\h WAROMA

          BARUA YA PAULO KWA
                 WAROMA

\c 1

1 Kutoka kwangu mimi Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, na mtume
niliyeteuliwa na kuitwa kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema ya Mungu.

2 Hapo kale, Mungu aliwaahidia watu hii Habari Njema kwa njia ya
manabii wake katika Maandiko Matakatifu.
3 Hii Habari Njema inamhusu Mwana wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo,
ambaye mintarafu ubinadamu wake, alikuwa mzawa wa Daudi;
4 mintarafu utakatifu wake wa kimungu, alithibitishwa kwa uwezo mkuu
kwamba ni Mwana wa Mungu kwa kufufuliwa kutoka wafu.
5 Kwa njia yake, mimi nimepewa neema ya kuwa mtume, ili kwa ajili
yake niwaongoze watu wa mataifa yote wapate kuamini na kutii.
6 Ninyi ni miongoni mwa watu hao; mmeitwa muwe watu wake Yesu
Kristo.

7 Basi, ninawaandikia ninyi nyote mlioko Roma ambao Mungu
anawapenda, akawateua muwe watu wake. Nawatakieni neema na amani kutoka
kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

Shukrani kwa Mungu

8 Awali ya yote, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa
ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inasikika duniani kote.
9 Mungu, ambaye ninamtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri
Habari Njema ya Mwanae, ni shahidi wangu kwamba ninawakumbukeni
10 daima katika sala zangu. Namwomba Mungu akipenda, anipatie nafasi
nzuri ya kuja kwenu sasa.
11 Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi
ya kiroho na kuwaimarisha.
12 Ndiyo kusema, tutaimarishana: imani yenu itaniimarisha mimi, na
yangu itawaimarisha ninyi.

13 Ndugu zangu, nataka mjue kwamba mara nyingi nilikusudia
kuwatembeleeni, lakini mpaka sasa nimezuiwa. Ningependa kupata mafanikio
mema kati yenu kama nilivyopata kati ya watu wa mataifa mengine.
14 Ninalo jukumu kwa watu wote, waliostaarabika na wasiostaarabika,
wenye elimu na wasio na elimu.
15 Ndiyo maana ninatamani pia kuihubiri Habari Njema kwenu ninyi
mlioko huko Roma.

Nguvu ya Injili

16 Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu
inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na wasio Wayahudi pia.
17 Kwa maana Habari Njema inaonyesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali
watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka
mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Mwadilifufa kwa imani ataishi.”
\fm a
\fr 1:17
\fk Mwadilifu kwa imani ataishi;
\fk
\is au
\ie mwadilifu ataishi kwa amani

Kosa la binadamu

18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na
uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli
usijulikane.
19 Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao;
maana Mungu mwenyewe ameyadhirisha.
20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu
wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza
kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo
hawana njia yoyote ya kujitetea!
21 Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili,
wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao
tupu zimejaa giza.
22 Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.
23 Wanaacha kumwabudu Mungu aishiye milele, na badala yake,
wanaabudu sanamu zilizo mfano wa binadamu ambaye hufa, mfano wa wanyama,
ndege, au wanyama watambaao.

24 Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao
na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao.
25 Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu
kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele!
Amina.

26 Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake
wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile.
27 Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile
ya mume na mke wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo
ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo
vyao viovu.

28 Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika
fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
29 Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa
wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya,
30 na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye
kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii
wazazi wao;
31 hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa
wengine.
32 Wanajua kwamba Sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi
mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya
mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo
hayohayo.

\c 2

Hukumu ya Mungu

1 Basi, rafiki, kama unawahukumu wengine, huwezi kamwe kujitetea
haidhuru wewe ni nani. Kwa maana, kwa kuwahukumu wengine, unajilaani
wewe mwenyewe kwa vile nawe unayafanya mambo yaleyale unayohukumu.
2 Tunajua kwamba hukumu ya Mungu kwa wale wanaofanya mambo kama hayo
ni hukumu ya haki.
3 Lakini wewe, rafiki, unayewahukumu wale wanaofanya mambo kama hayo
bali wewe pia unayafanya, je unadhani utaiepa hukumu ya Mungu?
4 Au labda unaudharau wema wake mkuu, uvumilivu wake na saburi yake,
bila kutambua kwamba wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate
kutubu?
5 Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajilundikia adhabu
kwa Siku ile ambayo ghadhabu ya Mungu na hukumu zake za haki
vitadhihirishwa.
6 Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake.
7 Wale wanaozingatia kutenda mema, kutafuta utukufu na heshima ya
Mungu na kutokufa, watapata uzima wa milele.
8 Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na
kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.
9 Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu.
Yatawapata Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.
10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wale wanaotenda
mema; Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.
11 Maana Mungu hambagui mtu yeyote.
\fr 2:6
\f Taz Zab 62:12

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua Sheria ya Mose wataangamia
ingawaje hawajui Sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua
Sheria watahukumiwa kisheria.
13 Mtu hafanywi kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kuisikia Sheria,
bali kwa kuitii Sheria.
14 Mathalan: watu wa mataifa mengine hawana Sheria ya Mose; lakini
kila wanapotimiza matakwa ya Sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao
wenyewe wanakuwa kipimo cha Sheria ingawa hawaijui Sheria.
15 Mwenendo wao unaonyesha kwamba matakwa ya Sheria yameandikwa
mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao
mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.
16 Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo
itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa
njia ya Yesu Kristo.

Wayahudi na Sheria yao

17 Na wewe, je? Wewe mwenyewe unajiita Myahudi; unaitumainia Sheria
na kujivunia kuwa wa Mungu;
18 kwa njia ya Sheria unajua matakwa ya Mungu na unaweza kuchagua
jambo jema;
19 wewe unajiona kuwa kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walio
gizani;
20 unajiona kuwa mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa wale wasiokomaa
bado. Unayo katika Sheria picha kamili ya elimu na ukweli.
21 Basi, wewe unawafundisha wengine; kwa nini hujifundishi wewe
mwenyewe? Unawahubiria wengine wasiibe, lakini kumbe wewe mwenyewe
unaiba.
22 Unasema: “Msizini,” na huku wewe unazini; unachukia sanamu za
miungu hali wewe unajitajirisha kwa kuiba katika nyumba za miungu.
23 Kwa kujigamba ati unayo Sheria ya Mungu, je huoni kwamba kwa
kuivunja Sheria unamdharau Mungu?
24 Kama vile Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Watu wa mataifa
mengine wamelikufuru jina la Mungu kwa sababu yenu ninyi Wayahudi!”
25 Kutahiriwa kwako kutakuwa na maana kama ukiitii Sheria. Lakini
kama unaivunja Sheria, basi, ni afadhali ungalibaki bila kutahiriwa.
26 Kama mtu wa mataifa mengine ambaye hakutahiriwa akitimiza matakwa
ya Sheria, hakika atafikiriwa kana kwamba ametahiriwa.
27 Watu wa mataifa mengine watakuhukumu wewe Myahudi kama ukiivunja
Sheria, ingawaje unayo maandishi ya Sheria na umetahiriwa, hali wao
wanaitii Sheria ingawa hawakutahiriwa.
28 Ndiyo kusema, si kila anayeonekana kwa nje kuwa Myahudi ni
Myahudi wa kweli, wala mtu hawi Myahudi wa kweli ati kwa kuwa
ametahiriwa kimwili.
29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule
ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la
maandishi ya Sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu,
bali kutoka kwa Mungu.

\c 3

1 Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa
kuna faida gani?
2 Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi
Wayahudi ujumbe wake.
3 Lakini itakuwaje iwapo baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je, jambo
hilo litaondoa uaminifu wa Mungu?
4 Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu
ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:

“Kila usemapo,
maneno yako ni ya haki;
na katika hukumu,
wewe hushinda.”

5 Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa
haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa
naongea kibinadamu).
6 Hata kidogo! Ingekuwa hivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu?

7 Labda utasema: “Ikiwa ukosefu wa uaminifu kwa upande wangu
unamdhihirisha Mungu kuwa mwaminifu zaidi na hivyo kumpatia utukufu,
basi singepaswa kuhukumiwa kuwa mwenye dhambi!”
8 Ni sawa na kusema: tufanye maovu ili tupate mema! Ndivyo wengine
walivyotukashifu kwa kutushtaki kwamba tumefundisha hivyo. Watahukumiwa
wanavyostahili!

Hakuna mtu yeyote aliye mwadilifu
\fr 3:10-12
\f Taz Zab 14:1-3; 53:1-3
\fr 3:13
\f Taz Zab 5:9; 140:3
\fr 3:14
\f Taz Zab 10:7
\fr 3:18
\f Taz Zab 36:1

9 Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora zaidi kuliko wengine?
Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi
na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.
10 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:

“Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu!

11 Hakuna mtu anayeelewa,

wala anayemtafuta Mungu.

12 Wote wamepotoka

wote wamekosa;
hakuna atendaye mema,
hakuna hata mmoja.

13 Makoo yao ni kama kaburi wazi,

ndimi zao zimejaa udanganyifu,
midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka.

14 Vinywa vyao vimejaa laana chungu.

15 Miguu yao iko mbioni kumwaga damu,

16 popote waendapo husababisha maafa na mateso;

17 njia ya amani hawaijui.

18 Hawajali kabisa kumcha Mungu.”

19 Tunajua kwamba Sheria huwahusu walio chini ya Sheria hiyo, hata
hawawezi kuwa na kisingizio chochote, na ulimwengu wote uko chini ya
hukumu ya Mungu.
20 Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele
yake Mungu kwa kuishika Sheria; kazi ya Sheria ni kumwonyesha tu mtu
kwamba ametenda dhambi.
\fr 3:20
\f taz Zab 143:2

Kukubaliwa na Mungu kwa imani

21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwakubali watu kuwa waadilifu
imekwisha dhihirishwa, tena bila kutegemea Sheria. Sheria na manabii
hushuhudia jambo hili.
22 Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa
Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi
wowote.
23 Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.
24 Lakini kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa
waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo anayewakomboa.
25 Mungu alimtoa Yesu kusudi, kwa damu yake, awe njia ya kuwaondolea
watu dhambi zao kwa imani yao kwake. Alifanya hivyo ili apate kuonyesha
kwamba yeye ni mwadilifu. Hapo zamani Mungu alikuwa mvumilivu bila
kuzijali dhambi za watu;
26 lakini sasa, wakati huu, anazikabili dhambi za watu apate
kuonyesha uadilifu wake. Kwa namna hiyo Mungu mwenyewe huonyesha kwamba
yeye ni mwadilifu na kwamba humkubali kuwa mwadilifu mtu yeyote
anayemwamini Yesu.

27 Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu
ya kutimiza Sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.
28 Maana mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa
kutimiza matakwa ya Sheria.
29 Au je, Mungu nu Mungu wa Wayahudi tu, ama pia wa watu wa mataifa
mengine? Naam, wa mataifa mengine pia.
30 Mungu ni mmoja, naye atawakubali Wayahudi kuwa waadilifu kwa
imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha Sheria? Hata kidogo; bali
tunaipa Sheria thamani yake kamili.

\c 4

Mfano wa Abrahamu

1 Tuseme nini basi, juu ya Abrahamu baba yetu?
2 Kama Abrahamu alikubaliwa kuwa mwadilifu kutokana na matendo yake,
basi, anacho kitu cha kujivunia mbele ya Mungu.
3 Kwa maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Abrahamu alimwamini
Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
4 Mfanyakazi hulipwa mshahara; mshahara wake si zawadi bali ni haki
yake.
5 Lakini mtu asiyetegemea matendo yake mwenyewe, bali anamwamini
Mungu ambaye huwasamehe waovu, basi, Mungu huijali imani ya mtu huyo, na
hivi humkubali kuwa mwadilifu.
6 Naye Daudi asema hivi juu ya furaha ya mtu ambaye Mungu amemkubali
kuwa mwadilifu bila kuyajali matendo yake:

7 “Heri wale waliosamehewa makosa yao

ambao makosa yao yamefutwa.

8 Heri mtu yule ambaye

Bwana hataziweka dhambi zake katika kumbukumbu.”
\fr 4:7-8
\f taz Zab 32:1-2

9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale
wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema:
“Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”
10 Je, Abrahamu alikubaliwa kabla ya kutahiriwa ama baada ya
kutahiriwa? Kabla ya kutahiriwa, na si baada ya kutahiriwa.
11 Abrahamu alitahiriwa baadaye, na kutahiriwa huko kulikuwa alama
iliyothibitisha kwamba Mungu alimkubali kuwa mwadilifu kwa sababu ya
imani yake aliyokuwa nayo kabla ya kutahiriwa. Kwa hiyo, Abrahamu
amekuwa baba wa wale wote ambao, ingawa hawakutahiriwa, wamemwamini
Mungu, wakafanywa waadilifu.
12 Vilevile yeye ni baba wa wale waliotahiriwa; lakini si kwa kuwa
wametahiriwa, bali kwa sababu wanafuata njia ileile ya imani baba yetu
Abrahamu aliyofuata kabla ya kutahiriwa.

Ahadi ya Mungu hupokelewa kwa imani

13 Mungu alimwahidi Abrahamu na wazawa wake kwamba ulimwengu
ungekuwa mali yao. Ahadi hiyo haikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitii
Sheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwa kuwa mwadilifu.
14 Maana kama watakaopewa hayo aliyoahidi Mungu ni wale tu wanaoitii
Sheria, basi, imani haina maana yoyote, nayo ahadi ya Mungu si kitu.
15 Sheria husababisha ghadhabu; lakini kama hakuna Sheria,
haiwezekani kuivunja.

16 Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi
hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni
kwa ajili ya wote: si kwa wale tu wanaoishika Sheria, bali pia kwa wale
waishio kwa imani kama Abrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote.
17 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Nimekuweka uwe baba wa
mataifa mengi.” Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu
alimwamini–Mungu ambaye huwapa wafu uzima, na kwa amri yake, vitu
ambavyo havikuwapo huwa.
18 Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila
matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko
Matakatifu yasemavyo: “Wazao wako watakuwa wengi kama nyota!”
19 Alikuwa mzee wa karibu miaka mia moja, lakini imani yake
haikufifia ingawa alijua kwamba mwili wake ulikuwa kama umekufa, na pia
mkewe, Sara, alikuwa tasa.
20 Abrahamu hakuionea mashaka ile ahadi ya Mungu; alipata nguvu
kutokana na imani, akamtukuza Mungu.
21 Alijua kwamba Mungu anaweza kuyatekeleza yale aliyoahidi.
22 Ndiyo maana Mungu alimkubali kuwa mwadilifu.
23 Inaposemwa, “Alimkubali,” haisemwi kwa ajili yake mwenyewe tu.
24 Jambo hili linatuhusu sisi pia ambao tunamwamini Mungu
aliyemfufua Yesu, Bwana wetu, kutoka wafu.
25 Yeye alitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka ili
tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na Mungu.

\c 5

Kukubalika mbele yake Mungu

1 Sasa, kwa vile tumekubaliwa kuwa wadilifu kwa imani, basi, tunayo
amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Kwa imani yetu, yeye ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu
ambamo sasa tunaishi. Basi, tunajivunia tumaini tulilo nalo la kushiriki
utukufu wa Mungu.
3 Naam, si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba
taabu huleta saburi,
4 nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini.
5 Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha miminia
mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

6 Tulipokuwa bado wanyonge, Kristo, wakati ulipotimia, alikufa kwa
ajili yetu sisi waovu.
7 Si rahisi mtu kufa kwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anaweza
kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
8 Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati
tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
9 Kwa kuwa sasa tumekubaliwa kuwa waadilifu kwa damu ya Kristo, ni
dhahiri zaidi kwamba atatuokoa katika ghadhabu ya Mungu.
10 Maana, tulipokuwa bado adui zake, Mungu alitupatanisha naye kwa
kifo cha Mwanae. Na kwa vile sasa tumepatanishwa naye, ni dhahiri zaidi
kwamba tutaokolewa kwa uzima wa Kristo.
11 Wala si hayo tu, ila tunafurahi pia katika Mungu kwa njia ya
Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametupatanisha na Mungu.

Adamu na Kristo

12 Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo
ikasababisha kifo. Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu,
kwa maana wote wametenda dhambi.
13 Kabla ya Sheria kuwako, dhambi ilikuwako ulimwenguni; lakini
dhambi haiwekwi katika kumbukumbu bila sheria.
14 Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo
kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya
kumwasi Mungu.
Adamu alikuwa kielelezo cha yule ambaye atakuja baadaye.
15 Lakini ipo tofauti: neema ya Mungu si kama dhambi ya Adamu.
Maana, ingawa dhambi ya mtu mmoja ilisababisha kifo kwa wote, kwa
fadhili ya mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, Mungu amewazidishia wote neema
na zawadi zake.
16 Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu, na dhambi ya mtu yule
mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini
baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.
17 Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja kifo kilianza kutawala kwa sababu
ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule
mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na
zawadi hiyo ya kukubaliwa kuwa waadilifu, watatawala katika uzima kwa
njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.

18 Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu
wote, kadhalika kitendo kimoja kiadilifu kinawapa uhuru na uzima.
19 Na kama kwa kutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye
dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi wakubaliwe kuwa
waadilifu.

20 Sheria ilitokea, ikasababisha kuongezeka kwa uhalifu; lakini pale
dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi.
21 Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala
kwa njia ya uadilifu, na kuleta uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo
Bwana wetu.

\c 6

Tunaishi kikamilifu kwa sababu ya Kristo

1 Tuseme nini basi? Je, twendelee kubaki katika dhambi ili neema ya
Mungu iongezeke?
2 Hata kidogo! Kuhusu dhambi sisi tumekufa–tutaendeleaje kuishi
tena katika dhambi?
3 Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu,
tulibatizwa na kuungana na kifo chake.
4 Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili
kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha
Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.

5 Maana, kama sisi tumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyo
hivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutoka wafu kama yeye.
6 Tunajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili
hali ya dhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wa dhambi.
7 Kwa maana, mtu aliyekufa, amenasuliwa kutoka katika nguvu ya
dhambi.
8 Basi, ikiwa tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi
pia pamoja naye.
9 Maana, tunajua kwamba Kristo amekwisha fufuliwa kutoka wafu na
hafi tena; kifo hakimtawali tena.
10 Hivyo, kwa kuwa alikufa–mara moja tu–dhambi haina nguvu tena
juu yake; na sasa anaishi maisha yake katika umoja na Mungu.
11 Hali kadhalika nanyi lazima mjione kuwa mmekufa kuhusu dhambi,
lakini kama mnaoishi katika umoja na Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.

12 Kwa hiyo, dhambi isiitawale tena miili yenu ambayo hufa, na hivyo
kuzitii tamaa zake.
13 Wala msitoe hata sehemu moja ya miili yenu iwe chombo cha kutenda
uovu na dhambi. Badala yake, jitoleeni ninyi wenyewe kwa Mungu kama watu
waliofufuliwa kutoka wafu; toeni nafsi zenu zote kwa Mungu kwa ajili ya
uadilifu.
14 Maana, dhambi haitawatawala ninyi tena, kwani hamko chini ya
Sheria, bali chini ya neema.

Jukumu la kuwa waadilifu

15 Basi, tuseme nini? Je, tutende dhambi ati kwa sababu hatuko chini
ya Sheria bali chini ya neema? Hata kidogo!
16 Mnajua kwamba mkijitolea ninyi wenyewe kama watumwa na kumtii
fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo–au watumwa wa dhambi, na
matokeo yake ni kifo, au wa utii, na matokeo yake ni kukubaliwa kuwa
waadilifu.
17 Ingawa mlikuwa watumwa wa dhambi zamani, sasa lakini–namshukuru
Mungu–mmetii kwa moyo wote yale maazimio na mafundisho mliyopokea.
18 Mlikombolewa kutoka utumwa wa dhambi, mkawa watumwa wa uadilifu.
19 (Hapa natumia lugha ya kawaida ya watu kwa sababu ya udhaifu wenu
wenyewe.) Kama vile wakati fulani mlivyojitolea ninyi wenyewe kutumikia
uchafu na uhalifu kwa ajili ya uovu, vivyo hivyo sasa jitoleeni nafsi
zenu wenyewe kutumikia uadilifu kwa ajili ya utakatifu.

20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na uadilifu.
21 Sasa, mlipata faida gani siku zile kutokana na mambo yale ambayo
mnayaonea aibu sasa? Maana, matokeo ya mambo haya ni kifo!
22 Lakini sasa, mmekwisha kombolewa kutoka utumwa wa dhambi na
mmekuwa watumishi wa Mungu; faida mliyo nayo sasa ni utakatifu, na
matokeo yake ni uzima wa milele.
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa
Mungu ni uzima wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu.

\c 7

Kielelezo kutokana na maisha ya ndoa

1 Ndugu zangu, bila shaka mtaelewa yafuatayo, maana ninawazungumzia
watu wanaojua Sheria. Sheria humtawala mtu wakati akiwa hai.
2 Mathalan: mwanamke aliyeolewa anafungwa na sheria muda wote mumewe
anapokuw hai; lakini mumewe akifa, hiyo sheria haimtawali tena huyo
mwanamke.
3 Hivyo mwanamke huyo akiishi na mwanamume mwingine wakati mumewe
yungali hai, ataitwa mzinzi; lakini mumewe akifa, mwanamke huyo yu huru
kisheria, na akiolewa na mwanamume mwingine, yeye si mzinzi.
4 Hali kadhalika ninyi ndugu zangu: ninyi pia mmekufa kuhusu Sheria
kwa kuwa ninyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye
aliyefufuliwa kutoka wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya
Mungu.
5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa
na Sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.
6 Lakini sasa tumekuwa huru kutoka vifungo vya Sheria, kwa sababu
tumekufa kuhusu lile jambo lililotufanya sisi watumwa. Sasa tunatumikia
kufuatana na maisha mapya ya Roho, na si kufuatana na hali ile ya kale
ya Sheria iliyoandikwa.

Sheria na dhambi

7 Je, tuseme basi, kwamba Sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila
Sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni
nini hasa kutamani mabaya, kama Sheria isingalikuwa imesema:
“Usitamani.”
8 Kwa kuitumia hiyo amri, dhambi ilipata fursa ya kuamsha kila aina
ya tamaa mbaya ndani yangu. Maana, bila Sheria dhambi ni kitu
kilichokufa.
9 Wakati mmoja mimi nilikuwa hai mbali na Sheria; lakini amri
ilipokuja, dhambi ilifufuka,
10 nami nikafa. Hiyo amri ambayo shabaha yake ilikuwa kuleta uhai,
kwangu imeleta kifo.
11 Maana, dhambi ilichukua fursa iliyopatiwa na amri hiyo,
ikanidanganya na kuniua.

12 Basi, Sheria yenyewe ni takatifu, na amri yenyewe ni takatifu, ni
ya haki na nzuri.
13 Je, hii inamaanisha kwamba kile kilicho kizuri kimesababisha kifo
changu? Hata kidogo! Iliyo ni kwamba, dhambi, ili ionekane dhahiri kuwa
ni dhambi, imekitumia kile kilicho kizuri na kusababisha kifo changu.
Hivyo dhambi, kwa njia ya ile amri, ilijionyesha kikamilifu jinsi ilivyo
mbaya mno.

Vita ndani ya mtu

14 Tunajua kwamba Sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kidunia,
mimi nimeuzwa kuwa mtumwa wa dhambi.
15 Sielewi nifanyacho, maana kile ninachotaka sikifanyi, bali kile
ninachochukia ndicho nikifanyacho.
16 Ikiwa basi, ninatenda kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha
kwamba nakubali kuwa ile Sheria ni nzuri.
17 Basi, si mimi hasa ninayefanya kitu hicho, bali ile dhambi iliyo
ndani yangu.
18 Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya
ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi
kulitekeleza.
19 Yaani, badala ya kufanya lile jambo jema ninalotaka, nafanya lile
baya nisilotaka.
20 Basi, kama ninafanya kinyume cha matakwa yangu, hii inamaanisha
kwamba si mimi ninayefanya hayo, bali ni ile dhambi iliyo ndani yangu.

21 Basi, nimegundua kanuni hii: ninataka kufanya jema, lakini
najikuta kwamba lile lililo baya ndilo ninalochagua.
22 Ndani kabisa katika moyo wangu naifurahia sheria ya Mungu.
23 Lakini naona kwamba kuna sheria nyingine inayofanya kazi mwilini
mwangu, sheria ambayo inapingana na ile inayokubaliwa na akili yangu.
Hiyo inanifanya niwe mtumwa wa sheria ya dhambi ifanyayo kazi mwilini
mwangu.
24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka katika mwili huu
unaonipeleka kifoni?
25 Shukrani kwa Mungu afanyaye hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu
Kristo!
Hii basi, ndiyo hali yangu: mimi binafsi, kwa akili yangu,
ninaitumikia sheria ya dhambi.

\c 8

Kuishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu
1 Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao
wameungana na Kristo.
2 Maana, sheria ya Roho iletayo uzima kwa kuungana na Kristo Yesu
imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo.
3 Mungu ametekeleza jambo lile ambalo Sheria haikuweza kutekeleza
kwa sababu ya udhaifu w binadamu. Mungu alimtuma Mwanae akiwa mwenye
mwili sawa na miili yetu sisi wenye dhambi, ili aikabili dhambi, na kwa
mwili huo akaiangamiza dhambi.
4 Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya Sheria yatekelezwe
kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu,
bali kwa nguvu ya Roho.
5 Maana, wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya mwili, hutawaliwa na
fikira za mwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya Roho
Mtakatifu, hutawaliwa na fikira za Roho.
6 Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uzima na amani.
7 Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu;
haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii.
8 Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

9 Lakini ninyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali
kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu.
Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.
10 Lakini kama Kristo yumo ndani yenu, ingawa miili yenu itakufa kwa
sababu ya dhambi, kwenu Roho ndiye uhai kwa sababu mmekubaliwa kuwa
waadilifu.
11 Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani
yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu
yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani
yenu.

12 Hivyo basi, ndugu zangu, tunalo jukumu, lakini si la kuishi
kufuatana na maumbile ya kibinadamu.
13 Kwa maana, kama mkiishi kufuatana na matakwa ya maumbile ya
kibinadamu, hakika mtakufa. Lakini, kama kwa njia ya Roho mnayaua
matendo yenu maovu, basi, mtaishi.
14 Wote wanaoongozwa na Roho wa MUngu ni watoto wa Mungu.
15 Kwa maana, Roho mliyempokea si Roho mwenye kuwafanya ninyi
watumwa na kuwatia tena hofu; sivyo, bali mmempokea Roho mwenye
kuwafanya ninyi watoto wa Mungu, na kwa nguvu ya huyo Roho, sisi
tunaweza kumwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”
16 Naye Roho mwenyewe anajiunga na roho zetu na kuthibitisha kwamba
sisi ni watoto wa Mungu.
17 Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote
Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na
Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia
utukufu wake.

Utukufu ujao

18 Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama
tukiyafananisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu.
19 Viumbe vyote vinatazamia kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto
wake.
20 Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, si
kwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenzi ya Mungu. Hata hivyo
yapo matumaini,
21 maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutoka katika utumwa wa
uharibifu, vishiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu.
22 Kwa maana tunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbe vyote vinalia
kwa maumivu kama ya kujifungua mtoto.
23 Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo
Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani
yetu, tukitazamia kufanywa watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.
24 Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa; lakini tumaini
halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani
anayetumaini kile ambacho tayari anakiona?
25 Kama tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado, basi,
tunakingojea kwa uvumilivu.

26 Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana
hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu
kwa mlio wa huzuni usioelezeka.
27 Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya
huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi
ya Mungu.

28 Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na
kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kufuatana na
kusudi lake.
29 Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate
kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
30 Basi, Mungu aliwaita wale aliokuwa amewateua; na hao aliowaita
aliwakubali kuwa waadilifu; na hao aliowakubali kuwa waadilifu
aliwashirikisha pia utukufu wake.

Upendo ya Mungu katika Kristo Yesu

31 Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande
wetu, nani awezaye kutupinga?
32 Mungu hakumhurumia hata mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili
yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?
33 Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu mwenyewe
huwaondolea hatia!
34 Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa,
tena alifufuka kutoka wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye
anatuombea!
35 Ni nani awezaye kututenga na mapendo ya Kristo? Je, ni taabu, au
dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kuuawa?
36 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:

“Kwa ajili yako,
twakikabili kifo kutwa kucha:
tunatendewa kama kondoo wa kuchinjwa.”

37 Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa
msaada wake yeye aliyetupenda.
38 Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha
na upendo wake: wala kifo, wala uhai; wala malaika, au nguvu nyingine za
mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala
mamlaka;
39 Wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe
chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu kwetu kwa njia ya
Kristo Yesu Bwana wetu.
\fr 8:36
\f Taz Zab 44:22

\c 9

Mungu na taifa lake teule

1 Nasema ukweli mtupu; nimeungana na Kristo nami sisemi uongo.
Dhamiri yangu ikiongozwa na Roho Mtakatifu inanithibitishia jambo hili
pia.
2 Nataka kusema hivi: nina huzuni kubwa na maumivu yasiyopimika
moyoni mwangu
3 kwa ajili ya watu wangu, walio damu moja nami! Kama ingekuwa kwa
faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.
4 Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake,
akawashirikisha utukufu wake; aliagana nao, akawapa Sheria yake, imani
ya kweli na ahadi zake.
5 Wao ni wajukuu wa mababu, naye Kristo, kadiri ya ubinadamu wake,
ametoka katika ukoo wao. Mungu atawalaye juu ya yote, na atukuzwe
milele! Amina.

6 Sisemi kwamba ahadi ya Mungu imebatilika; maana si watu wote wa
Israeli ni wateule wa Mungu.
7 Wala, si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila,
kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazao wake watatokana na Isaka.”
8 Nido kusema, wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu,
bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto
wake.
9 Maana ahadi yenyewe ni hii: “Nitakujia wakati maalum, naye Sara
atapata mtoto.”

10 Tena si hayo tu ila pia Rebeka naye alipata mapacha kwa baba
mmoja, yaani Isaka, babu yetu.
11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata
kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na
baya,
12 Rebeka aliambiwa kwamba yule mtoto wa kwanza atamtumikia yule wa
nyuma. Hivyo uchaguzi wa Mungu unategemea jinsi anavyoita mwenyewe, na
si matendo ya binadamu.
13 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Yakobo nilimpenda, lakini
Esau nilimchukia.”

14 Basi, tuseme nini? Je, Mungu amekosa haki? Hata kidogo!
15 Maana alimwambia Mose: “Nitamhurumia mtu yeyote ninayetaka
kumhurumia; nitamwonea huruma mtu yeyote ninayetaka.”
16 Kwa hiyo, yote hutegemea huruma ya Mungu, na si bidii au mapenzi
ya mtu.
17 Maana Maandiko Matakatifu yasema hivi kwa Farao: “Nilikufanya
mfalme ili kwa njia yako, uwezo wangu ujulikane, na jina langu
litangazwe popote duniani.”
18 Ni wazi,basi, kwamba Mungu humhurumia yeyote anayetaka
kumhurumia, na akipenda kumfanya mtu awe mkaidi, hufanya hivyo.

Ghadhabu na huruma ya Mungu

19 Labda utaniuliza: “Ikiwa mambo yako hivyo, Mungu anawezaje
kumlaumu mtu? Nani awezaye kuyapinga mapenzi yake?”
20 Lakini, ewe binadamu, u nani hata uthubutu kumhoji Mungu? Je,
chungu chaweza kumwuliza mfinyanzi wake: “Kwa nini umenitengeneza namna
hii?”
21 Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu
viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matumizi ya heshima, na kingine kwa
matumizi ya kawaida.

22 Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu. Alitaka kuonyesha ghadhabu yake na
kujulisha uwezo wake, Basi, alikuwa na saburi sana, akiwavumilia wale
ambao walikuwa lengo la ghadhabu yake, ambao walistahili kuangamizwa.
23 Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia
sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha
kuupokea utukufu wake.
24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si tu kutoka miongoni mwa Wayahudi
bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.
25 Maana ndivyo asemavyo katika kitabu cha Hosea:

“Wale waliokuwa <Si watu wangu>
nitawaita: <Watu wangu!>
Naye <Sikupendi>
ataitwa: <Mpenzi wangu!>

26 Na pale walipoambiwa:

<Ninyi si wangu>
hapo wataitwa:
<Watoto wa Mungu hai.”>
\m
27 Naye nabii Isaya, kuhusu Israeli anapaaza sauti: “Hata kama
watoto wa Israeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu
watakaookolewa;
28 maana, Bwana ataitekeleza upesi hukumu yake kamili juu ya
ulimwengu wote.”
29 Ni kama Isaya alivyosema hapo awali: “Kama Bwana Mwenye Nguvu
asingalituachia baadhi ya watoto wa Israeli, tungalikwisha kuwa kama
Sodoma, tungalikwisha kuwa ma Gomora.”

Israeli na Habari Njema

30 Basi, tuseme nini? Ni hivi: watu wa mataifa ambao hawakutafuta
kukubaliwa kuwa waadilifu, wamekubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya
imani,
31 hali watu wa Israeli waliokuwa wakitafuta Sheria iletayo
kukubaliwa kuwa waadilifu, hawakuipata.
32 Kwa nini? Kwa sababu walitegemea matendo yao badala ya kutegemea
imani. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa
33 kama yesemavyo Maandiko Matakatifu:

“Tazama!
Naweka huko Sioni jiwe likwazalo,
mwamba utakaowafanya watu waanguke.
Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa!”

\c 10

1 Ndugu zangu, ninataka na kutazamia kwa moyo wangu wote hao wananchi
wenzangu wakombolewe. Tena nawaombea kwa Mungu daima.
2 Maana naweza kuthibitisha kwa niaba yao kwamba wanayo bidii ya
kumtafuta Mungu; lakini bidii hiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli.
3 Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu,
na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe, na hivyo hawakuikubali njia
hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu.
4 Maana kwa kuja kwake Kristo, Sheria imefikia kikomo chake, ili
kila mtu anayeamini akubaliwe kuwa mwadilifu.

Ukombozi kwa wote

5 Kuhusu kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa kuitii Sheria, Mose aliandika
hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya Sheria ataishi.”
6 Lakini, kuhusu kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa njia ya imani,
yasemwa hivi: “Usiseme moyoni mwako: <Nani atapanda mpaka mbinguni?>
(yaani, kumleta Kristo chini);
7 wala usiseme: <Nani atashuka mpaka Kuzimu> (yaani, kumleta Kristo
kutoka kwa wafu).”
8 Maandiko Matakatifu yesema hivi, “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu
nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani
tunayoihubiri.
9 Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini
moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka.
10 Maana tunaamini kwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; na
tunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa.
11 Maandiko Matakatifu yasema: “Kila amwaminiye hatakuwa na sababu
ya kuaibika.”
12 Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na
wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote
wamwombao.
13 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina
la Bwana, ataokolewa.”

14 Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije
kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama
hakuna mhubiri?
15 Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko
Matakatifu: “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari
Njema!”
16 Lakini wote hawakuipokea hiyo Habari Njema. Maana Isaya alisema:
“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”
17 Hivyo basi, imani inatokana na kuusikiliza ujumbe, na huo ujumbe
unatokana na neno la Kristo.

18 Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia;
kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:

“Sauti yao imeenea duniani kote;
maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
\m
19 Tena nauliza: je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu?
Mose mwenyewe ni kwa kwanza kujibu:

“Nitawafanyeni mwaonee wivu
watu ambao si taifa;
nitawafanyeni muwe na hasira
juu ya taifa la watu wapumbavu.”
\m
20 Tena Isaya anathubutu hata kusema:

“Wale ambao hawakunitafuta wamenipata;
nimejionyesha kwao wasiouliza habari zangu.”
\m
21 Lakini kuhusu Israeli anasema:

“Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
\fr 10:18
\f Taz Zab 19:4

\c 11

Huruma ya Mungu kwa Israeli

1 Basi, nauliza: je, Mungu amewakataa watu wake? Hata kidogo! Mini
binafsi ni Mwisraeli mzawa wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.
2 Mungu hakuwakataa watu wake aliowateua tangu mwanzo. Mnakumbuka
yasemavyo Maandiko Matakatifu juu ya Eliya wakati alipomnung’unikia
Mungu kuhusu Israeli:
3 “Bwana, wamewaua manabii wako na kubomoa madhabahu yako. Ni mimi
tu peke yangu niliyebaki, nao wanataka kuniua?”
4 Je, Mungu alimjibu nini? Alimwambia: “Nimejiwekea elfu saba ambao
hawakumwabudu Baali.”
5 Basi, ndivyo ilivyo pia wakati huu wa sasa: ipo idadi ya waliobaki
ambao Mungu aliwateua kwa sababu ya neema yake.
6 Uteuzi wake unatokana na neema yake, na si kwa sababu ya matendo
yao. Maana, kama uteuzi wake ungetegemea matendo ya watu, neema yake
haingekuwa neema tena.

7 Sasa, je? Watu wa Israeli hawakukipata kile walichokuwa
wanakitafuta; lakini wote walioteuliwa walikipata. Wengine walipumbazwa,
8 kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Mungu ameifanya mioyo yao kuwa mizito,
na mpaka leo hii
hawawezi kuona kwa macho yao
wala kusikia kwa masikio yao.”
\m
9 Naye Daudi anasema:

“Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa,
waanguke na kuadhibiwa.

10 Macho yao yatiwe giza

wasiweze kuona.
Migongo yao ipindike kwa taabu daima!”
\fr 11:9-10
\f Taz Zab 69:22-23

11 Basi, nauliza: je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa?
Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa
mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu.
12 Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na
utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine.
Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha baraka nyingi
zaidi.

Ukombozi wa watu wa mataifa mengine

13 Basi, sasa nawaambieni ninyi watu wa mataifa mengine: Maadamu
mimi nimekuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine, ninajivunia huduma
yangu,
14 nipate kuwafanya wananchi wenzangu wawaonee ninyi wivu, na hivyo
nipate kuwaokoa baadhi yao.
15 Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe
na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!

16 Ikiwa kipande cha kwanza cha mkate kimewekwa wakfu, mkate wote
umewekwa wakfu; mizizi ya mti ikiwa mizuri, na matawi yake huwa mazuri
pia.
17 Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali
pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Ninyi watu wa mataifa
mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na
utomvu wa mzeituni bustanini.
18 Basi, msiwadharau wale waliokatwa kama matawi! Na, hata kama kuna
la kujivunia, kumbukeni kwamba si ninyi mnaoitegemeza mizizi, bali
mizizi ndiyo inayowategemeza ninyi.

19 Lakini utasema: “Matawi yalikatwa kusudi mimi nipandikizwe
mahali pake.”
20 Sawa! Yalikatwa kwa sababu ya kukosa imani, bali wewe unasimama
kwa imani yako. Lakini usijivune; ila uwe na tahadhari.
21 Kwa maana, ikiwa Mungu hakuwahurumia Wayahudi ambao ni kama
matawi ya asili, je, unadhani atakuhurumia wewe?
22 Kumbuka, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali
kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika
wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.
23 Nao Wayahudi, hali kadhalika; wakiacha utovu wao wa imani,
watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.
24 Ninyi watu wa mataifa mengine, kwa asili ni kama tawi la mzeituni
mwitu, lakini mmeondolewa huko, mkapandikizwa katika mzeituni bustanini
mahali ambapo kwa asili si penu. Lakini, Wayahudi kwa asili ni kama
mzeituni bustanini, na itakuwa jambo rahisi zaidi kwao kupandikizwa tena
katika mti huohuo wao.

Kuongoka kwa Israeli

25 Ndugu zangu, napenda mjue ukweli huu uliofichika msije mkajiona
wenye akili sana. Ukaidi wa Wayahudi ulikuwa ni wa muda tu, mpaka watu
wa mataifa mengine watakapokuwa wamemfikia Mungu.
26 Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yesemavyo
Maandiko Matakatifu:

“Mkombozi atakuja kutoka Sioni,
atauondoa uovu wa Yakobo.

27 Hili ndilo agano nitakalofanya nao

wakati nitakapoziondoa dhambi zao.”

28 Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa adui wa
Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa
waliteuliwa, bado ni rafiki wa Mungu kwa sababu ya baba zao.
29 Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti
kwamba amefanya hivyo.
30 Hapo awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata
huruma yake kutokana na kuasi kwao.
31 Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi, Wayahudi
wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu.
32 Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili wapate
kuwahurumia wote.

Mungu asifiwe

33 Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake
hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko
Matakatifu:

34 “Nani aliyepata kuyajua mawazo ya Bwana?

Nani awezaye kuwa mshauri wake?

35 Au, nani aliyempa yeye kitu kwanza

hata aweze kulipwa tena kitu hicho?”
\m
36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na
kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.

\c 12

Maisha katika utumishi wa Mungu

1 Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi,
nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko
iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya
kumwabudu.
2 Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko
ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua
mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na
kamilifu.

3 Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote:
msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe
na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
4 Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
5 Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana
na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
6 Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa.
Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
7 Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha
kufundisha na afundishe.
8 Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye
kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na
asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo
kwa furaha.

9 Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote
ovu, zingatieni jema.
10 Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa
heshima.
11 Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia
Bwana.
12 Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika
shida na kusali daima.
13 Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni
kwa ukarimu.

14 Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni
baraka na wala msiwalaani.
15 Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
16 Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali
jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.

17 Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.
18 Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu
wote.
19 Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo;
maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu;
mimi nitalipiza asema Bwana.”
20 Tena, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula;
akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu
kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
21 Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

\c 13

Utii kwa viongozi wa nchi

1 Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana
mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu.
2 Anayepinga mamlaka ya viongozi anapinga agizo la Mungu; nao
wafanyao hivyo wanajiletea hukumu wenyewe,
3 Maana, watawala hawasababishi hofu kwa watu wema, ila kwa watu
wabaya. Basi, wataka usimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanya mema naye
atakusifu;
4 maana yeye ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwa faida yako.
Lakini ukifanya mabaya, basi, huna budi kumwogopa, maana anao kweli
uwezo wa kutoa adhabu. Yeye ni mtumishi wa Mungu na huitekeleza ghadhabu
ya Mungu kwao watendao maovu.
5 Kwa hiyo ni lazima kuwatii wenye mamlaka, si tu kwa sababu ya
kuogopa ghadhabu ya Mungu, bali pia kwa sababu dhamiri inadai hivyo.

6 Kwa sababu hiyohiyo ninyi hulipa kodi; maana viongozi hao
humtumikia Mungu ikiwa wanatimiza wajibu wao.
7 Mpeni kila mtu haki yake; mtu wa ushuru, ushuru; wa kodi, kodi; na
astahiliye heshima, heshima.

Kupendana kidugu

8 Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana.
Ampendaye jirani yake ameitekeleza Sheria.
9 Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote,
zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda
mwenyewe.”
10 Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, kwa mapendo Sheria
yote hutimizwa.

11 Zaidi ya hayo, ninyi mnajua tumo katika wakati gani: sasa ndio
wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu u karibu zaidi sasa
kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.
12 Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo
yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga.
13 Mwenendo wetu uwe wa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana;
tusiwe na ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu.
14 Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu
za maumbile na kuziridhisha.

\c 14

Usimhukumu ndugu yako

1 Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya
mawazo yake binafsi.
2 Watu huhitilafiana: mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu;
lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani.
3 Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila
kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila
kitu, maana Mungu amemkubali.
4 Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine?
Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara,
maana Bwana anaweza kumsimamisha.

5 Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko
nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja
na afuate msimamo wa akili yake.
6 Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya
kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa
kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula
chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia
anamshukuru Mungu.
7 Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake
mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe
8 maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa
ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.
9 Maana Kristo alikufa, akafufuka ili wapate kuwa Bwana wa wazima na
wafu.
10 Kwa nini, basi wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini
wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha
Mungu.
11 Maana Maandiko yanasema:

“Kama niishivyo, asema Bwana
kila mtu atanipigia magoti,
na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.”
\m
12 Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja yake mbele ya Mungu.

Usimkwaze ndugu yako

13 Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo
kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
14 Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu
chochote kilicho najisi kwa asili yake; lakini, mtu akidhani kwamba kitu
fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi.
15 Kama ukimhuzunisha ndugu yako kwa sababu ya chakula unachokula,
basi mwenendo wako hauongozwi na mapendo. Usikubali hata kidogo chakula
chako kiwe sababu ya kupotea kwa mtu mwingine ambaye Kristo alikufa kwa
ajili yake!
16 Basi, msikubalie kitu mnachokiona kuwa kwenu ni kitu chema
kidharauliwe.
17 Maana Utawala wa Mungu si shauri la kula na kunywa, bali
unahusika na kuwa na uadilifu, amani na furaha iletwayo na Roho
Mtakatifu.
18 Anayemtumikia Kristo namna hiyo humpendeza Mungu, na kukubaliwa
na watu.

19 Kwa hiyo tuyazingatie daima mambo yenye kuleta amani, na
yanayotusaidia kujengana.
20 Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya ubishi juu ya
chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho
kitamfanya mtu aanguke katika dhambi.
21 Afadhali kuacha kula nyama, kunywa divai, au kufanya chochote
ambacho chaweza kumsababisha ndugu yako aanguke.
22 Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule
ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
23 Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa
kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na,
chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.

\c 15

Acheni ubinafsi

1 Sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale walio
dhaifu wayakabili matatizo yao. Tusijipendelee sisi wenyewe tu.
2 Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake kwa wema ili huyo
apate kujijenga katika imani.
3 Maana Kristo hakujipendelea mwenyewe; ila alikuwa kama yasemavyo
Maandiko: “Kashfa zote walizokutolea wewe zimenipata mimi.”
4 Maana yote yalioandikwa yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi
ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na Maandiko hayo Matakatifu
tupate kuwa na matumaini.
5 Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni ninyi kuwa
na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,
6 ili ninyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba
wa Bwana wetu Yesu Kristo.
\fr 15:3
\f Taz Zab 69.9
\fr 15:9
\f Taz Zab 18:49

Habari Njema kwa watu wote

7 Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo
alivyowakaribisheni.
8 Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyesha
uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate
kutimia;
9 ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu
ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Kwa sababu hiyo, nitakusifu
miongoni mwa watu wa mataifa.
Nitaziimba sifa za jina lako.”
\m
10 Tena Maandiko yasema:

“Furahini, enyi watu wa mataifa;
furahini pamoja na watu wake.”
\m
11 Na tena:

“Enyi mataifa yote, msifuni Bwana;
enyi watu wote, msifuni.”
\m
12 Tena Isaya asema:

“Atatokea mtu katika ukoo wa Yese,
naye atawatawala watu wa mataifa;
nao watamtumainia.”

13 Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na
amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu
ya Roho Mtakatifu.
\fr 15:11
\f Taz Zab 117:1

Huduma ya Paulo

14 Ndugu zangu, mimi binafsi nina hakika kwamba ninyi pia mmejaa
wema, elimu yote, na mnaweza kushauriana ninyi kwa ninyi.
15 Lakini nimewaandikia hapa na pale katika barua hii bila woga,
nipate kuwakumbusheni juu ya mambo fulani. Nimefanya hivyo kwa sababu ya
neema aliyonijalia Mungu
16 ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu
langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa
mengine wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, dhabihu iliyotakaswa
na Roho Mtakatifu.
17 Kwa hiyo, nikiwa nimeungana na Kristo Yesu, naweza kujivunia
huduma yangu kwa ajili ya Mungu.
18 Sithubutu kusema kitu kingine chochote isipokuwa tu kile ambacho
Kristo Yesu amekifanya kwa kunitumia mimi ili watu wa mataifa wapate
kutii. Amefanya hivyo kwa maneno na vitendo,
19 kwa nguvu ya miujiza na maajabu, na kwa nguvu ya Roho wa Mungu.
Basi, kwa kusafiri kila mahali, tangu kule Yerusalemu mpaka Iluriko,
nimeihubiri kikamilifu Habari Njema ya Kristo.
20 Nia yangu imekuwa daima kuihubiri Habari Njema popote pale ambapo
jina la Kristo halijapata kusikika, nisije nikajenga juu ya msingi wa
mtu mwingine.
21 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Watu wote ambao hawakuambiwa habari zote wataona;
nao wale ambao hawajapata kusikia, wataelewa.”

Mpango wa Paulo wa kutembelea Roma

22 Kwa sababu hiyo nilizuiwa mara nyingi kuja kwenu.
23 Lakini maadam sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa
kwa miaka mingi nimekuwa na nia kubwa ya kuja kwenu,
24 natumaini kufanya hivyo sasa. Ningependa kuwaoneni nikiwa
safarini kwenda Spania na kupata msaada wenu kwa safari hiyo baada ya
kufurahia kuwa kwa muda pamoja nanyi.
25 Lakini, kwa sasa nakwenda kuwahudumia watu wa Mungu kule
Yerusalem.
26 Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yemeamua kutoka mchango wao
kuwasaidia watu wa Mungu walio maskini huko Yerusalem.
27 Wao wenyewe wameamua kufanya hivyo; lakini, kwa kweli, hilo ni
jukumu lao kwa hao. Maana, ikiwa watu wa mataifa mengine wameshiriki
baraka za kiroho za Wayahudi, wanapaswa nao pia kuwahudumia Wayahudi
katika mahitaji yao ya kidunia.
28 Nitakapokwisha tekeleza kazi hiyo na kuwakabidhi mchango huo
uliokusanywa kwa ajili yao, nitawatembeleeni ninyi nikiwa safarini
kwenda Spania.
29 Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.

30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa kwa ajili ya Bwana wetu Yesu
Kristo, na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, mniunge mkono kwa
kuniombea kwa Mungu.
31 Ombeni nipate kutoka salama miongoni mwa wale wasioamini walioko
Uyahudi, nayo huduma yangu huko Yerusalem ipate kukubaliwa na watu wa
Mungu walioko huko.
32 Hivyo, Mungu akipenda, nitaweza kuja kwenu na moyo wa furaha,
nikapumzike pamoja nanyi.
33 Mungu aliye chanzo cha amani na awe nanyi nyote! Amina!

\c 16

Salamu kwa watu mbalimbali

1 Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika
kanisa la Kenkrea.
2 Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni
msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana
kwa watu wengi na kwangu pia.

3 Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu
katika utumishi wa Kristo Yesu.
4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili
shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu
wa mataifa mengine.
5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao.
Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza
katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo.
6 Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu waliofungwa
gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena
walikuwa Wakristo kabla yangu mimi.

8 Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana na Bwana.
9 Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika utumishi
wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku.
10 Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo umethibitishwa.
Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
11 Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa jamaa
yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana.

12 Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi wa
Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Bwana.
13 Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana, na mama
yake ambaye ni mama yangu pia.
14 Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme Patroba, Herma na ndugu
wote walio pamoja nao.
15 Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olumpa,
pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.

16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara ya upendo. Salamu kwenu
kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.

Mawaidha ya mwisho

17 Ndugu zangu, nawasihi muwafichue wote wanaosababisha mafarakano
na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho
mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,
18 maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali
wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za
kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.
19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa sababu ya
furaha yangu. Nawatakeni muwe na hekima katika mambo mema, na bila hatia
kuhusu mambo mabaya.
20 Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani
chini ya miguu yenu.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali kadhalika
Lukio, Yasoni, na Sosipatro, wananchi wenzangu, wanawasalimu.

22 Nami Tertio, ninayeandika barua hii nawasalimuni katika Bwana.

23 Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana kwake,
anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto,
wanawasalimu.fb
\fm b
\fr 16:23
\f
\is Baadhi ya makala zina aya 24:
\ie Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.

Sala ya kumsifu Mungu

24 missing
25 Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika
ile Habari Njema niliyohubiri juu ya ujumbe wa Yesu Kristo, na katika
ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi
zilizopita.
26 Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya
manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirisha kwa mataifa yote
ili wote waweze kuamini na kutii.

27 Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu kwa njia
ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina.
\z

\id 1CO SW47.ALL 19/03/90 SN SWAHILI FINAL DRAFT
\h 1 WAKORINTHO

          BARUA YA KWANZA YA PAULO KWA
                 WAKORINTHO

\c 1

1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya
Mungu, na ndugu Sosthene,
2 tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyi
mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu
wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo
aliye Bwana wao na wetu pia.

3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana
wetu Yesu Kristo.

Baraka za Mungu

4 Ninamshukuru Mungu wangu daima kwa ajili yenu kwa sababu
amewatunukia ninyi neema yake kwa njia ya Kristo Yesu.
5 Maana, kwa kuungana na Kristo mmetajirishwa katika kila kitu.
Mmejaliwa elimu yote na uwezo wote wa kuhubiri,
6 kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwa ndani yenu,
7 hata hampungukiwi kipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea
kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
8 Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia
Siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae
Yesu Kristo Bwana wetu.

Mgawanyiko katika jumuiya ya waumini

10 Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni
nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na
fikira moja na nia moja.
11 Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya
Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
12 Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema,
“Mimi ni wa Paulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,” mwingine: “Mimi
ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo,”.
13 Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwa kwa ajili
yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?
14 Namshukuru Mungu kwamba sikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenu
isipokuwa tu Krispo na Gayo.
15 Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jina langu. (((
16 Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa,
sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
17 Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena,
niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo
cha Kristo msalabani isibatilishwe.

Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu

18 Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la
kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi
tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.
19 Maana Maandiko Matakatifu yasema:

“Nitaiharibu hekima yao wenye hekima,
na elimu ya wataalamu nitaitupilia mbali.”
\m
20 Yu wapi basi, mwenye hekima? Yu wapi basi, mwalimu wa Sheria?
Naye bingwa wa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanya
hekima ya ulimwengu kuwa upumbavu.

21 Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa
njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale
wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni
upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.
22 Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima;
23 lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo
hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;
24 lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu
ya Mungu na hekima ya Mungu.
25 Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi
kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu,
kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.

26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye
hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu
wa tabaka ya juu.
27 Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni
upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo
ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo
duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo
ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.
29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu.
30 Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu
amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na
Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
31 Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Mwenye kutaka kujivuna,
basi, na ajivunie kazi ya Bwana.”

Ujumbe juu ya Yesu aliyesulubiwa
\c 2

1 Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu
kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu.
2 Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu
kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa.
3 Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi.
4 Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na
ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.
5 Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu,
na si hekima ya binadamu.

Hekima ya Mungu

6 Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa
kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa
dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
7 Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima
iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu
wetu.
8 Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana
wangalielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
9 Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona
wala sikio kuyasikia,
mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni,
hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”

10 Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake.
Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu.
11 Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu
huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa
Mungu.
12 Sasa sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho
atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu.

13 Basi sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima
ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo
ya kiroho kwa walio na huyo Roho.
14 Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo
mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu
kutambuliwa kwa msaada wa Roho.
15 Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila
kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine.
16 Maandiko yasema: “Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani
awezaye kumshauri?” Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.

Watumishi wa Bwana
\c 3

1 Ndugu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu mlio na huyo Roho.
Nilipaswa kusema nanyi kama watu wa kidunia, kama watoto wachanga katika
maisha ya Kikristo.
2 Ilinibidi kuwalisheni kwa maziwa, na si kwa chakula kigumu, kwani
hamkuwa tayari kukipokea. Hata sasa hamko tayari.
3 Maana bado mu watu wa kidunia. Je, si kweli kwamba bado uko wivu
na magombano kati yenu? Mambo hayo yanaonyesha wazi kwamba ninyi bado ni
watu wa kidunia, mnaishi mtindo wa kidunia.
4 Mmoja wenu anaposema, “Mimi ni wa Paulo”, na mwingine, “Mimi ni
wa Apolo”, je, hiyo haionyeshi kwamba mnaishi bado kama watu wa dunia
hii tu?

5 Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Sisi ni watumishi tu ambao
tuliwaleteeni ninyi imani. Kila mmoja wetu anafanya kazi aliyopewa na
Bwana.
6 Mimi nilipanda mbegu, Apolo akamwagilia maji; lakini aliyeiotesha
mbegu ni Mungu.
7 Wa maana si yule aliyepanda mbegu, au yule aliyemwagilia maji; wa
maana ni Mungu aliyeiwezesha mbegu kuota.
8 Yule aliyepanda na yule aliyemwagilia maji wote ni sawa, ingawa
kila mmoja atapokea tuzo lake kufuatana na jitihada yake mwenyewe.
9 Maana sisi ni ndugu, wafanyakazi pamoja na Mungu; na ninyi ni
shamba lake; ninyi ni jengo lake.

10 Kwa msaada wa neema aliyonipa Mungu, nimefaulu, kama mwashi stadi
mwenye busara, kuweka msingi ambao juu yake mtu mwingine anajenga. Basi,
kila mmoja awe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake.
11 Hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine badala ya ule
uliokwisha wekwa, yaani Yesu Kristo.
12 Juu ya msingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha au mawe
ya thamani; anaweza kutumia miti, majani au nyasi.
13 Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati Siku
ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyo itatokea na moto, na huo
moto utaipima na kuonyesha ubora wake.
14 Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto,
atapokea tuzo;
15 lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake;
lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni.

16 Je, hamjui kwamba ninyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa
Mungu anakaa ndani yenu?
17 Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana
hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni ninyi wenyewe.

18 Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye
hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya
kweli.
19 Maana, hekima ya kidunia ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwani
Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwanasa wenye hekima katika ujanja
wao.”
20 Na tena: “Bwana ajua kwamba mawazo ya wenye hekima hayafai.”
21 Basi, mtu asijivunie watu. Maana kila kitu ni chenu.
22 Paulo, Apolo na Kefa, ulimwengu, maisha na kifo; mambo ya sasa na
ya baadaye, yote ni yenu.
23 Lakini ninyi ni wa Kristo naye Kristo ni wa Mungu.
\fr 3:20
\f taz Zab 94:11

Utumishi wa mitume
\c 4

1 Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri
za mungu.
2 Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa
mwaminifu.
3 Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, au na mahakama ya
kibinadamu; wala sijihukumu.
4 Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi
kwamba sina lawama. Bwana ndiye anayenihukumu.
5 Basi, msihukumu kabla ya wakati wake acheni mpaka Bwana
atakapokuja. Yeye atayafichua mambo ya giza yaliyofichika, na kuonyesha
wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifa anayostahili
kutoka kwa Mungu.

6 Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni
kielelezo kwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe
maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na
mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na
ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?

8 Haya, mmekwisha shiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalme
bila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweli watawala, ili nasi pia tuweze
kutawala pamoja nanyi.
9 Nafikiri Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa,
kama watu waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya
ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu.
10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye
busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, ninyi ni wenye nguvu.
Ninyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa.
11 Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa
makofi, hatuna malazi.
12 Tena twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe.
Tukitukanwa, tunawatakia baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia;
13 tukisingiziwa, tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kama
uchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi ni takataka!

14 Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha ninyi, bali kwa
ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi.
15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya
Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristo mimi
ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.

16 Kwa hiyo, nawasihi: fuateni mfano wangu.
17 Ndiyo maana nimemtuma Timetheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi
na mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika
kuishi maisha ya Kikristo; njia ninayofundisha kila mahali katika
makanisa yote.

18 Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja
tena kwenu.
19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo
nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye
majivuno, bali pia kila wanachoweza kufanya.
20 Maana Utawala wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu.
21 Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo
na upole?

Ukosefu wa uadilifu katika kanisa
\c 5

1 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi miongoni mwenu; tena ni
uzinzi mbaya ambao haujapata kuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu.
Nimeambiwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!
2 Mnawezaje kujivuna? Ingekuwa afadhali kwenu kuomboleza, na huyo
aliyefanya kitu hicho aondolewe miongoni mwenu.
3 Nami, kwa upande wangu, ingawa kwa mwili niko mbali nanyi, hata
hivyo kwa roho niko hapo pamoja nanyi: na hivyo, kama vile nipo hapo,
nimekwisha mhukumu huyo aliyefanya jambo hilo la aibu.
4 Wakati mnapokusanyika pamoja kwa jina la Bwana Yesu, nami nikiwa
pamoja nanyi kwa roho, basi, kwa uwezo wa Bwana wetu Yesu,
5 mkabidhini mtu huyo kwa Shetani ili mwili wake uharibiwe na roho
yake iweze kuokolewa Siku ile ya Bwana.

6 Majivuno yenu hayafai! Je, hamjui kwamba chachu kidogo huchachusha
donge lote la unga?
7 Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge
jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo, Pasaka
yetu, amekwisha tolewa tambiko.
8 Basi, tufanye karamu hiyo si kwa chachu ile ya kale, chachu ya
ubaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, mkate wa usafi na kweli.

9 Niliwaandikia katika barua yangu msishirikiane na wazinzi.
10 Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio
wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa
hao wote ingewalazimu ninyi kuihama dunia hii kabisa!
11 Nilichoandika ni hiki: msishirikiane na ndugu Mkristo aliye
mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi mlevi na mlaghai. Mtu
wa namna hiyo, hata kula msile naye.

12 Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu
atawahukumu. Je, ninyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu
ninyi wenyewe?
13 Mfukuzeni mbali nanyi huyo mwovu!

Mashtaka ya ndugu waumini
\c 6

1 Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu muumini mbele ya mahakama
ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
2 Je, hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwa basi,
ulimwengu utahukumiwa nanyi, kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika
mambo madogo?
3 Je, hamjui kwamba, licha ya kuhukumu mambo ya kawaida ya kila
siku, tutawahukumu hata malaika?
4 Mnapokuwa na mizozo juu ya mambo ya kawaida, je, mnawaita wawe
mahakimu watu ambao hata hawalijali kanisa?
5 Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye
hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
6 Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu yake
mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini.

7 Kwa kweli huko kushtakiana tu wenyewe kwa wenyewe kwabainisha
kwamba mmeshindwa kabisa! Je, haingekuwa jambo bora zaidi kwenu
kudhulumiwa! Haingekuwa bora zaidi kwenu kunyang’anywa mali yenu?
8 Lakini, badala yake, ninyi ndio mnaodhulumu na kunyang’anya; tena,
hayo mnawafanyia ndugu zenu!
9 Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu?
Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu,
wazinzi, au walawiti,
10 wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang’anyi, hao wote
hawatashiriki Utawala wa Mungu.
11 Baadhi yenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywa
watakatifu, na kupatanishwa na Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo na
kwa Roho wa Mungu wetu.

Tumieni miili yenu kwa utukufu wa Mungu

12 Mtu anaweza kusema: “Kwangu mimi kila kitu ni halali.” Sawa;
lakini si kila kitu kinafaa. Nakubali kwamba kila kitu ni halali kwangu
lakini sitaki kutawaliwa na kitu chochote.
13 Unaweza kusema: “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa
ajili ya chakula.” Sawa; lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili
wa mtu si kwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili ya kumtumikia Bwana,
naye Bwana ni kwa ajili ya mwili.
14 Basi, Mungu aliyemfufua Bwana kutoka wafu atatufufua nasi pia kwa
nguvu yake.

15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya mwili wa Kristo? Je,
mnadhani naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa
sehemu ya mwili wa kahaba? Hata kidogo!
16 Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja
naye–kama ilivyoandikwa: “Nao wawili watakuwa mwili mmoja.”
17 Lakini aliyejiunga na Bwana huwa roho moja naye.
18 Jiepusheni kabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zote hutendwa nje ya
mwili lakini mzinzi hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
19 Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye
ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Ninyi basi, si mali yenu
wenyewe.
20 Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa
ajili ya kumtukuza Mungu.

Suala juu ya kuoa
\c 7

1 Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi;
2 lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe
na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
3 Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu
alio nao kwa mumewe.
4 Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali
kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.
5 Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa
kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara,
ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu.

6 Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri.
7 Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja
anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine
kile.

8 Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba
ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
9 Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni
afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.

10 Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke
asiachane na mumewe;
11 lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la,
apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.

12 Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa
mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali
kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
13 Na, kama mwanamke Mkristo anaye mume asiyeamini, na huyo
mwanamume akakubali kuendelea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe.
14 Kwa maana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana
na mkewe; na huyo mke asiyeamini hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na
mumewe. Vinginevyo watoto wao wangekuwa si wa Mungu; kumbe sasa ni
watoto wake Mungu.
15 Hata hivyo, ikiwa yule asiyeamini anataka kumwacha mwenzake aliye
Mkristo, basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo, mume au mke, atakuwa
huru. Maana Mungu amewaiteni ninyi muishi kwa amani.
16 Wewe mama Mkristo, unawezaje kuwa na hakika kwamba hutaweza
kumwokoa mume wako? Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa na hakika
kwamba hutaweza kumwokoa mkeo?

Ishi kama ulivyoitwa na Mungu

17 Kwa vyovyote kila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa
na Bwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizo langu kwa
makanisa yote.
18 Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba
hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
19 Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilicho muhimu ni
kuzishika amri za Mungu.
20 Basi, kila mmoja na abaki kama alivyokuwa wakati alipoitwa.
21 Je, wewe ulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakini
ukipata fursa ya kuwa huru, itumie.
22 Maana yeye aliyeitwa na Bwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huru wa
Bwana. Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwa mtu huru, huwa mtumwa wa
Kristo.
23 Nyote mmenunuliwa kwa bei; kwa hiyo msiwe tena watumwa wa watu.
24 Ndugu zangu, kila mmoja wenu basi, na abaki na Mungu kama
alivyokuwa wakati alipoitwa.

Kuhusu wasiooa na wajane

25 Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana;
lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili
kuaminiwa.
26 Basi, kutokana na shida iliyopo sasa nadhani ingefaa mtu abaki
kama alivyo.
27 Je, umeoa? Basi, usitake kuachana na mkeo. Wewe hukuoa? Basi,
usitake kuoa.
28 Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa
hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia
hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate ninyi.

29 Ndugu, nataka kusema hivi: muda uliobaki ni mfupi. Na tangu sasa
wale waliooa na waishi kama vile hawakuoa;
30 wenye kulia wawe kama hawalii, na wenye kufurahi wawe kama
hawafurahi; wanaonunua wawe kama hawana kitu;
31 nao wenye shughuli na dunia hii wawe kama vile hawana shughuli
sana nayo. Maana ulimwengu huu, kama tuujuavyo, unapita.

32 Ningependa ninyi msiwe na wasiwasi. Mtu asiye na mke
hujishughulisha na kazi ya Bwana jinsi atakavyompendeza Bwana.
33 Mtu aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia jinsi
atakavyompendeza mkewe,
34 naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha
na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini
mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi
atakavyompendeza mumewe.

35 Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuio.
Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia
moja.

36 Kama mtu anaona kwamba hamtendei vyema mchumba wake asipomwoa, na
kama tamaa zake zinamshinda, na afanye atakavyo; waoane tu; hatakuwa
ametenda dhambi.
37 Lakini kama huyo mwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooa
na kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamua namna ya kufanya, basi,
anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyo mwenzake bikira.
38 Kwa maneno mengine: yule anayeamua kumwoa huyo mchumba wake
anafanya vema; naye anayeamua kutomwoa anafanya vema zaidi.

39 Mwanamke huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo.
Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na
mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
40 Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo
alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.

Vyakula vilivyotambikiwa sanamu
\c 8

1 Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi
sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno;
lakini mapendo hujenga.
2 Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama
inavyompasa.
3 Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye.

4 Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba
sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.
5 Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata
kama wako miungu na mabwana wengi,
6 hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote,
ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo,
ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia
yake.

7 Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine
waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula
huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri
zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
8 Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha
kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.

9 Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani
dhaifu waanguke katika dhambi.
10 Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye
ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo
wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
11 Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili
yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
12 Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao
dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
13 Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu,
sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika
dhambi.

Haki na jukumu la mitume
\c 9

1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu
Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?
2 Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi
mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya
kuungana kwenu na Bwana.

3 Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii:
4 Je, hatuna haki ya kula na kunywa?
5 Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara zetu, kama
vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa?
6 Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu
kwa kufanya kazi?
7 Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani
asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa
maziwa ya mifugo yake?

8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemi
hivyo?
9 Imeandikwa katika Sheria ya Mose: “Usimfunge kinywa ng’ombe
anapoliwata nafaka.” Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng’ombe?
10 Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya
yaliandikwa kwa ajili yetu; kwani yule anayelima na yule anayevuna, wote
wawili wana haki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno.
11 Ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo
kubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia?
12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je,
sisi hatuna haki zaidi kuliko hao?
Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili kila
kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.
13 Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao
Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo
sadaka?
14 Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate
riziki zao kutokana nayo.

15 Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala
siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko
kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure.
16 Ikiwa ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo
ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!
17 Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia
malipo; lakini maadam naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni
jukumu nililopewa nitekeleze.
18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya
kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa
kuihubiri.

19 Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa
wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
20 Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani,
ingawa mimi siko chini ya Sheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili
niwapate hao walio chini ya Sheria.
21 Na kwa wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria,
ili niwapate hao walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko
nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
22 Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio
dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao
kwa kila njia.

23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki
baraka zake.
24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio
wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
25 Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili
wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya
kudumu daima.
26 Ndivyo basi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyo
ninavyopigana, na si kama bondia anayetupa ngumi zake hewani.
27 Naupa mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili,
nisije mimi mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine.
\il 5
ic
\is Taji (1 Kor 9:24,25)
\ie

\c 10

1 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi
wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.
2 Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile
bahari.
3 Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,
4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka
ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao
zilisambazwa jangwani.

6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi
tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo
Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”
8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja
watu ishirini na tatu elfu.
9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na
nyoka.
10 Wala msinung’unike kama baadhi yao walivyonung’unika,
wakaangamizwa na Mwangamizi!

11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na
yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili.
12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni
mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na
majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo
salama.

14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.
15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo
nisemayo.
16 Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa
hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki
mwili wa Kristo?
17 Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili
mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
18 Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula
vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.
19 Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu
ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya
sanamu?
20 Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu
wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na
ushirika na pepo.
21 Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi
kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.
22 Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu
zaidi kuliko yeye?

Kila kitu kwa ajili ya utukufu wa Mungu

23 Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni
halali lakini si vyote vinajenga.
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
\fr 10:26
\f taz Zab 24:1

25 Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa
sababu ya dhamiri zenu;
26 maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya
Bwana.”
27 Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda,
basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya
dhamiri zenu.
28 Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,”
basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri,
msile.
29 Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri
yake huyo aliyewaambieni.
Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa
nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?”

31 Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa
ajili ya utukufu wa Mungu.
32 Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la
Mungu.
33 Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila
kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.

\c 11

1 Niigeni mimi kama ninavyomwiga Kristo.

Kufunika kichwa wakati wa ibada

2 Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu
mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
3 Lakini napenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kila
mwanamume, na mwanamume ni kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha
Kristo.
4 Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu
huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
5 Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe wa Mungu bila kufunika
kichwa chake, anamdharau mumewe; anayefanya hivyo ni sawa tu na mwanamke
aliyenyoa kichwa chake.
6 Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake.
Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi,
afadhali afunike kichwa chake.
7 Haifai mwanamume kufunika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano wa
Mungu na kioo cha utukufu wake Mungu; lakini mwanamke ni kioo cha
utukufu wa mwanamume.
8 Mwanamume hakutoka kwa mwanamke, ila mwanamke alitoka kwa
mwanamume.
9 Mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, ila mwanamke aliumbwa
kwa ajili ya mwanamume.
10 Ndiyo maana mwanamke hufunika kichwa chake, iwe ishara ya mamlaka
yaliyo juu yake, na pia kwa sababu ya malaika.
11 Hata hivyo, mbele ya Bwana mwanamke si kitu bila mwanamume, naye
mwanamume si kitu bila mwanamke.
12 Kama vile mwanamke alivyotokana na mwanamume, vivyo hivyo
mwanamume huzaliwa na mwanamke; kila kitu hutoka kwa Mungu.
13 Amueni wenyewe: Je, inafaa mwanamke kumwomba Mungu bila kuvaa
kitu kichwani?
14 Hata maumbile yenyewe huonyesha wazi kwamba kwa mwanamume kuwa na
nywele ndefu ni aibu kwake mwenyewe;
15 lakini kwa mwanamke kuwa na nywele ni heshima kwake; nywele zake
ndefu amepewa ili zimfunike.
16 Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue
kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana
desturi nyingine.

Karamu ya Bwana
\r
\is (Mat. 26:26-29; Marko 14:22-25; Luka 22:14-20)
\ie

17 Nikiwa bado nawapeni maagizo haya, siwezi hata kidogo kuwapa
ninyi hongera kuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyi waumini yaleta
hasara zaidi kuliko faida.
18 Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea
mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
19 maana ni lazima fikira tofauti ziweko miongoni mwenu, ili wale
walio thabiti wapate kutambulikana.
20 Kweli mnakutana, lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana!
21 Maana mnapokula kila mmoja hukikalia chakula chake mwenyewe, hata
hutokea kwamba baadhi yenu wana njaa, na wengine wamelewa!
22 Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau
kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini?
Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.

23 Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni:
kwamba, usiku ule Bwana Yesu aliotolewa, alitwaa mkate,
24 akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio
kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.”
25 Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: “Hiki ni
kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi,
kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”

26 Maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwatangaza
kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.
27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila
kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.
28 Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo
na anywe kikombe hicho;
29 maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana,
anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe.
30 Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine
kadhaa wamekufa.
31 Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo.
32 Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili
tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana kula chakula cha Bwana, kila
mmoja amngoje mwenzake.
34 Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na ale nyumbani kwake, ili
kukutana kwenu kusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine,
nitawapeni maelezo nitakapokuja.

Vipaji vya Roho Mtakatifu
\c 12

1 Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya:
2 Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa
na sanamu tupu.
3 Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi
kusema: “Yesu alaaniwe!” Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema:
“Yesu ni Bwana,” asipoongozwa na Roho Mtakatifu.

4 Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni
mmoja.
5 Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni
mmoja.
6 Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni
mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote.
7 Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote.
8 Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu
apendavyo Roho huyohuyo.
9 Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha
kuponya;
10 humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha
kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo
kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni,
na mwingine kipaji cha kuzifafanua.
11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu
kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.

Viungo vingi, lakini mwili mmoja

12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo
vyote–ingawaje ni vingi–hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa
Kristo.
13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa
au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na
sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.

14 Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.
15 Kama mguu ungejisemea: “Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si
mali ya mwili”, je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!
16 Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si
mali ya mwili”, je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
17 Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama
mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?
18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika
mwili kama alivyopenda.
19 Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20 Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni
mmoja.

21 Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe”, wala
kichwa hakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji ninyi.”
22 Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili
zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.
23 Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima
kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili
ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
24 ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe
ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile
kilichopungukiwa heshima,
25 ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote
vishughulikiane.
26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho.
Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.

27 Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo
cha mwili huo.
28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu
walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya,
kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
29 Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni
wenye kipaji cha kufanya miujiza?
30 Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha
kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?
31 Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa
nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.

Upendo
\c 13

1 Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama
sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
2 Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu,
nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata
nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.
3 Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili
wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.

4 Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu,
hajidai, wala hajivuni.
5 Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana
wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,
6 hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
7 Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
8 Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe
wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha
ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.
9 Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la
Mungu si kamili.
10 Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika, vyote visivyo
vikamilifu vitatoweka.

11 Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto,
nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu mzima, mambo ya
kitoto nimeyaacha.
12 Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo
baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapo
baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi.
13 Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini
lililo kuu kupita yote ni upendo.

Vipaji vingine vya Roho Mtakatifu
\c 14

1 Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji
vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
2 Mwenye kunena lugha ngeni hasemi na watu bali anasema na Mungu.
Yeye hunena kwa nguvu ya Roho mambo yaliyofichika.
3 Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, husema na watu
kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji na kuwatia moyo.
4 Mwenye kunena lugha ngeni anajijenga mwenyewe. Lakini mwenye
kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, analijenga kanisa.

5 Basi, ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni lakini
ningependelea hasa muwe na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, maana
mtu mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, ni wa maana zaidi
kuliko yule mwenye kusema lugha ngeni, isipokuwa tu kama yupo hapo mtu
awezaye kuyafafanua hayo mambo asemayo, ili kanisa lipate kujengwa.
6 Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha
ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama
nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au
mafundisho fulani.
7 Ndivyo ilivyo kwa vyombo visivyo na uhai vyenye kutoa sauti kama
vile filimbi au kinanda. Je, mtu anawezaje kuutambua wimbo unaochezwa
kama vyombo hivyo havitoi sauti waziwazi vinapopigwa?
8 La mgambo likilia bila kufuata taratibu zake, nani atajiweka
tayari kwa vita?
9 Hali kadhalika na ninyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye
kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea
hewani.
10 Zipo lugha mbalimbali ulimwenguni, na hakuna hata mojawapo isiyo
na maana.
11 Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani,
mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
12 Hali kadhalika na ninyi, maadam mna hamu ya kupata vipaji vya
Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.
13 Kwa hiyo, mwenye kunena lugha ngeni na aombe apate uwezo wa
kuzifafanua.
14 Maana, nikisali kwa lugha ngeni roho yangu ndiyo inayosali,
lakini akili yangu hubaki bure.
15 Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu, nitasali pia kwa
akili yangu; nitaimba kwa roho yangu, nitaimba pia kwa akili yangu.
16 Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye
katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina,”
kama haelewi unachosema?
17 Sala yako ya shukrani yaweza kweli kuwa bora, lakini huyo
mwingine haitamfaidia.

18 Namshukuru Mungu kwamba mimi nasema kwa lugha ngeni zaidi kuliko
ninyi nyote.
19 Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno
matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno
elfu ya lugha ngeni.
20 Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu muwe
kama watoto wachanga lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu
waliokomaa.
21 Imeandikwa katika Sheria:

“Bwana asema hivi:
<Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni,
na kwa midomo ya wageni,
nitasema na watu hawa,
hata hivyo, hawatanisikiliza.”>

22 Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili
ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji
cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa
ajili ya wasioamini.

23 Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema
kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je,
hawatasema kwamba ninyi mna wazimu?
24 Lakini, wote wakiwa wanautangaza ujumbe wa Mungu, akija mtu wa
kawaida au asiyeamini, yote atakayosikia yatamhakikishia ubaya wake
mwenyewe; yote atakayosikia yatamhukumu.
25 Siri za moyo wake zitafichuliwa, naye atapiga magoti na kumwabudu
Mungu akisema: “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi.”

Utaratibu katika kanisa

26 Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo,
mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu,
mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue
yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
27 Wakiwepo watu wenye vipaji vya kusema kwa lugha ngeni, waseme
wawili au watatu, si zaidi, tena mmojammoja; na aweko mtu wa kufafanua
yanayosemwa.
28 Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusema lugha
ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe na Mungu.
29 Kuhusu wale wenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, waseme
wawili au watatu, na wengine wayapime maneno yao.
30 Ikiwa mmoja anaposema mwingine wa wasikilizaji amepata ufunuo
kutoka kwa Mungu, basi, yule anayesema anyamaze.
31 Maana nyote mwaweza kutangaza ujumbe wa Mungu, mmoja baada ya
mwingine, ili nyote mpate kujifunza na kutiwa moyo.
32 Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni lazima kitawaliwe na huyo
mwenye hicho kipaji.
33 Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani.
34 Kama ilivyo desturi katika makanisa yote ya watu wa Mungu,
wanawake wakae kimya katika mikutano ya waumini. Hawana ruhusa kusema;
ila wawe watii kama isemavyo Sheria.
35 Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani,
maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.

36 Je, mnadhani neno la Mungu limetoka kwenu ninyi au kwamba
limewajieni ninyi peke yenu?
37 Kama mtu yeyote anadhani kwamba yeye ni mjumbe wa Mungu au kwamba
anacho kipaji cha Roho, na ajue kwamba haya ninayowaandikia ninyi ni
amri ya Bwana.
38 Lakini mtu asiyetambua hayo, basi, mtu asimjali mtu huyo.

39 Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswa kuwa na hamu ya kutangaza
ujumbe wa Mungu; lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni.
40 Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.

Ufufuo wa Kristo
\c 15

1 Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni
nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake.
2 Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno
niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.
\fr 15:3
\f taz Zab 53:5-12
\fr 15:4
\f taz Zab 16:8-10

3 Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi
niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na
Maandiko Matakatifu;
4 kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa;
5 kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.
6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao
wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
7 Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote.
8 Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu
aliyezaliwa kabla ya wakati.
9 Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume na wala sistahili
kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu.
10 Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema
yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa,
ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.
11 Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye,
haidhuru, hiki ndicho tunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini.

Ufufuo wetu

12 Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu,
baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
13 Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka;
14 na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na
imani yenu haina maana.
15 Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu,
maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye
hakumfufua–kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.
16 Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo
hakufufuka.
17 Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali
bado katika dhambi zenu.
18 Zaidi ya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana na Kristo
wamepotea kabisa.
19 Kama matumaini yetu katika Kristo yanahusu tu maisha haya ya
sasa, basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote
duniani.

20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, limbuko
lao wale waliolala katika kifo.
21 Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo
hivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa na mtu mmoja.
22 Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo
hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo.
23 Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza, halafu wale
walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja.
24 Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi
Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na
nguvu.
25 Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda adui zake
na kuwaweka chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.
27 Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu
yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya
miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo
la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
28 Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo
naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya
Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
\fr 15:25
\f taz Zab 110:1
\fr 15:27
\f taz Zab 8:6

29 Kama hakuna ufufuo, je watu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu
wanatumainia kupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwa kwa
ajili yao?
30 Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa?
31 Ndugu, mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juu
yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu inanifanya nitangaze
jambo hili.
32 Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana
kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu
hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”

33 Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.
34 Amkeni! Anzeni kuishi vema, na acheni kutenda dhambi. Baadhi yenu
hawamjui Mungu kabisa. Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu!

Mwili wa ufufuo

35 Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na
mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?”
36 Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza
haitaota.
37 Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si
mmea mzima ambao hutokea baadaye.
38 Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu
hupata mwili wake wa pekee.

39 Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna
moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na
miili ya samaki pia ni ya namna nyingine.
40 Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya
mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine.
41 Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo
huhitilafiana kwa uzuri.

42 Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kama vile mbegu, mwili
huzikwa ardhini ukiwa katika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwa
katika hali ya kutoharibika.
43 Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu; huzikwa
katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenye nguvu.
44 Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho.
Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwili wa kiroho.
45 Maana Maandiko yasema: “Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe
mwenye uhai;” lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima.
46 Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili
wa kawaida kisha ule mwili wa kiroho.
47 Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili
alitoka mbinguni.
48 Wote walio wa dunia wako kama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo;
wale walio wa mbinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni.
49 Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo, vivyo
hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni.

50 Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu
hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa
na hali ya kutoharibika.

51 Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote
tutageuzwa
52 wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua.
Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa
tena, na sisi tutageuzwa.
53 Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya
kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.
54 Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya
kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo
ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa:

“Kifo kimeangamizwa ushindi umekamilika!”

55 “Kifo, ushindi wako uko wapi?

Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”
\m
56 Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake
katika Sheria.
57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana
wetu Yesu Kristo.

58 Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni
daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya
katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Mchango wa kusaidia ndugu waumini
\c 16

1 Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama
nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.
2 Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya
mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja.
3 Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni
mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
4 Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.

Mipango ya Paulo

5 Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia–maana nataraji kupitia
Makedonia.
6 Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja
nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari
yangu kokote nitakakokwenda.
7 Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari.
Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.

8 Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.
9 Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa
wapinzani nao ni wengi.

10 Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati
yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.
11 Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari
yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na
ndugu zetu.

12 Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu
wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara
itakapowezekana.

Maneno ya mwisho

13 Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.
14 Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.

15 Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa
kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu
wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu,
16 muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu
afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao.

17 Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika;
wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu.
18 Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa
kuwakumbuka watu wa namna hii.

19 Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na
watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana.
20 Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya
mapendo ya Mungu.

21 Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe.
22 Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA–BWANA, njoo!

23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
24 Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu.
\z

\id 2CO SW48.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT
\h 2 WAKORINTHO

          BARUA YA PILI YA PAULO KWA
                 WAKORINTHO

\c 1

1 Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu
Timotheo, tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho, na
watu wote wa Mungu kila mahali katika Akaya.
2 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana
Yesu Kristo.

Shukrani kwa Mungu

3 Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye
huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote.
4 Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate
kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea
kutoka kwa Mungu.
5 Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri
hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye.
6 Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu.
Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji ninyi na kuwaunga mkono mpate
nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi.
7 Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua
kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.

8 Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu
hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea
kuishi.
9 Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe
kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu
sisi wenyewe.
10 Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea
kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena,
11 ninyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema
tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe
sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.

Badiliko katika safari ya Paulo

12 Sisi tunajivunia kitu kimoja: dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba
tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu
tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali neema
ya Mungu.
13 Tunawaandikia ninyi mambo mnayoweza kuyasoma na kuyaelewa.
Ninatumaini kwamba mtaelewa vizuri kabisa,
14 maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba
katika ile Siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi
tunavyowaonea ninyi fahari.

15 Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili
mpate baraka maradufu.
16 Nilikusudia kupita kwenu nikiwa safarini kwenda Makedonia, na
wakati wa kurudi pia, ili nipate msaada wenu kwa safari yangu kwenda
Yudea.
17 Je, mnadhani nilipopanga hivyo nimekuwa kama mtu asiye na
msimamo? Je, mnadhani kwamba ninafanya uamuzi wangu kwa fikira za
kibinadamu na kwamba nasema “Ndiyo” na “Siyo” papo hapo?
18 Mungu ni ukweli mtupu; basi, kile tulichowaambia ninyi si jambo
la “Ndiyo” na “Siyo”.
19 Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na
Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo”; bali
yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.
20 Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa
sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya
kumtukuza Mungu.
21 Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na ninyi pia katika
Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu;
22 ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa mali yake yeye na kutujalia Roho
mioyoni mwetu kama dhamana ya mambo yote ambayo ametuwekea.

23 Mungu ndiye shahidi wangu–yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja
tena Korintho, kwa sababu tu ya kuwahurumieni.
24 Hatutaki kutumia mabavu juu ya imani yenu; ninyi mko imara katika
imani yenu. Wajibu wetu ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya furaha yenu.

\c 2

1 Basi nimeamua nisiwatembelee tena kuwatia huzuni.
2 Maana nikiwahuzunisha ninyi, basi, ni nani atakayenifariji? Ni
walewale niliowahuzunisha!
3 Ndiyo maana niliwaandikia–sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na
ninyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba, mimi
nikifurahi, ninyi nyote pia mnafurahi.
4 Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko
moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha ninyi,
bali kwa ajili ya kuwaonyesheni kwamba nawapenda mno.

Msamaha

5 Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi–ila
amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
6 Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.
7 Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili
asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.
8 Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda.
9 Madhumuni yangu kuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kama mko
tayari kutii katika kila jambo.
10 Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe–kama
kweli ninacho cha kusamehe–nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
11 ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango
yake ilivyo.

Wasiwasi wa Paulo mjini Troa

12 Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nilikuta mlango
u wazi kwa ajili ya kazi ya Bwana.
13 Lakini nilifadhaika sana kwa kutomkuta ndugu yetu Tito. Ndiyo
maana niliwaaga wote pale nikaenda Makedonia.

Ushindi kwa msaada wa Kristo

14 Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa
ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu
nzuri, kila mahali.
15 Maana sisi ni kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristo anamtolea
Mungu, harufu nzuri inayofikia wote wanaookolewa na wanaopotea.
16 Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale
wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika
kazi ya namna hiyo?
17 Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu;
sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na
Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.

Watumishi wa Agano Jipya
\c 3

1 Je, tunaanza tena kujipendekeza? Je, tunahitaji barua ya
utambulisho kwenu, au kutoka kwenu, kama watu wengine?
2 Ninyi wenyewe ni barua yetu; barua iliyoandikwa mioyoni mwetu kila
mtu aione na kuisoma.
3 Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono
yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu hai;
imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu.

4 Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa
Mungu kwa njia ya Kristo.
5 Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe,
ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
6 maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si
agano la sheria iliyoandikwa, bali Agano la Roho. Maana sheria
iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uzima.

7 Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje
mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa
Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mng’ao wake. Tena
mng’ao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho
kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
8 basi, huduma ya Roho ina utukufu mkuu zaidi.
9 Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta
hukumu, ni wazi kwamba huduma ile iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu
itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
10 Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja
hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
11 Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu
wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu
zaidi.

12 Kwa vile hili ndilo tumaini letu, sisi twasema kwa uhodari mkuu.
13 Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake
kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mng’ao uliokuwa
unafifia.
14 Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la
Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu
anapoungana na Kristo.
15 Naam, mpaka hivi leo kila isomwapo Sheria ya Mose akili zao huwa
zimefunikwa.
16 Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa.
17 Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo
uhuru.
18 Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, twaonyesha kama
katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo
mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

Hazina za Roho katika vyombo vya udongo
\c 4

1 Basi, Mungu, kwa huruma yake, ametukabidhi kazi hii na hivyo hatufi
moyo.
2 Tumeyaacha kabisa mambo yote ya aibu na ya kisirisiri. Hatuishi
tena kwa udanganyifu, wala kwa kulipotosha neno la Mungu; bali
tunaudhihirisha ukweli kwa kuufanya ukweli, na hivyo kujiweka chini ya
uamuzi wa dhamiri za watu mbele ya Mungu.
3 Maana, kama Habari Njema tunayohubiri imefichika, imefichika tu
kwa wale wanaopotea.
4 Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza
akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa
Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu.
5 Maana hatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiri Yesu Kristo
aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwa watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.

6 Mungu ambaye alisema, “Mwanga na uangaze kutoka gizani,” ndiye
mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa
Mungu uangazao katika uso wa Kristo.

7 Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili
ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi
wenyewe.
8 Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka,
lakini hatukati tamaa;
9 twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa
chini, hatukuangamizwa.
10 Kila wakati tumekuwa tukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo,
ili uhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu.
11 Naam, katika maisha yetu yote tunakabiliwa na kifo daima kwa
ajili ya Yesu, ili uzima wake Yesu udhihirike katika miili yetu
inayokufa.
12 Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani
yenu uhai unafanya kazi.
\fr 4:13
\f taz Zab 116:10

13 Maandiko Matakatifu yasema: “Niliamini, ndiyo maana nilinena.”
Nasi pia, tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini, na kwa sababu hiyo
twanena.
14 Tunajua kwamba yule aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi pia
pamoja na Yesu na kutuweka mbele yake pamoja nanyi.
15 Yote haya ni kwa faida yenu; ili kama vile neema ya Mungu
inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi vivyo hivyo watu wengi zaidi
watoe shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.

Kuishi kwa imani

16 Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje
yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku.
17 Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu: lakini itatupatia
utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho.
18 Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali
visivyoonekana. Maana vinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vile
visivyoonekana ni vya milele.

\c 5

1 Maana tunajua kwamba hema hii ambayo ndani yake tunaishi sasa hapa
duniani, yaani mwili wetu, itakapong’olewa, Mungu atatupa makao mengine
mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
2 Na sasa, katika hali hii, tunaugua, tukitazamia kwa hamu kubwa
kuvikwa makao yetu yaliyo mbinguni.
3 Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya
Mungu bila vazi.
4 Tukiwa bado katika hema hii ya duniani, tunalia kwa kukandamizwa;
si kwamba tunataka kuuvua mwili huu wa kufa, ila tuna hamu ya kuvalishwa
ule usiokufa, ili kile chenye kufa kimezwe kabisa na uhai.
5 Mungu mwenyewe alitutayarishia mabadiliko hayo, naye ametupa Roho
wake awe dhamana ya yote aliyotuwekea.

6 Tuko imara daima. Tunajua kwamba kuishi katika mwili huu tu ni
kukaa mbali na Bwana.
7 Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona.
8 Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya,
tukahamie kwa Bwana.
9 Lakini jambo la maana zaidi, tunataka kumpendeza, iwe tunaishi
hapa duniani au huko.
10 Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha
Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya
wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.

Kupatanishwa na Mungu kwa njia ya Kristo

11 Basi, sisi tunajua umuhimu wa kumcha Bwana, na hivyo tunajitahidi
kuwavuta watu. Mungu anatujua waziwazi, nami natumaini kwamba nanyi pia
mnatujua kinaganaga.
12 Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka
kuwapa ninyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu
wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.
13 Ikiwa tumeonekana kuwa wendawazimu, hiyo ni kwa ajili ya Mungu;
na ikiwa tunazo akili zetu timamu, hiyo ni kwa faida yenu.
14 Maana mapendo ya Kristo yanatumiliki sisi ambao tunatambua ya
kwamba mtu mmoja tu amekufa kwa ajili ya wote, na hiyo ina maana kwamba
wote wanashiriki kifo chake.
15 Alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi kwa ajili
yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa, akafufuliwa kwa ajili
yao.

16 Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama
kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
17 Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale
yamepita, hali mpya imefika.
18 Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya
Kristo, akatupa nasi jukumu la kuwapatanisha watu naye.
19 Ndiyo kusema: Mungu, amekuwa akiupatanisha ulimwengu naye kwa
njia ya Kristo, bila kutia maanani dhambi zao binadamu. Yeye ametupa
ujumbe kuhusu kuwapatanisha watu naye.

20 Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia
sisi kuwasihi ninyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na
Mungu.
21 Kristo hakuwa na dhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike na dhambi
kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu
wake Mungu.

\c 6

1 Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile
neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.
2 Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa
wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa, sasa ndiyo siku
ya wokovu!

3 Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi
kumwekea mtu yeyote kizuio chochote.
4 Badala yake, tunajionyesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila
kitu: kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu.
5 Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi
tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula.
6 Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu,
uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki,
7 kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha
yetu upande wa kulia na upande wa kushoto.
8 Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa.
Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli;
9 kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote, kama waliokufa,
lakini mwonavyo, sisi ni wazima kabisa.
10 Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi
daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi;
twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.

11 Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko
wazi kabisa.
12 Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu
ninyi wenyewe, na si kwa upande wetu.
13 Sasa nasema nanyi kama watoto wangu, wekeni mioyo yenu wazi kama
nasi tulivyofanya.

Onyo kuhusu mitindo ya watu wasiomjua Mungu

14 Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli?
Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
15 Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Muumini ana uhusiano gani
na asiyeamini?
16 Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi
ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema:

“Nitafanya makao yangu kwao,
na kuishi kati yao;
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.”

17 Kwa hiyo Bwana asema pia:

“Ondokeni kati yao,
mkajitenge nao,
msiguse kitu najisi,
nami nitawapokea.

18 Mimi nitakuwa Baba yenu,

nanyi mtakuwa watoto wangu, waume kwa wake,
asema Bwana Mwenye Uwezo.”

\c 7

1 Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewa ahadi hizi zote, na tujitakase
na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu, tuwe watakatifu
kabisa, na tuishi kwa kumcha Mungu.

Furaha ya Paulo

2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote,
hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.
3 Sisemi mambo haya kwa ajili ya kumhukumu mtu; maana, kama
nilivyokwisha sema, ninyi mko mioyoni mwetu, tufe pamoja, tuishi pamoja.
4 Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu
yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.

5 Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande
tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi; ndani hofu.
6 Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge alitupa moyo sisi pia
kwa kuja kwake Tito.
7 Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo
mliompa ninyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo
na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.

8 Maana, hata kama kwa barua ile yangu nimewahuzunisha, sioni sababu
ya kujuta. Naam, naona kwamba barua hiyo iliwatia huzuni lakini kwa
muda.
9 Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu
imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa
Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru ninyi kwa vyovyote.
10 Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu, husababisha badiliko la
moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta.
Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
11 Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo:
ninyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na
kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Ninyi
mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.

12 Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule
aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane
wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
13 Ndiyo maana sisi tulifarijika sana.
Siyo kwamba tulifarijika tu, ila pia Tito alitufurahisha kwa furaha
aliyokuwa nayo kutokana na jinsi mlivyomchangamsha moyo.
14 Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo
sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia ninyi
mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli mtupu.
15 Hivyo upendo wake wa moyo kwenu unaongezeka zaidi akikumbuka
jinsi ninyi nyote mlivyo tayari kutii, na jinsi mlivyomkaribisha kwa
hofu nyingi na kutetemeka.
16 Nafurahi sana kwamba naweza kuwategemea ninyi kabisa katika kila
jambo.

Ukarimu wa Kikristo
\c 8

1 Ndugu, tunapenda kuwapa habari juu ya neema ambazo Mungu ameyajalia
makanisa ya Makedonia.
2 Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao
ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa
maskini sana.
3 Naweza kushuhudia kwamba walikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao na
hata zaidi. Kwa hiari yao wenyewe,
4 walitusihi sana wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya
kuwasaidia watu wa Mungu.
5 Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza
walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia,
kufuatana na mapenzi ya Mungu.
6 Kwa sababu hiyo, tulimsihi Tito aliyeianza kazi hiyo awasaidieni
pia muitekeleze huduma hii ya upendo miongoni mwenu.
7 Ninyi mna kila kitu: imani, uwezo wa kusema, elimu; bidii yote ya
kutenda mema, na upendo wenu kwetu. Hivyo, tunatazamia muwe wakarimu
katika huduma hii ya upendo.

8 Siwapi ninyi amri, lakini nataka tu kuonyesha jinsi wengine
walivyo na bidii ya kusaidia ili nipate kujua jinsi upendo wenu ulivyo
wa kweli.
9 Maana, ninyi mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo: yeye, ingawa
alikuwa na kila kitu, alijifanya maskini kwa ajili yenu, ili kutokana na
umaskini wake, awatajirishe.
10 Kuhusu jambo hili, basi, nawapeni shauri hili: inafaa kwenu
kutekeleza sasa yale mliyoanza mwaka jana. Ninyi mlikuwa wa kwanza
kuchukua hatua na kuamua kufanya hivyo.
11 Basi, kamilisheni shughuli hiyo; na kama vile mlivyokuwa na hamu
kubwa ya kusaidia, basi, fanyeni bidii vivyo hivyo, kadiri ya uwezo
wenu, kuikamilisha.
12 Maana ikiwa mtu ana moyo wa kusaidia, Mungu hupokea kila
anachoweza kutoa: hadai zaidi.
13 Ninyi hampaswi kuongezewa taabu kusudi wengine wapunguziwe mzigo
wao; sivyo, ila ni lazima tujali usawa na haki.
14 Kila mlicho nacho sasa cha ziada kiwasaidie wale wanaohitaji, ili
nao wakati watakapokuwa na ziada, wawasaidie ninyi katika mahitaji yenu,
na hivyo kuwe na usawa.
15 Kama Maandiko yasemavyo: “Aliyekusanya kwa wingi hakuwa na
ziada, na yule aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”

Tito na wenzake

16 Namshukuru Mungu aliyeweka ndani ya moyo wa Tito hamu hiyo niliyo
nayo mimi ya kuwasaidia.
17 Si tu kwamba alikubali ombi letu, ila pia alikuwa na hamu kubwa
ya kusaidia, hata akaamua kwa hiari yake mwenyewe kuja kwenu.
18 Pamoja naye, tunamtuma ndugu mmoja ambaye sifa zake katika
kueneza Habari Njema zimeenea katika makanisa yote.
19 Zaidi ya hayo, yeye amechaguliwa na makanisa awe mwenzetu
safarini wakati tunapopeleka huduma hii yetu ya upendo, huduma
tunayoifanya kwa ajili ya utukufu wa Bwana na uthibitisho wa nia yetu
njema.

20 Tunataka kuepa lawama zinazoweza kutokea kuhusu usimamizi wetu
juu ya zawadi hii karimu.
21 Nia yetu ni kufanya vema, si tu mbele ya Bwana, lakini pia mbele
ya watu.

22 Basi, pamoja na ndugu hao, tumemtuma ndugu yetu mwingine ambaye
mara nyingi tumempa majaribio mbalimbali, tukamwona kuwa ni mwenye hamu
kubwa ya kusaidia; hata sasa amekuwa na moyo zaidi kwa sababu ana imani
sana nanyi.
23 Tito ni mwenzangu; tunafanya kazi pamoja kwa ajili yenu; lakini
kuhusu hawa ndugu zetu wengine, wanaokuja pamoja nao, hao ni wajumbe wa
makanisa, na utukufu kwa Kristo.
24 Basi, waonyesheni uthabiti wa upendo wenu, makanisa yapate kuona
kweli kwamba fahari ninayoona juu yenu ni ya halali.

Msaada kwa Wakristo
\c 9

1 Si lazima kuandika zaidi kuhusu huduma hiyo yenu kwa ajili ya watu
wa Mungu.
2 Ninajua jinsi mlivyo na moyo wa kusaidia, na nilijivuna juu yenu
kuhusu jambo hilo mbele ya watu wa Makedonia. Niliwaambia: “Ndugu zetu
wa Akaya wako tayari tangu mwaka jana.” Hivyo, moto wenu umekwisha
wahimiza watu wengi zaidi.
3 Basi, nimewatuma ndugu zetu hao, ili fahari yetu juu yenu ionekane
kwamba si maneno matupu, na kwamba mko tayari kabisa na msaada wenu kama
nilivyosema.
4 Isije ikawa kwamba watu wa Makedonia watakapokuja pamoja nami
tukawakuta hamko tayari, hapo sisi tutaaibika–bila kutaja aibu
mtakayopata ninyi wenyewe–kwa sababu tutakuwa tumewatumainia kupita
kiasi.
5 Kwa hiyo, nimeona ni lazima kuwaomba hawa ndugu watutangulie kuja
kwenu, wapate kuweka tayari zawadi yenu kubwa mliyoahidi; nayo ionyeshe
kweli kwamba ni zawadi iliyotolewa kwa hiari na si kwa kulazimishwa.

6 Kumbukeni: “Apandaye kidogo huvuna kidogo; apandaye kwa wingi
huvuna kwa wingi.”
7 Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si
kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa
kwa furaha.
8 Mungu anaweza kuwapeni ninyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate
daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika
kila kazi njema.
9 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:

“Yeye hutoa kwa ukarimu,
huwapa maskini,
wema wahudumu milele.”
\fr 9:9
\f taz Zab 112:9

10 Na Mungu ampaye mkulima mbegu na mkate kwa chakula, atawapa ninyi
pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya ziote, ziwe na kuwapa mavuno mengi
ya ukarimu wenu.
11 Yeye atawatajirisha ninyi daima kwa kila kitu, ili watu wapate
kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi zenu wanazozipokea kwa mikono yetu.
12 Maana huduma hii takatifu mnayoifanya si tu kwamba itasaidia
mahitaji ya watu wa Mungu, bali pia itasababisha watu wengi wamshukuru
Mungu.
13 Kutokana na uthibitisho unaoonyeshwa kwa huduma hii yetu, watu
watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo
mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.
14 Kwa hiyo watawaombea ninyi kwa moyo kwa sababu ya neema ya pekee
aliyowajalieni Mungu.
15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

Paulo anajitetea kuhusu kazi yake
\c 10

1 Mimi Paulo mwenyewe ambaye naonekana kuwa mpole nikiwa pamoja
nanyi, lakini mkali wakati nikiwa mbali nanyi, nawasihini kwa huruma na
wema wake Kristo.
2 Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana
nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba
tunaishi kidunia.
3 Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.
4 Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia,
ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za
uongo,
5 na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu
ya Mungu; tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo.
6 Mkisha kuwa wakamilifu katika kutii, sisi tuko tayari kuadhibu
kila namna ya kutotii.

7 Ninyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani
kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia
ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
8 Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo
aliotupa–uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa–hata hivyo sijutii hata
kidogo.
9 Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha ninyi kwa barua zangu.
10 Mtu anaweza kusema: “Barua za Paulo ni kali na zenye maneno
mazito, lakini yeye mwenyewe anapokuwa pamoja nasi ni mtu dhaifu, na
hata anapoongea maneno yake ni kama si kitu.”
11 Mtu asemaye hivyo heri akumbuke kwamba hakuna tofauti ya yale
tunayoandika katika barua wakati tuko mbali, na yale tutakayofanya
wakati tutakapokuwa nanyi.

12 Kwa vyovyote hatungethubutu kujiweka au kujilinganisha na wale
watu wanaojisifia wenyewe. Watu wenye kujifanya wao kuwa kipimo cha
kujipimia, na watu wanaojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, ni wapumbavu.
13 Lakini sisi hatutajivuna kupita kiasi; kujivuna huko kutabaki
katika kile kipimo cha kazi aliyotukabidhi Mungu, kazi ambayo tunaifanya
pia kwenu.
14 Na kwa vile ninyi mu katika mipaka hiyo, hatukuipita tulipokuja
kwenu, tukiwaleteeni Habari Njema juu ya Kristo.
15 Basi, hatujivunii kazi waliyofanya wengine zaidi ya kipimo
tulichopewa; ila tunatumaini kwamba imani yenu itazidi miongoni mwenu
kufuatana na kipimo alichotuwekea Mungu.
16 Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali
nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine
mahali pengine.

17 Lakini kama yasemavyo Maandiko: “Mwenye kuona fahari na aone
fahari juu ya alichofanya Bwana.”
18 Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa
na Bwana.

Paulo na mitume wa uongo
\c 11

1 Laiti mngenivumilia kidogo, hata kama mimi ni mjinga kiasi fulani!
Naam, nivumilieni kidogo.
2 Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana ninyi ni kama
bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
3 Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo
alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu
wa kweli kwa Kristo.
4 Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule
tuliyemhubiri, ninyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au
habari njema tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!

5 Sidhani kwamba mimi ni mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”
6 Labda sina ufasaha wa lugha, lakini elimu ninayo; jambo hili
tumelionyesha wazi kwenu, kila mahali na kila wakati.

7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara;
nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi. Je, nilifanya vibaya?
8 Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na
makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao
nipate kuwatumikia ninyi.
9 Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu
waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa
mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea
kufanya hivyo.
10 Naahidi kwa ule ukweli wa Kristo ulio ndani yangu, kwamba hakuna
kitakachoweza kunizuia kujivunia jambo hilo popote katika Akaya.
11 Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu eti siwapendi ninyi? Mungu
anajua kwamba nawapenda!

12 Nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa, ili nisiwape nafasi
wale wanaotafuta nafasi, nafasi ya kujivuna kwamba eti wanafanya kazi
kama sisi.
13 Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu
wanojisingizia kuwa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa
malaika wa mwanga!
15 Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake
wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile
wanachostahili kufuatana na matendo yao.

Mateso ya Paulo kama mtume

16 Tena nasema: Mtu asinifikirie kuwa mpumbavu. Lakini kama
mkifikiri hivyo, basi, nichukueni kama mpumbavu ili nami nipate kuwa na
cha kujivunia angaa kidogo.
17 Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili
la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
18 Maadam wengi hujivuna kwa sababu za kidunia, nami pia nitajivuna.
19 Ninyi ni wenye busara, ndiyo maana hata mnawavumilia wapumbavu!
20 Mnamvumilia hata mtu anayewafanya ninyi watumwa, mtu mwenye
kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
21 Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu.
Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia
kitu–nasema kama mtu mpumbavu–mimi nathubutu pia.
22 Je, wao ni Waebrania? Hata mimi. Je, wao ni Waisraeli? Hata mimi.
Wao ni wazawa wa Abrahamu? Hata mimi.
23 Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi–nanena hayo kiwazimu–ni
mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi,
nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na
nimekaribia kifo mara nyingi.
24 Mara tano nilichapwa vile viboko thelathini na tisa vya Wayahudi.
25 Nilipigwa viboko mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu
nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda
mchana kutwa.
26 Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na
hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa
watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za
baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo
27 Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi;
nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi
bila nguo.
28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za
makanisa yote.
29 Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote
akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
\il 5
ic
\is Meli (2 Kor. 11:25)
\ie

30 Ikinilazimu kujivuna, basi, nitajivunia udhaifu wangu.
31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu–jina lake litukuzwe milele–yeye
anajua kwamba sisemi uongo.
32 Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa, aliyekuwa chini ya mfalme
Areta, alikuwa akiulinda mji wa Damasko ili apate kunikamata.
33 Lakini, ndani ya kapu kubwa, niliteremshwa nje kupitia katika
nafasi ukutani, nikachopoka mikononi mwake.

Maono na ufunuo
\c 12

1 Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono
na ufunuo alivyonijalia Bwana.
2 Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita
alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa
mwili au kwa roho; Mungu ajua.)
3 Narudia: najua kwamba mtu huyo alinyakuliwa mpaka peponi. (Lakini
sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua.)
4 Huko akasikia mambo ya siri ambayo binadamu hastahili kuyatamka.
5 Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi
binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
6 Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana
ningekuwa nasema ukweli mtupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie
zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.

7 Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe
majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye
kunipiga nisijivune kupita kiasi.
8 Nilimsihi Bwana mara tatu kuhusu jambo hili ili linitoke.
9 Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana
uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa
kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo nakubali kwa radhi udhaifu, madharau, taabu, udhalimu na
mateso, kwa ajili ya Kristo; maana ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa
na nguvu.

Wasiwasi wa Paulo juu ya Wakorintho

11 Nimekuwa kama mpumbavu, lakini, ninyi mmenilazimisha kuwa hivyo.
Ninyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa
vyovyote, mimi si mdogo zaidi kuliko hao “mitume wakuu.”
12 Miujiza na maajabu yaonyeshayo wazi kwamba mimi ni mtume
yalifanyika miongoni mwenu kwa uvumilivu wote.
13 Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu
kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani
kwa kuwakoseeni haki hiyo!
14 Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua.
Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni ninyi wenyewe. Ni kawaida ya
wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
15 Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea
mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati
kwa kuwa mimi nawapenda ninyi mno?

16 Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu
mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
17 Je, mimi niliwanyonyeni kwa njia ya mjumbe yeyote niliyemtuma
kwenu?
18 Mimi nilimwita Tito, nikamtuma kwenu na ndugu yetu mwingine. Je,
Tito aliwanyonyeni? Je, hamjui kwamba sisi tumekuwa tukiongozwa na roho
yuleyule, na mwenendo wetu ni mmoja?

19 Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe
mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa
tumeungana na Kristo. Mambo hayo, yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya
kuwajenga ninyi.
20 Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali
nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa
huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyano,
kunong’ona, majivuno na fujo kati yenu.
21 Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu
atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa
wale waliotenda dhambi lakini hawakujutia huo uchafu, tamaa zao mbaya na
uzinzi waliokuwa wamefanya.

Maonyo ya mwisho na salamu
\c 13

1 Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa
kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
2 Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema
tena nikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale
wengine, nitakapokuja, watakiona cha mtema kuni.
3 Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo
si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
4 Maana hata kama alisulubiwa kwa sababu ya udhaifu, lakini sasa
anaishi kwa uwezo wa Mungu. Sisi pia tu dhaifu kwa kuungana naye lakini
tutaishi naye kwa uwezo wa Mungu kwa ajili yenu.

5 Jichunguzeni ninyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani.
Jichunguzeni ninyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani
yenu? Kama sivyo, basi ninyi mmeshindwa.
6 Lakini natumaini kwamba ninyi mnajua kuwa sisi hatukushindwa.
7 Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane
kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi
tunaonekana kuwa tumeshindwa.
8 Maana hatuwezi kuupinga ukweli; uwezo tulio nao ni wa kuuendeleza
ukweli.
9 Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; kwa hiyo
tunaomba mpate kuwa wakamilifu.
10 Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu
nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana;
naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
11 Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri
yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa mapendo na amani
atakuwa pamoja nanyi.

12 Salimianeni kwa ishara ya upendo. Watu wote wa Mungu huku
wanawasalimuni.

13 Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na umoja wa Roho
Mtakatifu, viwe nanyi nyote.
\z

\id GAL SW49.ALL 19-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PAULO KWA
                 WAGALATIA

\h WAGALATIA
\c 1

1 Mimi Paulo mtume,
2 na ndugu wote walio pamoja nami, tunayaandikia makanisa yaliyoko
Galatia. Mimi nimepata kuwa mtume si kutokana na mamlaka ya binadamu,
wala si kwa nguvu ya mtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na wa Mungu Baba
aliyemfufua Yesu kutoka wafu.
3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka
kwa Bwana Yesu Kristo.

4 Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na
mapenzi ya Mungu wetu na Baba, ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu
mbaya wa sasa.
5 Kwake yeye uwe utukufu milele! Amina.

Injili kamili

6 Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi yule
aliyewaita kwa neema ya Kristo, mkafuata Habari Njema ya namna nyingine.
7 Lakini hakuna “Habari Njema” nyingine. Ukweli ni kwamba wako
watu wanaowavurugeni, watu wanaotaka kuipotosha Habari Njema ya Kristo.
8 Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni,
atawahubirieni Habari Njema tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi
huyo na alaaniwe!
9 Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote
anawahubirieni Habari Njema ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha
pokea, huyo na alaaniwe!

10 Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je,
nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe
mtumishi wa Kristo.

Paulo alivyopata wito wake

11 Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Habari Njema niliyoihubiri si
ujumbe wa kibinadamu.
12 Wala mimi sikuipokea kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na
mtu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia.

13 Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa
kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu
kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
14 Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu
katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo
ya wazee wetu.

15 Lakini Mungu, kwa neema yake, alikuwa ameniteua hata kabla
sijazaliwa, akaniita nimtumikie.
16 Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudi niihubiri Habari
Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
17 na bila kwenda kwanza Yerusalemu kwa wale waliopata kuwa mitume
kabla yangu, nilikwenda kwanza Arabia, kisha nikarudi tena Damasko.
18 Ilikuwa tu baada ya miaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemu
kuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi na tano.
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake
Bwana.
20 Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua; sisemi uongo.

21 Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia.
22 Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo
kule Yudea.
23 Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: “Mtu yule aliyekuwa
akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu
kuiangamiza.”
24 Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.

Paulo na mitume wengine
\c 2

1 Baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yerusalemu pamoja na
Barnaba; nilimchukua pia Tito pamoja nami.
2 Kwenda kwangu kulitokana na ufunuo alionipa Mungu. Katika kikao
cha faragha niliwaeleza hao viongozi ujumbe wa Habari Njema niliohubiri
kwa watu wa mataifa. Nilifanya hivyo kusudi kazi yangu niliyokuwa
nimefanya, na ile ninayofanya sasa isije ikawa bure.
3 Lakini, hata mwenzangu Tito, ambaye ni Mgiriki, hakulazimika
kutahiriwa,
4 ingawa kulikuwa na ndugu wengine wa uongo waliotaka atahiriwe.
Watu hawa walijiingiza kwa ujanja na kupeleleza uhuru wetu tulio nao
katika kuungana na Kristo Yesu, ili wapate kutufanya watumwa.
5 Hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Habari Njema ubaki
nanyi daima.

6 Lakini watu hawa wanaosemekana kuwa ni viongozi–kama kweli
walikuwa hivyo au sivyo, kwangu si kitu, maana Mungu hahukumu kwa
kuangalia mambo ya nje–watu hawa hawakuwa na kitu cha kuongeza katika
Habari hii Njema kama niihubirivyo.
7 Badala yake, walitambua kwamba Mungu alikuwa amenituma kuhubiri
Habari Njema kwa watu wa mataifa mengine kama vile Petro alivyokuwa
ametumwa kuihubiri kwa Wayahudi.
8 Maana, yule aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi, ndiye
aliyeniwezesha nami pia kuwa mtume kwa watu wa mataifa mengine.
9 Basi, Yakobo, Kefa na Yohane, ambao waonekana kuwa viongozi wakuu,
walitambua kwamba Mungu alinijalia neema hiyo, wakatushika sisi mkono,
yaani Barnaba na mimi, iwe ishara ya ushirikiano. Sisi ilitupasa
tukafanye kazi kati ya watu wa mataifa mengine, na wao kati ya Wayahudi.
10 Wakatuomba lakini kitu kimoja: tuwakumbuke maskini; jambo ambalo
nimekuwa nikijitahidi kutekeleza.

Paulo anamkaripia Petro

11 Lakini Kefa alipofika Antiokia nilimpinga waziwazi maana alikuwa
amekosea.
12 Awali, kabla ya watu kadhaa waliokuwa wametumwa na Yakobo
kuwasili hapo, Petro alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine.
Lakini, baada ya hao watu kufika, aliacha kabisa kula pamoja na watu wa
mataifa mengine, kwa kuogopa kikundi cha waliosisitiza tohara.
13 Hata ndugu wengine Wayahudi walimuunga mkono Petro katika kitendo
hiki cha unafiki, naye Barnaba akakumbwa na huo unafiki wao.
14 Basi, nilipoona kuwa msimamo wao kuhusu ukweli wa Habari Njema
haukuwa umenyooka, nikamwambia Kefa mbele ya watu wote: “Ingawa wewe ni
Myahudi, unaishi kama watu wa mataifa mengine na si kama Myahudi!
Unawezaje, basi kujaribu kuwalazimisha watu wa mataifa mengine kuishi
kama Wayahudi?”

Wayahudi na watu wa mataifa mengine huokolewa kwa imani
\fr 2:16
\f taz Zab 143:2

15 Kweli, sisi kwa asili ni Wayahudi, na si watu wa mataifa mengine
hao wenye dhambi!
16 Lakini, tunajua kwa hakika kwamba mtu hawezi kukubaliwa kuwa
mwadilifu kwa kuitii Sheria, bali tu kwa kumwamini Yesu Kristo. Na sisi
pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kukubaliwa kuwa waadilifu kwa
njia ya imani yetu kwa Kristo, na si kwa kuitii Sheria.
17 Sasa, ikiwa katika kutafuta kukubaliwa kuwa waadilifu kwa
kuungana na Kristo sisi tunaonekana kuwa wenye dhambi, je, jambo hili
lina maana kwamba Kristo anasaidia utendaji wa dhambi? Hata kidogo!
18 Lakini ikiwa ninajenga tena kile nilichokwisha bomoa, basi
nahakikisha kwamba mimi ni mhalifu.
19 Maana, kuhusu Sheria hiyo, mimi nimekufa; Sheria yenyewe iliniua,
nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. Mimi nimeuawa pamoja na Kristo
msalabani,
20 na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani
yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana
wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu.
21 Sipendi kuikataa neema ya Mungu. Kama mtu huweza kukubaliwa kuwa
mwadilifu kwa njia ya Sheria, basi, Kristo alikufa bure!

Imani au Sheria
\c 3

1 Enyi Wagalatia, mmekuwa wajinga kweli! Ni nani aliyewaloga? Habari
juu ya kusulubiwa kwake Yesu Kristo ilielezwa waziwazi mbele ya macho
yenu.
2 Napenda kujua tu kitu kimoja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa
Mungu kwa sababu ya kutimiza matakwa ya Sheria ama kwa sababu ya
kuisikia na kuiamini Habari Njema?
3 Je, mu wajinga kiasi hicho? Ninyi mlianza yote kwa msaada wa Roho
je, mnataka sasa kumaliza kwa nguvu zenu wenyewe?
4 Je, mambo yale yote yaliyowapata ninyi yamekuwa bure tu?
Haiwezekani!
5 Je, Mungu huwajalia Roho na kutenda miujiza kati yenu ati kwa
sababu mnatimiza yanayotakiwa na sheria, ama kwa sababu mnasikia Habari
Njema na kuiamini?

6 Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: yeye alimwamini Mungu, naye
Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.
7 Sasa basi jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto
halisi wa Abrahamu.
8 Maandiko Matakatifu yalionyesha kabla kwamba Mungu atawakubali
watu wa mataifa kuwa waadilifu kwa njia ya imani. Hivyo Maandiko
Matakatifu yalitangulia kumtangazia Abrahamu Habari Njema: “Katika wewe
mataifa yote yatabarikiwa.”
9 Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu
aliyeamini.

10 Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na Sheria, wako
chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: “Yeyote asiyeshika
na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria, yuko chini ya
laana.”
11 Ni dhahiri kwamba Sheria haiwezi kumfanya mtu akubaliwe kuwa
mwadilifu; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Mwadilifu kwa imani
ataishi.”
12 Lakini Sheria haitegemei imani, ila Maandiko yasema: “Mwenye
kutimiza yanayotakiwa na Sheria ataishi.”

13 Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya Sheria kwa kujitwalia
laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote
aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”
14 Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu
iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani,
tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidia.

Sheria na ahadi

15 Ndugu, nitawapeni mfano kutoka maisha yetu ya kila siku. Fikirini
juu ya mkataba kati ya watu wawili. Mkataba ukisha fanyika na kutiwa
sahihi hapana mtu anayeuweka kando au kuuongezea kitu.
16 Basi, Abrahamu alipewa ahadi, yeye pamoja na mzawa wake. Maandiko
hayasemi: “Na wazawa wake,” yaani wengi, bali yasema, “Na mzawa
wake,” yaani mmoja, naye ndiye Kristo.
17 Ninachotaka kusema ni hiki: Mungu alifanya agano lake
akalithibitisha; Sheria ambayo ilitokea miaka mia nne na thelathini
baadaye, haiwezi kulitangua hilo agano wala kuibatilisha hiyo ahadi.
18 Maana, kama urithi ya Mungu inategemea Sheria, basi, haiwezi
kutegemea tena ahadi ya Mungu. Kumbe, lakini Mungu alimkirimia Abrahamu
kwa sababu aliahidi.
19 Ya nini basi, Sheria? Iliongezwa hapo ili kuonyesha uhalifu ni
kitu gani, mpaka atakapokuja yule mzawa wa Abrahamu aliyepewa ile ahadi.
Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi.
20 Ama hakika, mpatanishi hahitajiwi ikiwa jambo lenyewe lamhusu mtu
mmoja; na Mungu ni mmoja.

Madhumuni ya Sheria

21 Je, Sheria inapingana na ahadi za Mungu? Hata kidogo! Maana, kama
kungalitolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi, tungeweza
kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria.
22 Lakini sivyo; Maandiko Matakatifu yamekwisha sema kwamba
ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi; na hivyo, kwa kumwamini
Yesu Kristo, wenye kuamini watimiziwe ile ahadi.

23 Kabla ya kujaliwa imani, Sheria ilitufanya wafungwa mpaka imani
hiyo iliyokuwa inakuja ifunuliwe.
24 Basi, hiyo Sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo,
ili kwa njia ya imani, tukubaliwe kuwa waadilifu.
25 Tangu kufika kwa hiyo imani, Sheria si mlezi wetu tena.

26 Kwa njia ya imani, ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika
kuungana na Kristo.
27 Ninyi nyote mliobatizwa mkaungana na Kristo ni kama vile mmemvaa
Kristo.
28 Hivyo, hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na
mtu huru, mwanamume na mwanamke. Nyote ni kitu kimoja katika kuungana na
Kristo Yesu.
29 Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wazawa wa Abrahamu, na mtapokea
yale aliyoahidi Mungu.

\c 4

1 Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa
ingawaje mali yote ni yake.
2 Wakati huo wote yuko chini ya walezi na wadhamini mpaka wakati ule
uliowekwa na baba yake.
3 Hali kadhalika na sisi tulipokuwa bado watoto, tulikuwa watumwa wa
pepo watawala wa ulimwengu.
4 Lakini wakati ule maalumu ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe
aliyezaliwa na mwanamke, akaishi chini ya Sheria
5 apate kuwakomboa wale waliokuwa chini ya Sheria ili sisi tufanywe
wana wa Mungu.

6 Kwa vile sasa ninyi ni wana, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae mioyoni
mwenu, Roho ambaye hulia “Aba,” yaani “Baba.”
7 Basi, wewe si mtumwa tena, bali mwana. Na ikiwa ni mwana, basi,
wewe utapokea yote Mungu aliyowawekea watoto wake.

Wasiwasi wa Paulo juu ya Wagalatia

8 Zamani hamkumjua Mungu na hivyo mkatumikia miungu isiyo miungu
kweli.
9 Lakini sasa, kwa vile mnamjua Mungu, au tuseme mnajulikana na
Mungu, mnawezaje tena kurudi kwa wale pepo maskini na dhaifu hata kutaka
kuwatumikia tena?
10 Bado mnaadhimisha siku, miezi na miaka!
11 Nahofu kwamba labda kazi niliyoifanya kwa ajili yenu imepotea
bure!

12 Ndugu, nawasihi muwe kama mimi, kwa vile hata mimi nimekuwa kama
ninyi. Hamkunitendea ubaya wowote.
13 Mnajua kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia fursa ya
kuwahubirieni Habari Njema kwa mara ya kwanza.
14 Hata hivyo, wakati ule hamkunidharau wala kunikataa kwa sababu ya
udhaifu wangu ingawa mlishawishiwa kufanya hivyo; lakini mlinipokea kama
malaika wa Mungu, kama vile ningekuwa Kristo Yesu mwenyewe.
15 Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati
ule mngaliweza hata kuyang’oa macho yenu na kunipa mimi.
16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu ya kuwaambieni ukweli?
17 Hao watu wengine wanawahangaikia ninyi, lakini nia zao si njema.
Wanataka kuwatenganisha nami ili ninyi muwahangaikie wao.
18 Kwa kweli ni jambo jema daima kuwahangaikia wengine katika mambo
mema, na si tu wakati mimi nipo pamoja nanyi.
19 Watoto wangu, kama vile mama mja mzito anavyotaabika wakati wa
kujifungua, mimi nataabika tena kwa ajili yenu mpaka hapo hali yake
Kristo itakapoundwa ndani yenu.
20 Laiti ningekuwa pamoja nanyi sasa, maana ningalipata msimamo
ufaao juu yenu! Nina wasiwasi sana nanyi!

Mfano wa Hagari na Sara

21 Niambieni, enyi mnaopenda kutawaliwa na sheria: Je, mnasikia
isemavyo Sheria?
22 Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Abrahamu alikuwa na
watoto wawili: mmoja kwa mwanamke mtumwa, na wa pili kwa mwanamke huru.
23 Yule wa mwanamke mtumwa alizaliwa kama kawaida, lakini yule wa
mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu.
24 Mambo hayo yamekuwa mfano; mama hao wawili ni mfano wa maagano
mawili; la kwanza ni lile lililofanyika mlimani Sinai, mwakilishi wake
ni Hagari, na watoto wake wanazaliwa utumwani.
25 Hagari anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabia, na ni mfano wa
Yerusalemu ya sasa, ulio mtumwa pamoja na watoto wake.
26 Lakini Yerusalemu ya juu mbinguni ni mji ulio huru, nao ni mama
yetu.
27 Maana imeandikwa:

“Furahi, ewe uliye tasa usiyezaa;
paaza sauti wewe usiyepata kujifungua mtoto;
maana watoto wa yule aliyeachwa ni wengi zaidi
kuliko wa yule aliye na mume.”

28 Sasa, basi, ndugu zangu, ninyi ni watoto wa Mungu kutokana na
ahadi yake kama alivyokuwa Isaka.
29 Lakini kama vile siku zile yule mtoto aliyezaliwa kwa njia ya
kawaida alimdhulumu yule aliyezaliwa kwa uwezo wa Roho wa Mungu, vivyo
hivyo na siku hizi.
30 Lakini Maandiko Matakatifu yasemaje? Yasema: “Mfukuze mama
mtumwa pamoja na mwanawe; maana mtoto wa mtumwa hatarithi pamoja na
mtoto wa mama huru.”
31 Kwa hiyo, basi, ndugu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mama
huru.

Hifadhini uhuru wenu
\c 5

1 Kristo alitupa uhuru akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala
msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa.
2 Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali
kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.
3 Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika
Sheria yote.
4 Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria,
basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.
5 Kwa upande wetu, lakini, sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Roho
tunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani.
6 Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa
hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo.
\il 5
ic
\is Ng’ombe waliofungwa nira (Gal. 5:1)
\ie

7 Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia
ukweli?
8 Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni.
9 “chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!”
10 Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba
ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo
anayewavurugeni–awe nani au nani–hakika ataadhibiwa.

11 Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba
kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa
hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu
yoyote.
12 Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!

13 Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe
kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana
kwa upendo.
14 Maana Sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja:
“Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
15 Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini
msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!

Maisha ya kiroho na ya kidunia

16 Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi
hamtafuata tena tamaa za kidunia.
17 Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa
ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani;
kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.
18 Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.

19 Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati,
ufisadi;
20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo,
mabishano, mafarakano;
21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena
kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi
yao katika ufalme wa Mungu.

22 Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani,
uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,
23 upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo
hayo.
24 Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na
mawazo yake mabaya na tamaa zake.
25 Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.
26 Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.

Tuvumiliane na kusaidiana
\c 6

1 Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, ninyi mnaoongozwa
na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole,
mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa.
2 Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.
3 Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya
mwenyewe.
4 Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa
mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu
ya kujilinganisha na mtu mwingine.
5 Maana kila mmoja anao mzigo wake mwenyewe wa kubeba.

6 Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake
riziki zake.

7 Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho
atakachovuna.
8 Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini
akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele.
9 Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno
kwa wakati wake.
10 Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na
hasa ndugu wa imani yetu.

Mawaidha ya mwisho na salamu

11 Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu
mwenyewe.
12 Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka
kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu:
kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.
13 Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka
ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.
14 Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana
wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa
kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.
15 Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe
kipya.
16 Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na
huruma kwa Israeli–Wateule wa Mungu.

17 Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo
mwilini mwangu ni zile za Yesu.

18 Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Kristo. Amina.
\z

\id EPH SW50.ALL 19/03/90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PAULO KWA
                 WAEFESO

\h WAEFESO
\c 1

1 Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, nawaandikia
ninyi watu wa Mungu huko Efeso, mlio waaminifu katika kuungana na Kristo
Yesu.
2 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana
Yesu Kristo.

Baraka za kiroho katika Kristo

3 Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika
kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho
mbinguni.
4 Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katika
kuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bila hitilafu mbele yake. Kwa
sababu ya upendo wake,
5 Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto
wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia.
6 Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu katika Mwanae
mpenzi!

7 Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu
zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake
8 aliotukirimia bila kipimo! Kwa hekima na ujuzi wake wote
9 Mungu alitekeleza kile alichonuia, akatujulisha mpango wake
uliofichika, ambao alikuwa ameazimia kuutekeleza kwa njia ya Kristo.
10 Mpango huo ambao angeutimiza wakati utimiapo ni kukusanya pamoja
viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo.

11 Kila kitu hufanywa kufuatana na mpango na uamuzi wa Mungu; naye
Mungu ametuteua sisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katika kuungana na
Kristo, kufuatana na azimio alilofanya tangu mwanzo.
12 Basi, sisi tuliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswa kuusifu
utukufu wa Mungu!

13 Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli
yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu,
ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho
Mtakatifu aliyetuahidia.
14 Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia
watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa
wote walio wake. Tuusifu utukufu wake!

Sala ya Paulo

15 Kwa sababu hiyo, tangu niliposikia juu ya imani yenu kwa Bwana
Yesu na mapendo yenu kwa watu wa Mungu,
16 sijaacha kamwe kumshukuru Mungu kwa ajili yenu. Ninawakumbuka
katika sala zangu
17 ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Baba mtukufu, awajalieni Roho
wake atakayewapa hekima na kuwafunulieni Mungu mpate kumjua.
18 Namwomba Mungu aifunue mioyo yenu iweze kuuona mwanga wake, mpate
kutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufu mkuu wa zawadi
alizowawekea watu wake,
19 mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu
sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na nguvu
ile kuu mno
20 aliyomfufua nayo Kristo kutoka wafu, akamketisha kulia kwake
mbinguni.
21 Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu;
anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na
katika ulimwengu ujao.
22 Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa
kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote.
23 Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu wake yeye anayekamilisha
vitu vyote kila mahali.
\fr 1:20
\f taz Zab 110:1
\fr 1:22
\f taz Zab 8:5

Kutoka kifo na kuingia katika uzima
\c 2

1 Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu.
2 Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu,
mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala
sasa watu wasiomtii Mungu.
3 Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa
zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili
zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.

4 Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo
yasiyopimika,
5 hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya
hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu ninyi mmeokolewa.
6 Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye,
tukatawale pamoja naye mbinguni.
7 Ndivyo alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu
wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo
Yesu.
8 Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo
hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu.
9 Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia
kitu.
10 Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu,
alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia
tuyatende.

Umoja katika Kristo

11 Ninyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine–mnaoitwa,
“wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa
sababu ya kile wanachoifanyia miili yao)–kumbukeni mlivyokuwa zamani.
12 Wakati ule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya
Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu yoyote katika lile agano la
zile ahadi. Mlikuwa bila matumaini Mungu hapa duniani.
13 Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, ninyi ambao hapo awali
mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.
14 Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na
watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe
aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui.
15 Aliiondoa ile Sheria ya Wayahudi pamoja na amri zake na kanuni
zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika
umoja naye na hivyo kuleta amani.
16 Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake
aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.

17 Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu ninyi
watu wa mataifa mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi
ambao walikuwa karibu na Mungu.
18 Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa
mengine, tunaweza kumwendea Baba katika Roho mmoja.

19 Basi, ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia
pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
20 Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye
Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi.
21 Yeye ndiye mwenye kulitengeneza jengo lote na kulikuza hata liwe
hekalu takatifu kwa ajili ya B wana.
22 Katika kuungana naye, ninyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine,
muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.

Jukumu la Paulo kwa mataifa mengine
\c 3

1 Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili
yenu, namwomba Mungu.
2 Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake,
alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu.
3 Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika.
(Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili,
4 nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa
siri hiyo ya Kristo.)
5 Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu
amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.
6 Siri yenyewe ni hii: kwa njia ya Habari Njema watu wa mataifa
mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za
Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile
aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.

7 Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Habari Njema kwa neema ya pekee
aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
8 Mimi ni mdogo kuliko watu wote wa Mungu; lakini amenijalia neema
yake, ili niwahubirie watu wa mataifa utajiri wake Kristo usiopimika,
9 tena niwaangazie watu wote waone jinsi mpango wa Mungu uliofichika
unavyotekelezwa. Mungu aliye Muumba wa vitu vyote alificha siri hiyo
yake tangu milele,
10 kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni
wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi.
11 Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele
ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
12 Basi, katika kuungana na Kristo, na kwa njia ya imani katika
Kristo, sisi tunathubutu kumkaribia Mungu kwa uhodari.
13 Kwa hiyo, nawaombeni msife moyo kwa sababu ya mateso ninayopata
kwa ajili yenu, maana hayo ni kwa ajili ya utukufu wenu.

Upendo wa Kristo

14 Kwa sababu hiyo, nampigia magoti Baba,
15 aliye asili ya jamaa zote duniani na mbinguni.
16 Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalieni kwa
uwezo wa Roho wake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu,
17 naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Namwomba mpate kuwa na
mzizi na msingi katika mapendo
18 kusudi muweze kufahamu pamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendo
wa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu, kwa kimo na kina.
19 Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe
kabisa utimilifu wote wa Mungu.

20 Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu, aweza
kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria;
21 kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu,
nyakati zote, milele na milele! Amina.

\c 4

Umoja katika jumuiya
1 Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi
muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
2 Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni ninyi
kwa ninyi kwa mapendo.
3 Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia
amani iliyo kati yenu.
4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na
Mungu ni moja.
5 Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja;
6 kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya
kazi katika yote na yuko katika yote.
\fr 4:8
\f taz Zab 68:18

7 Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na
Kristo.
8 Kama yasemavyo Maandiko:

“Alipopaa mbinguni juu kabisa,
alichukua mateka;
aliwapa watu zawadi.”
\m
9 Basi, inaposemwa: “alipaa juu,” ina maana gani? Maana yake ni
kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani.
10 Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaa juu ya mbingu
zote apate kuujaza ulimwengu.
11 Ndiye aliyewapa watu zawadi: wengine aliwajalia wawe mitume,
wengine manabii, wengine wawe waeneza Habari Njema, wengine wachungaji
na walimu.
12 Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili
ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo,
13 na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu;
tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
14 Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko
na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu, ili
wawapotoshe wengine kwa hila.
15 Ila, sisi tukisema ukweli kwa moyo wa mapendo tutakua zidi katika
kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa;
16 chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja,
na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo
kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika
upendo.

Maisha mapya katika Kristo

17 Basi, kwa jina la Bwana, nawaonyeni: msiishi tena kama watu
wasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwa upuuzi mtupu,
18 na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uzima wa Mungu, kwa
sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao.
19 Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa
pupa kila aina ya mambo ya aibu.

20 Lakini ninyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo.
21 Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi
wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu.
22 Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale
uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu.
23 Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu.
24 Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na
ambayo hujionyesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.
\fr 4:26
\f taz Zab 4:4
\fr 5:2
\f taz Zab 40:6

25 Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake
ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo.
26 Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi,
na wala msikae na hasira kutwa nzima.
27 Msimpe Ibilisi nafasi.
28 Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema
kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.
29 Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara
maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili
yawaneemeshe wasikilizaji wenu.
30 Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu maana Roho huyo ni alama ya
Mungu kwenu kwamba ninyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja
ambapo Mungu atawakomboeni.
31 Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele, matusi!
Achaneni na kila uovu!
32 Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe
mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.

Kuishi katika mwanga
\c 5

1 Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi.
2 Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa
ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko
impendezayo Mungu.

3 Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule
au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu.
4 Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu;
maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.
5 Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi
ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia
chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu.

6 Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu
ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.
7 Basi, msishirikiane nao.
8 Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga
kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga:
9 maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli.
10 Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana.
11 Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni.
12 Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja.
13 Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake
hudhihirishwa;
14 na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko
yasema:

“Amka wewe uliyelala,
fufuka kutoka wafu,
naye Kristo atakuangaza.”

15 Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu,
bali kama wenye hekima.
16 Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya.
17 Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana.
18 Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho
Mtakatifu.
19 Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho;
mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
20 Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana
wetu Yesu Kristo.

Wake na waume

21 Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo.
22 Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana.
23 Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na
mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili
wake.
24 Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii
waume zao katika mambo yote.

25 Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda
kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.
26 Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada
ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji,
27 kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa
lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
28 Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.
((
29 Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia,
huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa,
30 maana sisi ni viungo vya mwili wake.)
31 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa hiyo, mwanamume
atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa
mwili mmoja.”
32 Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba
yamhusu Kristo na kanisa lake.
33 Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama
nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.

Watoto na wazazi wao
\c 6

1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
2 “Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo
imeongezewa ahadi, yaani,
3 “Upate fanaka na miaka mingi duniani.”

4 Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika
nidhamu na mafundisho ya Kikristo.

Watumwa na wakuu wao

5 Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na
tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia
Kristo.
6 Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao,
bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni
watumishi wa Kristo.
7 Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
8 Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu
huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
9 Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni
kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana
yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.

Vita vya kiroho

10 Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa
msaada wa nguvu yake kuu.
11 Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za
Ibilisi.
12 Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita
dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu
na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.
13 Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika
muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho,
muwe bado thabiti.

14 Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu,
uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,
15 na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni
mwenu.
16 Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu,
iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.
17 Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama
upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.
18 Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa
nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa
Mungu.
19 Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema,
niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.
20 Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko
kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama
inipasavyo.

Salamu za mwisho

21 Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana,
atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
22 Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.

23 Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu
Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
24 Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo
kwa mapendo yasiyo na mwisho.
\z

\id COL SW52.ALL 20-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PAULO KWA
                 WAKOLOSAI

\h WAKOLOSAI
\c 1

1 Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu
Timotheo,
2 tunawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu
waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka
kwa Mungu Baba yetu.

3 Daima tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, wakati
tunapowaombea.
4 Maana tumesikia juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na juu ya
upendo wenu kwa watu wote wa Mungu.
5 Wakati ujumbe ule wa kweli, yaani Habari Njema, ilipowafikieni kwa
mara ya kwanza, mlipata kusikia juu ya lile tumaini linalopatikana
kwake. Kwa sababu hiyo imani na upendo wenu vinategemea jambo lile
mnalotumainia ambalo mmewekewa salama mbinguni.
6 Habari Njema inazidi kuzaa matunda na kuenea ulimwenguni kote kama
vile ilivyofanya kwenu ninyi tangu siku ile mliposikia juu ya neema ya
Mungu na kuitambua ilivyo kweli.
7 Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi
mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
8 Yeye alitupa habari za upendo wenu mliojaliwa na Roho.
9 Kwa sababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daima tangu tulipopata
habari zenu. Tunamwomba Mungu awajazeni ujuzi kamili wa mapenzi yake,
awajazeni hekima yote na elimu iletwayo na Roho wake.
10 Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima
yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya
matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.
11 Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili mweze
kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
12 Na kwa furaha, mshukuruni Baba aliyewawezesha ninyi kuwa na
sehemu yenu katika mambo yale Mungu aliyowawekea watu wake katika
utawala wa mwanga.
13 Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika
ufalme wa Mwanae mpenzi,
14 ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaani dhambi zetu
zinaondolewa.

Kristo na kazi yake

15 Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana;

ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

16 Maana kwa njia yake vitu vyote viliumbwa duniani na mbinguni,

vitu vinavyoonekana na visivyoonekana:
wenye enzi, watawala, wakuu na wenye mamlaka.
Vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.

17 Kristo alikuwako kabla ya vitu vyote;

kwa kuungana naye, vyote vyadumu mahali pake.

18 Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa;

yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili.
Yeye ndiye mwanzo,
mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu,
ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.

19 Maana Mungu alipenda utimilifu wote uwe ndani yake.

20 Kwa njia yake Mungu alivipatanisha naye vitu vyote

naam, viumbe vyote mbinguni na duniania;
alileta amani kwa damu ya Kristo msalabani.

21 Hapo kwanza ninyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake
kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu.
22 Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu
amewapatanisha naye, kusudi awalete mbele yake mkiwa watakatifu, safi na
bila lawama.
23 Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani
hiyo, na msikubali kusukumwa mbali na tumaini lile mlilopata wakati
mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Habari
Njema ambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbe duniani.

Huduma ya Paulo katika makanisa

24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu
hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso
ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa.
25 Nami nimefanywa kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na mpango wake
Mungu ambao alinikabidhi kwa faida yenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza
kwa ukamilifu ujumbe wake,
26 ambao ni siri aliyowaficha binadamu wote tangu milele, lakini
sasa amewajulisha watu wake.
27 Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu
ambayo ni kwa ajili ya watu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo
yuko ndani yenu, na jambo hilo lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki
utukufu wa Mungu.
28 Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na
kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele
ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo.
29 Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia
nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu.

\c 2

1 Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa
ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona
kwa macho.
2 Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika
upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo
wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.
3 Ndani yake zimefichika hazina zote za hekima na elimu.

4 Basi, nawaambieni, msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa maneno
ya uongo hata kama ni ya kuvutia sana.
5 Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja
nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao
pamoja katika imani yenu kwa Kristo.

Maisha kamili katika Kristo

6 Maadamu ninyi mmemkubali Kristo Yesu kuwa Bwana, basi, ishini
katika muungano naye.
7 Mnapaswa kuwa na mizizi ndani yake, kujijenga juu yake na kuwa
imara katika imani yenu kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.

8 Angalieni basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima
ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu na
ya pepo watawala, na wala si Kristo mwenyewe!
9 Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote
wa Mungu,
10 nanyi mmepewa uzima kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya
pepo watawala wote na wakuu wote.

11 Katika kuungana na Kristo ninyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara
ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo
inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
12 Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo,
mlifufuliwa pia pamoja naye kwa imani yenu katika nguvu ya Mungu ambaye
alimfufua Kristo kutoka wafu.
13 Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na
kwa sababu ninyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa
ninyi uzima pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote;
14 alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na
masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
15 Juu ya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na
wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama
mateka katika msafara wa ushindi wake.

16 Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu
vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya Mwezi mpya au Sabato.
17 Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli
wenyewe ndiye Kristo.
18 Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa
sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa
uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira
danganifu za kidunia
19 na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya
uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa
viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.

Kufa na kuishi pamoja na Kristo

20 Ninyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa kutoka nguvu za
pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile
mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
21 “Msishike hiki,” “Msionje kile,” “Msiguse kile!”
22 Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu
vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
23 Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima katika namna ya
ibada ya kujitakia wenyewe, unyenyekevu wa uongo na kuutendea mwili kwa
ukali; lakini kwa kweli, haifai chochote kuzuia tamaa za mwili.
\fr 3:1
\f taz Zab 110:1

\c 3

1 Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule
Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu.
2 Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.
3 Maana ninyi mmekufa na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo
katika Mungu.
4 Uzima wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi
pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.

Maisha ya kale na maisha mapya

5 Basi, komesheni kabisa kila kitu kilicho ndani yenu ambacho
chahusika na mambo ya kidunia: uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na
uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).
6 Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi.
7 Wakati mmoja ninyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo,
mlipotawaliwa nayo.
8 Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa,
uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
9 Msiambiane uongo, kwani ninyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja
na matendo yake yote,
10 mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba
wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu.
11 Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi,
aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu
aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.

12 Ninyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo
basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
13 Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote
dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe ninyi.
14 Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo kwani upendo huunganisha
kila kitu katika umoja ulio kamili.
15 Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo
ninyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
16 Ujumbe wa Kristo ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote.
Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni zaburi, nyimbo na
tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani.
17 Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la
Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.

Wajibu wa jamii katika maisha mapya

18 Enyi akina mama, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo
Bwana.
19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza
Bwana.

21 Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.

22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na
si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila
fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
23 Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si
kwa ajili ya mtu.
24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake.
Mtumikieni Kristo Bwana!
25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana
ubaguzi.

\c 4

1 Nanyi wakuu, watendeeni watumwa wenu kwa uadilifu na haki,
mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni.

Maagizo

2 Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru
Mungu.
3 Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri
ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa
kifungoni.
4 Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna
itakayodhihirisha siri hiyo.

5 Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkitumia
vizuri kila nafasi mliyo nayo.
6 Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na ya kuvutia, na
mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Salamu za mwisho

7 Ndugu yetu mpenzi Tukiko, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi
mwenzetu katika kazi ya Bwana, atawapeni habari zangu zote.
8 Ndiyo maana namtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwa kuwaambieni
habari zetu.
9 Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye
ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika
hapa.

10 Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali
kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake;
akifika kwenu mkaribisheni).
11 Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi
waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja
nami kwa ajili ya Utawala wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
12 Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu
anawasalimuni. Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpate kusimama
imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
13 Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu
na kwa ajili ya watu wa Laodikea na Hierapoli.
14 Luka, daktari wetu mpenzi, na Dema, wanawasalimuni.

15 Salamu zetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimuni dada Nimfa
pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
16 Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa
Laodikea; na ninyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata kwao.
17 Mwambieni Arkipo aitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa na
Bwana.
18 Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu,
mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
\z

\id 1TH SW53.ALL 14-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA KWANZA YA PAULO KWA
                 WATHESALONIKE

\h 1 WATHESALONIKE
\c 1

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya
kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu
Kristo.

Maisha na imani ya Wathesalonike

2 Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi nyote na
kuwakumbukeni daima katika sala zetu.
3 Maana, mbele ya Mungu Baba yetu, twakumbuka jinsi mnavyoonyesha
imani yenu kwa matendo, jinsi upendo wenu unavyowawezesha kufanya kazi
kwa bidii, na jinsi tumaini lenu katika Bwana wetu Yesu Kristo lilivyo
thabiti.
4 Ndugu, twajua kwamba Mungu anawapenda na kwamba amewateua muwe
watu wake,
5 maana wakati tulipowahubirieni ile Habari Njema haikuwa kwa maneno
tu, bali pia kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, tukiwa na hakika kwamba
ujumbe huo ulikuwa wa kweli. Mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi;
tuliishi kwa manufaa yenu.
6 Ninyi mlifuata mfano wetu, na kumwiga Bwana. Ingawa mliteswa sana,
mliupokea ujumbe huo kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.
7 Kwa hiyo ninyi mmekuwa mfano mzuri kwa waumini wote wa Makedonia
na Akaya.
8 Maana, kutokana na bidii yenu ujumbe wa Bwana umesikika si tu huko
Makedonia na Akaya, bali imani yenu kwa Mungu imeenea popote. Tena
hatuhitaji kusema zaidi.
9 Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: jinsi
mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu mkamgeukia Mungu aliye hai
na wa kweli,
10 na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, Yesu, ambaye
Mungu alimfufua kutoka wafu, na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya
Mungu inayokuja.

Utumishi wa Paulo huko Thesalonike
\c 2

1 Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa
bure.
2 Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya
kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu
alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.
3 Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia
mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.
4 Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba
tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu
hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu
mpaka ndani.
5 Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu na maneno matamu ya
kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi
fulani; Mungu ni shahidi!
6 Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka
kwa mtu yeyote,
7 ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani
kwenu. Lakini sisi tulikuwa Wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto
wake.
8 Tuliwapenda ninyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu
Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa
wapenzi wetu!

9 Ndugu, mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika.
Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku
kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu.
10 Ninyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo
wetu kati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri, mwadilifu na usio na
lawama.
11 Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba
anavyowatendea watoto wake mwenyewe.
12 Tuliwapeni moyo, tuliwafarijini na kuwahimiza ili mpate kuishi
maisha yampendezayo Mungu ambaye aliwaiteni mshiriki Utawala na utukufu
wake.

13 Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni
ujumbe wa Mungu, ninyi mliusikia mkaupokea, si kama vile ujumbe wa
binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu
anafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
14 Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya
Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Ninyi
mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na
wenzao Wayahudi,
15 ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia.
Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!
16 Hata walijaribu kutuzuia kuwahubiria watu wa mataifa mengine
ujumbe utakaowaletea wokovu. Ndivyo walivyokamilisha orodha ya dhambi
zote walizotenda siku zote. Lakini sasa hasira ya Mungu imewaangukia.

Nia ya kuwatembelea Wathesalonike

17 Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana
huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye,
tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
18 Kwa hiyo tuliamua kuwatembeleeni tena. Nami, Paulo, nilijaribu
kuja kwenu zaidi ya mara moja, lakini Shetani alituzuia.

19 Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari
ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndio
tumaini letu na furaha yetu.
20 Naam, ninyi ni utukufu wetu na furaha yetu!

\c 3

1 Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi. Basi, tuliamua kubaki kule
Athene peke yetu,
2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi
mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo.
Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,
3 kusudi imani ya mtu yeyote miongoni mwenu isije ikafifia kwa
sababu ya taabu hizo. Ninyi mnajua kwamba tunapaswa kupata mateso.
4 Maana, tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; na
kama mjuavyo ndivyo ilivyotukia.
5 Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na
hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi
aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!

6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha
kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na
kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
7 Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso
yetu yote,
8 kwani sasa tunaishi kweli ikiwa ninyi mnasimama imara katika
kuungana na Bwana.
9 Sasa twaweza kumshukuru Mungu wetu kwa ajili yenu. Tunamshukuru
kwa furaha tuliyo nayo mbele yake kwa sababu yenu.
10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili
atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote
kilichopungua katika imani yenu.

11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe, na Bwana wetu Yesu
atutayarishie njia ya kuja kwenu.
12 Bwana awawezeshe ninyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na
zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda ninyi.
13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na
watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu
atakapokuja pamoja na wote walio wake.

Maisha yampendezayo Mungu
\c 4

1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa
kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa
tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.
2 Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana
Yesu.
3 Mungu anataka ninyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha
ya zinaa.
4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa
utakatifu na heshima,
5 na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua
Mungu.
6 Basi, mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili.
Tulikwisha waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu
wanaofanya mambo hayo.
7 Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika
utakatifu.
8 Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali
amdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.

9 Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini.
Ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.
10 Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika
Makedonia. Basi, ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi.
11 Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie
mambo yake mwenyewe na afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama
tulivyowaagiza pale awali.
12 Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio
Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji
yenu.

Bwana anakuja

13 Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki
dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini.
14 Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi
tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki
wakiwa wanamwamini.

15 Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana; sisi tulio hai, ambao
tutakuwa tumebaki, wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia
wale waliokwisha fariki dunia.
16 Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta
ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale
waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika
mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.
18 Basi, farijianeni kwa maneno haya.

Muwe tayari kwa siku ya Bwana
\c 5

1 Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira
yatakapotukia mambo haya.
2 Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi
ajavyo usiku.
3 Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”
ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla
kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu
hawataweza kuepukana nayo.
4 Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni
ghafla kama vile mwizi.
5 Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi
si watu wa usiku, wala wa giza.
6 Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na
kiasi.
7 Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku.
8 Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi.
Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na
tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma.
9 Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali
tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai
au tumekufa.
11 Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama
mnavyofanya sasa.

Maagizo ya mwisho na salamu

12 Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu,
wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo.
13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya.
Muwe na amani kati yenu.

14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo
watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.
15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia
yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.

16 Furahini daima,
17 salini kila wakati
18 na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu
kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.

19 Msimpinge Roho Mtakatifu;
20 msidharau unabii.
21 Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema,
22 na epukeni kila aina ya uovu.

23 Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna
na kuzilinda nafsi zenu–roho, mioyo na miili yenu–mbali na hatia
yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
24 Yeye anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.

25 Ndugu, tuombeeni na sisi pia.

26 Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.

27 Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua
hii.

28 Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
\z

\id 2TH SW54.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PILI YA PAULO KWA
                 WATHESALONIKE

\h 2 WATHESALONIKE
\c 1

1 Mimi Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya
kanisa la Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba yetu na wa Bwana
Yesu Kristo.

2 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa
Bwana Yesu Kristo.

Hukumu wakati wa kuja kwake Kristo

3 Ndugu, tunapaswa kushukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa
kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu
kunaongezeka sana.
4 Ndio maana sisi tunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu.
Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika
udhalimu wote na mateso mnayopata.

5 Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na
matokeo yake ninyi mtastahili Utawala wake ambao kwa ajili yake
mnateseka.
6 Mungu atafanya jambo la haki: atawalipa mateso wale wanaowatesa
ninyi,
7 na kuwapeni nafuu ninyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo
hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake na
wakuu
8 na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale
wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu.
9 Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu
wake mkuu,
10 wakati atakapokuja Siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake
na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwao,
kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.

11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezeshe
muyastahili maisha aliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake,
atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
12 Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka
kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya
Bwana Yesu Kristo.

Yule Mwovu
\c 2

1 Sasa yahusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa kwetu
pamoja tukae naye. Ndugu, tunawaombeni sana
2 msifadhaike upesi moyoni, na wala msitiwe wasiwasi kwa sababu ya
madai kwamba Siku ya Bwana imekwisha fika. Labda inadhaniwa kwamba jambo
hili limetokana na uaguzi fulani, mahubiri au barua inayosemekana kuwa
imetoka kwetu.
3 Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile. Maana
Siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule Uasi Mkuu utokee na yule Mwovu
aonekane ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.
4 Yeye atapinga kila kitu wanachokiona watu kuwa ni mungu, au
wanachokiabudu. Naam, hata ataingia na kuketi ndani ya Hekalu la Mungu
akijidai kuwa Mungu.

5 Je, hamkumbuki kwamba niliwaambieni haya yote wakati nilipokuwa
pamoja nanyi?
6 Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho.
Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
7 Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini
hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
8 Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua
kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng’ao wa kuja kwake.
9 Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya
miujiza na maajabu ya uongo,
10 na kutumia udanganyifu wa kila namna kwa wale walio katika mkumbo
wa kupotea. Hao watapotea kwa sababu hawakuupokea na kuupenda ule ukweli
ili waokolewe.
11 Ndiyo maana Mungu amewaweka chini ya nguvu ya upotovu, wauamini
uongo.
12 Matokeo yake ni kwamba wote wasioamini ukweli, ila wafurahia
dhambi, watahukumiwa.

Mmeteuliwa mpate kuokolewa

13 Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu,
ninyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate
kuokolewa kwa nguvu ya Roho mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu
katika ukweli.
14 Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema
tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu
wa Bwana wetu Yesu Kristo.
15 Basi, ndugu, simameni imara na zingatieni yale mafundisho
tuliyowafundisheni kwa mahubiri yetu na barua zetu.

16 Tunamwomba Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu
ambaye alitupenda, na kwa neema yake akatujalia faraja ya milele na
tumaini jema,
17 aifariji mioyo yenu na kuwaimarisheni ili mweze daima kutenda na
kusema yaliyo mema.

Tuombeeni kwa Mungu
\c 3

1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi
na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si
wote wanaoamini ujumbe huu.

3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Yeye atawaimarisheni na kuwalinda
salama na yule Mwovu.
4 Naye Bwana anatupatia tumaini kubwa juu yenu, na hatuna shaka
kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaambieni.

5 Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika
uvumilivu tunaopewa na Kristo.

Jukumu la kufanya kazi

6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe
na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
7 Ninyi wenyewe mnajua kwamba mnapaswa kufuata mfano wetu. Sisi
tulipokuwa nanyi hatukuwa wavivu;
8 hatukula chakula kwa mtu yeyote bila ya kumlipa. Tulifanya kazi
kwa bidii na taabu mchana na usiku ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote kati
yenu.
9 Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila
kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
10 Tulipokuwa pamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, “Mtu asiyefanya
kazi, asile.”

11 Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu
ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza
katika mambo ya watu wengine.
12 Kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo tunawaamuru na kuwaonya watu
hao wawe na nidhamu na kufanya kazi ili wajipatie maslahi yao wenyewe.

13 Lakini ninyi ndugu, msichoke kutenda mema.
14 Huenda kwamba huko kuna mtu ambaye hatautii huu ujumbe
tunaowapelekeeni katika barua hii. Ikiwa hivyo, basi, mfichueni mtu huyo
na msiwe na uhusiano wowote naye kusudi aone aibu.
15 Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu.

Maneno ya mwisho

16 Bwana mwenyewe ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote
kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote.

17 Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo!
Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.

18 Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
\z

\id 1TI SW55.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA KWANZA YA PAULO KWA
                 TIMOTHEO

\h 1 TIMOTHEO
\c 1

1 Mimi Paulo, mtume wa Yesu Kristo kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na
Yesu Kristo tumaini letu,
2 nakuandikia Timotheo mwanangu halisi katika imani.
Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Kristo
Yesu Bwana wetu.

Maonyo kuhusu mafundisho ya uongo

3 Napenda ukae huko Efeso, kama nilivyokuomba nilipokuwa ninakwenda
Makedonia. Wako watu fulani huko wanaofundisha mafundisho ya uongo.
Wakomeshe watu hao.
4 Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu,
ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao
kwa imani.
5 Shabaha ya amri hii ni kuhimiza mapendo yatokayo katika moyo safi,
dhamiri njema, na imani ya kweli.
6 Watu wengine wamepotoka na kugeukia majadiliano yasiyo na maana.
7 Wanapenda kuwa walimu wa Sheria, lakini hawaelewi maneno yao
wenyewe au mambo wanayosisitiza.

8 Twajua kwamba Sheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo.
9 Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya
watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na
wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na
mama zao, au wauaji wowote wale;
10 sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba
watu, waongo, na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni
kinyume cha mafundisho ya kweli.
11 Mafundisho hayo hupatikana katika Habari Njema ambayo mimi
nimekabidhiwa niihubiri, Habari Njema ya Mungu mtukufu na mwenye heri.

Shukrani kwa ajili ya huruma ya Mungu

12 Namshukuru Bwana wetu Yesu Kristo aliyenipa nguvu kwa ajili ya
kazi yangu. Namshukuru kwa kuniona mimi kuwa ni mwaminifu, akaniteua
nimtumikie,
13 ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu.
Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo
sikujua nilichokuwa ninafanya.
14 Lakini Bwana wetu alinijalia neema yake kwa wingi, akanipa imani
na upendo katika kuungana na Kristo Yesu.
15 Usemi huu ni wa kuaminika, na tena unafaa kukubaliwa kabisa:
Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Nami ni mkosefu
zaidi kuliko hao wote,
16 lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aonyeshe uvumilivu wake
wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na
kupokea uzima wa milele.
17 Kwake yeye aliye Mfalme wa milele na asiyekufa, yeye aliye Mungu
pekee–kwake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina.

18 Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya
unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako
katika kupigana vita vizuri,
19 na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine
hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
20 Miongoni mwao ni Humenayo na Aleksanda ambao nimewakabidhi kwa
Shetani, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.

Mafundisho kuhusu sala
\c 2

1 Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani
zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote,
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi
maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
3 Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu,
4 ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
5 Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na
Mungu, binadamu Kristo Yesu,
6 ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa
uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia.
7 Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa
mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi
uongo!

8 Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu
waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila
hasira wala ubishi.
9 Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara
kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka
nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa,
10 bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu.
11 Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa
kujifunza.
12 Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume;
anapaswa kukaa kimya.
13 Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa.
14 Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye
aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu.
15 Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu
katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.

Viongozi katika kanisa
\c 3

1 Msemo huu ni wa kweli: mtu akitaka kuwa kiongozi katika kanisa,
huyo anatamani kazi nzuri.
2 Basi, kiongozi wa kanisa anapaswa awe mtu asiye na lawama;
anapaswa awe na mke mmoja tu, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni
lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha;
3 asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani;
asiwe mtu wa kupenda fedha;
4 anapaswa awe mtu awezaye kuongoza vema nyumba yake, na kuwafanya
watoto wake wawe watii kwa heshima yote.
5 Maana kama mtu hawezi kuongoza vema nyumba yake, atawezaje
kulitunza kanisa la Mungu?
6 Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi
katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi
alivyohukumiwa.
7 Anapaswa awe mwenye sifa njema kati ya watu walio nje ya kanisa,
ili asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa Ibilisi.

Wasaidizi katika kanisa

8 Wasaidizi katika kanisa wanapaswa pia kuwa watu wenye tabia njema
na wanyofu; wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha;
9 wanapaswa kuzingatia kwa dhamiri njema ukweli wa ndani wa imani.
10 Ni lazima kwanza wathibitishwe, na wakionekana kuwa wanafaa,
basi, watoe huduma yao.
11 Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasiowasengenya watu,
wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
12 Msaidizi katika kanisa lazima awe na mke moja tu, na awezaye
kuongoza vema watoto wake na nyumba yake.
13 Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo
mzuri, na wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.

Siri kuu

14 Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi
karibuni.
15 Lakini kama nikicheleweshwa, basi, barua hii itakufahamisha
mwenendo tunaopaswa kuwa nao katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la
Mungu aliye hai, na ambalo ni nguzo na msingi wa ukweli.
16 Hakuna mashaka yoyote juu ya ukuu wa siri ya dini yetu:

Alionekana katika umbo la kibinadamu
alithibitishwa na Roho kuwa ni mwadilifu,
akaonekana na malaika.
Alihubiriwa kati ya mataifa,
aliaminiwa popote ulimwenguni,
akachukuliwa juu mbinguni katika utukufu.

Waalimu wa uongo
\c 4

1 Roho asema waziwazi kwamba siku za baadaye watu wengine
wataitupilia mbali imani; watazitii roho danganyifu na kufuata
mafundisho ya pepo.
2 Mafundisho ya namna hiyo yanaenezwa na watu waongo wadanganyifu,
ambao dhamiri zao ziko kama zimechomwa kwa chuma cha moto.
3 Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuona na pia kula vyakula
fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na
ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.
4 Kila kitu alichoumba Mungu ni chema, wala hakuna kinachohitaji
kukataliwa, bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani,
5 kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike
kwa Mungu.

Mtumishi mwema wa Yesu Kristo

6 Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa
Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya
kweli, ambayo wewe umeyafuata.
7 Lakini achana na hadithi zile zisizo za kidini na ambazo hazina
maana. Jizoeshe kuishi maisha ya uchaji wa Mungu.
8 Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana
faida za kila namna, maana yanatuahidia uzima katika maisha ya sasa, na
pia hayo yanayokuja.
9 Usemi huo ni wa kusadikika kabisa na unastahili kukubaliwa.
10 Sisi tunajitahidi na kufanya kazi kwa bidii kwani tumemwekea
tumaini letu Mungu aliye hai ambaye ni Mwokozi wa watu wote, na hasa
wale wanaoamini.

11 Wape maagizo hayo na mafundisho hayo.
12 Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini
jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako,
upendo, imani na maisha safi.
13 Tumia wakati wako na juhudi yako katika kusoma hadharani Maandiko
Matakatifu, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
14 Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa
kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
15 Fikiri kwa makini juu ya hayo yote na kuyatekeleza kusudi
maendeleo yako yaonekane na wote.
16 Angalia sana mambo yako mwenyewe, na mafundisho yako. Endelea
kufanya hayo maana ukifanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale
wanaokusikiliza.

Wajibu kwa waumini
\c 5

1 Usimkemee mtu mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako.
Watendee vijana kama ndugu zako,
2 wanawake wazee kama mama yako, na wasichana kama dada zako, kwa
usafi wote.

3 Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
4 Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza
kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa
wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya
Mungu.
5 Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu
tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
6 Lakini mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa,
ingawa yu hai.
7 Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama.
8 Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa
nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko
mtu asiyeamini.

9 Usimtie katika orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza
miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
10 na awe mwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wake vizuri,
aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu,
aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema.
11 Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile
zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo watataka
kuolewa tena,
12 na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.
13 Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata
nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia
katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa
kusema.
14 Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na
kutunza nyumba zao ili adui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu
juu yetu.
15 Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.
16 Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye
anapaswa kuwatunza na si kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze
kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.

17 Wazee wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki
maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.

18 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Usimfunge ng’ombe kinywa
anapopura nafaka.” na tena “Mfanyakazi astahili malipo yake.”
19 Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na
mashahidi wawili au watatu.
20 Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate
kuogopa.

21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya
malaika watakatifu uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala
kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
22 Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia
Bwana. Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.

23 Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako,
kwani unaugua mara kwa mara.

24 Dhambi za watu wengine huonekana waziwazi, nazo zawatangulia
kwenye hukumu; lakini dhambi za wengine huonekana tu baadaye.
25 Vivyo hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo
si dhahiri hayawezi kufichika.

\c 6

1 Watumwa wote wanapaswa kuwaheshimu wakuu wao ili kusiwe na sababu
ya watu kulitukana jina la Mungu na mafundisho yetu.
2 Watumwa ambao wakuu wao ni Wakristo wasiwadharau kwani ni ndugu
zao. Badala yake, wanapaswa kuwatumikia hata vizuri zaidi, maana hao
wanaopata faida kutokana na kazi yao ni waumini ambao wanawapenda.

Mafundisho ya uongo na utajiri wa ukweli
Unapaswa kufundisha na kuhubiri mambo haya.
3 Mtu yeyote anayefundisha kinyume cha mambo haya, na ambaye
hakubaliani na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo na mafundisho
ya dini,
4 huyo amejaa majivuno na wala hajui chochote. Ni mtu wa kupenda
ubishi na magombano juu ya maneno matupu, na hiyo husababisha wivu,
ugomvi, matusi, shuku mbaya,
5 na ubishi usio na kikomo kutoka kwa watu ambao akili zao
zimeharibika, na ambao hawana tena ukweli. Wanadhani dini ni njia ya
kujipatia utajiri.

6 Kweli dini humfanya mtu awe tajiri sana, ikiwa anatosheka na vitu
alivyo navyo.
7 Maana hatukuleta kitu chochote hapa duniani, wala hatutachukua
chochote.

8 Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika
navyo.
9 Lakini wale wanaotaka kutajirika huanguka katika majaribu, na
kunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbaya za kipumbavu, ambazo huwavuta
mpaka kwenye uharibifu na maangamizi.
10 Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu
wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani,
na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi.

Mawaidha kwa Timotheo

11 Lakini wewe, mtu wa Mungu, jiepushe na mambo hayo. Zingatia
uadilifu, uchaji wa Mungu, imani, mapendo, subira na unyenyekevu.
12 Piga mbio kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani,
ukajipatie tuzo la uzima wa milele, uliloitiwa wakati ulipokiri imani
yako mbele ya mashahidi wengi.
13 Mbele ya Mungu anayevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Yesu Kristo
aliyetoa ushahidi na kukiri ukweli mbele ya Pontio Pilato,
14 nakuamuru ushike maagizo yako na kuyatii kwa uaminifu mpaka Siku
ile atakapotokea Bwana wetu Yesu Kristo.
15 Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao uliopangwa na Mungu mwenye
heri na aliye Mtawala pekee, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.
16 Yeye peke yake anaishi milele, katika mwanga usioweza kukaribiwa
na mtu. Hakuna mtu aliyepata kumwona au awezaye kumwona. Kwake iwe
heshima na uwezo wa milele! Amina.

17 Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa,
wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali
wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie.
18 Waamuru watende mema, wawe matajiri katika matendo mema, na wawe
wakarimu na walio tayari kuwashirikisha wengine mali zao.
19 Kwa namna hiyo watajiwekea hazina ambayo itakuwa kwao msingi
imara kwa wakati ujao. Hapo wataweza kujipatia uzima ambao ni uzima wa
kweli.

20 Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na
majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita
watu wengine: “Elimu”.
21 Maana wengine wamejidai kuwa na hiyo elimu, na matokeo yake
wamepoteza imani.

Nawatakieni nyote neema!
\z

\id 2TI SW56.ALL 19-03-90 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PILI YA PAULO KWA
                 TIMOTHEO

\h 2 TIMOTHEO
\c 1

1 Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili
niutangaze ule uzima tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,
2 nakuandikia wewe mwanangu mpenzi Timotheo.
Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu
Bwana wetu.

Shukrani na maneno ya kutia moyo

3 Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama
walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka daima katika
sala zangu.
4 Nakumbuka machozi yako na ninatamani usiku na mchana kukuona, ili
nijazwe furaha.
5 Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako
Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.
6 Ndio maana nakukumbusha ukiweke motomoto kile kipaji ulichopewa na
Mungu wakati nilipokuwekea mikono yangu.
7 Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali
alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.

8 Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa
sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika
mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unazopewa na Mungu.
9 Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa
sababu ya matendo yetu wenyewe bali kwa sababu ya kusudi lake na neema
yake. Alitujalia neema hiyo katika Kristo Yesu kabla mwanzo wa nyakati;
10 lakini sasa imefunuliwa kwetu kwa kuja kwake Mwokozi wetu Yesu
Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema
akadhihirisha uzima usio kufa.

11 Mungu amenichagua mimi niwe mtume na mwalimu kwa ajili ya
kuhubiri Habari Njema,
12 nami nateseka mambo haya kwa sababu hiyo. Lakini niko bado timamu
kabisa kwani namjua yule niliyemwamini, tena nina hakika kwamba yeye
aweza kukilinda salama kile alichonikabidhi, mpaka Siku ile.
13 Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha, na
kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo
Yesu.
14 Jambo lile bora ulilokabidhiwa lilinde kwa nguvu ya Roho
Mtakatifu anayeishi ndani yetu.

15 Kama unavyojua, watu wote mkoani Asia wameniacha, miongoni mwao
wakiwa Fugelo na Hermogene.
16 Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha
rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
17 ila mara tu alipofika Roma, alianza kunitafuta kwa bidii mpaka
akanipata.
18 Bwana amjalie huruma katika Siku ile! Nawe wajua vizuri mengi
aliyonifanyia huko Efeso.

Askari mwaminifu wa Yesu Kristo
\c 2

1 Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika
kuungana na Kristo Yesu.
2 Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi
wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha
wengine pia.
3 Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo yesu.
4 Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida ili
aweze kumpendeza mkuu wa jeshi.
5 Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi
kama asipozitii sheria za michezo.
6 Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya
kwanza ya mavuno.
7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uyaelewe yote.

8 Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka wafu, aliyekuwa wa ukoo
wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri.
9 Kwa sababu ya kuihubiri Habari Njema mimi nateseka na nimefungwa
minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa
minyororo,
10 na hivyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili
wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao
huleta utukufu wa milele.
11 Usemi huu ni wa kweli:

“Ikiwa tulikufa pamoja naye,
tutaishi pia pamoja naye.

12 Tukiendelea kuvumilia,

tutatawala pia pamoja naye.
Tukimkana,
naye pia atatukana.

13 Tukikosa kuwa waaminifu,

yeye hubaki mwaminifu daima,
maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”

Mfanyakazi aliyekubaliwa na Mungu

14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya, na kuwaonya mbele ya Mungu
waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu
mkuu kwa wale wanaousikia.
15 Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi
ambaye haoni haya juu ya kazi yake, na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe
wa kweli.
16 Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ya kipumbavu; kwani hayo
huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu.
17 Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni
mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto.
18 Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu
wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake
yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na
“Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”

20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna:
vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni
vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
21 Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote
maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu,
anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema.
22 Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani,
pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi.
23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta
magomvi.
24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote,
mwalimu mwema na mvumilivu,
25 ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu
akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli.
26 Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa
Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake.

\c 3

Siku ya mwisho

1 Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.
2 watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno,
wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na
shukrani na waovu;
3 watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma,
wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema;
4 watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa
kuliko kumpenda Mungu.
5 Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana
nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.
6 Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake
dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za
kila aina;
7 wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia
ujuzi wa huo ukweli.
8 Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga
Mose.
9 Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao
utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.

Maagizo ya Mwisho

10 Wewe lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu,
makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo
wangu, subira yangu,
11 udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko
Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini
Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
12 Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana
na Kristo Yesu lazima adhulumiwe.
13 Watu waovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi kwa
kuwadanganya wengine na kudanganyika wao wenyewe.
14 Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa, ukaukubali
kabisa. Unawajua wale waliokuwa walimu wako.
15 Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu
ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa
Kristo Yesu.
16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na
yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na
kuwaongoza watu waishi maisha adili,
17 ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa
kufanya kila tendo jema.

\c 4

1 Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu
watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:
2 hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au
wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa
uvumilivu wote.
3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila
watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia
mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.
4 Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya
kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.

6 Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na
wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani
nimeitunza.
8 Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu,
tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi
tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.

Maagizo

9 Fanya bidii kuja kwangu karibuni.
10 Dema ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake
Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia.
11 Luka peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje
naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu.
12 Nilimtuma Tukiko kule Efeso.
13 Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa;
niletee pia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi.
\il 5
ic
\is Vitabu vya ngozi katika maktaba (2 Tim. 4:13)
\ie

14 Yule sonara aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana
atamlipa kufuatana na hayo matendo yake.
15 Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.

16 Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama
upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!
17 Lakini, Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza
kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa
katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.
18 Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka
katika Utawala wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele!
Amina.

Salamu za mwisho

19 Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
20 Erasto alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa
sababu alikuwa mgonjwa.

21 Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na
Klaudia wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.

22 Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.
\z

\id TIT SW57.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PAULO KWA
                 TITO

\h TITO
\c 1

1 Mimi Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo naandika.
Mimi nimechaguliwa kuijenga imani ya wateule wa Mungu na kuwaongoza
waufahamu ukweli wa dini yetu,
2 ambayo msingi wake ni tumaini la kupata uzima wa milele. Mungu
ambaye hasemi uongo, alituahidia uzima huo kabla ya mwanzo wa nyakati,
3 na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake.
Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo nuutangaze kufuatana na amri ya Mungu,
Mwokozi wetu.

4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani
tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka
kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.

Kazi ya Tito kule Krete

5 Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa
yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka
maagizo yangu:
6 mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke
mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa
wakorofi au wakaidi.
7 Maana kwa vile kiongozi wa kanisa ni mkurugenzi wa kazi ya Mungu,
anapaswa kuwa mtu asiye na hatia. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa
hasira, mlevi, mkorofi au mchoyo.
8 Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu
mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
9 Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama
unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho
ya kweli na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.

10 Maana, wako watu wengi, hasa wale walioongoka kutoka dini ya
Kiyahudi, ambao ni wakaidi, wanaowapotosha wengine kwa upumbavu wao.
11 Lazima kukomesha maneno yao, kwani wanavuruga jumuiya nzima kwa
kufundisha mambo ambayo hawapaswi kufundisha; wanafanya hivyo kwa nia
mbaya ya kupata faida ya fedha.
12 Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema:
“Wakrete, husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na
wavivu!”
13 Naye alitoboa ukweli kwa sababu hiyo, unapaswa kuwakaripia
vikali, ili wawe na imani kamilifu.
14 Wasiendelee kushikilia hadithi tupu za Kiyahudi na maagizo ya
kibinadamu yanayozuka kwa watu walioukataa ukweli.
15 Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote
kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na
akili zao zimechafuliwa.
16 Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo
yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo
lolote jema.

Mafundisho ya kweli
\c 2
1 Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho safi.
2 Waambie wazee kwamba wanapaswa kuwa na kiasi, wawe na busara na
wataratibu; wanapaswa kuwa timamu katika imani yao, upendo na uvumilivu.

3 Hali kadhalika waambie wanawake wazee wawe na mwenendo wa uchaji
wa Mungu; wasiwe wachongezi, au watumwa wa pombe. Wanapaswa kufundisha
mambo mema,
4 ili wawazoeze kina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto,
5 wawe na kiasi na safi, waangalie vizuri mambo ya nyumbani, na
wawatii waume zao, ili ujumbe wa Mungu usije ukadharauliwa.

6 Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi.
7 Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo
mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
8 Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili adui zako waaibike
wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.

9 Watumwa wanapaswa kuwatii wakuu wao na kuwapendeza katika mambo
yote. Wasibishane nao,
10 au kuiba vitu vyao. Badala yake wanapaswa kuonyesha kwamba wao ni
wema na waaminifu daima, ili, kwa matendo yao yote, wayapatie sifa njema
mafundisho juu ya Mungu, Mwokozi wetu.

11 Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu
wote.
12 Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia;
tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu
huu wa sasa,
13 tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati
utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika
uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na
hamu ya kutenda mema.
\fr 2:14
\f taz Zab 130:8

15 Basi, fundisha mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza
na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.

Maisha ya Kikristo
\c 3

1 Wakumbushe watu kuwastahi watawala na wenye mamlaka, kuwatii na
kuwa tayari kwa kila namna kutenda mambo yote mema.
2 Waambie wasimtukane mtu yeyote; bali waishi kwa amani na
masikizano, wawe daima wapole kwa kila mtu.
3 Maana, wakati mmoja sisi tulikuwa wapumbavu, wakaidi na wapotovu.
Tulikuwa watumwa wa tamaa na anasa za kila aina. Tuliishi maisha ya uovu
na wivu; watu walituchukia nasi tukawachukia.
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu, Mwokozi wetu,
ulipofunuliwa,
5 alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema
tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya
Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa
kutuosha kwa maji.
6 Mungu alitumiminia Roho Mtakatifu bila kipimo kwa njia ya Yesu
Kristo, Mwokozi wetu,
7 ili kwa neema yake tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na kuupokea
uzima wa milele tunaoutumainia.
8 Jambo hili ni kweli.
Ninakutaka uyatilie mkazo mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu,
wawe na hamu ya kuutumia wakati wao katika kutenda mema, ambayo ni mambo
mazuri na ya manufaa kwa watu.
9 Lakini jiepushe na ubishi wa kipumbavu, ugomvi na mabishano juu ya
Sheria. Mambo hayo hayana faida yoyote na ni ya bure tu.
10 Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili,
kisha achana naye.
11 Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake
zathibitisha kwamba amekosea.

Mawaidha ya mwisho

12 Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja
Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.
13 Jitahidi kumsaidia mwana sheria Zena na Apolo ili waweze kuanza
ziara zao na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji.
14 Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda
mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.

15 Watu wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu
katika imani.
Nawatakieni nyote neema ya Mungu.
\z

\id PHM SW58.ALL 5/12/89 SN SWAHILI FINAL DRAFT

          BARUA YA PAULO KWA
                 FILEMONI

\h FILEMONI
\c 1

1 Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo,
ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu
2 na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na
askari mwenzetu Arkupo.

3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa
Bwana yesu Kristo.

Upendo na imani ya Filemoni

4 Kila wakati ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru
Mungu
5 maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo
wako kwa watu wote wa Mungu.
6 Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na
ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na
Kristo.
7 Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana!
Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu.

Ombi kwa ajili ya Onesimo

8 Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako
katika Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya.
9 Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya
hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa
kwa ajili yake.
10 Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni
mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
11 Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu,
lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia.

12 Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe.
13 Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo
kifungoni kwa sababu ya Habari Njema.
14 Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi
kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako
wewe mwenyewe na si kwa kulazimika.

15 Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena
kuwa naye daima.
16 Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa: yeye ni
ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa
maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana.

17 Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena kama vile
ungenipokea mimi mwenyewe.
18 Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako, basi,
unidai mimi.
19 Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe:
\is Mimi Paulo nitalipa!
\ie (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi
yako.)
20 Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili ya jina la
Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo.

21 Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua
kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
22 Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa
sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni.

Salamu za mwisho

23 Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu.
24 Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu,
wanakusalimu.

25 Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.