wa Yesu Kristo
\r
\is (Luka 3:23-38)
\ie

1 Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo
orodha ya ukoo wake:

2 Abrahamu alimzaa Isaka,

Isaka alimzaa Yakobo,
Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake,

3 Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari),

Faresi alimzaa Hesroni,
Hesroni alimzaa Rami,

4 Rami alimzaa Aminadabu,

Aminadabu alimzaa Nashoni,
Nashoni alimzaa Salmoni,

5 Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu).

Boazi na Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi,
Obedi alimzaa Yese,

6 naye Yese alimzaa Mfalme Daudi.

Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa mke wa Uria).

7 Solomoni alimzaa Rehoboamu,

Rehoboamu alimzaa Abiya,
Abiya alimzaa Asa,

8 Asa alimzaa Yehoshafati,

Yehoshafati alimzaa Yoramu,
Yoramu alimzaa Uzia,

9 Uzia alimzaa Yothamu,

Yothamu alimzaa Ahazi,
Ahazi alimzaa Hezekia,

10 Hezekia alimzaa Manase,

Manase alimzaa Amoni,
Amoni alimzaa Yosia,

11 Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni.

12 Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni:

Yekonia alimzaa Shealtieli,
Shealtieli alimzaa Zerobabeli,

13 Zerobabeli alimzaa Abiudi,

Abiudi alimzaa Eliakimu,
Eliakimu alimzaa Azori,

14 Azori alimzaa Zadoki,

Zadoki alimzaa Akimu,
Akimu alimzaa Eliudi,

15 Eliudi alimzaa Eleazeri,

Eleazeri alimzaa Mathani,
Mathani alimzaa Yakobo,

16 Yakobo alimzaa Yosefu, aliyekuwa mume wake Maria, mama yake Yesu,
aitwaye Kristo.

17 Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka
Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa
mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka
wakati wa Kristo.

Kuzaliwa kwa Yesu
\r
\is (Luka 2:1-7)
\ie

18 Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake,
alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na
mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
19 Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha
hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.
20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea
katika ndoto, akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua
Maria awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
21 Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye
atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”

22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema
kwa njia ya nabii:

23 “Bikira atachukua mimba,

atamzaa mtoto wa kiume,
naye ataitwa Emanueli”
(maana yake, “Mungu yu pamoja nasi”).
\m
24 Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo
alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani.
25 Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa
kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.

\c 2

Wageni kutoka mashariki

1 Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode
alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota
kutoka mashariki walifika Yerusalemu,
2 wakauliza, “Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa?
Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.”

3 Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi
wote wa Yerusalemu.
4 Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria,
akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”
5 Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii
alivyoandika:

6 <Ewe Bethlehemu katika nchi ya Yuda,

kwa vyovyote wewe si mdogo kabisa kati ya viongozi wa Yuda;
maana kwako atatokea kiongozi
atakayewaongoza watu wangu, Israeli.”>

7 Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza
wakati hasa ile nyota ilipowatokea.
8 Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa
makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami
niende nikamwabudu.”

9 Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda.
Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia
hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
10 Walipoiona hiyo nyota, walifurahi mno.
11 Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria
mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao,
wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane.
\il 5
ic
\is Ubani (Mat. 2:11)
\ie

12 Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode; hivyo wakarudi
makwao kwa njia nyingine.

Kukimbilia Misri

13 Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu
katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake,
mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode
anakusudia kumwua huyu mtoto.”

14 Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake,
akaondoka usiku, akaenda Misri.
15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili
neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie:

“Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”

Watoto wachanga wanauawa

16 Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa
wamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuru watoto wote wa kiume mjini
Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake
wauawe. Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale
wataalamu wa nyota.
17 Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia:

18 “Sauti imesikika mjini Rama,

kilio na maombolezo mengi.
Raheli anawalilia watoto wake,
wala hataki kutulizwa,
maana wote wamefariki.”

Kutoka Misri

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu
katika ndoto kule Misri,
20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena
katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo
wamekwisha kufa.”
21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake,
akarejea katika nchi ya Israeli.

22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa
mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya
kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya,
23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno
yaliyonenwa kwa njia ya manabii:

“Ataitwa Mnazare.”

\c 3

Mahubiri ya Yohane Mbatizaji
\r
\is (Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yoh. 1:19-28)
\ie

1 Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa
la Yudea:
2 “Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
3 Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake
aliposema:

“Sauti ya mtu imesikika jangwani:
<Mtayarishieni Bwana njia yake,
nyoosheni vijia vyake.”>

4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda
wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya
mwituni.
5 Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu
zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
6 wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.

7 Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili
awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea
kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
8 Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
9 Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, <Baba yetu ni
Abrahamu!> Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe
watoto wa Abrahamu.
10 Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti
usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
11 Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini
yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata
kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure
nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto
usiozimika.”
\il 5
ic
\is Kupura nafaka (Mat. 3:12)
\ie

Yesu anabatizwa
\r
\is (Marko 1:9-11; Luka 3:21-22)
\ie

13 Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani,
akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
14 Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, “Je, wewe unakuja
kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.”
15 Lakini Yesu akamjibu, “Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa
namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka.” Hapo Yohane
akakubali.

16 Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla
mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua
juu yake.
17 Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa,
nimependezwa naye.”
\fr 3:17
\f Taz Zab 2:7

\c 4

Kujaribiwa kwa Yesu
\r
\is (Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)
\ie

1 Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na
Ibilisi.
2 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
3 Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa
Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu:

<Binadamu hataishi kwa mikate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.”>

5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka
juu ya mnara wa hekalu,
6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana
imeandikwa:

<Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.”>

7 Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:

<Usimjaribu Bwana, Mungu wako.”>

8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha
falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9 akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na
kuniabudu.”
10 Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:

<Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.”>

11 Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
\fr 4:6
\f Taz Zab 91:11-12

Yesu anaanza kazi Galilaya
\r
\is (Marko 1:14-15; Luka 4:14-15)
\ie

12 Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda
Galilaya.
13 Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari
ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
14 Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii
Isaya:

15 “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,

kuelekea baharini ng’ambo ya mto Yordani,
Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!

16 Watu waliokaa gizani

wameona mwanga mkubwa.
Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo,
mwanga umewaangazia!”

17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana
ufalme wa mbinguni umekaribia!”

Yesu anawaita wavuvi wanne
\r
\is (Marko 1:16-20; Luka 5:1-11)
\ie

18 Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu
wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa
wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
19 Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa
watu.”
20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
\il 5
ic
\is Wavuvi (Mat. 4:18)
\ie

21 Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo
na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba
yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,
22 nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.

Yesu anafundisha watu na kuponya wagonjwa
\r
\is (Luka 6:17-19)
\ie

23 Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha
katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu.
Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
24 Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote
wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya
taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa,
walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
25 Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu,
Yudea na ng’ambo ya mto Yordani, walimfuata.

\c 5

Hotuba mlimani

1 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi.
Wanafunzi wake wakamwendea,
2 naye akaanza kuwafundisha:

Furaha ya kweli
\r
\is (Luka 6:20-23)
\ie

3 “Heri walio maskini rohoni,

maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4 Heri walio na huzuni,

maana watafarijiwa.

5 Heri walio wapole,

maana watairithi nchi.

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu,

maana watashibishwa.

7 Heri walio na huruma,

maana watahurumiwa.

8 Heri wenye moyo safi,

maana watamwona Mungu.

9 Heri wenye kuleta amani,

maana wataitwa watoto wa Mungu.

10 Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu,

maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11 “Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na
kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
12 Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo
ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
\fr 5:5
\f Taz Zab 37:11
\fr 5:8
\f Taz Zab 24:3-4

Chumvi na mwanga
\r
\is (Marko 9:50; Luka 14:34-35)
\ie

13 “Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake
itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na
watu.

14 “Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima
hauwezi kufichika.
15 Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu
ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili
wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

Kuhusu Sheria

17 “Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho
ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
18 Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita,
hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa,
mpaka yote yametimia.
19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na
kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika
Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine,
huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
20 Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na
walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.

Kuhusu hasira
\r
\is (Luka 12:57-59)
\ie

21 “Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: <Usiue!
Atakayeua lazima ahukumiwe.>
22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake,
lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani.
Anayemwita ndugu yake: <Pumbavu> atastahili kuingia katika moto wa
Jehanamu.
23 Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka
kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na
ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.

25 “Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda
mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu
atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
26 Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya
mwisho.

Kuhusu uzinzi

27 “Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: <Usizini!>
28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha zini naye moyoni mwake.
29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling’oe ukalitupe
mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako,
kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.
30 Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali.
Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote
uende katika moto wa Jehanamu.

Kuhusu talaka
\r
\is (Mat. 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18)
\ie

31 “Ilikwisha semwa pia: <Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati
ya talaka.>
32 Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa
sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa
talaka, anazini.

Kuhusu kiapo

33 “Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: <Usivunje kiapo
chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.>
34 Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni
kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa
Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele
mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Ukisema, <Ndiyo>, basi iwe <Ndiyo>; ukisema <Siyo>, basi iwe
kweli <Siyo>. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
\fr 5:35
\f Taz Zab 48:2

Kuhusu kulipiza kisasi
\r
\is (Luka 6:29-30)
\ie

38 “Mmesikia kwamba ilisemwa: <Jicho kwa jicho, jino kwa jino.>
39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu
akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
40 Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache
achukue pia koti lako.
41 Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe
kilomita mbili.
42 Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.

Kuwapenda maadui
\r
\is (Luka 6:27-28, 32-36)
\ie

43 “Mmesikia kwamba ilisemwa: <Mpende jirani yako na kumchukia adui
yako.>
44 Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale
wanaowadhulumu ninyi
45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye
huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu
wanyofu na waovu.
46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi?
Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
47 Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha
kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo
mkamilifu.

\c 6

Kuhusu kuwasaidia maskini

1 “Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi
mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.

2 “Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki
wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli
nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
3 Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata rafiki
yako asijue ufanyalo.
4 Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika,
atakutuza.

Kuhusu sala
\r
\is (Luka 11:2-4)
\ie

5 “Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na
kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli
nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
6 Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha
umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika,
atakutuza.

7 “Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao
hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
8 Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya
kumwomba.
9 Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali:

<Baba yetu uliye mbinguni:
Jina lako litukuzwe.

10 Ufalme wako ufike.

Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.

11 Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.

12 Utusamehe makosa yetu,

kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.

13 Usitutie katika majaribu,

lakini utuokoe na yule Mwovu.>fa
\fm a
\fr 6:13
\f
\is Baadhi ya makala za zamani zina; Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu,
na utukufu, hata milele. Amina.
\ie

14 “Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi pia.
15 Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe
ninyi makosa yenu.

Kuhusu kufunga

16 “Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso
zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao
wamekwisha pata tuzo lao.
17 Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako,
18 ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba
yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika atakutuza.

Hazina mbinguni
\r
\is (Luka 12:33-34)
\ie

19 “Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu,
na wezi huingia na kuiba.
20 Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi
kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.
21 Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.

Mwanga wa mwili
\r
\is (Luka 11:34-36)
\ie

22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote
utakuwa katika mwanga.
23 Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa katika
giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza
la kutisha mno.

Mungu na mali
\r
\is (Luka 16:13)
\ie

24 “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia
mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau
huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.

Wasiwasi
\r
\is (Luka 12:22-31)
\ie

25 “Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na
kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa
ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si
zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana
ghala yoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si
wa thamani kuliko hao?
27 Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza
kuuongeza muda wa maisha yake?

28 “Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya
porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
29 Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote
hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
30 Ikiwa basi Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko
na kesho latupwa motoni, je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyi watu
wenye imani haba!

31 “Basi, msiwe na wasiwasi: <Tutakula nini, tutakunywa nini,
tutavaa nini!>
32 Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu
wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.
33 Bali, zingatieni kwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo
mengine yote mtapewa kwa ziada.
34 Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo
ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.

\c 7

Kuhusu kuwahukumu wengine
\r
\is (Luka 6:37-38, 41-42)
\ie

1 “Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
2 kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi
mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho
Mungu atakachotumia kwenu.
3 Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo
hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
4 Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, <Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi
jichoni mwako>, wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
5 Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo
ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni
mwa ndugu yako.

6 “Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua
ninyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.

Omba, tafuta, bisha
\r
\is (Luka 11:9-13)
\ie

7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi
mtafunguliwa.
8 Maana, aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye hufunguliwa.
9 Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate,
atampa jiwe?
10 Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka?
11 Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu
vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale
wanaomwomba.

12 “Watendeeni wengine yale mnayotaka wao wawatendee ninyi. Hii
ndiyo maana ya Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.

Mlango mwembamba
\r
\is (Luka 13:24)
\ie

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia
inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni
mpana; waendao njia hiyo ni wengi.
14 Lakini njia inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba, na mlango wa
kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua
njia hiyo.

Mti hujulikana kwa matunda yake
\r
\is (Luka 6:43-44)
\ie

15 “Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana
kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti
ya miiba, au tini katika mbigili? La!
17 Basi, mti mwema huzaa matunda mema, na mti mbaya huzaa matunda
mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi
kuzaa matunda mema.
19 Kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa motoni.
20 Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao.
\il 5
ic
\is Mti hujulikana kwa matunda yake (Mat. 7:16)
\ie

Siwajui ninyi
\r
\is (Luka 13:25-27)
\ie

21 “Si kila aniambiaye, <Bwana, Bwana,> ataingia katika Ufalme wa
mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni.
22 Wengi wataniambia Siku ile ya hukumu: <Bwana, Bwana! kwa jina
lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya
miujiza mingi.>
23 Hapo nitawaambia: <Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu,
enyi watenda maovu.>
\fr 7:23
\f Taz Zab 6:8

Wajenzi wawili
\r
\is (Luka 6:47-49)
\ie

24 “Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na
kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu
ya mwamba.
25 Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga
nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya
mwamba.

26 “Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia,
anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
27 Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga
nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena kwa kishindo kikubwa.”

Mamlaka ya Yesu

28 Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa
na mafundisho yake.
29 Hakuwa kama walimu wao wa Sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.

\c 8

Yesu anamponya mtu mwenye ukoma
\r
\is (Marko 1:40-45; Luka 5:12-16)
\ie

1 Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata.
2 Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, “Bwana,
ukitaka, waweza kunitakasa!”
3 Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, “Nataka!
Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
4 Kisha Yesu akamwambia, “Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila
nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose
kuwathibitishia kwamba umepona.”

Yesu anamponya mtumishi wa ofisa Mroma
\r
\is (Luka 7:1-10)
\ie

5 Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, ofisa mmoja Mroma
alimwendea, akamsihi
6 akisema, “Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa
kupooza na anaumwa sana.”

7 Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.”
8 Huyo ofisa akamwambia, “Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani
mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
9 Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao
askari chini yangu. Namwambia mmoja, <Nenda!> naye huenda; na mwingine,
<Njoo!> naye huja; na mtumishi wangu, <Fanya kitu hiki!> naye hufanya.”

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa
wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika
Israeli aliye na imani kama hii.
11 Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na
magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo
katika Ufalme wa mbinguni.
12 Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa
nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno.”
13 Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, “Nenda nyumbani; na iwe
kama ulivyoamini.” Na mtumishi wake akapona saa ileile.

Yesu anaponya watu wengi
\r
\is (Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)
\ie

14 Yesu alifika nyumbani kwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petro
amelala kitandani, ana homa kali.
15 Basi, Yesu akamgusa huyo mama mkono, na homa ikamwacha;
akasimama, akamtumikia.

16 Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na
pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia
watu wote waliokuwa wagonjwa.
17 Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie:

“Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu,
ameyachukua magonjwa yetu.”

Wanaostahili kuwa wafuasi
\r
\is (Luka 9:57-62)
\ie

18 Yesu alipoona kundi la watu limemzunguka, aliwaamuru wanafunzi
wake waende ng’ambo ya ziwa.
19 Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, “Mwalimu, mimi
nitakufuata kokote uendako.”
20 Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini
Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.”

21 Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia,
“Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu.”
22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao.”

Yesu anaamuru dhoruba itulie
\r
\is (Marko 4:35-41; Luka 8:22-25)
\ie

23 Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye.
24 Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza
kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi.
25 Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe,
tunaangamia!”
26 Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?”
Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.
27 Watu wakashangaa, wakasema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata
pepo na mawimbi vinamtii!”

Yesu anaponya watu wawili wenye pepo wabaya
\r
\is (Marko 5:1-20; Luka 8:26-39)
\ie

28 Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi,fb ng’ambo ya ziwa, na
huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea
makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu
aliyethubutu kupita katika njia hiyo.
29 Nao wakaanza kupiga kelele, “Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa
Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?”
\fm b
\fr 8:28
\fk Wagerasi;
\f
\is au
\ie Gadara.

30 Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa.
31 Basi, hao pepo wakamsihi, “Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu
tuwaingie nguruwe wale.”
32 Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao,
wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule
mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.

33 Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko
walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa
wamepagawa.
34 Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na
walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.

\c 9

Yesu anamponya mtu aliyepooza
\r
\is (Marko 2:1-12; Luka 5:17-26)
\ie

1 Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake.
2 Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya
kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Jipe
moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako.”
3 Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, “Mtu huyu
anamkufuru Mungu!”

4 Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, “Kwa nini mnawaza mabaya
mioyoni mwenu?
5 Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, <Umesamehewa dhambi zako>, au
kusema, <Simama, utembee>?
6 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe
watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Inuka,
chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.”

7 Huyo mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akaenda nyumbani kwake.
8 Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa;
wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.

Mathayo anaitwa
\r
\is (Marko 2:13-17; Luka 5:27-32)
\ie

9 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu
mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu
akamwambia, “Nifuate.” Naye Mathayo akainuka, akamfuata.

10 Yesu alipokuwa nyumbanifc ameketi kula chakula, watoza ushuru
wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
11 Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, “Mbona
mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
\fm c
\fr 9:10
\fk nyumbani;
\f
\is yaani nyumbani kwa Mathayo.
\ie

12 Yesu aliwasikia, akasema, “Watu wenye afya hawahitaji daktari;
wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye
dhambi.
13 Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: <Nataka huruma, wala si
dhabihu.> Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”

Suala juu ya kufunga
\r
\is (Marko 2:18-22; Luka 5:33-39)
\ie

14 Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu,
wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi
wako hawafungi?”
15 Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza
wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika
ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.

16 “Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu.
Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa
pameraruka pataongezeka.
17 Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu.
Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba
vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote
viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”

Binti wa ofisa na mama mmoja wanaponywa
\r
\is (Marko 5:21-43; Luka 8:40-56)
\ie

18 Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika,
akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini,
tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi.”
19 Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake, akamfuata.

20 Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na
miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
21 Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: “Nikigusa tu vazi lake,
nitapona.”
22 Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, “Binti, jipe moyo!
Imani yako imekuponya.” Mama huyo akapona saa ileile.

23 Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga
filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
24 akasema, “Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu.” Nao
wakamcheka.
25 Basi, umati wa watu ulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshika
huyo msichana mkono, naye akasimama.
26 Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote.

Yesu anaponya vipofu wawili

27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili
walimfuata wakipiga kelele, “Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
28 Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye
akawauliza, “Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?” Nao
wakamjibu, “Naam, Mheshimiwa.”
29 Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, “Na iwe kwenu kama
mnavyoamini.”
30 Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali:
“Msimwambie mtu yeyote jambo hili.”
31 Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile
yote.

Yesu anamponya bubu

32 Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja
aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
33 Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza
kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, “Jambo kama hili halijapata
kuonekana katika Israeli!”
34 Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, “Anawatoa pepo kwa nguvu ya
mkuu wa pepo wabaya.”

Yesu anawahurumia watu

35 Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika
masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya
magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
36 Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa
sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
37 Hapo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi, lakini
wavunaji ni wachache.
38 Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.”

\c 10

Mitume kumi na wawili
\r
\is (Marko 3:13-19; Luka 6:12-16)
\ie

1 Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kutoa
pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
2 Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni
aitwae Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane
ndugu yake;
3 Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtoza ushuru;
Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;
4 Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.

Yesu anawatuma mitume kumi na wawili
\r
\is (Marko 6:7-13; Luka 9:1-6)
\ie

5 Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya:
“Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa
Wasamaria.
6 Ila nendeni kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo.
7 Mnapokwenda hubirini hivi: <Ufalme wa mbinguni umekaribia.>
8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo.
Mmepewa bure, toeni bure.
9 Msichukue mifukoni mwenu dhahabu, wala fedha, wala sarafu za
shaba.
10 Msichukue mkoba wa kuombea njiani, wala koti la ziada, wala
viatu, wala fimbo. Maana mfanyakazi anastahili riziki yake.

11 “Mkiingia katika mji wowote au kijiji, tafuteni humo mtu yeyote
aliye tayari kuwakaribisheni, na kaeni naye mpaka mtakapoondoka mahali
hapo.
12 Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake.
13 Kama wenyeji wa nyumba hiyo wakiipokea salamu hiyo, basi, amani
yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei, basi amani yenu
itawarudia ninyi.
14 Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi
mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakung’uteni mavumbi miguuni
mwenu kama onyo kwao.
15 Kweli nawaambieni, Siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa
kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.

Udhalimu
\r
\is (Marko 13:9-13; Luka 21:12-17)
\ie

16 “Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe
na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
17 Jihadharini na watu, maana watawapeleka ninyi mahakamani na
kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
18 Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate
kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
19 Basi, watakapowapeleka ninyi mahakamani, msiwe na wasiwasi
mtasema nini au namna gani; wakati utakapofika, mtapewa la kusema.
20 Maana si ninyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye
ndani yenu.

21 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanawe,
nao watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
22 Watu wote watawachukieni kwa sababu ya jina langu. Lakini
atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.

23 “Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine.
Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli
kabla Mwana wa Mtu hajafika.

24 “Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu
kuliko bwana wake.
25 Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama
bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaita
watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?

Anayestahili kuogopwa
\r
\is (Luka 12:2-7)
\ie

26 “Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na
kila kilichofichwa kitafichuliwa.
27 Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na
jambo mlilosikia likinong’onezwa, litangazeni hadharani.
28 Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali
zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika
moto wa Jehanamu.
29 Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakini hata mmoja wao
haanguki chini bila kibali cha Baba yenu.
30 Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa
zote.
31 Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamani kuliko shomoro wengi.
\il 5
ic
\is Shomoro (Mat. 10:29)
\ie

Kumkiri na kumkana Kristo
\r
\is (Luka 12:8-9)
\ie

32 “Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia
nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
33 Lakini yeyote atakayenikana hadharani, nami nitamkana mbele ya
Baba yangu aliye mbinguni.

Mafarakano
\r
\is (Luka 12:51-53; 14:26-27)
\ie

34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta
amani bali upanga.
35 Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati
ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake.
36 Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.

37 “Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi,
hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili.
39 Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza
maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.

Tuzo
\r
\is (Marko 9:41)
\ie

40 “Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na
anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
41 Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii, atapokea tuzo la
nabii. Anayemkaribisha mtu mwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokea tuzo
la mtu mwema.
42 Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa
kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwe
kupata tuzo lake.”

\c 11

Ujumbe kutoka kwa Yohane mbatizaji
\r
\is (Luka 7:18-35)
\ie

1 Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzi kumi na wawili maagizo, alitoka
hapo, akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2 Yohane mbatizaji akiwa gerezani alipata habari juu ya matendo ya
Kristo. Basi, Yohane akawatuma wanafunzi wake,
3 wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?”
4 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na
kuyaona:
5 vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa na
viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari
Njema.
6 Heri mtu yule asiyekuwa na mashaka nami.”

7 Basi, hao wajumbe wa Yohane walipokuwa wanakwenda zao, Yesu
alianza kuyaambia makundi ya watu habari za Yohane: “Mlikwenda kutazama
nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
8 Lakini mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumtazama mtu aliyevaa
mavazi maridadi? Watu wanaovaa mavazi maridadi hukaa katika nyumba za
wafalme.
9 Basi, mlikwenda kuona nini? Nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii.

10 “Huyu ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu:

<Tazama, hapa namtuma mjumbe wangu, asema Bwana,
akutangulie na kukutayarishia njia yako.>
\m
11 Kweli nawaambieni, miongoni mwa watoto wote wa watu, hajatokea
aliye mkuu kuliko Yohane mbatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisa
katika Ufalme wa mbinguni, ni mkubwa kuliko yeye.
12 Tangu wakati wa Yohane mbatizaji mpaka leo hii, Ufalme wa
mbinguni unashambuliwa vikali, na watu wakali wanajaribu kuunyakua kwa
nguvu.
13 Mafundisho yote ya manabii na sheria yalibashiri juu ya nyakati
hizi.
14 Kama mwaweza kukubali basi, Yohane ndiye Eliya ambaye angekuja.
15 Mwenye masikio na asikie!

16 “Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana
waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja kwa
kingine:

17 <Tumewapigieni ngoma

lakini hamkucheza;
tumeimba nyimbo za huzuni
lakini hamkulia!>
\m
18 Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao
wakasema: <Amepagawa na pepo.>
19 Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: <Mtazameni
huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wahalifu!> Hata hivyo,
hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”

Miji isiyoamini
\r
\is (Luka 10:13-15)
\ie

20 Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya
miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kubadili nia zao mbaya:
21 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza
iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake
wangalikwisha vaa mavazi ya gunia na kujipaka majivu zamani, ili
kuonyesha kwamba wametubu.
22 Hata hivyo nawaambieni, Siku ya hukumu, ninyi mtapata adhabu
kubwa kuliko Tiro na Sidoni.
23 Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa
mpaka Kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule
Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
24 Lakini nawaambieni, Siku ya hukumu itakuwa nafuu zaidi kwa watu
wa Sodoma, kuliko kwako wewe.”

Njoni kwangu mkapumzike
\r
\is (Luka 10:21-22)
\ie

25 Wakati huo Yesu alisema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu
na dunia, maana umewaficha wenye hekima mambo haya, ukawafumbulia watoto
wadogo.
26 Naam Baba, ndivyo ilivyokupendeza.

27 “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila
Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda
kumjulisha.
28 Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami
nitawapumzisha.
29 Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na
mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu.
30 Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

\c 12

Kuhusu Sabato
\r
\is (Marko 2:23-28; Luka 6:1-5)
\ie

1 Wakati huo, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano siku ya
Sabato. Basi, wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kukwanyua masuke ya
ngano, wakala punje zake.
2 Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi
wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato.”

3 Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na
wenzake wakati walipokuwa na njaa?
4 Yeye aliingia katika Nyumba ya Mungu pamoja na wenzake, wakala ile
mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa
kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
5 Au je, hamjasoma katika Sheria kwamba kila siku ya Sabato makuhani
huivunja Sheria Hekaluni, lakini hawafikiriwi kuwa na hatia?
6 Basi, nawaambieni kwamba hapa pana kikuufd kuliko Hekalu.
7 Kama tu mngejua maana ya maneno haya: <Nataka huruma wala si
dhabihu>, hamngewahukumu watu wasio na hatia.
8 Maana Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato.”
\fm d
\fr 12:6
\fk pana kikuu;
\f
\is Baadhi ya makala za baadaye zina;
\ie yupo mkuu.

Mtu mwenye mkono uliopooza
\r
\is (Marko 3:1-6; Luka 6:6-11)
\ie

9 Yesu alitoka hapo, akaenda katika sunagogi lao.
10 Kulikuwa na mtu mmoja mwenye mkono uliopooza. Basi, watu
wakamwuliza Yesu, “Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato?”
Walimwuliza hivyo wapate kisa cha kumshtaki.

11 Lakini Yesu akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana kondoo wake
ambaye ametumbukia shimoni; je, hatamshika na kumtoa humo siku ya
Sabato?
12 Mtu ana thamani kuliko kondoo! Basi, ni halali kutenda mema siku
ya Sabato.”
13 Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, nao
ukawa mzima kabisa kama ule mwingine.
14 Basi, Mafarisayo wakatoka nje, wakashauriana jinsi
watakavyomwangamiza Yesu.

Mtumishi mteule wa Mungu

15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi
walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,
16 akawaamuru wasiwaambie watu habari zake,
17 ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie:

18 “Hapa ni mtumishi wangu niliyemteua,

mpendwa wangu anipendezaye moyoni.
Nitaiweka Roho yangu juu yake,
naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.

19 Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele,

wala sauti yake haitasikika barabarani.

20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

wala utambi ufukao moshi hatauzima,
mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.

21 Katika jina lake mataifa yatakuwa na tumaini.”

Yesu na Beelzebuli
\r
\is (Marko 3:20-30; Luka 11:14-23)
\ie

22 Hapo watu wakamletea Yesu kipofu mmoja ambaye alikuwa bubu kwa
sababu alikuwa amepagawa na pepo. Yesu akamponya hata, akaweza kusema na
kuona.
23 Umati wote wa watu ulishangaa ukasema, “Je, huenda ikawa huyu
ndiye Mwana wa Daudi?”
24 Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, wakasema, “Mtu huyu
anawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo.”

25 Yesu, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote
uliogawanyika makundimakundi yanayopingana, hauwezi kudumu, na mji
wowote au jamaa yoyote iliyogawanyika makundimakundi yanayopingana,
itaanguka.
26 Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi,
ufalme wake utasimamaje?
27 Ninyi mnasema ati nawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli; je,
watoto wenu huwafukuza kwa uwezo wa nani? Kwa sababu hiyo wao ndio
watakaowahukumu ninyi.
28 Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi
jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.

29 “Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na
kumnyang’anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu?
Hapo ndipo atakapoweza kumnyang’anya mali yake.

30 “Yeyote asiyejiunga nami, anapingana nami; na yeyote
asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.
31 Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru
zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini
yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika
ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

Mti na matunda yake
\r
\is (Luka 6:43-45)
\ie

33 “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mema; ufanyeni
kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda
yake.
34 Enyi kizazi cha nyoka! Mnawezaje kusema mambo mema hali ninyi ni
waovu? Maana mtu husema kutokana na yale yaliyojaa moyoni.
35 Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya
hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.

36 “Basi, nawaambieni, Siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya
kila neno lisilofaa wanalosema.
37 Maana kwa maneno yako, utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno
yako, utahukumiwa kuwa na hatia.”

Kutaka ishara
\r
\is (Marko 8:11-12; Luka 11:29-32)
\ie

38 Kisha baadhi ya walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamwambia Yesu,
“Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”
39 Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka
ishara; hamtapewa ishara nyingine, ila tu ile ishara ya nabii Yona.
40 Jinsi Yona alivyokaa siku tatu kutwa kucha tumboni mwa nyangumi,
ndivyo naye Mwana wa Mtu atakavyokaa ndani ya ardhi siku tatu kutwa
kucha.
41 Watu wa Ninewi watatokea siku ya hukumu, nao watakihukumu kizazi
hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri
ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!
42 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa,
naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali
akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna
kikuufe kuliko Solomoni.
\fm e
\fr 12:41,42
\fk kuna kikuu;
\f Taz 12:6

Kurudi kwa pepo mchafu
\r
\is (Luka 11:24-26)
\ie

43 “Pepo mchafu akifukuzwa kwa mtu, huzururazurura jangwani
akitafuta mahali pa kupumzika asipate.
44 Hapo hujisemea: <Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka.> Lakini
anaporudi na kuikuta tupu, imefagiwa na kupambwa,
45 huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote
huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko
hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”

Jamaa halisi ya Yesu
\r
\is (Marko 3:31-35; Luka 8:19-21)
\ie

46 Yesu alikuwa bado anasema na umati wa watu wakati mama yake na
ndugu zake walipofika na kusimama nje, wakitaka kusema naye.
47 Basi, mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje,
wanataka kusema nawe.”
48 Lakini Yesu akamjibu mtu huyo, “Mama yangu ni nani? Na ndugu
zangu ni kina nani?”
49 Kisha akaunyosha mkono wake kuelekea wanafunzi wake, akasema,
“Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu!
50 Maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni,
huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu.”

\c 13

Mfano wa mpanzi
\r
\is (Marko 4:1-9; Luka 8:4-8)
\ie

1 Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi
kando ya ziwa.
2 Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua,
akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
3 naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano.
“Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja
wakazila.
5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi.
Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
6 Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na
nguvu, zikanyauka.
7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na
kuzisonga.
8 Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa:
nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.
9 Mwenye masikio na asikie!”

Shabaha ya kusema kwa mifano
\r
\is (Marko 4:10-12; Luka 8:9-10)
\ie

10 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, “Kwa nini unasema na
watu kwa mifano?”
11 Yesu akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa
mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
12 Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na
kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
13 Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini
hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
14 Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya:

<Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa;
Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.

15 Maana akili za watu hawa zimepumbaa,

wameyaziba masikio yao,
wameyafumba macho yao.
La sivyo, wangeona kwa macho yao.
wangesikia kwa masikio yao,
wangeelewa kwa akili zao,
na kunigeukia, asema Bwana,
nami ningewaponya.>

16 “Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio
yenu yanasikia.
17 Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona
yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.

Maelezo ya mfano wa mpanzi
\r
\is (Marko 4:13-20; Luka 8:11-15)
\ie

18 “Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
19 Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile
mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile
kilichopandwa moyoni mwake.
20 Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe
huo na mara akaupokea kwa furaha.
21 Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea
kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu
vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara.
22 Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu
asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali
huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda.
23 Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu
ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia,
mwingine sitini na mwingine thelathini.”

Mfano wa magugu

24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni
unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
25 Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati
ya ngano, akaenda zake.
26 Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza
kuonekana.
27 Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia,
<Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa
magugu yametoka wapi?>
28 Yeye akawajibu, <Adui ndiye aliyefanya hivyo.> Basi, watumishi
wake wakamwuliza, <Je, unataka twende tukayang’oe>
29 Naye akawajibu, <La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang’oa na
ngano pia.
30 Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo
nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu
ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.”>

Mfano wa mbegu ya haradali
\r
\is (Marko 4:30-32; Luka 13:18-19)
\ie

31 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni
unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika
shamba lake.
32 Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa
kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga
viota katika matawi yake.”

Mfano wa chachu
\r
\is (Luka 13:20-21)
\ie

33 Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na
chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga
wote ukaumuka.”

Kutumia mifano
\r
\is (Marko 4:33-34)
\ie

34 Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote
bila kutumia mifano,
35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie:

“Nitasema kwa mifano;
nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
\fr 13:35
\f Taz Zab 78:2

Yesu anafafanua mfano wa magugu

36 Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake
wakamwendea, wakamwambia, “Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani.”

37 Yesu akawaambia, “Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao
Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.
39 Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa
nyakati na wavunaji ni malaika.
40 Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo
itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati;
41 Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika
Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda
maovu,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga
meno.
43 Kisha, wale wema watang’ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao.
Sikieni basi, kama mna masikio!

Mfano wa hazina iliyofichika

44 “Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani.
Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza
yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.

Mfano wa lulu

45 “Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja
mwenye kutafuta lulu nzuri.
46 Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote
aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile.

Mfano wa wavu wa samaki

47 “Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini,
ukanasa samaki wa kila aina.
48 Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki
wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.
49 Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea,
watawatenganisha watu wabaya na watu wema,
50 na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na
kusaga meno.”

Hatima

51 Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu,
“Naam.”
52 Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye
mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye
katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

Yesu anakataliwa huko Nazareti
\r
\is (Marko 6:1-6; Luka 4:16-30)
\ie

53 Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo,
54 akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika
sunagogi hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na
maajabu?
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa
Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi
haya yote?”
57 Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii
hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
58 Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini
kwao.

\c 14

Kifo cha Yohane mbatizaji
\r
\is (Marko 6:14-29; Luka 9:7-9)
\ie

1 Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu.
2 Basi, akawaambia watumishi wake, “Mtu huyu ni Yohane mbatizaji,
amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani
yake.”

3 Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo
na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake.
Sababu hasa ni
4 kwamba alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuishi na huyo
mwanamke!”
5 Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao
Yohane alikuwa nabii.

6 Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya
Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa,
7 hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba.
8 Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, “Nipe papahapa
katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji.”
9 Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa
sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe.
10 Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane.
11 Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye
akampelekea mama yake.
12 Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika.
Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.

Yesu anawapa chakula watu zaidi ya elfu tano
\r
\is (Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yoh. 6:1-14)
\ie

13 Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua,
akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari,
wakamfuata kwa miguu toka mijini.
14 Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea
huruma, akawaponya wagonjwa wao.

15 Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia,
“Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende
vijijini wakajinunulie chakula.”
16 Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni ninyi chakula.”
17 Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki
wawili.”
18 Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.”
19 Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate
mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu.
Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
20 Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki,
wakajaza vikapu kumi na viwili.
21 Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila
kuhesabu wanawake na watoto.

Yesu anatembea juu maji
\r
\is (Marko 6:45-52; Yoh. 6:15-21)
\ie

22 Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie
ng’ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.
23 Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa
jioni, yeye alikuwa huko peke yake,
24 na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa,
lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
25 Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea
juu ya maji.
26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na
hofu, wakasema, “Ni mzimu!” Wakapiga kelele kwa hofu.
27 Mara, Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
28 Petro akamwambia, “Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee
juu ya maji nije kwako.”
29 Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile
mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
30 Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa
sauti, “Bwana, niokoe!”
31 Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, “Ewe
mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?”
32 Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.
33 Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, “Hakika
wewe ni Mwana wa Mungu.”

Yesu anaponya wagonjwa Genesareti
\r
\is (Marko 6:53-56)
\ie

34 Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.
35 Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu
hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,
36 wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote
waliomgusa walipona.

\c 15

Mapokeo ya mababu
\r
\is (Marko 7:1-13)
\ie

1 Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheria wakafika kutoka Yerusalemu,
wakamwendea Yesu, wakamwuliza,
2 “Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa
wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!”
3 Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe
na hamuijali Sheria ya Mungu?
4 Mungu amesema: <Waheshimu baba yako na mama yako,> na
<Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe>.
5 Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza
kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: <Kitu hiki
nimemtolea Mungu,>
6 basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno
la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.
7 Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:

8 <Watu hawa, asema Mungu,

huniheshimu kwa maneno tu,
lakini mioyoni mwao wako mbali nami.

9 Kuniabudu kwao hakufai,

maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.”>

Vitu vinavyomtia mtu najisi
\r
\is (Marko 7:14-23)
\ie

10 Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na
muelewe!
11 Kitu kinachomtia mtu najisi si kile kiingiacho kinywani, bali
kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi.”

12 Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, “Je, unajua kwamba
Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?”
13 Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye
mbinguni hakuupanda, utang’olewa.
14 Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu
akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni.”
15 Petro akadakia, “Tufafanulie huo mfano.”
16 Yesu akasema, “Hata nyinyi hamwelewi?
17 Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na
baadaye hutupwa nje chooni?
18 Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo
yanayomtia mtu najisi.
19 Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi,
uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.
20 Hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi. Lakini kula chakula bila kunawa
mikono hakumtii mtu najisi.”

Imani ya mama mmoja
\r
\is (Marko 7:24-30)
\ie

21 Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na
Sidoni.
22 Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti:
“Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na
pepo.”
23 Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi, wanafunzi wake wakamwendea,
wakamwambia, “Mwambie aende zake kwa maana anatufuatafuata akipiga
kelele.”
24 Yesu akajibu, “Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama
kondoo.”
25 Hapo huyo mama akaja, akapiga magoti mbele yake, akasema,
“Mheshimiwa, nisaidie.”
26 Yesu akamjibu, “Si sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia
mbwa.”
27 Huyo mama akajibu, “Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula
makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
28 Hapo Yesu akamjibu, “Mama, imani yako ni kubwa; basi, ufanyiwe
kama unavyotaka.” Yule binti yake akapona tangu saa hiyo wakati huohuo.

Yesu anawaponya watu wengi

29 Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwa Galilaya, akapanda
mlimani, akaketi.
30 Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu
na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake,
naye Yesu akawaponya.
31 Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea,
waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona;
wakamsifu Mungu wa Israeli.

Yesu anawapa chakula watu elfu nne
\r
\is (Marko 8:1-10)
\ie

32 Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, “Nawaonea watu hawa
huruma kwa sababu kwa siku tatu wamekuwa nami, wala hawana chakula.
Sipendi kuwaacha waende bila kula wasije wakazimia njiani.”
33 Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula
cha kuwatosha watu wengi hivi?”
34 Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba na
visamaki vichache.”
35 Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini.
36 Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu,
akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
37 Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya makombo, wakajaza
vikapu saba.
38 Hao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake
na watoto.
39 Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la
Magadani.

\c 16

Watu wanamtaka Yesu afanye ishara
\r
\is (Marko 8:11-13; Luka 12:54-56)
\ie

1 Mafarisayo na Masadukayo walimwendea Yesu, na kwa kumjaribu,
wakamwomba afanye ishara itokayo mbinguni.
2 Lakini Yesu akawajibu, “Wakati wa jioni ukifika ninyi husema:
<Hali ya hewa itakuwa nzuri kwa maana anga ni jekundu!>
3 Na alfajiri mwasema: <Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana
anga ni jekundu na tena mawingu yametanda!> Basi, ninyi mnajua sana
kusoma majira kwa kuangalia anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi
hamjui.
4 Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa
ishara yoyote isipokuwa tu ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.

Chachu ya Mafarisayo na Masadukayo
\r
\is (Marko 8:14-21)
\ie

5 Wanafunzi wake walipokwisha vukia upande wa pili wa ziwa,
walijikuta wamesahau kuchukua mikate.
6 Yesu akawaambia, “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya
Mafarisayo na Masadukayo!”
7 Lakini wao wakawa wanajadiliana: “Anasema hivyo kwa kuwa
hatukuchukua mikate.”
8 Yesu alijua mawazo yao, akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba!
Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate?
9 Je, hamjaelewa bado? Je, hamkumbuki nilipoimega ile mikate mitano
kwa ajili ya wale watu elfu tano? Je, mlijaza vikapu vingapi vya
makombo?
10 Au, ile mikate saba waliyogawiwa wale watu elfu nne, je,
mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?
11 Inawezekanaje hamwelewi ya kwamba sikuwa nikisema juu ya mikate?
Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo!”
12 Hapo wanafunzi wakafahamu kwamba aliwaambia wajihadhari siyo na
chachu ya mikate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Petro anamkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu
\r
\is (Marko 8:27-30; Luka 9:18-21)
\ie

13 Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi
wake, “Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?”
14 Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane mbatizaji, wengine
Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
15 Yesu akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?”
16 Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye
hai.”
17 Yesu akasema, “Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si
binadamu aliyekufunulia ukweli huu, ila Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwambaff huu
nitalijenga kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda.
19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga
duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani,
kitafunguliwa pia mbinguni.”
20 Kisha akawaonya wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye
ndiye Kristo.
\fm f
\fr 16:18
\fk Petro…mwamba;
\f
\is Kigiriki ni Petros, na Pepra ni mwamba
\ie

Yesu anazungumza juu ya mateso na kifo chake.
\r
\is (Marko 8:31-9:1; Luka 9:22-27)
\ie

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi
wake: “Ni lazima mimi niende Yerusalemu, na huko nikapate mateso mengi
yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na walimu wa Sheria.
Nitauawa, na siku ya tatu nitafufuliwa.”
22 Hapo Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea: “Isiwe hivyo
Bwana! Jambo hili halitakupata!”
23 Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu
Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungu bali ni ya
kibinadamu!”

24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kama mtu yeyote anataka
kuwa mfuasi wangu, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake,
anifuate.
25 Maana, mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza;
26 lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali
amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha
yake?
27 Maana, Mwana wa Mtu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na
malaika wake, na hapo ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo
yake.
28 Kweli nawaambieni, wako wengine papahapa ambao hawatakufa kabla
ya kumwona Mwana wa Mtu akija katika Ufalme wake.”
\fr 16:27
\f Taz Zab 62:12

\c 17

Yesu anageuka sura
\r
\is (Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)
\ie

1 Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane
nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.
2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang’aa kama
jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
4 Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo
hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose
na kimoja cha Eliya.”

5 Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti
ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa,
ninayependezwa naye, msikilizeni.”
6 Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
7 Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!”
8 Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie
mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.”
10 Kisha wanafunzi wakamwuliza, “Mbona walimu wa Sheria wanasema
ati ni lazima kwanza Eliya aje?”
11 Yesu akawajibu, “Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
12 Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali
walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo
mikononi mwao.”
13 Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya
Yohane mbatizaji.
\fr 17:5
\f Taz Zab 2:7

Yesu anamponya mtoto mwenye pepo
\r
\is (Marko 9:14-29; Luka 9:37-43a)
\ie

14 Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea
Yesu, akampigia magoti,
15 akasema, “Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana
kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
16 Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya.”
17 Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka!
Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa
huyo mtoto.”
18 Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto
akapona wakati huohuo.

19 Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, “Kwa
nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?”
20 Yesu akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni
kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali,
mtaweza kuuambia mlima huu: <Toka hapa uende pale,> nao utakwenda.
Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu.”fg
\fm g
\fr 17:21
\f
\is Baadhi ya makala zina aya ya 21: “Pepo wa namna hii hawezi
kuondolewa ila kwa sala na kufunga.”
\ie

Yesu anaongea tena juu ya kifo na ufufuo wake
\r
\is (Marko 9:30-32; Luka 9:43b-45)
\ie

21 missing
22 Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Mtu
atakabidhiwa kwa watu.
23 Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi
wakahuzunika mno.

Kulipa zaka ya Hekalu

24 Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya
Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, “Je, mwalimu wenu hulipa fedha
ya zaka?”
25 Petro akajibu, “Naam, hulipa.” Basi, Petro alipoingia ndani ya
nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, “Simoni, wewe
unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina
nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?”
26 Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya
basi, wananchi hawahusiki.
27 Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua
samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta
fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili
yako.”

\c 18

Ni nani aliye mkuu?
\r
\is (Marko 9:33-37; Luka 9:46-48)
\ie

1 Wakati ule wanafunzi walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Ni nani aliye
mkuu katika Ufalme wa mbinguni?”
2 Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamisha kati yao,
3 kisha akasema, “Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama
watoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
4 Yeyote anayejinyenyekesha kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa
katika Ufalme wa mbinguni.
5 Yeyote anayemkaribisha mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu,
ananikaribisha mimi.

Vikwazo
\r
\is (Marko 9:42-48; Luka 17:1-2)
\ie

6 “Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini,
ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa
kwenye kilindi cha bahari.
7 Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine.
Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yule
atakayevisababisha.

8 “Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali
nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kuliko
kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako
miwili.
9 Na kama jicho lako likikukosesha, ling’oe na kulitupa mbali nawe.
Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa
katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.

Mfano wa kondoo aliyepotea
\r
\is (Luka 15:3-7)
\ie

10 “Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Nawaambieni,
malaika wao huko mbinguni wako daima mbele ya Baba yangu aliye
mbinguni.fh
11 missing
12 Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje?
Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yule
aliyepotea.
13 Akimpata, nawaambieni kweli, humfurahia huyo kuliko awafurahiavyo
wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
14 Hali kadhalika, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa
wadogo apotee.
\fm h
\fr 18:10
\f
\is Baadhi ya makala zina aya ya 11:
\ie Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea.
\is (taz Luka 19:10)
\ie

Kusahihishana

15 “Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu.
Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
16 Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa
mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
17 Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na
awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.

Kukataza na kuruhusu

18 “Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni,
na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.
19 Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa
duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni
atawafanyia jambo hilo.
20 Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina
langu, mimi nipo hapo kati yao.”

Mfano wa mtumishi asiyesamehe

21 Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je, ndugu yangu
akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?”
22 Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
23 Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja
aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
24 Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha
talanta elfu kumi.
25 Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru
wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili
deni lilipwe.
26 Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema,
<Unisubiri nami nitakulipa deni lote.>
27 Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha
aende zake.

28 “Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi
wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata,
akamkaba koo akisema, <Lipa deni lako!>
29 Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, <Unisubiri nami
nitalipa deni langu lote.>
30 Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo
atakapolipa lile deni.

31 “Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana,
wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
32 Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, <Wewe ni
mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
33 Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama
nilivyokuhurumia?>

34 “Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi
aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
35 Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila
mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”

\c 19

Kuhusu talaka
\r
\is (Marko 10:1-12)
\ie

1 Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, alitoka Galilaya, akaenda
katika mkoa wa Yudea, ng’ambo ya mto Yordani.
2 Watu wengi walimfuata huko, naye akawaponya.

3 Mafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, “Je, ni
halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?”
4 Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba
Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke,
5 na akasema: <Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama
yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?>
6 Kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi,
alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”

7 Lakini wao wakamwuliza, “Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamke
apewe hati ya talaka na kuachwa?”
8 Yesu akawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu
ya ugumu wa mioyo yenu.
9 Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote
atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke
mwingine, anazini.”

10 Wanafunzi wake wakamwambia, “Ikiwa mambo ya mume na mkewe ni
hivyo, ni afadhali kutooa kabisa.”
11 Yesu akawaambia, “Si wote wanaoweza kulipokea fundisho hili,
isipokuwa tu wale waliojaliwa na Mungu.
12 Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu
wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na
wengine wameamua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye
kulipokea fundisho hili na alipokee.”

Yesu anawabariki watoto wadogo
\r
\is (Marko 10:13-16; Luka 18:15-17)
\ie

13 Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na
kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
14 Yesu akasema, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie;
maana Ufalme wa mbinguni ni wa watu walio kama watoto hawa.”
15 Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo.

Kijana tajiri
\r
\is (Marko 10:17-31; Luka 18:18-30)
\ie

16 Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani
chema ili niupate uzima wa milele?”
17 Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja
tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uzima, shika amri.”

18 Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akasema, “Usiue,
usizini, usiibe, usitoe ushahidi wa uongo,
19 waheshimu baba yako na mama yako; na, mpende jirani yako kama
unavyojipenda mwenyewe.”

20 Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia tangu utoto
wangu; sasa nifanye nini zaidi?”
21 Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze
mali yako uwape maskini hiyo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni,
kisha njoo unifuate.”
22 Huyo kijana aliposikia hayo, alienda zake akiwa mwenye huzuni,
maana alikuwa na mali nyingi.

23 Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni, itakuwa
vigumu sana kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.
24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu
la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.”
25 Wale wanafunzi waliposikia hivyo walishangaa, wakamwuliza, “Ni
nani basi, awezaye kuokoka?”
26 Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili
haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”

27 Kisha Petro akasema, “Na sisi je? Tumeacha yote tukakufuata;
tutapata nini basi?”
28 Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi
katika kiti cha enzi cha utukufu wake katika ulimwengu mpya, ninyi
mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi
na mawili ya Israeli.
29 Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au
watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata
uzima wa milele.
30 Lakini walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho
watakuwa wa kwanza.

\c 20

Wafanyakazi katika shamba la mizabibu

1 “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu,
ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba
lake.
2 Akapatana nao kuwalipa dinari moja kwa siku, kisha akawapeleka
katika shamba lake la mizabibu.
3 Akatoka mnamo saa tatu asubuhi, akaona watu wengine wamesimama
sokoni, hawana kazi.
4 Akawaambia, <Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la
mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.>
5 Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na
saa tisa, akafanya vivyo hivyo.
6 Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu
wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, <Mbona mmesimama hapa
mchana kutwa bila kazi?>
7 Wakamjibu: <Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri.> Yeye akawaambia,
<Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu.>

8 “Kulipokuchwa, huyo mwenye shamba alimwambia mtunza hazina wake,
<Waite wafanyakazi ukawalipe mshahara wao, ukianzia na wale walioajiriwa
mwisho, na kumalizia na wale wa kwanza.>
9 Basi, wakaja wale walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakapokea
kila mmoja dinari moja.
10 Wale wa kwanza walipofika, walikuwa wanadhani watapewa zaidi;
lakini hata wao wakapewa kila mmoja dinari moja.
11 Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnung’unikia yule bwana.
12 Wakasema, <Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda
wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi
ngumu kutwa na jua kali?>

13 “Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, <Rafiki, sikukupunja kitu!
Je, hukupatana nami mshahara wa denari moja?
14 Chukua haki yako, uende zako. Napenda kumpa huyu wa mwisho sawa
na wewe.
15 Je, sina haki ya kufanya na mali yangu nipendavyo? Je, unaona
kijicho kwa kuwa mimi ni mwema?”>

16 Yesu akamaliza kwa kusema, “Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa
kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Yesu anazungumza mara ya tatu juu ya kifo chake
\r
\is (Marko 10:32-34; Luka 18:31-34)
\ie

17 Yesu alipokuwa anakwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi
kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
18 “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu
atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu
auawe.
19 Watamkabidhi kwa watu wa mataifa mengine ili adhihakiwe, apigwe
viboko na kusulubiwa; lakini siku ya tatu atafufuliwa.”

Ombi la mama wa Yakobo na Yohane
\r
\is (Marko 10:35-45)
\ie

20 Hapo mama yao wana wa Zebedayo alimjia Yesu pamoja na wanawe,
akapiga magoti mbele yake na kumwomba kitu.
21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Huyo mama akamwambia, “Ahidi
kwamba katika Ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako
wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto.”
22 Yesu akajibu, “Hamjui mnaomba nini. Je, mnaweza kunywa kikombe
nitakachokunywa mimi?” Wakamjibu, “Tunaweza.”
23 Yesu akawaambia, “Kweli mtakunywa kikombe changu, lakini kuketi
kulia au kushoto kwangu si kazi yangu kupanga; jambo hilo watapewa wale
waliowekewa tayari na Baba yangu.”

24 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakawakasirikia hao
ndugu wawili.
25 Hivyo Yesu akawaita, akawaambia, “Mnajua kwamba watawala wa
mataifa hutawala watu wao kwa mabavu na wakuu hao huwamiliki watu wao.
26 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila yeyote anayetaka kuwa mkuu kati
yenu sharti awe mtumishi wa wote;
27 na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.
28 Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na
kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”

Yesu anawaponya vipofu wawili
\r
\is (Marko 10:46-52; Luka 18:35-43)
\ie

29 Yesu alipokuwa anaondoka mjini Yeriko, umati wa watu ulimfuata.
30 Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na
waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaaza sauti:
“Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
31 Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao
wakazidi kupaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
32 Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie
nini?”
33 Wakamjibu, “Mheshimiwa, tunaomba macho yetu yafumbuliwe.”
34 Basi, Yesu akawaonea huruma, akawagusa macho yao, na papo hapo
wakaweza kuona, wakamfuata.

\c 21

Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe
\r
\is (Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yoh. 12:12-19)
\ie

1 Yesu na wanafunzi wake walipokaribia Yerusalemu na kufika Bethfage
katika mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
2 akawaambia, “Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu na mtamkuta
punda amefungwa na mtoto wake. Wafungueni mkawalete kwangu.
3 Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, <Bwana anawahitaji,> naye
atawaachieni mara.”
4 Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii yatimie:

5 “Uambieni mji wa Sioni:

Tazama, Mfalme wako anakujia!
Ni mpole na amepanda punda,
mwana punda, mtoto wa punda.”

6 Hivyo, wale wanafunzi walienda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza.
7 Wakamleta yule punda na mtoto wake, wakatandika nguo zao juu yao
na Yesu akaketi juu yake.
8 Umati mkubwa wa watu ukatandaza nguo zao barabarani, na watu
wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani.
9 Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaaza
sauti:

“Hosana Mwana wa Daudi!
Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!
Hosana Mungu juu mbinguni!”
\fr 21:9
\f Taz Zab 118:25-26

10 Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu
wakawa wanauliza, “Huyu ni nani?”
11 Watu katika ule umati wakasema, “Huyu ni nabii Yesu, kutoka
Nazareti katika mkoa wa Galilaya.”

Yesu anawafukuza wafanyabiashara Hekaluni
\r
\is (Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yoh. 2:13-22)
\ie

12 Basi, Yesu akaingia Hekaluni, akawafukuza nje watu waliokuwa
wanauza na kununua vitu ndani ya Hekalu; akazipindua meza za wale
waliokuwa wanavunja fedha, na viti vya wale waliokuwa wanauza njiwa.
13 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: <Nyumba
yangu itaitwa nyumba ya sala.> Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la
wanyang’anyi.”

14 Vipofu na vilema walimwendea huko Hekaluni, naye Yesu akawaponya.
15 Basi, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu
aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaaza sauti zao Hekaluni
wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika.
16 Hivyo wakamwambia, “Je, husikii wanachosema?” Yesu akawajibu,
“Naam, nasikia! Je hamjasoma Maandiko haya Matakatifu?

<Kwa vinywa vya watoto wadogo na wanyonyao
unajipatia sifa kamilifu.”>

17 Basi, akawaacha, akatoka nje ya mji na kwenda Bethania, akalala
huko.
\fr 21:16
\f Taz Zab 8:2

Mtini usiozaa
\r
\is (Marko 11:12-14, 20-24)
\ie

18 Yesu alipokuwa anarudi mjini asubuhi na mapema, aliona njaa.
19 Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta
hauma chochote ila majani matupu. Basi akauambia, “Usizae tena matunda
milele!” Papo hapo huo mtini ukanyauka.
20 Wanafunzi walipouona walishangaa wakisema, “Kwa nini mtini huu
umenyauka ghafla?”
21 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani bila
kuwa na mashaka, mnaweza si tu kufanya hivyo, bali hata mkiuambia mlima
huu: <Ng’oka ukajitose baharini,> itafanyika hivyo.
22 Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba katika sala, mtapata.”

Suala juu ya mamlaka ya Yesu
\r
\is (Marko 11:27-33; Luka 20:1-8)
\ie

23 Yesu aliingia Hekaluni, akawa anafundisha. Alipokuwa akifundisha,
makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa
mamlaka gani? Nani amekupa mamlaka haya?”

24 Yesu akawajibu, “Na mimi nitawaulizeni swali moja; mkinijibu,
basi nami nitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.
25 Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa nani? Je, yalitoka
mbinguni ama kwa watu?” Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi:
“Tukisema, <Yalitoka mbinguni>, atatuuliza, <Basi, mbona hamkumsadiki?>
26 Na tukisema, <Yalitoka kwa watu,> tunaogopa umati wa watu maana
wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii.”
27 Basi, wakamjibu, “Hatujui!” Naye Yesu akawaambia, “Nami pia
sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.

Mfano wa wana wawili

28 “Ninyi mnaonaje; mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwambia
yule wa kwanza, <Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katika shamba la
mizabibu.>
29 Yule kijana akamwambia, <Sitaki!> Lakini baadaye akabadili nia,
akaenda kufanya kazi.
30 Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye
akamjibu, <Naam baba!> Lakini hakwenda kazini.
31 Je, ni nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba
yake?” Wakamjibu, “Yule mtoto wa kwanza.”
Basi, Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, watoza ushuru na
waasherati wataingia katika Ufalme wa Mungu kabla yenu.
32 Maana Yohane alikuja kwenu akawaonyesha njia njema ya kuishi,
nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na waasherati walimwamini. Hata
baada ya kuona hayo yote ninyi hamkubadili mioyo yenu, na hamkusadiki.”

Mfano wa shamba la mizabibu na wakulima
\r
\is (Marko 12:1-12; Luka 20:9-19)
\ie

33 Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye
nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba
kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha
kwa wakulima, akasafiri kwenda nchi ya mbali.
34 Wakati wa mavuno ulipofika, aliwatuma watumishi wake kwa wale
wakulima, ili wakachukue sehemu ya mavuno yake.
35 Wale wakulima wakawakamata hao watumishi; mmoja wakampiga,
mwingine wakamwua na mwingine wakampiga mawe.
36 Huyo mtu akawatuma tena watumishi wengine, wengi kuliko wa safari
ya kwanza. Wale wakulima wakawatendea namna ileile.
37 Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: <Watamheshimu
mwanangu.>
38 Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa
wao: <Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake!>
39 Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu,
wakamwua.

40 “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje
hao wakulima?”
41 Wao wakamjibu, “Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba
atawapa wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wa
mavuno.”

42 Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko
Matakatifu?

<Jiwe walilokataa waashi
sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.
Bwana ndiye aliyefanya jambo hili,
nalo ni la ajabu sana kwetu!>
\fr 21:42
\f Taz Zab 118:22-23

43 “Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na
kupewa watu wa mataifa mengine wenye kutoa matunda yake.”fi
\fm i
\fr 21:44
\f
\is Baadhi ya makala zina aya ya 44:
\ie “Atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na
likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
\is (taz. Luka 20:18)
\ie

44 missing
45 Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia hiyo mifano yake
walitambua kwamba alikuwa anawasema wao.
46 Kwa hiyo wakawa wanatafuta njia ya kumtia nguvuni, lakini
waliwaogopa watu kwa sababu wao walimtambua yeye kuwa nabii.

\c 22

Mfano wa karamu ya arusi
\r
\is (Luka 14:15-24)
\ie

1 Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:
2 “Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe
karamu ya arusi.
3 Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini
walioalikwa hawakutaka kufika.
4 Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, <Waambieni wale
walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng’ombe
wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.>
5 Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake,
mwingine kwenye shughuli zake,
6 na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.
7 Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize
wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
8 Kisha akawaambia watumishi wake: <Karamu ya arusi iko tayari
kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.
9 Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni
waje arusini.>
10 Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote,
wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.

11 “Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye
hakuvaa mavazi ya arusi.
12 Mfalme akamwuliza, <Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi?>
Lakini yeye akakaa kimya.
13 Hapo mfalme akawaambia watumishi, <Mfungeni miguu na mikono
mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.”>
14 Yesu akamaliza kwa kusema, “Wengi wamealikwa, lakini wachache
wameteuliwa.”

Kulipa kodi kwa Kaisari
\r
\is (Marko 12:13-17; Luka 20:20-26)
\ie

15 Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa
Yesu kwa maneno yake.
16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha
Herode. Wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na
kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote,
maana cheo cha mtu si kitu kwako.
17 Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?”
18 Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, “Enyi
19 Nionyesheni fedha ya kulipia kodi.” Nao wakamtolea sarafu ya
fedha. sarafu ya fedha.
20 Basi, Yesu akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?”
21 Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi,
mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.”
22 Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.

Kuhusu ufufuo
\r
\is (Marko 12:18-27; Luka 20:27-40)
\ie

23 Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale
wasemao kwamba wafu hawafufuki.
24 Basi, wakamwambia, “Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila
kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu
yake watoto.
25 Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha
akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.
26 Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.
27 Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.
28 Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani
miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa.”

29 Yesu akawajibu, “Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko
Matakatifu wala nguvu ya Mungu!
30 Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama
malaika mbinguni.
31 Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale
aliyowaambieni Mungu?
32 Aliwaambia, <Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo!> Basi,
yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”
33 Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho
yake.

Amri kuu
\r
\is (Marko 12:28-34; Luka 10:25-28)
\ie

34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha
Masadukayo, wakakutana pamoja.
35 Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,
36 “Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?”
37 Yesu akamjibu, “<Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa
roho yako yote na kwa akili yako yote.>
38 Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.
39 Ya pili inafanana na hiyo: <Mpende jirani yako kama unavyojipenda
wewe mwenyewe.>
40 Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri
hizi mbili.”

Kuhusu Mwana wa Daudi
\r
\is (Marko 12:35-37; Luka 20:41-44)
\ie

41 Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,
42 “Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?”
Wakamjibu, “Wa Daudi.”
43 Yesu akawaambia, “Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho
Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:

44 <Bwana alimwambia Bwana wangu:

keti upande wangu wa kulia,
mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.>
\m
45 Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo <Bwana,> anawezaje kuwa
mwanawe?”
46 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo
hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
\fr 22:44
\f Taz Zab 110:1

\c 23

Yesu anawalaumu walimu wa Sheria na Mafarisayo
\r
\is (Marko 12:38-39; Luka 11:43,46; 20:45-46)
\ie

1 Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,
2 “Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria
ya Mose.
3 Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini
msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao
wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye
maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za
makoti yao.
6 Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika
masunagogi.
7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na
watu: <Mwalimu.>
8 Lakini ninyi msiitwe kamwe <Mwalimu,> maana mwalimu wenu ni mmoja
tu, nanyi nyote ni ndugu.
9 Wala msimwite mtu yeyote <Baba> hapa duniani, maana Baba yenu ni
mmoja tu aliye mbinguni.
10 Wala msiitwe <Viongozi,> maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye
Kristo.
11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.
12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.

Yesu analaumu unafiki
\r
\is (Marko 12:40; Luka 11:39-42,44,52; 20:47)
\ie

13 “Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga
mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe
hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.fj
\fm j
\fr 23:13
\f
\is Baadhi ya makala zina aya ya 14:
\ie Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya
wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu
hiyo mtapata adhabu kali.
\is (taz. Marko 12:40)
\ie

14 missing
15 “Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri
baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu.
Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu
kuliko ninyi wenyewe.

16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa
Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo
hicho kinamshika.
17 Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au
Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?
18 Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa
kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
19 Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au
madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu?
20 Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote
kilichowekwa juu yake.
21 Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule
akaaye ndani yake.
22 Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa
huyo aketiye juu yake.
23 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu
zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku
mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya
ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
24 Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza
ngamia!
\il 5
ic
\is Jira (Mat. 23:23)
\ie

25 “Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha
kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata
kwa unyang’anyi na uchoyo.
26 Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa
safi pia.

27 “Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama
makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri,
lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini
kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

Adhabu inakuja
\r
\is (Luka 11:47-51)
\ie

29 “Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga
makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
30 Mwasema: <Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu
hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!>
31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu
waliowaua manabii.
32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!
33 Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto
wa Jehanamu?
34 Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima
na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga
viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema
iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na
hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua
Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya
mambo haya.

Jinsi Yesu alivyoupenda mji wa Yerusalemu
\r
\is (Luka 13:34-35)
\ie

37 “Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe
wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako
kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa
yake, lakini hukutaka.
38 Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.
39 Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema:

<Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.”>
\il 5
ic
\is Kuku na vifaranga vyake (Mat. 23:37)
\ie
\fr 23:39
\f Taz Zab 118:26

\c 24

Yesu anazungumza juu ya kuteketezwa kwa Hekalu

1 Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake
walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu.
2 Yesu akawaambia, “Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli
nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine;
kila kitu kitaharibiwa.”

Taabu na mateso
\r
\is (Marko 13:3-13; Luka 21:7-19)
\ie

3 Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi
walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Twambie mambo haya yatatukia lini?
Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”
4 Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
5 Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: <Mimi
ndiye Kristo,> nao watawapotosha watu wengi.
6 Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana
hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
7 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na
ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
8 Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.

9 “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote
yatawachukieni kwa ajili ya jina langu.
10 Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
12 Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
13 Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.
14 Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu
itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.

Dhiki kuu
\r
\is (Marko 13:14-23; Luka 21:20-24)
\ie

15 “Basi, mtakapoona <Chukizo Haribifu> lililonenwa na nabii
Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake),
16 hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani.
17 Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani
mwake.
18 Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
19 Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya
Sabato!
21 Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako
tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena.
22 Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye
angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.

23 “Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: <Kristo yuko hapa> au <Yuko
pale,> msimsadiki.
24 Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo.
Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata
wateule wa Mungu.
25 Sikilizeni, nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati.
26 Basi, wakiwaambieni, <Tazameni, yuko jangwani,> msiende huko; au,
<Tazameni, amejificha ndani,> msisadiki;
27 maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi,
ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu.
28 Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

Kuja kwake Mwana wa Mtu
\r
\is (Marko 13:24-27; Luka 21:25-28)
\ie

29 “Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi
hautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu
zitatikiswa.
30 Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila
yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu
ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi.
31 Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao
watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho
huu wa mbingu hadi mwisho huu.

Mfano wa mtini
\r
\is (Marko 13:28-31; Luka 21:29-33)
\ie

32 “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza
kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi
umekaribia.
33 Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka,
jueni kwamba yuko karibu sana.fk
34 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo
yote kutukia.
35 Naam, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita
kamwe.
\fm k
\fr 24:33
\fk yuko karibu sana;
\f
\is au
\ie wakati u karibu tayari kuanza.

Hakuna ajuaye siku wala saa
\r
\is (Marko 13:32-37; Luka 17:26-30, 34-36)
\ie

36 “Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja
lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake ndiye
ajuaye.
37 Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa
kuja kwake Mwana wa Mtu.
38 Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na
kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina.
39 Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba
wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja.
40 Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na
mwingine ataachwa.
41 Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na
mwingine ataachwa.
42 Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.
43 Lakini kumbukeni jambo hili: kama mwenye nyumba angejua siku
mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.
44 Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja
saa msiyoitazamia.”

Mtumishi mwaminifu na asiye mwaminifu
\r
\is (Luka 12:41-48)
\ie

45 Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na
mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape
chakula kwa wakati wake?
46 Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta
akifanya hivyo.
47 Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake
yote.
48 Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: <Bwana wangu
anakawia kurudi,>
49 kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa
pamoja na walevi,
50 bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua.
51 Atamkatilia mbali na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko
kutakuwa na kilio na kusaga meno.
\fm l
\fr 24:51
\fk Atamkata vipandevipande;
\f
\is au
\ie atamtupa nje.

\c 25

Mfano wa wanawali kumi

1 “Wakati huo, Ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi
waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye
busara.
3 Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya
mafuta.
4 Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na
taa zao.
5 Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wanawali wote wote
walisinzia, wakalala.
6 Usiku wa manane kukawa na kelele: <Haya, haya! Bwana arusi
anakuja; nendeni kumlaki.>
7 Hapo wale wanawali wote wakaamka, wakazitayarisha taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara: <Tupeni mafuta yenu
kidogo maana taa zetu zinazimika.>
9 Lakini wale wenye busara wakawaambia, <Hayatatutosha sisi na
ninyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!>
10 Basi, wale wanawali wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana
arusi akafika, na wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye
katika jumba la arusi, kisha mlango ukafungwa.
11 Baadaye wale wanawali wengine wakaja, wakaita: <Bwana, bwana,
tufungulie!>
12 Lakini yeye akawajibu, <Nawaambieni kweli, siwajui ninyi.”>
13 Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala
saa.

Mfano wa watumishi watatu
\r
\is (Luka 19:11-27)
\ie

14 “Itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ng’ambo: aliwaita
watumishi wake, akawakabidhi mali yake.
15 Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: mmoja sarafu tano za
fedha ziitwazo talanta, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja,
kisha akasafiri.
16 Mara yule aliyekabidhiwa talanta tano akafanya kazi nazo akapata
faida talanta tano.
17 Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida
talanta mbili.
18 Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaenda akachimba shimo
ardhini, akaificha fedha ya bwana wake.

19 “Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu
ya matumizi na mapato ya fedha yake.
20 Mtumishi aliyekabidhiwa talanta tano akaja amechukua zile talanta
tano faida, akamwambia, <Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana
talanta tano zaidi faida niliyopata.>
21 Bwana wake akamwambia, <Vema, mtumishi mwema na mwaminifu.
Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo nitakukabidhi makubwa. Njoo
ufurahi pamoja na bwana wako.>

22 “Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta
mbili faida, akisema, <Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta
mbili zaidi faida niliyopata.>
23 Bwana wake akamwambia, <Vema, mtumishi mwema na mwaminifu.
Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo
ufurahi pamoja na bwana wako.>

24 “Lakini yule aliyekabidhiwa talanta moja akaja, akasema, <Bwana,
najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya
pale ambapo hukutawanya.
25 Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali
yako.>

26 “Bwana wake akamwambia, <Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua
kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo
sikutawanya.
27 Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami
ningelichukua mtaji wangu na faida yake!
28 Basi, mnyang’anyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi.
29 Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na
kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
30 Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko
kutakuwa na kilio na kusaga meno.>

Hukumu ya mwisho

31 “Wakati Mwana wa Mtu atakapokuja katika utukufu wake na malaika
wote wakiwa pamoja naye, hapo ataketi juu ya kiti chake cha enzi
kitukufu,
32 na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha
watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
33 Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa
kushoto.

34 “Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, <Njoni
enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni Ufalme mliotayarishiwa tangu
kuumbwa kwa ulimwengu.
35 Maana nilikuwa na njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu
nanyi mkanipa maji; nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha;
36 nilikuwa uchi, mkanivika; nilikuwa mgonjwa nanyi mkaja
kunitazama; nilikuwa gerezani nanyi mkaja kunitembelea.>
37 Hapo, hao watu wema watamjibu mfalme <Bwana, ni lini tulikuona
mwenye njaa nasi tukakupa chakula, au ukiwa na kiu nasi tukakunywesha
maji?
38 Ni lini tulikuona ukiwa mgeni nasi tukakukaribisha, au bila nguo
nasi tukakuvika?
39 Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au mfungwa nasi tukaja
kukutazama?>
40 Mfalme atawajibu, <Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea
mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.>

41 “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, <Ondokeni
mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele
aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.
42 Maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu
nanyi hamkunipa maji.
43 Nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha; nilikuwa mgonjwa na
mfungwa nanyi hamkuja kunitazama.>

44 “Hapo nao watajibu, <Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa au
kiu, ukiwa mgeni au bila nguo, ukiwa mgonjwa au mfungwa, nasi hatukuja
kukuhudumia?>
45 Naye atawajibu, <Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea
mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.>
46 Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale
waadilifu watakwenda kwenye uzima wa milele.”

Mpango wa kumwua Yesu
\r
\is (Marko 14:1-2; Luka 22:1-2; Yoh. 11:45-53)
\ie
\c 26

1 Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,
2 “Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka,
na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”

3 Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja
katika ukumbi wa Kayafa, Kuhani Mkuu.
4 Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
5 Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije
kukatokea ghasia kati ya watu.

Yesu anapakwa mafuta Bethania
\r
\is (Marko 14:3-9; Yoh. 12:1-8)
\ie

6 Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,
7 mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani
kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia
hayo marashi kichwani.
8 Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini
hasara hii?
9 Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa
hizo fedha.”

10 Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu
mama? Yeye amenitendea jambo jema.
11 Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja
nanyi daima.
12 Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.
13 Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa
ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka
yeye.”

Yuda anaamua kumsaliti Yesu
\r
\is (Marko 14:10-11; Luka 22:3-6)
\ie

14 Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa
makuhani wakuu,
15 akawaambia, “Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?”
Wakamhesabia sarafu thelathini za fedha;
16 na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.

Yesu anafanya karamu ya Pasaka pamoja na wanafunzi wake
\r
\is (Marko 14:12-21; Luka 22:7-14,21-23; Yoh. 13:21-30)
\ie

17 Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu,
wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi
chakula cha Pasaka?”
18 Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie:
<Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na
wanafunzi wangu.”>
19 Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka.

20 Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake
kumi na wawili.
21 Walipokuwa wakila, Yesu akasema, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu
atanisaliti.”
22 Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja,
“Bwana! Je, ni mimi?”
23 Yesu akajibu, “Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli
ndiye atakayenisaliti.fm
24 Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu
yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu!
Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”

25 Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, “Mwalimu!
Je, ni mimi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.”
\fm m
\fr 26:23
\f
\is Kula pamoja ilikuwa ishara ya urafiki.
\ie

Karamu ya Bwana
\r
\is (Marko 14:22-26; Luka 22:14-20; 1 Kor. 11:23-25)
\ie

26 Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega,
akawapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni mle; huu ni mwili wangu.”
27 Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema,
“Nyweni nyote;
28 maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano,fn damu
inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi.
29 Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile
nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
\fm n
\fr 26:28
\fk agano;
\f
\is Baadhi ya makala zina;
\ie agano jipya.

30 Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa
Mizeituni.

Yesu anatangaza kwamba Petro atamkana
\r
\is (Marko 14:27-31; Luka 22:31-34; Yoh. 13:36-38)
\ie

31 Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na
mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema:

<Nitampiga mchungaji,
na kondoo wa kundi watatawanyika.>
\m
32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya.”
33 Petro akamwambia Yesu “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe
na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe.”
34 Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoo
hajawika, utanikana mara tatu.”
35 Petro akamwambia, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe,
sitakukana kamwe.” Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Yesu anasali bustanini Gethsemane
\r
\is (Marko 14:32-42; Luka 22:39-46)
\ie

36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia
wanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.”

37 Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na
huzuni na mahangaiko.
38 Hapo akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa.
Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
39 Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: “Baba
yangu, kama inawezekana, aacha kikombefo hiki cha mateso kinipite;
lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe.”
40 Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro,
“Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i
tayari lakini mwili ni dhaifu.”
\fm o
\fr 26:39
\fk kikombe;
\f
\is ishara ya huzuni na mateso.
\ie

42 Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani
kikombefp hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako
yafanyike.”
43 Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa
yamebanwa na usingizi.
\fm p
\fr 26:42
\k kikombe;
\f Taz 26:39

44 Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno
yaleyale.
45 Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala
na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa
kwa watu wenye dhambi.
46 Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.”

Yesu anatiwa nguvuni
\r
\is (Marko 14:43-50; Luka 22:47-53; Yoh. 18:3-12)
\ie

47 Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao, mara akaja Yuda, mmoja wa
wale kumi na wawili. Pamoja naye walikuja watu wengi wenye mapanga na
marungu ambao walitumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
48 Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara
akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
49 Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, “Shikamoo, Mwalimu!”
Kisha akambusu.
50 Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya ulichokuja kufanya.” Hapo wale
watu wakaja, wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.

51 Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono,
akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata
sikio.
52 Hapo Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako alani, maana yeyote
anayeutumia upanga, atakufa kwa upanga.
53 Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara
angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
54 Lakini yatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayo kwamba ndivyo
inavyopaswa kuwa?”

55 Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia
nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba
mimi ni mnyang’anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na
hamkunikamata!
56 Lakini haya yote yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie.”
Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

Yesu mbele ya baraza
\r
\is (Marko 14:53-65; Luka 22:54-55,63-71; Yoh. 18:13-14, 19-24)
\ie

57 Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa,
Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu wa Sheria na wazee.
58 Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia
ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.

59 Basi, makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo
dhidi ya Yesu wapate kumwua,
60 lakini hawakupata ushahidi wowote, ingawa walikuja mashahidi
wengi wa uongo. Mwishowe wakaja mashahidi wawili,
61 wakasema, “Mtu huyu alisema: <Ninaweza kuliharibu Hekalu la
Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.”>
62 Kuhani Mkuu akasimama, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu
hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
63 Lakini Yesu akakaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, “Nakuapisha
kwa Mungu aliye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!”
64 Yesu akamwambia, “Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu sasa
mtamwona Mwana wa Mtu ameketi upande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu ya
mawingu ya mbinguni.”

65 Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru!
Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
66 Ninyi mwaonaje?” Wao wakamjibu, “Anastahili kufa!”
67 Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa
wanampiga makofi,
68 wakasema, “Haya Kristo, tutabirie; ni nani amekupiga!”

Petro anamkana Yesu
\r
\is (Marko 14:66-72; Luka 22:56-62; Yoh. 18:15-18;25-27)
\ie

69 Petro alikuwa ameketi nje uani. Basi, mtumishi mmoja wa kike
akamwendea, akasema, “Wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”
70 Petro akakana mbele ya wote akisema, “Sijui hata unasema nini.”
71 Alipokuwa akitoka mlangoni, mtumishi mwingine wa kike akamwona,
akawaambia wale waliokuwa pale, “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa
Nazareti.”
72 Petro akakana tena kwa kiapo: “Simjui mtu huyo.”
73 Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro,
wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako
unakutambulisha.”
74 Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, “Simjui mtu
huyo!” Mara jogoo akawika.
75 Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: “Kabla jogoo
hajawika, utanikana mara tatu.” Basi, akatoka nje akalia sana.

\c 27

Yesu anapelekwa kwa Pilato
\r
\is (Marko 15:1; Luka 23:1-2; Yoh. 18:28-32)
\ie

1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya
mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa
mkoa.

Kifo cha Yuda
\r
\is (Mat. 1:18-19)
\ie

3 Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha
mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu
thelathini za fedha.
4 Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.”
Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
5 Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda
akajinyonga.
6 Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai
kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
7 Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe
mahali pa kuzika wageni.
8 Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
9 Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walizichukua sarafu
thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga
bei,
10 wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.”

Pilato anamhoji Yesu
\r
\is (Marko 15:2-5; Luka 23:3-5; Yoh. 18:33-38)
\ie

11 Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa
akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia,
“Wewe umesema.”
12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu
neno.
13 Hivyo Pilato akamwuliza, “Je, husikii mashtaka hayo yote
wanayotoa juu yako?”
14 Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa
akashangaa sana.

Yesu anapewa hukumu ya kifo
\r
\is (Marko 15:6-16; Luka 23:13-25; Yoh. 18:39-19:16)
\ie

15 Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa
kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
16 Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
17 Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, “Mwataka
nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Barabafq ama Yesu aitwae Kristo?”
18 Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu
ya wivu.
\fm q
\fr 27:17
\fk Baraba;
\f
\is aliitwa pia Yesu.
\ie

19 Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake
akampelekea ujumbe: “Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana
leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”
20 Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba
afunguliwe na Yesu auawe.
21 Mkuu wa mkoa akawauliza, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka
nimfungue?” Wakamjibu, “Baraba!”
22 Pilato akawauliza, “Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?”
Wote wakasema, “Asulubiwe!”
23 Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Wao wakazidi
kupaaza sauti: “Asulubiwe!”

24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba
maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule
umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu;
shauri lenu wenyewe.”
25 Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto
wetu!”
26 Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa
Yesu asulubiwe.

Askari wanamdhihaki Yesu
\r
\is (Marko 15:16-20; Yoh. 19:2-3)
\ie

27 Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu,
wakamkusanyikia kikosi kizima.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
29 Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea
pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake,
wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
30 Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake,
kisha wakampeleka kumsulubisha.

Yesu anasulubiwa
\r
\is (Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yoh. 19:17-27)
\ie

32 Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni,
mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu
la kichwa,”
34 wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja
akakataa kunywa.

35 Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
36 Wakaketi, wakawa wanamchunga.
37 Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa,
“Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.”
38 Wanyang’anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande
wa kushoto na mwingine upande wa kulia.

39 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa
vyao na kusema,
40 “Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu?
Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka
msalabani!”
41 Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na
wazee walimdhihaki wakisema,
42 “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni
mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
43 Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi,
Mungu na amwokoe kama anamtaka.”
44 Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
\fr 27:34
\f Taz. Zab 69:21
\fr 27:35
\f Taz Zab 22:18
\fr 27:39
\f Taz Zab 22:7; 109:25
\fr 27:43
\f Taz Zab 22:8

Yesu anakufa msalabani
\r
\is (Marko 15:33-41; Luka 23:44-49; Yoh. 19:28-30)
\ie

45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika
giza.
46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eli, Eli, lema
sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
47 Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema,
“Anamwita Eliya.”
48 Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki,
akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
49 Wengine wakasema, “Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.”
50 Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.

51 Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka
chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa
wakafufuliwa;
53 nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia
katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.

54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona
tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema,
“Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao
ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na
Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
\fr 27:46
\f Taz Zab 22:1
\fr 27:48
\f Taz Zab 69:21

Kuzikwa kwake Yesu
\r
\is (Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yoh. 19:38-42)
\ie

57 Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya,
jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
58 Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato
akaamuru apewe.
59 Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
60 akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika
mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi,
akaenda zake.
61 Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi
kulielekea kaburi.

Kaburi linalindwa

62 Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani
wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
63 Wakasema, “Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu
alisema kabla ya kufa ati, <Baada ya siku tatu nitafufuka.>
64 Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi
wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa
mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali.”
65 Pilato akawaambia, “Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri
mjuavyo.”
66 Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile
jiwe na kuacha hapo askari walinzi.

\c 28

Kufufuka kwa Yesu
\r
\is (Marko 16:1-10; Luka 24:1-12; Yoh. 20:1-10)
\ie

1 Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili,
Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
2 Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka
kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
3 Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
4 Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa
kama wamekufa.
5 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Ninyi msiogope!
Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
6 Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali
alipokuwa amelala.
7 Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka
kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya,
mimi nimekwisha waambieni.”

8 Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi
kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.

9 Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: “Salamu.” Hao wanawake
wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
10 Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope! Nendeni mkawaambie ndugu zangu
waende Galilaya, na huko wataniona.”

Taarifa ya walinzi wa kaburi

11 Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa
lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya
mambo yote yaliyotukia.
12 Basi, wakakutana pamoja na wazee, na baada ya kushauriana,
wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha
13 wakisema, “Ninyi mtasema hivi: <Wanafunzi wake walikuja usiku,
wakamwiba sisi tukiwa tumelala.>
14 Na kama mkuu wa mkoa akijua jambo hili, sisi tutasema naye na
kuhakikisha kuwa ninyi hamtapata matatizo.”
15 Wale walinzi wakazichukua zile fedha, wakafanya kama
walivyofundishwa. Habari hiyo imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.

Yesu anawatokea wanafunzi wake
\r
\is (Marko 16:14-18; Luka 24:36-49; Yoh. 20:19-23; Mat. 1:6-8)
\ie

16 Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima
aliowaagiza Yesu.
17 Walipomwona, wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka.
18 Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni
na duniani.
19 Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi
wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
20 Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja
nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”